Huyu ni Mungu wa aina gani anaacha niteseke kiasi hiki?

Huyu ni Mungu wa aina gani anaacha niteseke kiasi hiki?

Mungu yuko ndani yako wew....acha kufuata watu wengine wanachofanya...

Hebu msikilize vzr Huyo Mungu wako. Utafanikiwa

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Unajua bwana MUNGU wetu huwa anaombwa maombi na viumbe wake na kuna viumbe wengine huwa wanaomba maombi yao vizuri sana kiasi kwamba hata MUNGU mwenyewe akiskiliza maombi yao huwa anafurahi kupita kiasi kwa jinsi wanavyomuomba, sasa kwa vile MUNGU anavyofurahi jinsi anavyofanyiwa maombi na kumiminiwa sifa, huwa anatamani aendelee kuombwa hivyo hivyo ndio maana anachelewesha kukupa coz anajua akikupa mapema utaacha kummiminia sifa zaidi kama ulikuwa ukimmiminia hapo mwanzo.

Ila kikubwa tu ni kuendelea kuamini uwepo wake na utukufu alionao kuwa yeye hashindwi na jambo liwalo lote, unaweza kukata tamaa juu yake hii leo wakati yeye alipanga kesho tu iwe siku yako na akupe hitaji la moyo wako ambalo ulilihangaikia kwa muda mrefu sana, mwisho kile chote ulichokianza tangu mwanzo ikawa work done is equal to zero.
 
na namuomba mungu wangu akumalize kabisa kwanini usiende kwa mungu wako kawe mwamposa atakupa kila kitu
 
Wakuu
Najitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kwa miaka kadhaa hapo nyuma mpaka leo mwaka wa tano huu bila kutetereka.

Kama ni kuumia nimeumia sana. Kuna muda nafikia stage najiuliza ya kwamba hivi kama yupo MUNGU wetu tunayemuabudu, kumuimba na kumsifu kila uchao, je anaweza niacha naendelea kuteseka namna hii?
Unataka Upate nini, au umekosa nini ?

Kupata au kukosa ni kwamba haufuati Kanuni Husika ya unachotafuta (you need to play the game) Huwezi kupanda Bangi ukaomba ili upate mchicha, na ukipanda mchicha hata usipoomba utavuna mchicha..., usipovuna kinachokosena huenda ni mbole au maji au eneo halifai na sio (uwepo au kutokuwepo kwa Mungu)
 
Unafanya kazi kwa bidii
Huna maradhi yaliyokulaza hospital
Uko timamu
Unapumua pumzi ya bure na bado unahoji kweli?
Bado hajaumwa huyo ataomba sala zote, binadamu tunakuwaga wajanja tu tunapokuwa wazima
 
Wakuu
Najitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kwa miaka kadhaa hapo nyuma mpaka leo mwaka wa tano huu bila kutetereka.

Kama ni kuumia nimeumia sana. Kuna muda nafikia stage najiuliza ya kwamba hivi kama yupo MUNGU wetu tunayemuabudu, kumuimba na kumsifu kila uchao, je anaweza niacha naendelea kuteseka namna hii?
Si ushukuru hata unakaa kwenye kazi moja miaka 5 wengine kili tukipata kazi au biashara ikipanda tuu lazima ipotee yaan utajiri unauchungulia tuu alafu unashuka hadi chini kabisa hata jero hupati... ndoa inavunjika unajikuta kama kituko duniani but hatufikii hatua yakukufuru uwepo wake bali tunalia na kipimo cha jaribu lake katka maisha yetu
 
Always unapojisikia upo desperate, ama haupo unapotaka kuwepo maishani hebu waangalie wa chini yako. Angalia wanavyostruggle. Halafu mlani shetani na umshukuru Mungu kwa alipokufikisha.

Huu ni UBINAFSI...

Kwahiyo kwakuwa wewe unateketea Mimi nikiungua ni SAWA?

#YNWA
 
Binadamu tunajipalilia makaa ya mawe wenyewe, kumlaumu Mungu bila sababu ya msingi.

Unapomuomba Mungu asilimia 90 ya maombi yawe ni kumpa shukrani Mungu.

Ukifanya tathimini ya maisha yako mengi ni ya kumshukuru Mungu kuliko hata hicho unachomwomba akubarikie ukipate/ukifanikishe.
 
Kila Jambo huja kwa wakati wake...

Usikate tamaa.. ... Maadam upo hai nawe utapata kilicho chako!
 
Wakuu
Najitahidi sana kufanya kazi kwa bidii kwa miaka kadhaa hapo nyuma mpaka leo mwaka wa tano huu bila kutetereka.

Kama ni kuumia nimeumia sana. Kuna muda nafikia stage najiuliza ya kwamba hivi kama yupo MUNGU wetu tunayemuabudu, kumuimba na kumsifu kila uchao, je anaweza niacha naendelea kuteseka namna hii?
Kama vipi jiuwe umfuate sasa unataka akufuate yeye??
 
Back
Top Bottom