econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Huyu mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga anatakiwa ashauriwe asiongee yote akasahau kesho. Mwanzo alisema CHADEMA walimpitisha Lissu kugombea Urais huku wakijua hawezi kushinda. Hii kauli ilikuwa inakivua chama nguo mbele za watu. Kuonesha kwamba CHADEMA haina haja ya kushika madaraka bali inaigiza tu na kupoteza watu muda.
Leo katoa kauli nyingine ya kuudhi. Amedai ya kwamba Heche hawezi kuwa hata mwenyekiti wa Kijiji. Ntobi anasahau ya kwamba Heche amewahi kuwa Diwani wa Tarime , Mwenyekiti wa BAVICHA, Mbunge wa Tarime na hata mjumbe wa kamati Kuu. Leo kudai hawezi kuwa mwenyekiti wa Kijiji ni dharau ya juu. Hizi dharau za machawa wa Mbowe sio nzuri hata kidogo. Hata Kama hawampendi Heche na Lissu ila wachunge kauli zao.