Huyu Polisi wa zamani Marehemu Mkama Sharp alikuwa na Kipaji gani ambacho Polisi wengi wa sasa hawana?


Sijamdhihaki mkuu, zaidi ya kuwa smart kikazi pia alikuwa anaweza kukupiga mkwara mpk ukatepeta.
 
Kwa taarifa tu mtoto wake yupo ni askari ana cheo inspecta
 
Sio kukukamata unaongozana,aliua na uwezo wa kukuambia nikukute kituoni na masela wanatangulia wenyewe kituoni,mimi binafsi nilikutana naye osterbay polisi wakati huo ni staff sagent(major kipolisi),mbwembwe zake ni hizo hizo,maana nilivyokutana naye alimake sure najua kua kabeba bastora,RIP kamanda Mkama Sharp
 

Mheshimiwa ‘An Eagle’, Marehemu Mkama Sharp asingezuia maandamano...ya kwenda wapi? Tunapenda sana maandamano.
 
Alikuwa anajimix na masela, kilaji sana
Alikuwa chapachapa sana, ukiwa na sooo kumalizana naye syo issue alikuwa muelewa sana

Ova
 
Wale wazee wa Ajax pressure wanamtambua zaidi[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Nkama sharp..hahahaha Mungu amrehemu rafiki wa masela alikuwa na burudani zake shamba la bibi pale nilisikiaga kisa kimoja na watoto wa keko sijui ilikuwa kweli..!!
 
Kwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
 
kuna usemi "Simba ni mkali lakini watoto wake wananyonya" kwa mikwara hiyo ameshindwa kukalea kabinti kake katika maadili mazuri yule anajiita Tunda.
 
Yupo huyo kamanda..si ndio babayake Tunda? Kale katoto machepele? Huyo kamanda achana nae kabisa
 
Jamaa yupo kiteto,hajastaafu Bado.ni ocd nadhani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…