Huyu Polisi wa zamani Marehemu Mkama Sharp alikuwa na Kipaji gani ambacho Polisi wengi wa sasa hawana?

Moro kulikuwa na afande saba sita sijui yupo wapi
"SABA SITA" kwa sasa yuko wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara kama (OCD).Huyu jamaa miaka ya nyuma alinyoosha vibaka na majambazi waliokuwa wanasumbua Arusha, alikuwa yeye na Kachero mmoja aliyekuwa anaitwa Robert Bro mmoja alikuwa anapenda sana kupiga cheni kubwa kubwa na kupush ndinga za hatari, kiasi kwamba unaweza kujua ni msela flani kumbe Kachero. Huyo Robert naye sijui siku hizi yuko wapi.
 
Huyu Nkama Sharp kafa muda tu alizaliwa na pacha mwenzie huwezi kuwatofautisha ukiwaona
kabla hajaamia manzese kwenye nyumba yake aliishi
mtaa wa kibambawe namba 16 sisi tulikuwa na nyumba namba 14
night star waliimba kimbia mbio mbio mkama sharp anakuja
kafa kwenye 2008 zaidi ya miaka 10
 
Pale kibambawe alikuwa makali mmoja wa mjini maarufu Baba Jua unamfahamu? Marehemu nae daaa huyo Nkama Sharp alikuwa anamugopa mbaya
 
Tena alikumbana na kashfa ya wizi akaswekwagwa ndani nakumbuka
 
Sema kila zama na kitabu chake,waharifu Wa kipindi hiko nao walikuwa waoga na hawatumii akili na mbinu,waharibu Wa siku hizi wakiona unaweka usiku,wanadili na Wewe kwanza ,wakimaliza ndo mengine yafuatie
 
Nakumbuka enzi tunacheza disco Mbowe na YMCA kulikuwa na magangwe wa mjini
 
Mimi huyu Sajent Sharp nilikua nakutana nae mipirani miaka hiyo, hasa inapocheza Timu za Simba na Yanga. Pia pale Karume Stadium kulikua na Derby ingine ya BOOM v/s ASHANT ndo alikuwepo huyu Mwamba.

Watu walikua wakimuogopa vile alivokua amepigilia. Yaan amejikoki silaha za kutosha utadhani yuko vitani.

Saa zingine mashabiki husogea hadi kwenye Pitch sababu ya Uwanja kujaa, ila akipita huyu jamaa hata haongei kitu na mashabiki wenyewe hurudi nyuma kuupa nafasi Uwanja.
 
Niliwahi sikia tetesi kuwa kabla ya mauti alipatiksna na ukwasi Benk wa uliozidi kipato chake,na akatiwa hatiani Ni kweli!?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huu uzi ni wa mda mrefu sana ila nami naomba niseme jambo kidogo,
Baada ya kusoma uzi huu wa uzalendo wa askari na kubakia na lawama kubwa kwa maaskari wa sasa, nikweli kabisa kwa sasa kukutana na askari mwadilifu ni ngumu mno, naomba nami kumshukuru afande mmoja japo nimejitahidi kumtafuta kwa sasa japo nipate jina lake na hata kumpa mkono wa shukrani na pia ajue hata mimi leo ni nani na ajue kuwa maisha ni duara katika dunia hii.

Ilikuwa mwaka 2011 wakati nimehitimu shahada yangu ya kwanza nikaenda Mwanza kutafuta maisha, maisha nayo yakawa magumu kweli hadi nikaingia kwenye utapel wa kuuza viwanja vya watu kwa kutumia mihuri bandia na kugushi nyakaraka nyingi za serikali.

Siku moja nikanasa kwa mjanja mmoja ambae nilitaka nimpige zaidi ya milion 7 hivi ila akashtukia dakika za mwishoni kabisa wananzego wakanikamata na kukuchora vibao kadhaa na baadae kunipeleka kituo cha Police, baada ya kufikishwa police nimetoa maelezo bila kupindisha chochote pale nikaingizwa ndani na nililala na siku ya pili alikuja kuniita na kumbe kesi yangu alipewa yeye baada kunipeleka chumba cha mahojiano huku akinichukua maelezo, bila kusita nami niliongea ukweli mtupu bila kuficha jambo lolote.

Baada ya maelezo hayo kumalizika akaniambia kaka mbona elimu yako nzuri tu kwa nini unajiingiza huku kwenye kifo na huku unajuwa majuto yake? Nilimjibu tu kuwa kiukweli hapa mimi ni mjinga na shetani katumia nafasi hii kutaka kuniangamiza.

Baada ya kumpa majibu yale alikaa kimya mda mrefu sana, kaniuliza una ndugu wa kukuwekea dhamana nikamjibu sina ,je rafiki yeyote ambae mnafanya hizi Dili ?,nikamjibu hizi dili napiga mwenyewe sina rafiki, je nyumbani kwenu hakuna mtu wa kuja huku Mwanza?, nikamjibu naogopa kuwaambia nitaficha wapi sura yangu?
Baada ya maswali hayo kaanza kunifungulia vifungu vya sheria ambavyo nitatiwa hatia navyo na vile nitaitumikia adhabu yangu, machozi yalinitoka ghafla, akaniambia usilie najuwa umefanya jambo bila kujuwa madhara yake.

Baadae akampigia jamaa simu alienikamatisha jamaa akaja kituoni akamsomea vifungu vya sheria na kumuomba anisamehe na ujinga wangu umenifanya nifanye kitu bila kujuwa madhara yake, jamaa nae bila hiana alicheka kidogo akasema mie huyu kijana kwanza nimempenda kuongea ukweli wake ni kweli kajutia kosa lake hivyo namsamehe lakini kulingana na elimu yake aliyonayo basi naenda kumtafutia ajira na naahidi atakuwa mtu mwema na atakuwa rafiki yangu.

Ndipo yule afande alisimama akaniambia Mungu akutunze na naomba uchukue kila kitu chako uondoke hapa, ukweli machozi yalinitoka tena na kumshukuru tena na tena yule afande.

Ukweli ni kwamba bado wapo watu wenye utu japo ni wachache sana ila ukweli bado wapo.
Mungu akubariki afande mahali ulipo japo sikuoni natamani nikuone nikusaidie hata ada ya mwanao kwa upendo tu wa kawaida japo najuwa ungekutana nami leo na kunifahamu sijui kama ungeongea na mimi najua ungekuwa unaniogopa na kufikiri vingine Mungu wa mbinguni akutunze

Ahsante Mchungaji DR.Jacob Mutashi Mungu akutunze umalizie uzee mwema ulichokifanya kwangu ni zaidi ya kufanya jambo.
 
Duu one in million
 
Dah safi sana, maafande wa dizaini ya akina Mkama wapo wengi tu nimekutana nao, nimeishi nao, yaan mpaka unashangaa kweli maaskari wa namna hii bado wapo kweli? 😳 ILA WAPO KABISAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…