onlyalvira
JF-Expert Member
- Dec 9, 2013
- 1,499
- 3,113
Mkuu nisingekuona ningeshangaa[emoji28][emoji28]
Alishanikamataga sana huyu Enzi hizo
Mpk tukawa washkaji
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alishanikamataga sana huyu Enzi hizo
Mpk tukawa washkaji
Ova
Kwahiyo sisi tuliokuja mjini na mbio za mwenge tukae pembeni sio?Watakao changia hapa wengi wa mjini Kkoo na vitingoji vyake. Wengine mtasoma comments tuu!
Nakumbuka siku ile Nelson Mandela ametoka jela na kuja Tanzania tulikatiza Barabara mitaa ya Uhuru Gerezani alitusumbua sana na ule msafara wa Mzee Mandela hata kutua nchini ulikuwa bado..
R. I. P Mkama alimuliki kikundi cha Mchiliku enzi za Hisani gari kubwa..
🤣🤣🤣🤣🤣Kwahiyo sisi tuliokuja mjini na mbio za mwenge tukae pembeni sio?
nipo mkuuUnamkumbuka kitonsa, alikuwa bonge la mtu ndio walikuwa wa mwanzo kuendesha gari la polisi la kupeleka wahabusu mahakamani (karandinga)
nipo mkuuUnamkumbuka kitonsa, alikuwa bonge la mtu ndio walikuwa wa mwanzo kuendesha gari la polisi la kupeleka wahabusu mahakamani (karandinga)
Huyu mzee si baba mzazi wa video vixen, TundaKwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
Kweli kabisaBado wapo japo ni wachache sana mkuu
Zamani nlikuwa mtu wa mazabe sana
Mpk makomeo alinipaga Jina la mazabe
Yaani mchafu alikuwa anasubiri hpa
Kuibukiwa na wazee ilikuwa kama kwenda disco
Ova
Baada ya kustaafu alichukuliwa na Wizara ya Maliasili kuwatrain askari wanyamapori katika chuo cha wanyamapori Pasiansi Mwanza na pia katika mashirika kama TAWA, TANAPA na NCAA nowdays amebase sana upande wa NCAAYupo kamanda Tossi huyu alikuwa RPC Kagera miaka ya 2010 kipindi hicho uharifu ulikuwa unatishia usalama wa wananchi mkoani Kagera kutokana na wimbi la wakimbizi waliopelekea kuwepo kwa vitendo vya utekaji wa magari ya abiria hata binafsi kwenye misitu ya Biharamulo.
Kamanda Tossi alipofika mkoani Kagera alitangaza vita na waharifu wa aina zote kwenye vyombo vya habari na kufanya mazoezi makari kwa lengo ka kukabiliana na mjambazi. Kamanda Tossi alikuwa jitu la miraba minne lakini kwenye mazoezi alikuwa ikilala anateleza kama nyoka, alikuwa mwepesi sana ukilinganganisha na umri na umbo lake. Siku moja akiwa anatoka Biharamulo alikoswakoswa risasi na majambazi yakamtuia ujumbe wa simu kuwa hiyo ni ishara ya makaribisho.
Alipofika Bukoba Mjini kesho yake asubuhi sana alitiisha mkutano wa askari wrote, kisha akaamrisha wife wasalimishe simu zao kwake, kuwa wangerudishiwa baada ya Massa 48.
Alipanga operation na askari wake na wandishi wa habari na kuelekea msitu wa Biharamulo tayari kikosi cha inteligensua kilishabaini maeneo majambazi yaliko.
Aliongoza operation hiyo na kiwauwa majambazi wote, isipokuwa kamanda wao ambaye kwa mujibu wa mashuda risasi ilikuwa haipenyi kwenye mwili wake inasemekana walijaribu kummaliza kwa shoka na visu ikashindikana, Kamanda Tossi akatoa amri jambazi hiyo mchawi afungwe kwenye mti na kamba kuanzia miguuni mpaka kichwani chini ya ulinzi mkali Ali waone hatima yake. Jambazu alikufa kwa njaa baada ya wiki moja.
Heko kamanda Tossi sana Kagera tutakukumbuka daima kwa weledi ujasili na uzalendo uliotukuka. Sijui yuko wapi huyu Kamanda mwenye Picha yake atuwekee hapa.
Quote meUlikutana na Binaadamu kweli na siyo Mtu, katika Maisha siku zote omba Mungu ukutane na Wanadamu na siyo Watu!!
Zanaki Secondary 😂😂Kwahiyo sisi tuliokuja mjini na mbio za mwenge tukae pembeni sio?
Hata uwanja wa Taifa aka shamba la bibi aliwanyoosha waruka ukuta. Mtaa wa Kongo ndo vibaka walikuwa hawafurukuti.
Alikuwa na mambo mengi na Vituko vingi tu ila binafsi nakumbuka kila alipokuwa akienda katika Vijiwe vya Masela wa enzi hizo wenyewe Masela walikuwa wanapiga Magoti na wanajisalimisha Kwake na ama Bangi walizokuwa nazo na Vitu vya Uwizi walivyoiba na walikuwa wakiongoza wenyewe Kituoni Polisi.
Marehemu Nkama Sharp ndiyo alikuwa Polisi pekee Jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa hata akikukamata humbishii, unamtii na kweli hata Wewe mwenyewe unaamini kuwa ulikosea. Na alikuwa ni Polisi ambaye hana Uonevu na kuna muda alikuwa akiona unataabika au huna Msaada Kituoni basi anaweza Yeye kwa Huruma yake akakusaidia tena bila hata ya Kumpa Rushwa na ukatoka na hata ukitoka ulikuwa hurudii tena Makosa au Uhalifu.
Alikuwa na Uwezo wa Kipekee na Kipaji cha namna yake ambacho leo hii ni Nadra sana kukiona kwa Mapolisi wengi wa miaka hii ya sasa. Na nina uhakika kwa jinsi alivyokuwa Mweledi na ana Msimamo kama angekuwepo hadi miaka hii ya sasa kuna baadhi ya Maandamano ya Kisiasa wala asingekuwa anaiingilia au kuwasumbua Watu tofauti na Polisi wa sasa ambao kila Kukicha wao wanasema kuwa huwa wanatekeleza Maagizo kutoka Juu ( siyo Mbinguni kwa Mungu Baba )
Nashauri kama ikiwezekana Jeshi la Polisi nchini Tanzania litafute namna ya Kumuenzi huyu Marehemu Nkama Sharp ambaye Binafsi pia nakumbuka aliwahi kutufanya Mimi na baadhi ya Wenzangu tugawane Mitaa ile ya Jirani na Shule ya Muhimbili kwa Kumkimbia baada ya Kuambiwa kuwa tulikuwa tunafanya Fujo katika Mechi moja tuliyocheza na Wababe wa miaka hiyo Shule ya Tambaza na nakumbuka katika hali ya Kumkimbia niliweza Kupoteza Kiatu changu cha Mguu wa Kushoto na nilipofika Nyumbani nilipewa Kipigo cha maana ila nikashukuru kuwa ni bora nimepigwa na Wazazi kuliko ningeishia Mikononi mwa Marehemu Nkama Sharp.
Nasisitiza tena Marehemu Nkama Sharp aenziwe tafadhali na Mapolisi wa sasa hebu muigeni huyu Afande ili nanyi tuwapende.