Huyu single mother nasitisha mara moja kumuoa

Huyu single mother nasitisha mara moja kumuoa

Huu Uzi utapata wachangiaji wengi, single mothers utafikili walijipa mimba wenyewe in the other side na sisi tunaogopa wanaume waliozaa tayari.
Tabia za mtu zinahusiana nini na kujipa mimba mwenyewe?! Kinachozungumziwa hapa ni tabia au misimamo ya mwanamke ambaye amepata mtoto na mwanaume ambaye wameshindwa kuishi pamoja na kulea mtoto.

Hizi lawama zote hapa ni za kulaumu tabia za kuwa na maamuzi ya kukosa busara kwa kudharau mwanaume aliyejitoa kuwa na mwanamke mwenye mtoto tayari kisha kumrejea mwanaume ambaye ndie chanzo cha kuvuruga maisha yake.

Mbona kwenye mjadala mnapenda sana kuhamisha magoli as if ujumbe unakuwa unawachoma? Ina maana wewe husomi wanachoandika watu na msingi wa malalamiko upo eneo gani?!

Kwan wanawake kupewa ujauzito na kutelekezwa imeanza leo?! Si ni tokea miaka ya nyuma. Ila miaka hii wanawake wanaopata watoto na kutelekezwa wamekuwa na utomvu wa nidhamu na kutokuwa na discipline ya kujiheshimu na kumheshimisha mwanaume aliyeamua kujitoa kwaajiri yake na kubeba mizigo ya mwanaume ambaye ulimchagua wewe kwa utashi wako uzembe wako na kuamua kuazaa nae mtoto ambaye aligomea kumtunza pamoja na mama yake.

Sasa wewe unateteaje upumbavu kama huo na kugeuza geuza maneno hapa ionekane wanaume wanalaumu wanawake bila sababu yoyote
 
Mimi nilimkataa siku hio hio maana alinipa a/c zake za social media niende nione watoto wake, nikamuona Jamaa yake nikaona hii sio nzuri maana Jamaa alikua ni muislam na alimbadirisha hadi dini akawa amesilimu sasa nikaona hii sio sawa ila yeye akawa ananiganda nikaachana nae tu hadi leo hatuna mawasiliano yoyote na yeye, ingawa Jamaa yake walikuja wakatengana tena

Yaan huyu Jamaa alimkuta tayari ana mtoto mmoja hata mimi wakati nipo nae alikua na mtoto mmoja ambae alizaa na mhuni mmoja wa Arusha ambae baba yake anafanya Biashara za Madini

Hadi sasa amebaki kua single mother tu maana ndoa yake ilivunjika,

Nisiseme mengi acha niishie hapo tu naona kuna kitu utakua umekielewa japo kwa kidogo tu
Sawa nakuelewa, hiyo ni kwa upande wako upo hivyo.

Je ni kweli kwamba wanaume huwa hawarudi kwa ma-ex wao na kutaka kurudiana au kuwala tu?


Mbona wapo sana tu wakibembeleza kurudi? Hiyo ni tabia tu ipo kotekote. Unaweza ukamwacha mtu ukaenda kwa mwingine ukakuta afadhali ya kule ulikotoka.
 
Sawa Nafaka but hiyo ni akili ya mtu, si kwasababu amezaa. Msihalalishe kuwa kila aliyezaa huwa anarudi kwa aliyezaa naye. Kuna watu wana misimamo yao. Hata ambao hawajazaa huwa wanarudi kwa ma ex.
Hapa unatetea nini sasa kwa mfano ukiulizwa maana its like upo guilty of something sasa unatetea.
 
Kumbe mmeshaona single mother's ni watu wa hovyo, wasio na mapenzi ya kweli. Swali kwenu kwanini bado mnawatongoza? Mnawaoa? Kwa akili yangu, kitu kama ni hatari nakiepuka kabisa. Waacheni, mdate na wasiozaa halafu tuone, je hao ni Malaika na hamtalalamika tena? Tuko hapa...
Single mother matatizo yao ni Makubwa hayana tiba
 
Mkuu single mother wengine watoto wao wana kuwa na Baba wawili
Ndio hapo utaielewa vizuri akili ya single mother, ni mwekezaji anapiga huku anapiga na huku anapiga wote wanampa pesa ya matumizi ya mtoto, sio wawili tu mkiingia line mkajichanganya vibaya kwa single mother mmoja mnaweza mkajikuta mmepangwa hata watano na wote msijuane ila kila mmoja anamwambia huyu ni mwanao, na wewe kidume ukaamini

Juzi kuna mwamba alikua anagombana na single mother wake alimtoa mkoa wakaja kuishi nae huku, sasa Jamaa sijui ilikuaje akashika simu ya huyo mwanamke kuna namba alikua anataka aichukue ili awasiliane na mtu, bahati mbaya kuna meseji ikaingia Jamaa alikua hana kawaida kabisa ya kupekua simu ya huyo mwanamke

Sasa alipoona ile meseji ikabidi aingie kufuatialia nini kinaendelea, alichokikuta alijuta kwanini aliingia kusoma zile convo ikabidi amuite amuonyeshe na kumuuliza hiki nini kinachoendelea mwanamke kuona vile akaona ameyakanyaga akaondoka akamwachia Jamaa watoto hadi leo hajarudi, jamaa akampigia mama wa huyo mwanamke ili kumueleza anaambiwa binti yupo kwa mama yake na watoto kawaacha huku kwa jamaa, kamuacha mtoto mdogo ambae bado ananyonya Jamaa anashinda na mtoto ofisini kwake na kichupa cha maziwa

Wewe omba usimuliwe tu yasikukute
 
Best yangu ni singo maza kaolewa alikuwa hana mawasiliano na huyo ex baba mtoto now katafuta namba kazipata mawasiliano moto[emoji91] anakula pesa za matumizi na kamwambia mwanae huyo ni anko,

na mtoto alimuacha na miezi sita kalelewa na baba wa sasa,

sasa anapanga safari akaonane nae,amesema anamuaga mumewe anaenda kumsalimia bibi yake na anajua hawezi mkatalia,

namtizamaaaa[emoji849][emoji849][emoji849]
Daaah bora umesema ukweli wa rafiki yako.
 
Coz mwanzo alikiwa anatumia simu yangu kwasiliana na huyo mzazi, nikaona hili litaniletea shida nikamwambia tu ukweli unachokifanya sio vizuri mumeo akijua itakuwaje? Nikamwambia nyie ndiyo mnaosababisha walio na watoto wanaonekana sio wa kuolewa kwa hayo mambo,,

Now kanunuliwa simu kubwa na huyo bwana,

Kubwa kuliko kasema amemuambia ampe mimba nyingine[emoji16]
Hana akili,atakosa vyote atazalishwa tena ataachwa hapo na ndoa itakufa.
 
vipi kuhusu single father's na wenyewe pia wasioe maana hawana tofauti na hao wakina Dada waliozalishwa wakaachwa
Wote ni wale wale tena bora hata mwanamke anakukataa kupasha kiporo lakini kwa mwanaume yupo kama kondoo anaongoza machinjioni
 
Kama una hofu ya MUNGU na unapenda haki. Tafuta namba mpya mpigie simu mwanaume ujulishe kilakitu. Halafu kaa kimya. Rafiki wa kweli huwa anatenda haki sio kumfichia madhambi mwenzake.
[emoji102][emoji102][emoji102] daa wewe embu usimshauri hivyo walikotafutana hakuwepo
 
Hapo vip!!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtu ambaye nilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa January, nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo, na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion. Hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuwa ni binti mwenye msimamo kwenye mahusiano.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi, ila wakati tukiwa mwaka wa tatu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi. Jamaa akafanikiwa kumuweka kwenye himaya yake. Kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti, ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahairisha harusi mara kwa mara ila kafanikiwa kuzaa naye mtoto, ila baadaye wakaingia kwenye misuguano wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto, anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu. Anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiano akapata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe, nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba, nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake. Anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

1. Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyuma

2. Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambulishwa katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasababu kama yupo sereous akesahau kule pa zamani na kusonga mbele na njia mpya...

Mimi ni mtu ni kazi yangu na biashara zangu, sasa naona kwasababu hana kazi labda anaona apate mahali ambapo atapunguza makali fulani ya stress za mahusiono na maisha may be.

Binafsi naona niwe naye karibu amzee yule kiumbe then niangalie ustarabu mwingine ila asilani sintoweza kumoa tena...m
Unakaribishwa kwa ushauri
Umesema Wana mtoto me naona yeye kwenda kwenye msiba wa Babu wa mtoto wake sio vibaya ndugu sema una gubu sana
 
Back
Top Bottom