Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Ahsante sana kwa kunisahihisha! Ila niliambiwa booster / nutrients zenye salfa ni hatari kwenye mifugo. Hivyo niliziogopa kuzitumia.
 
Nitasubiri kwa hamu sana, nina mpango wa kuanza hiyo system, kuna watu waliweka hadi namba za simu humu ila baada ya kuwafuatilia kwa kina hakuna aliyekua anatoa msaada, wote ni kama wapiga dili tu, huyu anakwambia nutrients 30,000/ Ltr mwingine 100,000/Ltr yani full kukatishana tamaa, mwingine kaweka namba ya mdogo wake ambaye hata hajui hydroponic fodder ni nini!!! Nitag please nahitaji kujifunza kutoka kwa mtu ambaye anafanya practical ikiwezekana nitembelee shamba darasa ili kujifunza zaidi
 
Unampigia mtu akupe maelekezo ya awali anakwambia tuma hela kwanza ya kitabu, kuna kila kitu kwenye hicho kitabu, ukinunua unakuta amecopy humuhumu kwenye hili jukwaa ameongezea tupicha twa google basi. Watu wamekua na roho ya shetani sana sijui hata kwanini
 
Mimi nimelifanyia kazi na kuhusu gharama sio kubwa kivile. Nutrients nilinunua lita moja Tshs. 54,000/= Water purifier nimenunua lita moja Tshs 12,000/= Mbegu nanunua kila ninapotaka kutengeneza. Na hii ni kulingana na idadi ya mifugo niliyo nayo. Ila leo nataka kujaribisha zao jingine tofauti na chakula cha kuku na tayari nimeishapata horodha ya mahitaji.
 
Kiukweli ukikutana na mtaalam wala hautatumia muda mwingi kuelewa kinachoendelea. Mimi atakayehitaji maelezo namkaribisha - tena hatua kwa hatua. Kikubwa ni kuandaa muda wa kupeana maelekezo. Ukifanikiwa wewe unakuwa umesaidia jamii.
 
Kwa jinsi nilivyo na uhitaji wa hiyo system nitasafiri hadi unapofanyia hiyo system nijifunze kwa uzuri zaidi, uko mkoa gani?
 
Kwa jinsi nilivyo na uhitaji wa hiyo system nitasafiri hadi unapofanyia hiyo system nijifunze kwa uzuri zaidi, uko mkoa gani?
Wala sio kitu cha kusema ni complicated system .. mi huwa nafanya kwa vifaa nilivyonavyo ili mradi nifate maelekezo ya kitaalam. Kwanza mpaka sasa naoteshea ndani kwa sababu sijajenga sehemu maalum kwa ajili ya shughuli hiyo.
Niko Mwanza city - Karibu sana!
 
Mkuu naomba unisaidie na mimi
 
Uko wapi na una bei gani? mi nahitaji kwa sababu nimeanza kupata watu / wafugaji wanataka niwandalie chakula kwa ajili ya mifugo yao!
Nipo dsm mkuu nauza kila gunia laki moja.
 
Hii kitu wala ainashida sana otesha kwa vifaa ulivyo navyo namatokeo yanakua mazuri sana kama mm
Kawaida picha huwa inabeba ujumbe mkubwa sana zaidi ya maandishi / maneno. Umefanya jambo la maana, kwangu mimi nilikuwa nawaza kununua trei ila baada ya kuona hizo picha ulopost hapo - sinunui tena trei.
 
Tumia booster ambazo zipo reach in NPK ama tumia maji tu pekee bila hata booster napozungumza reach in NPK manake suphur isiwepo at all ama kwa 0.001%
Naendeleea kukushukuru kwa mchango wako wa mawazo. Mawazo ni sawa na ndoano
 
Kawaida picha huwa inabeba ujumbe mkubwa sana zaidi ya maandishi / maneno. Umefanya jambo la maana, kwangu mimi nilikuwa nawaza kununua trei ila baada ya kuona hizo picha ulopost hapo - sinunui tena trei.
[emoji15] [emoji12] [emoji12] [emoji12] ndo ivyo mkuu ukijiongeza unatengeneza vitu vya maana kwa garama ndogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…