Hypocrite Kenyans to repatriate somalians

Unamrudisha mtu Mohadishu leo halafu unasema umefanya ubinadamu!

Maisha ya westgate kwa siku 5 ndiyo maisha ya Mogadishu kila siku, sasa unapowapeleka westgate ya mogadishu kwa hisani huo ndio ubinadamu kweli.

Sisi tumekaa na wakimbizi milioni 2 kwa miaka 5. Tukawapa uraia.
Wale waliokataa wakakimbia msituni na kuleta vurugu za ujambazi tuliwapakia katika malori na kuwabwaga kwao.
Huo ndio ubinadamu kinyume chake walitakiwa wafungwe kwa kuishi isivyo halali.

Uninadamu anao Mtanzania aliyemsaidia msumbiji siyo mkenya aliyechochea vurugu kwa kumsaidia RENAMO
Ubinadamu anao Mtanzania alimsaidia south Afrika siyo Kenya alisaidiana na kaburu.

Katika suala la ubinadamu Kenya haina historia hata ya bahati, pengine ya unafiki.
Kwa hili Kenya wakubali kuwa ni wanafiki wazuri san
 
Unataka tuhesabu jinsi wakenya wakivyojaa tz kuanzia kwenye brothels hadi maofisini na magulioni.
Hivi wewe unapoteza point, hoja sio Wakenya waliopo Tanzania ama vice versa, bali ni jinsi gani ya kuhakikisha jinsi gani tunadumisha maendeleo Afrika bila kukandamizana ama kuoneana. Wasomali sisi tumehusika katika kujenga nchi yao na kuwawezesha kurudi nyumbani kwa hiari. Wengi wamepata uraia ila kuna wengi wanataka rudi nyumbani maanake kuna utulivu. Hatuwalazimishi kwa malori. Ni shughuli ambayo inafanyika kwa uelewano.
 
<br>
Wewe tatizo lako unaonekana kutegemea sana uvumi kitaani wakati wa kahawa, inafaa ieleweke hali ya utulivu imewarudi Wasomali na hata kuna Wakenya wanaofanya biashara Mogadishu sasa hivi. Kaka jifunze kutizama habari za kanda. Check hii&nbsp;<a href="http://www.youtube.com/watch?v=veDj2r8eE0s">http://www.youtube.com/watch?v=veDj2r8eE0s</a>
Zaidi soma hapa The African Story Challenge
 
How can you do that with thugs holding AK47
 
Wewe unafanya spinning ambazo media za Kenya zimekuwa zinafanya kila siku.
Hadi sasa kuna wakimbizi wapo na wala hawajafukuzwa.

Hakuna taifa linaloweza kuishi na watu wasiojulikana wapo wapi wanafanya nini.
Hujawahi kuona madhara ya wahamiaji harama wanavyotes.

Marekani inarudisha wahamaiaji haram, Israel inarudisha wahamiaji harama. Uingereza imeweka sheria kali kuhusu wahamiaji haram. Juzi Norway imepakiza ndege nzima ya wasomali ambao ni wahamiaji haramu.
Kenya ilishawafukuza wahamiaji haram kutoka Isleigh, nilikuwa naishi South C by then, nimeona.

Whamaiaji harama walipaswa wafunguliwe mashtaka na wafungwe. Wale waliokutwa na silaha walipaswa ahabu kali zaidi ya kurudishwa kwa malori. NDio rtumeondoa wahamaiaji harama Kenya wanafuata kile kile walichokuwa wanakilaani.

Kuhusu human right Kenya haina moral authority yoyote mbele ya dunia kuzungumzia hilo.
Hakuna Mkenya mwenye ubinadamu isipokuwa aliyefariki. Period.
 
They should go and blow themselves out of Kenya territory
They were born and raised in Kenya, and therefore they are Kenyans by citizenship.
As a matter of fact EAC needs Somalia than any other country
 
And kenya is becoming the only bastard papa in eac
 
Wacha kulinganisha nchi zilizoendelea na sie hoi wa Mungu Afrika. Marekani na Uingereza hatawakiwafukuza Waafrika kiholela hawana la kupoteza. Lakini sie majirani Afrika hatufai kufanyiana unyama wa aina hiyo. Wasomali kweli wanashukuru sana kwa yale tumewafanyia kwa kipindi kirefu. Wenzao wametulipua kwa mabomu nia yao kutufanya tuchoke na kuwafurusha hawa wazuri lakini wapi.
Somalia kama nchi ilikua imevurugika kabisa hadi chini, lakini tumeshiriakiana na wao na kuwainua hadi sasa wan katiba, bunge, na rais. Wengi wamepata uraia Kenya na wale wana nia ya kurudi tunawasaidia. Sasa kuna utulivu na wameanza ukulima kambambe.
Vilevile tumehusika sana katika kuboresha Sudan kusini na sasa wapo wengi wanarudi nyumbani kuendeleza katika ujenzi wa taifa.
Kama kweli Kenya iliwahi kuhusika katika zoezi la kuwapakia majirani wake kwenye malori, basi hiyo ni jambo mbaya sana linafaa kulaaniwa. Wakongo, Watanzania, Waganda nk wapo maelfu nchini Kenya na shughuli aina mbali. Haswa nawapenda sana Wachagga wa kutoka Tanzania, jamaa hawa wana bidii mithili ya mchwa, wanafanya biashara za kila aina Kenya, hawana muda wa kulalamika kiholela na uvivu.
 
Kweli nyani haoni makalio yake!
Operatio Kimbunga ilipoanza ilikuwa kelele kila kona ya EAC sasa mnafukuza wasomali tunaomba tuzisikie zile kelele zilizokuwa zinailaumu TZ kwa kuwatimua wahamiaji haramu.
 
Wewe hujui historia ya Tanzania na Wasomali.
Asili ya Wasomali ni wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Vita ilipofumuka Wasomali walitaka kurudi kwao. Tanzania ikawaambia warudi kwao kwani ni miaka 500 au zaidi walikuwa wananchi wa nchi hii. Wameruhusiwa kuishi nyumbani kwao Handeni na walitengenezewa kambi.
Hawakupewa ukimbizi au nini kwasababu wao ni raia wa asili wa nchi hii na wanarudi kwao.

Tanzania ndio imefunza jeshi la Polisi la hao wasomali kwa gharama zake. Hiyo ni sehemu tu ya uhusiano wa kindugu na Wasomali. Sisi hatuwasaidii bali tunawashirikisha kama raia wa nchi hii.
Kama Kenya mnaanza kuwapa maeneo ya kilimo sisi tunawaambia karibuni nyumbani na wanarudi bila passport wala nini.

Kenya inafahmika duniani kwa unyama wa kuua waoto na akina mama mchana kweupe. Ndio nchi ambayo rais na makamu wake wanatakiwa the Hague.
Kwa ubinadamu wa Tanzania pamoja na kuichafua kwa kutumia media Tanzania imetumia influence yake na kuishawishi mahakama ya The Hague kumruhusu Rutio arudi na Uhuru asiende ili kushughulikia matatizo ya nyumbani.Tanzania ni rafiki wa mahakama ya the Hague kwa utaratibu wa mahakama hiyo.

Sisi hatuhesabu nchi ngapi tumezisadia. Tuna historia kubwa ya kuwasaidia wachina kuingia UN. Tunahistoria kuanzia middle east kwa Wapalestina hadi south Africa, Latin America hadi ulaya ya kati.
Historia yetu inajulikana na wala si ya kutengeneza.

Leo mkenya aliyechoma akina mama na watoto kanisani ndiye awe na ubinadamu!
Mkenya aliyemsaidia RENAMO /Savimbi na Kaburu Voster asimame kuzungumzia haki za biinadamu.
Mkenya anajua haki ya binadamu kweli! Usaidie mauaji halafu useme unasaidia haki za binadamu

Watakaofuata sheria wataishi Tanzania, wahuni kama wale wanaojificha maporini na silaha kuteka mabasi tutawapakia katika maloria na kuwabwaga makwao. Yes, tuna uwezo huo na tunasababu hizo na tumefanya hivyo tena mchana. Kenya wameandika sana katika magazeti sisi tunapakia katika malori. Kenya atuambie nini kuhusu human right!

Hatufanyi unafiki kama ule wa kuwaondoa Wasomali Isleigh nyakati za usiku na wengine kutandikwa risasi kwasababu tu ni wasomali. Wasomali wanaoishi Isleigh ni wakimbizi ndani ya nchi ya Kenya, wanawindwa kama paa au swala.
Ukiishi Isleigh wewe ni halali polisi wa Kenya ajifunzie kupiga risasi.
 

Ni vigumu kudebate na mtu kama wewe maana naona uelewa wako upo tu katika ushindani. Hamna sehemu yoyote nimeongea mabaya ya Tanzania. Sielewi hili unalitoa wapi kuhusu Tanzania dhidi ya Kenya. Machungu yako yamekuziba hata uelewa. Kama ni kuwapa uraia Wasomali basi sisi hata tumevunja rekodi maana mkoa mzima mkubwa wa kaskazini ni Wasomali watupu. Mkuu wa majeshi amewahi kuwa Msomali na hata jeshi la polisi. Eastleigh unaweza dhani Mogadishu maana tumewapa sehemu yote kwa ajili ya biashara na makazi.
Yeyote anayehusika na uhuni basi ni lazima apakiwe kwa malori, hiyo ndio kauli dunia nzima, ila si kuwakuta watu manyumbani wakiwa na amani na kuwapakia wote hadi watoto.
Mauaji yaliotokea nchini Kenya yalikua kwa sababu za siasa mbaya, na waliochangia kwa haya bado wapo wanazurura hii ni baada ya kuwasingizia waliopo sasa ICC. Sote tunaelewa yaliyotokea. Kitu naelewa kuhusu sisi Wakenya ni kuwa hatuvumilii uongozi mbaya, lazima tufanye jambo hata kama atakufa wa mwisho.
 

Kamanda,

kuna kitu inaitwa 'geo-politics'...at times its best and safe to say 'its the shoe wearer who knows where the
shoe pinches'. Kwa hivyo hao Wakenya na wanyarwanda walokua wakiwashikia bango wabongo, hawakujua
wanalofanya au better yet, it was mere political posturing at play.

Wasomali si watu jamani...tusidanganyane, Mie nimeishi nao kona zote EA na pia huku ughaibuni. They can
take you to the limits in no time. Mie naona wakirudishwa ni sawa tu...hususan wale haramu.
 

..if Kenya allows for dual citizenship then it is even better.

..those Somalis wont feel inadequate once they attain Kenyan citizenship since they won't have to renounce their Somali citizenship.

..I think Kenya should just open her borders to every Somali, the same way u urge Tanzania to open her borders to all East African nationals.
 
Opening or not opening of borders by Tanzania is prerogative of its state, has nothing to do with us. Our borders are open to all members of EAC, and as for Somalis, we are doing much more than just opening the borders, we are helping them rebuild.
 
Opening or not opening of borders by Tanzania is prerogative of its state, has nothing to do with us. Our borders are open to all members of EAC, and as for Somalis, we are doing much more than just opening the borders, we are helping them rebuild.

..I meant u should open your borders to Somalis and give them every right like Kenyan citizens.

..what rebuilding r u doing in Somalia. Mlikuwa mmelala miaka yote and u let Somalia descend into anarchy.
 
..I meant u should open your borders to Somalis and give them every right like Kenyan citizens.

..what rebuilding r u doing in Somalia. Mlikuwa mmelala miaka yote and u let Somalia descend into anarchy.
Citizenship is given to the willing, we can't force them.
Hamna haja ku-debate na wewe kuhusu kuwasaidia Wasomali maana unaonyesha kutokujua chochote ila ignorance na machungu yasioeleweka.
 
Citizenship is given to the willing, we can't force them.
Hamna haja ku-debate na wewe kuhusu kuwasaidia Wasomali maana unaonyesha kutokujua chochote ila ignorance na machungu yasioeleweka.

..but Kenya has to put that offer on the table, and some will take it, and those who refuse can be repatriated. that is what Tanzania did to Burundi and Rwanda refugees we were hosting.

..Tatizo lenu Wakenya mnajifanya mnajua sana. Mlijaribu kutufundisha on what to do with illegal immigrants in Tanzania. sasa ndiyo tunawauliza why dont u try what ever u were preaching on us with Somali refugees that are in ur country??
 
Sina haja ya kurudia maneno ninayoyasema mara mia moja ndio yaweze kuingia akilini. Kenya hatuna haja kuwafundisha Watanzania jinsi ya kushughulikia wahamiaji, hiyo ni yenu na majirani zenyu, haituhusu. Na vile vile sio lazima tufuate mfano wenu, maana kila nchi inanchangamoto zake. Waburundi hawakua wanajilipua Dar kwa mabomu. I rest my case can't control the level of your thickness in understanding. Sichangii tena kwenye huu mjadala maana naona muko fixated bila uelewa wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…