I am depressed. Naombeni ushauri

Take home ya mume 800k
Take home ya mke 2300k

Jumla ya pesa ya familia kwa ajili ya kula, mavazi, elimu na maendeleo 800k. Ikizidi hapo hiyo ni favor tu...

Mwanaume kama unataka uishi walau 70yrs lazima mambo mengine yakae kisogoni.
 
Reactions: Ccc
Mwanamke unajiita ngangali utakua mbisha sana wewe

Au wewe ndo muhasisis wa ngangali na ngunguli
 
Yaan kwa mishahara yenu hiyo bado mnawaza kuomba mtaji sehemu?
Kwann mtoto umpeleke shule ya gharama kubwa wakati mtaji huna?Tatzo wanawake mnapenda show off sana.

Issue ndogo tu kama hyo inakupa depression kweli?Think twice

Anyway pole dada
Kaka kwenye ndoa kipato Cha mwanaume ndio kipato cha familia
 
Kuishi na Ke ni ngumu sana, inahitaji akili sana maana huenda hata hiyo shule(sijui gharama yake) mke ndio amesema mtoto aende, wakati gharama za shule ni kubwa na jamaa hana huo uwezo. Wanawake wana tabia ya kuigana, ameona watoto wa jirani wanasoma shule X anataka wa kwake nae aende huko bila kuangalia kipato cha mume.

Jamaa nae kuona hivyo anaangalia tu, anakuangalia aone utaenda nalo hadi wapi, si umeamua ku-take lead mwenyewe!! Mwisho lazima mkae kwenye drawing table mpange, ingekuwa hiyo 2300k+800k inawekwa mezani na kupangiwa majukumu, usingekuja ĥapa kutafuta ushauri, ndoa ya wawili wenye 40+ ilitakiwa kuvuka haya matatizo mda sana.
 
Nakumbuka nilipo kuwa na miaka 18, anko ali Nikuta nyumbani naangalia cartoon.

ali sema kijana naona ume amua kuwa mume wa pili nyumbani kwa dada yangu, haya we kimburu beba nguo tuondoke😂😃
 
Kwa hio akili yako pata tu depression.. kwanza huna tatizo lolote... Eshimu ndoa yako msikilize mmeo... 2.3 + 0.8 =3.1M
Na mnalipwa hio Hela kila mwezi mmeshindwaje kukaa kama familia mtatue changamoto za kawaida kama hizo
 
unanikandamiza kwa kuwa nimesema kipato changu mkuu? nimejibu hapo juu shule ni ya kanisa na alishauri yeye mtoto aende shule ya kanisa. hapo tatizo ni mimi kivipi?
 
Hizi ndoa mnazoingia kichwa kichwa bila kujuana kiundani matokeo yake ndo haya.
 
Kwa hio akili yako pata tu depression.. kwanza huna tatizo lolote... Eshimu ndoa yako msikilize mmeo... 2.3 + 0.8 =3.1M
Na mnalipwa hio Hela kila mwezi mmeshindwaje kukaa kama familia mtatue changamoto za kawaida kama hizo
kwahiyo tatizo ni mimi? kwanini hujaona tatizo zaidi ya mimi kuwa tatizo? je nikikwambia hata hiyo laki 8 yake ameanza kuhudumia miezi kadhaa iliyopita baada ya kukuta wali maharage kila siku bado utasema tatizo ni mimi?
 
Saidia nyumbani ila usimsahau mume wako.
ni kweli kiasili mwanamke anatakiwa ahudumiwe ila sio lazima kipato chako hakijitoshelezi.
bado unaweza pambania mtoto akasoma kwa ushauri tu tafuta thread za LIKUD kuhusu shule za English Medium kwa wale wenye vipato vidogo.
#ISHI NA MUME WAKO WEWE MWENYEWE HUJAKAMILIKA.
 
Wanawake pesa zao ni tamu kwelikweli!

Bora angeoa jobless tu akakaa home kulea kuliko huyu anayemkalia kooni mumewe awe ombaomba badala azungumzie hata kuweka akiba biashara ianze kama mradi wa familia na ukisimama vyema mkope.

A beggar at 40+!,hata mimi ningekataa.

Unayajua mahusiano ya ndugu wa kibongo? Akuanzime mtaji?
 
Wanawake wabinafsi utawajua tu na wala hawajifichi,maana chuki yao kwa Mwanaume asiyempenda huwa haijifichi!!
 
Miaka 40+, watu wazima wawili hamna hata kipande cha ardhi? Ikitokea mmefumba macho leo huyo mtoto wenu atarithi hiyo flatscreen?

Achana na maneno ya marafiki, achana na magroup ya wamama walioshindikana......watu wanafiki sana, huko kwenye magroup wanajifanya hawachangii chochote kwenye familia, ila kiuhalisia wao ndo wanaendesha familia.

Kaa chini na mumeo, pangeni kwa pamoja, wekeni mshahara mezani muupangie matumizi ya pamoja, kisha muamini, let him lead......mume haelekezwi, mume anashauriwa kwa upole, kisha unamuachia siku kadhaa za kutafakari ulichomshauri........using'ang'anize kila unachotaka au unachoshauri afanye hapo hapo......wenzetu hawapo hivyo.
 
Siku moja nagusa simu nakuta mke wangu kamuhadithia mwenzie asitoe pesa Aache kila kitu afanye Mume wake , wakati kama juzi alitoka kunipa 3M ya issue fulani nilikwama , nikajua kumbe wanawake hua mnapotezana wenyewe maana , familia yoyote mkifanya umoja mnasonga mbele , mkianza ubinafsi na familia inasambaratika na Mnaishia kufa maskini , kama mwenzenu anapata pesa anataka Mume wake aombe kwao wakati wangekaa wakajadili wajichange waanze taratibu , kwanza wanakaa bure hawalipi Kodi ilitakiwa wasave wafanye mambo mengine, lakini pia 40+ kukaa bure kunadumaza akili Sana hawana bills ili akili ziwakae sawa
 
kwani hayo mambo ukiyafanya wewe kuna hasara gani?

wewe tafuta kiwanja na lipa ada then yeye muache kwenye chakula.

huwezi kumlazimisha mtu mzima,itakiwa anastarehe yake aipendayo.

build your future.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…