I am depressed. Naombeni ushauri

I am depressed. Naombeni ushauri

wanawake wajanja sana kuna kale kamsemo kao sasa baba flani ukifa bila kutujengea nyumba tutaishije,sasa uwezo wa kununua uwanja unao sasa kuna haja gani ya kuitwa mwili mmoja ubinafsi hata kwenye maswala ya msingi? jamaa amekuacha makusudi tu aone utafanya nini kwanini ufungue duka la peke ako kwanza,ujue majukwaa haya yana amsha wengi,anafikiria huyu uwezo wa kununua uwanja anao afu anataka mindo niwajibike kwa faida yake na watoto wake? maana ukishasikia mkeo anazungumzia kuhusu kununua uwanja ujue anajihami ukivuta abaki na sehemu ya kuishi, kingine mtoto kama ana akili ana akili tu maana anazaliwa nayo wasomi wengi unao waona ni zao la shule za kawaida sa kwanini umpeleke mtoto shule za gharama wakati huna uwezo?
 
Pole.
Mimi naona hamna haja yeye kuanza kuzunguka kwa kaka yake kuomba mtaji. Nyie wawili kama mke na mume ndio mlitakiwa msaidiane kwa kila hali. Mngetafuta namna ya kutumia mshahara wako na wake mpate ya biashara na msiwe na biashara ya mke au ya mume kuweni na biashara ya familia.
Siongezi
 
Acha show- off.

Kwa kipato chenu inatosha kusomesha na kujenga. Shida inaanzia kwako, tafuta shule nafuu.

Mwanamke mpu***vu huivunja nyumba yake kwa ___
 
una take home ya 2.3 , mumeo ana 8 laki alafu unamwambia mmeo mkakope au muombe mtaji toka kwa ndugu yake ili mfungue business ,
kaa nae zungumza na mumeo umuulize ni wapi umemkosea au kuna shida gani kati yenu mpaka ashindwe kukuskiliza ama nini angependa au anafkiria kufanya kupata maendeleo.
NB: mara nyingi wanawake mnawakosea waume zenu kwa tabia au kitu kidogo tu kiasi wanashindwa kupanga na ninyi maendeleo.
HAKUNA MWANAUME ASIYEPENDA MAENDELEO HASA AKIPATA MKE MWENYE AKILI YA MAISHA, ila kama unatabia ya kumfosi au kumcompare kimaendeleo hata na kaka ake (jua wanaume hatupendi kulinganishwa hata kidogo) au tabia ya kujifanya mjuaji sana na hata zingine zisizopendezwa kwa mume basi hio ndio source.
 
Habari great thinkers.

Nimekuwa msomaji kwa muda mrefu sana humu, ila imenilazimu nijiunge ili nitoe nilichonacho maana ninahisi kuzidiwa moyoni sipati kulala usiku. Nahitaji ushauri.

Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 6, nimeolewa miaka 8 iliyopita, nyumba tunayoishi tumepewa na mama mkwe kwa hiyo hatujajenga na wala hatulipi kodi. Najua unajiuliza hizi information za nini leta hoja, sawa nakuja na hoja.

Ni hivi mume wangu ana kipato cha kawaida tu kwa mwezi labda laki 8 take home. Binafsi nina kipato kwa mwezi kama 2.3m take home. baada tu ya kufunga ndo mume wangu alipoteza kazi kwahiyo alikaa nyumbani kuanzia 2017 akaja kupata kazi 2021 lakini tuliiishi bila shida.

Yeye kwao ni last born ana kaka na dada. Mimi kwetu ni wa pili kuzaliwa ila nahudumia wazazi pia. Kipindi yupo nyumbani ni kamwambia aongee na kaka yake amuazime mtaji wa kufanya biashara lakini mwenzangu alikuwa akikaa kimya, so miaka ikaenda mpaka alivyokuja kupata kazi.

Mwaka jana mwishoni nikagusia tena na kumpa idea ya biashara na alionekana kuipenda sana akasema sawa, na hiyo mwaka jana nilimwambia kwa kuwa mtoto anaingia darasa la kwanza hatuwezi kutegemea mshahara pekee. Ingawa mimi nimefungua biashara ila bado changa na pia ninafanyaga tender za kuprint, kufunga zawadi na kadhalika.

Mtoto tumemtafutia shule kwa pamoja na ada alikuwa anaijua tangu Novemba, nikamwmabia ngoja nikupunguzie mzigo nitalipia usafiri na uniform akasema sawa.

Nikawa namkumbusha kulipa ada anasema anakumbuka. juzi jumapili anasema hiyo ada kubwa sana hatoweza hiyo shule, imagine bado wiki shule zifunguliwe.

Baadae nikamuuliza kuhusu ile idea ya biashara vipi? mana haijalishi mtoto anasoma wapi jinsi anavyozidi kukua madarasa ndivyo gharama zinazidi, akasema mi mambo ya biashara siyawezi wala sijawahi kuyawaza, duuh nikabaki nimetoa macho, nikamuuliza mbona ile idea uliipenda na ukasema utaifanya utamuazima kaka yako mtaji akasema mi siwezi hayo mambo.

Haa, moyo wangu uliinama sana tangu hiyo siku nina mawazo sipati usingizi. Najiuliza niongee na kaka yake au dada yake wamshauri kama hawezi kutegemea kukua kimaendeleo kwa mshahara tu au nibaki nalo? na nikibaki nalo nifanyeje?

Hawazi kujenga, hawazi kununua kiwanja, 2024 january nilimwambia tuweke kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua kiwanja akaweka mwezi wa kwanza nadhani kwa kuwa nilimkalia kooni.

Baada ya hapo akawa hawezi kuna siku nikamuuliza akasema mi niache tu na hayo mambo. Nikaacha nikaendelea mwenyewe, ila peke yangu nguvu ni ndogo.

Naombeni ushauri jamani mimi ni mtu mzima nina 40+ nashindwa kuomba ushauri wa rafiki zangu mana ndo yataenezwa.

Nadhani ninaweza pata depression kama ningebaki navyo moyoni kichwa kinauma kwa kuwaza.

Naombeni ushauri tafadhali.
naomba uwe mshangazi wangu nimekuwahiii😂🤣😅😇
 
Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi,uliendelea kua na mumeo bila ya yeye kua na kazi kwa miaka 4 bila kinyongo,hongera sana kwa hilo,

Mume kapata mke wa maana ila mke kapata dume vivu lisilopenda kutake risk,ukimuendekeza huyo,hutafanya lolote la kimaendeleo kwenye maisha yako,fanya umafia kidogo,onyesha hali ngumu ya kimaisha hapo home ili akili imkae sawa ila huo umafia usihusu mwanao,yeye apate mahitaji yake yote.
 
Shida inaanza na umri wako 40 plus.Ni umri ambao unaanza kuwa serious kupita kiasi kama mwanmke sasa sijajua kama mume wako ni 40 plus au la.

Shida ya Pili ni wewe kumpa mume wako maelekezo ya nini ufanye hiyo ni kutangaza ugomvi wa kimya kimya wa nani anaamua mustakabali wa familia yake.

Kimsingi wewe una haiba na tabia ya SINGLE women,Independent women ambao uwa mara nyingi wanahitaji mume kwa ajili ya status symbol na mara nyingi wanankuwa na aina ya wanaume ambao wanawahitaji ikiwamo kimuonekano,kitabia,kiuchumi,kielimu n,k,

Usauri wangu ni huu.Kwanza kabisa Jaribu kumuelewa baby wako ni nini anachokitaka katika maisha yake/yenu.Tafutaeni kufanya vile ambavyo vinawapa furaha na mkumbuke kile ambaco kiliwafanya mkawa pamoja tangu mwanzoni.

Mtotot mmoja haweza kuwapa shida mapema hivyo kuhusu namna ya kumlea.

Kama kweli unaelekea kupata Depression basi tafuta mtaalamu wa Saikolojia uzungumze naye na ikiwezekana wewe na mumeo muende kwa therapy kabisa ili mtumie pesa zaidi na uzidi kumuudhi zaidi halafu muachane then labda depression yako itaongezeka ukiwa single.

Relax he will come around.
 
  • Kicheko
Reactions: rr4
Habari great thinkers.

Nimekuwa msomaji kwa muda mrefu sana humu, ila imenilazimu nijiunge ili nitoe nilichonacho maana ninahisi kuzidiwa moyoni sipati kulala usiku. Nahitaji ushauri.

Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 6, nimeolewa miaka 8 iliyopita, nyumba tunayoishi tumepewa na mama mkwe kwa hiyo hatujajenga na wala hatulipi kodi. Najua unajiuliza hizi information za nini leta hoja, sawa nakuja na hoja.

Ni hivi mume wangu ana kipato cha kawaida tu kwa mwezi labda laki 8 take home. Binafsi nina kipato kwa mwezi kama 2.3m take home. baada tu ya kufunga ndo mume wangu alipoteza kazi kwahiyo alikaa nyumbani kuanzia 2017 akaja kupata kazi 2021 lakini tuliiishi bila shida.

Yeye kwao ni last born ana kaka na dada. Mimi kwetu ni wa pili kuzaliwa ila nahudumia wazazi pia. Kipindi yupo nyumbani ni kamwambia aongee na kaka yake amuazime mtaji wa kufanya biashara lakini mwenzangu alikuwa akikaa kimya, so miaka ikaenda mpaka alivyokuja kupata kazi.

Mwaka jana mwishoni nikagusia tena na kumpa idea ya biashara na alionekana kuipenda sana akasema sawa, na hiyo mwaka jana nilimwambia kwa kuwa mtoto anaingia darasa la kwanza hatuwezi kutegemea mshahara pekee. Ingawa mimi nimefungua biashara ila bado changa na pia ninafanyaga tender za kuprint, kufunga zawadi na kadhalika.

Mtoto tumemtafutia shule kwa pamoja na ada alikuwa anaijua tangu Novemba, nikamwmabia ngoja nikupunguzie mzigo nitalipia usafiri na uniform akasema sawa.

Nikawa namkumbusha kulipa ada anasema anakumbuka. juzi jumapili anasema hiyo ada kubwa sana hatoweza hiyo shule, imagine bado wiki shule zifunguliwe.

Baadae nikamuuliza kuhusu ile idea ya biashara vipi? mana haijalishi mtoto anasoma wapi jinsi anavyozidi kukua madarasa ndivyo gharama zinazidi, akasema mi mambo ya biashara siyawezi wala sijawahi kuyawaza, duuh nikabaki nimetoa macho, nikamuuliza mbona ile idea uliipenda na ukasema utaifanya utamuazima kaka yako mtaji akasema mi siwezi hayo mambo.

Haa, moyo wangu uliinama sana tangu hiyo siku nina mawazo sipati usingizi. Najiuliza niongee na kaka yake au dada yake wamshauri kama hawezi kutegemea kukua kimaendeleo kwa mshahara tu au nibaki nalo? na nikibaki nalo nifanyeje?

Hawazi kujenga, hawazi kununua kiwanja, 2024 january nilimwambia tuweke kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua kiwanja akaweka mwezi wa kwanza nadhani kwa kuwa nilimkalia kooni.

Baada ya hapo akawa hawezi kuna siku nikamuuliza akasema mi niache tu na hayo mambo. Nikaacha nikaendelea mwenyewe, ila peke yangu nguvu ni ndogo.

Naombeni ushauri jamani mimi ni mtu mzima nina 40+ nashindwa kuomba ushauri wa rafiki zangu mana ndo yataenezwa.

Nadhani ninaweza pata depression kama ningebaki navyo moyoni kichwa kinauma kwa kuwaza.

Naombeni ushauri tafadhali.
Shida ni hapo yeye ni lastborn. Yaani Hawa wanatakiwa waoane wenyewe kwa wenyewe.
Total dependant, wengi wao hawajielewi hata akila kutoa chombo ni kazi au kufua hata handkerchief.
 
Last born huwa kipengele sana, namuonea huruma mwanamke atakaeolewa na mdogo wangu
 
Pole.
Mimi naona hamna haja yeye kuanza kuzunguka kwa kaka yake kuomba mtaji. Nyie wawili kama mke na mume ndio mlitakiwa msaidiane kwa kila hali. Mngetafuta namna ya kutumia mshahara wako na wake mpate ya biashara na msiwe na biashara ya mke au ya mume kuweni na biashara ya familia.
Nimekusoma zaidi ya mara 2 ukichangia hoja kwa ukomavu wa akili na busara ya hali ya juu.
Wewe ni mwanamke bora zaidi jf
 
Back
Top Bottom