I and the FATHER are one!

I and the FATHER are one!

Mungu ni MMOJA,
Mungu unayemuamini wewe ndio wanayemuamini wote ? Nadhani jibu la hapo utakuwa umepata kama ni Mmoja au la....

Kwahio kinachoweza kufanyika ni watu katika makundi yenu kuamini kulingana na miongozo / Katiba yenu (Vitabu na Sheria zenu)
 
KaZi yangu kama mwalimu,

Ni kuwaelewesha wote, wapagani Kwa wenye dini, waamini na wasioanini kuwa,

Mungu ni MMOJA, na Jina la Mungu huyo mmoja aitwa Yesu Kristo/ YESHUA HAMASHIACH.
 
Bible imetwambia asemaye hakuna Mungu ni mpumbavu.

Sasa muda wa kuhangaika na ninyi Sina.

Wapo wanaamini uwepo wa Mungu,hawajamwamini, hao ni kondoo Si mbuzi,

Hao ndio nitahangaika nao.
Ni thibitisha maneno ya biblia yametoka kwa Mungu , ambae wewe pia umeshindwa kumthibitisha🤔
 
Lucifer ni Malaika Si mtu.

Na Elimu atoayo Roho mtakatifu,Si iliyopo pekee,

Hata chakula Gani Nile Leo au nini nivae, niende wapi na nisiende wapi Leo au kesho ajua Yeye na kuniambia.

Ajua yote yaliyopita ,yaliyopo na yajayo.
Thibitisha Kama Lucifer ni malaika..
Na Mimi niluthibitishie kuwa hakuna Malaika anaitwa Lucifer wala aliyekuwa anaitwa Lucifer
 
KaZi yangu kama mwalimu,

Ni kuwaelewesha wote, wapagani Kwa wenye dini, waamini na wasioanini kuwa,

Mungu ni MMOJA, na Jina la Mungu huyo mmoja aitwa Yesu Kristo/ YESHUA HAMASHIACH.
All the best na kazi yako... ila sababu unachoelewesha ni abstract and at best Imani (unavyoamini wewe) huenda ukadhani una ufahamu kuliko wale unowafahamisha..., kwahio the only factual things ni mambo mawili;

Moja sababu kuna waalimu wengi kama wewe wenye mafundisho tofauti we can agree 100 percent kuna porojo nyingi...

Mbili sababu huyo unayesambaza message zake ni muweza yote asiyehitaji msaada sioni kwanini anahitaji messenger wa kumfayia kazi yake wakati anaweza akatoa taarifa automatically kama alivyokupatia wewe... Na kama anatoa hizo taarifa unajuaje huenda wewe bado upo kwenye foreni ya kuelewa, yaani zamu yako haijafika ya kutoka gizani ?
 
Nimetumwa na Mungu kuhubiri injili Kwa viumbe wote.

Aaminiye na ataokoka. Amen.
 
Thibitisha Kama Lucifer ni malaika..
Na Mimi niluthibitishie kuwa hakuna Malaika anaitwa Lucifer wala aliyekuwa anaitwa Lucifer
(Ezekiel 28:14.)

Amefunuliwa kama kerubi afurikaye na Si Lucifer.

Turudi kwenye mada.

I and the FATHER are one ( John 10:30).

Mungu Mmoja mwenye Jina YESU.
 
Ezekiel 28:14 Wala haizungumzii kuhusu Shetani wala lucifer..
Ngoja Nikupe Elimu kidogo..

Neno Cherubim au Keruv au Kerub "כְּרוּב"
Ni neno la Kiebrania Ambalo kwa maana nyingine halisi Huitwa kwa Neno la Kiaramu kĕ-raḇyā kwenye aramaic huandikwa ܟ݁ܪܒ݂ܝܐ...

maana nyingine linamaanisha "kama mtoto" au "mtoto mdogo." Linatokana na mzizi r-b-y, ambao mara nyingine hubeba maana zinazohusiana na ukuaji, udogo, au ujana, kulingana na muktadha.

Kwa hivyo, kĕ-raḇyā mara nyingi huchukuliwa kumaanisha "kuwa kama mtoto" katika muktadha wa kiroho au maandiko.

Katika maandiko ya kidini mengi sana , "kama mtoto" au kama Kijana mwema mara nyingi humaanisha hali ya kuwa na imani safi, unyenyekevu, au sifa zinazohusiana na watoto.

We Huoni Ishara ya Cherubi kidini ni Mtoto mdogo???
Unajua kwa nini..?

Sasa tukirudi kwenye Hilo fungu la Ezekiel 28:14..

Tena Mimi nakushauri anza kuanzia Ezekiel 28:11-19..

Halafu kwenya Tafasiri Toa neno.Kerubi weka "Kijana mwema", "Mwenye Imani safi" au Wema "Kama Mtoto" au Wek Unyenyekevu au "Mnyenyekevu"..

Uone jinsi maan Uliyokaririshwa Itakavyoyeyuka..

Ezekieli 28:11-19
11 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,

12 Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.

13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.

14 Wewe ulikuwa kerubi [Sasa hapa badala ya Kerubi Weka Ulikuwa Kijama Mnyenyekevu ,Au Kama mtoto mwema,au Mwenye Imani safi] mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.

15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.

16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.

17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.

19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele."

NA Hilo.ni Onyo kwa Mfalme wa Tiro na wala haina uhusiani na Shetani
 
Umepotoka Kweli Kweli,

Ni kheri kutoijua njia ya HAKI kuliko kuijua Kisha ukaiacha.

Ni sawa tu na chumvi iliyoharibika, uitie nini Ili iwe na faida tena kulitumia!!
 
Onyesha Mahali Nilipopotoka Mtumishi Niko.Tayari Kuendelea Kujifunza..
Maana Bado najifunza Vingi sana
 
Umepotoka Kweli Kweli,

Ni kheri kutoijua njia ya HAKI kuliko kuijua Kisha ukaiacha.

Ni sawa tu na chumvi iliyoharibika, uitie nini Ili iwe na faida tena kulitumia!!
Lakini Usisahau Biblia Hiyo hiyo inasema Tokeni kwao Enyi watu wangu msishiriki Dhambi zao wala Kikombe Chao (Ufunuo)
 
Ezekiel 28:14 Wala haizungumzii kuhusu Shetani wala lucifer..
Ngoja Nikupe Elimu kidogo..

Neno Cherubim au Keruv au Kerub "כְּרוּב"
Ni neno la Kiebrania Ambalo kwa maana nyingine halisi Huitwa kwa Neno la Kiaramu kĕ-raḇyā kwenye aramaic huandikwa ܟ݁ܪܒ݂ܝܐ...

maana nyingine linamaanisha "kama mtoto" au "mtoto mdogo." Linatokana na mzizi r-b-y, ambao mara nyingine hubeba maana zinazohusiana na ukuaji, udogo, au ujana, kulingana na muktadha.

Kwa hivyo, kĕ-raḇyā mara nyingi huchukuliwa kumaanisha "kuwa kama mtoto" katika muktadha wa kiroho au maandiko.

Katika maandiko ya kidini mengi sana , "kama mtoto" au kama Kijana mwema mara nyingi humaanisha hali ya kuwa na imani safi, unyenyekevu, au sifa zinazohusiana na watoto.

We Huoni Ishara ya Cherubi kidini ni Mtoto mdogo???
Unajua kwa nini..?

Sasa tukirudi kwenye Hilo fungu la Ezekiel 28:14..

Tena Mimi nakushauri anza kuanzia Ezekiel 28:11-19..

Halafu kwenya Tafasiri Toa neno.Kerubi weka "Kijana mwema", "Mwenye Imani safi" au Wema "Kama Mtoto" au Wek Unyenyekevu au "Mnyenyekevu"..

Uone jinsi maan Uliyokaririshwa Itakavyoyeyuka..

Ezekieli 28:11-19
11 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,

12 Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.

13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.

14 Wewe ulikuwa kerubi [Sasa hapa badala ya Kerubi Weka Ulikuwa Kijama Mnyenyekevu ,Au Kama mtoto mwema,au Mwenye Imani safi] mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.

15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.

16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.

17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.

19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele."

NA Hilo.ni Onyo kwa Mfalme wa Tiro na wala haina uhusiani na Shetani
Mfalme wa Tiro ametajwa kuwa alikuwa ndani ya Bustani ya Eden,

Lini Mfalme wa Tiro alianza kutawala?

Iweje awemo ndani ya Bustani ya Eden, afanye nini ?

Mfalme wa Tiro alikuwa mfalme wakati wa Nabii Daniel, lini aliingia Eden?

Ndipo sasa ujue,Kwa nje alikuwa mwanadamu, lakini ndani alikuwa Shetani mwenyewe.

Shetani / nyoka/ joka ndiye aliyekuwa Eden akamdanganya Eve kutomtii Mungu.

Wewe umeamua kumkataa Mungu na kugeukia Giza,

Wewe ni chumvi iliyoharibika, ni WA kutupwa jaani🤔
 
Umesahau kusimulia kwamba alikufa siku3 zenye jumla ya masaa 36 na kufufuka .
 
Yesu aliutoa uhai wake Kisha kurudisha tena katika mwili maana ndiye Mungu.

Hata sasa anaishi, ndio maana tunahubiri habari njema za Yesu aliyefufuka.

Aamin
 
Mkuu kulingana na biblia siku 3 ni masaa mangapi?
 
Krisha naye kwenye Bhagavad Gita anasema hivi:-
9.23

"Hata wale wanaoabudu miungu mingine kwa imani wananiabudu Mimi pia, Ee Arjuna, lakini kwa njia isiyo sahihi."

9.24
"Mimi ndiye mpokeaji na Bwana wa matoleo yote ya dhabihu, lakini kwa sababu hawanitambui kwa ukweli, wao hurudi tena kwenye mzunguko wa kuzaliwa na kifo."

9.25
"Wanaoabudu miungu wataenda kwa miungu, wanaoabudu mizimu wataenda kwa mizimu, wanaoabudu mababu wataenda kwa mababu, lakini wanaonitolea Mimi ibada watakuja Kwangu."
NDIYO

Haya maneno yanafanana kabisa na habari za Yesu kutoka kwenye vitabu vya Injili.

Kiuono na Ufikirifu mifumo, fizikia na metafizikia ya UTU ndiyo jambo lenye asili ya mtu/mwanadamu/mwana-wa-adamu na mtu wa mbingu/'Adamu mpya'...

Iwe ni Bhagavad Gita, ama Injili, maneno ya Yesu ama Krishna ni mambo ya Ufahamu Kristu/Ufahamu Krishna.

Kuna namna yake ya kufasili habari zake; labda kwa mtu asiye na uono na ufikirifu mifumo anaweza 'kupotea katika tafsiri'...

Krishna anamshawishi Arjuna kuangamiza ndugu zake 'Makafiri' katika uwanja wa mapambano ya Kurukshetra katika nchi ya Mahabharata...

Watu wa Ufahamu-JUA huja kwa habari na mashauri ya UKUU...

UKUU wa Yesu si jina; UKUU wa Yesu ni 'SHAURI la uhai' kupitiliza Uzima wa Miili.

Katika lugha yetu ya Kiswahili, tayari kuna utundu ulishatayarishwa wa maana na mapelekeo ya maana kwa mashauri ya Ukuu...

Neno 'Jina' lina asili moja na neno U-Imajinishi; ambapo uimajinishi neno lenye viambishi 'maji', kiambishi 'jini'; na tena vyote hivi viwili vinasili ya 'jinesesia'.

Jinesesia, lawa neno rasmi la Kiswahili kwa tafsiri ya neno 'Genesis'; wafasiri wa mwanzo wa vitabu vya Biblia walionelea bora kutumia neno 'Mwanzo' badala ya neno jingine lenye asili ya kigeni.

Genesis, kutoka kwenye lugha ya Kiingereza, ni kitabu cha Kwanza cha Musa kinachosimulia 'Habari za Mwanzo' wa mambo--mwanzo wa mambo ya 'Mbingu' na 'Nchi'...

Katika karne hii ya 21 tunazungumza mambo ya 'Mwanzo' kama 'Ontolojia ya Taasisi'...

SASA, neno Genesis lina etimolojia ile ile na neno 'Genie'--Jini kwa Kiswahili.

Kiuono na Ufikirifu mifumo, muktadha akilifu wa utendaji usiofuatisha nguvu za kawaida za miili ndiyo huzaa 'maajabu ya ulimwengu' unaofanyika kutokea kusiko kitu.

Ndivyo basi simulizi la mwanzo kabisa la Kitabu cha Kwanza cha Musa husimulia habari za Ulimwengu uliofanyika kwa dhamira, shauri na uimajinishi wa 'Roho wa Mungu'....

Vitu vyote kufanyika kwa mfano wetu ni shauri la 'Uimajinishi'; kwenye mashauri yajayo kwa lugha ya Kiingereza hili lingalitajwa kama 'Imagination'.

Kiuono na ufikirifu mifumo, muktadha wa uimajinishi ndiyo unaofanya 'nafsi' yeyote 'kufanana na Mungu'--Uwezo, Nguvu na Utukufu wa 'Roho wa Mungu' ni funguo ya 'Ontolojia ya Taasisi' kwa sisi sote kama viumbe wenye Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu.

Yote kuwezekana katika 'Yeye' atutiaye uzima ni shauri la 'Nia ya Unafsi Moja' katika 'Roho wa Mungu'.

Yesu kunukuliwa kusema yeye ni Njia na Kweli na Uzima ni 'SHAURI la nguvu' katika 'Nia ya Unafsi Moja' katika 'Roho wa Mungu'.

'Nia ya Unafsi Moja' katika 'Roho wa Mungu' ndiyo khasa 'Ufahamu Kristu'...

Mimi na Baba ni Moja ni ushuhudiaji wa dhamiri ya Imani katika Uweza na Utukufu--'I' kwa lugha ya Kiingereza hukazia 'Utu Nafsi' na angali 'I' katika 'Imani' vile vile U-I-majinishi hukazia nia ya 'Utu wa Nguvu' katika 'Maji ya Uzima Wote'...

Kitabu Jinesesia, hutaja esoteria ya 'maji, uso na roho' halafu kisha 'maji ya Juu' na 'maji ya Chini'...

SASA, mtu kusoma habari za jinesesia halafu kuzichukulia kama ni 'Taarifa Fulani ya Habari' ni njia rahisi ya kujipotosha ama tuseme 'kujizima data'...

Dunia ni tufe, siyo bapa... Mbingu na Nchi ni mambo ya 'uso' na 'vilindi vya maji'--Ontolojia ya Taasisi. Kadiri mtu anapopanua fahamu zake za akili, utambuzi na fahamu kuna namna huyu ataanza kubaini vitu vyote ni 'alama zinazoishi'; alama hizi huitika dhamiri na mafikara ya kujiwazia utu ama tukizo la madhahiri...

Vitu vyote, ikiwemo maisha yetu na mambo yetu ni matokeo ya sisi wenyewe kujiwazia utu na matukizo ya madhahiri.

Kwa hivyo wakati mmoja, In Shaa Allah, tutaelekezana habari za 'KUSALI' kwa ajili ya 'kutenda miujiza'--si kwa 'imani pofu' na mapokeo yasiyo na msaada bali kuharakishia 'mema ya nchi'.

Kwa kuwa tunaishi ulimwengu uliofungamana makusudi, ikiwa watu watajifunza kusali katika vikundi kwa 'neema na saburi' mengi yataanza kubadilika na uponyaji wa mataifa utadhihiri.

Tunaishi kwenye ulimwengu mbovu wa 'Miundo ya Tawala/Ontolojia ya Taasisi'; tukifahamu kuuishi mwongozo bora wa U-JUA-ji wa Njia na Kweli na Uzima basi Tutaubadilisha Ulimwengu unaotuzunguka--jambo ambalo katika mapokeo ya Ukristo husemwa ni 'Jina kutukuzwa, Ufalme Kuja/Mapenzi kutimizwa Duniani'...

Yesu anarudi na yuko na watu wote wa 'U-JUA-ji uliobarikika'...

UKUU wa Yesu si 'Jina' bali 'Imani'--imani ya kufanyika sawa sawa na 'Mapenzi ya Mbingu/Kweli iliyositirika'...

Jina la Utukufu, ni esoteria ya 'NENO'--Siri za Mbingu na Nchi ni 'Maandiko'... Maandiko ni 'Alama zinazoitika Nia na Dhamiri' ya 'Mtu wa Ufahamu wa Mbingu na Nchi'.

Jina la kutukuzwa ni 'fumbo la imani' kwa 'uwezo wa kutawala na kuyashinda' yale yote yanayofanyika kwa kujiwazia mabovu ya kimfumo... Ufahamu Kristu ni Usahihi wa Kimfumo; msingi khasa wa ile 'Sala ya Bwana'...

Ni rahisi kudhani Yesu anapenda 'uchawa'--kwa kuwa tunaishi kwenye ulimwengu wa 'majaribu' na watu kudhamiria utu usiobora wa 'Ukuu wa Mambo ya Dunia'--kutafuta sifa, kupendwa na kuinuliwa...

Yesu ni Simba...

Yesu ni Utu unaodhamiria mwangaza kwa ajili ya Mashauri ya Kiroho, Maadili na Miiko.

Yesu si 'Mnyonge' kwa kuwa ufundi wa dini umefaragua 'umungu-mtu' wa Yesu ili kuitengeneza ile njia ionekanayo sahihi katika jicho la mwanadamu...

Yesu asingelipenda watu/wanadamu 'wamtukuze' na huku wanakosa umbonishaji sahihi wa 'uso' na 'vilindi vya maji ya Uzima'... Kwa kuwa kufanya hivyo ni kazi bure tu.

Yesu ni Shujaa... asingelipenda watu wawe wanyonge na hali uweza, nguvu na utukufu upo na sisi sote na wakati wote; tunapokuwa tumejisahau na basi kujiwazia utu usiyo na kheri tunahitaji dawa iliyo ni 'kukumbuka' na ili basi kukumbukwa katika 'Roho wa Mungu'...​

View: https://www.youtube.com/watch?v=u7agieAGDw0
 
Mfalme wa Tiro ametajwa kuwa alikuwa ndani ya Bustani ya Eden,

Lini Mfalme wa Tiro alianza kutawala?

Iweje awemo ndani ya Bustani ya Eden, afanye nini ?

Mfalme wa Tiro alikuwa mfalme wakati wa Nabii Daniel, lini aliingia Eden?

Ndipo sasa ujue,Kwa nje alikuwa mwanadamu, lakini ndani alikuwa Shetani mwenyewe.

Shetani / nyoka/ joka ndiye aliyekuwa Eden akamdanganya Eve kutomtii Mungu.

Wewe umeamua kumkataa Mungu na kugeukia Giza,

Wewe ni chumvi iliyoharibika, ni WA kutupwa jaani🤔
Napenda Sana tukuze mjadala na kufungua vichwa vyetu ila NIMESHANGAA SANA ndugu yangu kipenzi Rabbon kuwa Umeshindwa Kujua Kuwa hata Shetani unae sema alitajwa katika Ezekieli 28:13 Kuwa alikuwa Edeni na Utukufu uliotajwa hapo Umesahau wamba Shetani hakuwahi kuwa edeni akiwa na Utukufu huo?

Ni kwamba Umesahau au umezibwa na Utetezi wa Doctrine uliyofundishwa kuwa unataka na Unatamani iwe kweli?

Au fungu la ufunuo hukulisoma jinsi shetani alivyotupwa na al8vyofika mpaka Kudanganya??

Ufunuo wa Yohana 12:7-9
[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Unasahau hata Makerubi kwenye Bustani ya Edeni walianza kuwekwa Baada ya Adamu kufanya Dhambi na sio kabla ya Adamu kufanya dhambi..

Mwanzo 3:24
[24]Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Kwahyo Unataka kusema Kuwa Shetani alianguka baada ya Adamu na Eva kufanya dhambi??
Au kabla ya kufanya dhambi..

Shetani hakuwa na Utukufu uliotajwa kwenye Ezekiel 28:13 Ila alikuea na Hasira na Watu wa Mungu iliotajwa kwenye Ufunuo 12:12..

Ninataka Kuamini kuwa kuamini Doctrine ya Ezekiel 28:11-19 Kuwa mazungumzo ni Shetani utakuwa Umeteleza vinginevyo utanipa Wakati wa Kulufundisha Nini maana Ya Edeni kwa Lugha ya Kinabii...

Edeni inayozungumziwa hapo sio Edeni halisia ambayo wewe unadhani kuwa mfalme wa tiro alikuwa Edeni..
Kama nilivyokupa maana ya Key-rabiya au Cherubi nyingine ni Mtu mkamilifu au Mnyenyekevu..

Unashindwa Kuelewa kama Alikuwa Mfalme aliyepakwa mafuta alikuw Akiishi Kwa amani na Katika misinginya Furaha aliyoamuru Mungu??

Edeni maana Yake ni Sehemu kamilifu na Sehemu yenye Raha na Sehemu Hiyo inayotajwa ndiyo hasa Sehemu ambayo mfalme Anaishi kwa hyo kukaa kwenye Raha hizo kama mfalme kiburi chake kikainuka ...

Ni kama Nikisema Rais ramia kwa sasa anaishi Edeni simaanishi kwamba Samia Yupe Edeni na Adamu na Hawa..

Mkuu soma maandiko ukiwa hauko Pre-Indoctrine utaelewa maandiko mengi sana..

Nahisi hata Roho mtakatfu anashindwa kukuelekeza kwa sababu tayari unakuwa na Maana yako ya MaaNdiko unayo kichwani na akiluelekeza Unabisha huku ukiona wewe huko sahihi kuliko yeye Jaribu Kumruhusu roho mtakatifu akuelekeze Bila kuwa na PRE Doctrine..
 
Back
Top Bottom