NDIYO
Haya maneno yanafanana kabisa na habari za Yesu kutoka kwenye vitabu vya Injili.
Kiuono na Ufikirifu mifumo, fizikia na metafizikia ya UTU ndiyo jambo lenye asili ya mtu/mwanadamu/mwana-wa-adamu na mtu wa mbingu/
'Adamu mpya'...
Iwe ni Bhagavad Gita, ama Injili, maneno ya Yesu ama Krishna ni mambo ya Ufahamu Kristu/Ufahamu Krishna.
Kuna namna yake ya kufasili habari zake; labda kwa mtu asiye na uono na ufikirifu mifumo anaweza 'kupotea katika tafsiri'...
Krishna anamshawishi
Arjuna kuangamiza ndugu zake '
Makafiri' katika uwanja wa mapambano ya Kurukshetra katika nchi ya Mahabharata...
Watu wa Ufahamu-JUA huja kwa habari na mashauri ya UKUU...
UKUU wa Yesu si jina; UKUU wa Yesu ni 'SHAURI la uhai' kupitiliza Uzima wa Miili.
Katika lugha yetu ya Kiswahili, tayari kuna utundu ulishatayarishwa wa maana na mapelekeo ya maana kwa mashauri ya Ukuu...
Neno 'Jina' lina asili moja na neno U-Imajinishi; ambapo uimajinishi neno lenye viambishi 'maji', kiambishi 'jini'; na tena vyote hivi viwili vinasili ya 'jinesesia'.
Jinesesia, lawa neno rasmi la Kiswahili kwa tafsiri ya neno 'Genesis'; wafasiri wa mwanzo wa vitabu vya Biblia walionelea bora kutumia neno 'Mwanzo' badala ya neno jingine lenye asili ya kigeni.
Genesis, kutoka kwenye lugha ya Kiingereza, ni kitabu cha Kwanza cha Musa kinachosimulia 'Habari za Mwanzo' wa mambo--mwanzo wa mambo ya 'Mbingu' na 'Nchi'...
Katika karne hii ya 21 tunazungumza mambo ya 'Mwanzo' kama 'Ontolojia ya Taasisi'...
SASA, neno Genesis lina etimolojia ile ile na neno 'Genie'--Jini kwa Kiswahili.
Kiuono na Ufikirifu mifumo, muktadha akilifu wa utendaji usiofuatisha nguvu za kawaida za miili ndiyo huzaa
'maajabu ya ulimwengu' unaofanyika kutokea kusiko kitu.
Ndivyo basi simulizi la mwanzo kabisa la Kitabu cha Kwanza cha Musa husimulia habari za Ulimwengu uliofanyika kwa dhamira, shauri na uimajinishi wa 'Roho wa Mungu'....
Vitu vyote kufanyika kwa mfano wetu ni shauri la 'Uimajinishi'; kwenye mashauri yajayo kwa lugha ya Kiingereza hili lingalitajwa kama 'Imagination'.
Kiuono na ufikirifu mifumo, muktadha wa uimajinishi ndiyo unaofanya 'nafsi' yeyote 'kufanana na Mungu'--Uwezo, Nguvu na Utukufu wa 'Roho wa Mungu' ni funguo ya 'Ontolojia ya Taasisi' kwa sisi sote kama viumbe wenye Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu.
Yote kuwezekana katika 'Yeye' atutiaye uzima ni shauri la 'Nia ya Unafsi Moja' katika 'Roho wa Mungu'.
Yesu kunukuliwa kusema yeye ni Njia na Kweli na Uzima ni 'SHAURI la nguvu' katika 'Nia ya Unafsi Moja' katika 'Roho wa Mungu'.
'Nia ya Unafsi Moja' katika 'Roho wa Mungu' ndiyo khasa 'Ufahamu Kristu'...
Mimi na Baba ni Moja ni ushuhudiaji wa dhamiri ya Imani katika Uweza na Utukufu--'I' kwa lugha ya Kiingereza hukazia 'Utu Nafsi' na angali 'I' katika 'Imani' vile vile U-I-majinishi hukazia nia ya 'Utu wa Nguvu' katika 'Maji ya Uzima Wote'...
Kitabu Jinesesia, hutaja esoteria ya 'maji, uso na roho' halafu kisha 'maji ya Juu' na 'maji ya Chini'...
SASA, mtu kusoma habari za jinesesia halafu kuzichukulia kama ni 'Taarifa Fulani ya Habari' ni njia rahisi ya kujipotosha ama tuseme 'kujizima data'...
Dunia ni tufe, siyo bapa... Mbingu na Nchi ni mambo ya 'uso' na 'vilindi vya maji'--Ontolojia ya Taasisi. Kadiri mtu anapopanua fahamu zake za akili, utambuzi na fahamu kuna namna huyu ataanza kubaini vitu vyote ni 'alama zinazoishi'; alama hizi huitika dhamiri na mafikara ya kujiwazia utu ama tukizo la madhahiri...
Vitu vyote, ikiwemo maisha yetu na mambo yetu ni matokeo ya sisi wenyewe kujiwazia utu na matukizo ya madhahiri.
Kwa hivyo wakati mmoja, In Shaa Allah, tutaelekezana habari za 'KUSALI' kwa ajili ya 'kutenda miujiza'--si kwa 'imani pofu' na mapokeo yasiyo na msaada bali kuharakishia 'mema ya nchi'.
Kwa kuwa tunaishi ulimwengu uliofungamana makusudi, ikiwa watu watajifunza kusali katika vikundi kwa 'neema na saburi' mengi yataanza kubadilika na uponyaji wa mataifa utadhihiri.
Tunaishi kwenye ulimwengu mbovu wa 'Miundo ya Tawala/Ontolojia ya Taasisi'; tukifahamu kuuishi mwongozo bora wa U-JUA-ji wa Njia na Kweli na Uzima basi Tutaubadilisha Ulimwengu unaotuzunguka--jambo ambalo katika mapokeo ya Ukristo husemwa ni 'Jina kutukuzwa, Ufalme Kuja/Mapenzi kutimizwa Duniani'...
Yesu anarudi na yuko na watu wote wa 'U-JUA-ji uliobarikika'...
UKUU wa Yesu si 'Jina' bali 'Imani'--
imani ya kufanyika sawa sawa na 'Mapenzi ya Mbingu/Kweli iliyositirika'...
Jina la Utukufu, ni esoteria ya 'NENO'--Siri za Mbingu na Nchi ni 'Maandiko'... Maandiko ni 'Alama zinazoitika Nia na Dhamiri' ya 'Mtu wa Ufahamu wa Mbingu na Nchi'.
Jina la kutukuzwa ni 'fumbo la imani' kwa 'uwezo wa kutawala na kuyashinda' yale yote yanayofanyika kwa kujiwazia mabovu ya kimfumo...
Ufahamu Kristu ni Usahihi wa Kimfumo; msingi khasa wa ile 'Sala ya Bwana'...
Ni rahisi kudhani Yesu anapenda 'uchawa'--kwa kuwa tunaishi kwenye ulimwengu wa 'majaribu' na watu kudhamiria utu usiobora wa 'Ukuu wa Mambo ya Dunia'--kutafuta sifa, kupendwa na kuinuliwa...
Yesu ni Simba...
Yesu ni
Utu unaodhamiria mwangaza kwa ajili ya Mashauri ya Kiroho, Maadili na Miiko.
Yesu si 'Mnyonge' kwa kuwa ufundi wa dini umefaragua 'umungu-mtu' wa Yesu ili kuitengeneza ile njia ionekanayo sahihi katika jicho la mwanadamu...
Yesu asingelipenda watu/wanadamu 'wamtukuze' na huku wanakosa umbonishaji sahihi wa 'uso' na 'vilindi vya maji ya Uzima'... Kwa kuwa kufanya hivyo ni kazi bure tu.
Yesu ni Shujaa... asingelipenda watu wawe wanyonge na hali uweza, nguvu na utukufu upo na sisi sote na wakati wote; tunapokuwa tumejisahau na basi kujiwazia utu usiyo na kheri tunahitaji dawa iliyo ni 'kukumbuka' na ili basi kukumbukwa katika 'Roho wa Mungu'...