I have been scammed 1,100$ through Forex

I have been scammed 1,100$ through Forex

Eti tuma withdrawal fee ya $ 2 000 ? Si wakate huko huko wanipe $ 1 700?

Lingine...eti mtu a -trade kwa ajili yangu.

Anisaidie nipate faida kisha nikajichukulie pesa niliyosaidiwa na mtu fulani kuitafuta.

Jiulize kwanini yeye asitrade mwenyewe? Anauhakika hiyo faida yako anaweza kuimake sasa kwanini atafute kidogo kutoka kwako wakati akifanya mwenyewe anapata kingi?

Trade mwenyewe.

Yaani bora kubet kuliko utapeli huu wa wazi kabisa
 
Matatizo mengine tunayatafuta wenyewe. Yaani mtu anakuahidi profit ya 500% na wewe unakubali na kuingia kichwa kichwa! Tamaa nyingi, mbele kiza.
 
Pole sana ao wadada wapo wengiiii mnoooo.mi huwa wakini dm nawatongoza,kwanza siku akaniuliza unatokea nch gani nikamwambia tanzania akanambia anao wateja weng tz nikamtongoza mwisho nikamwambia sipo interest n biz yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi Ndugu zangu naandika hii ili kuwapa umakini Na haya mambo ya Forex mwanzo nilifanya Forex kupitia Templer FX nikapoteza Pesa nyingi Na BoT ilivyoingilia ikabidi niachane nayo, then kwenye Instragram nikaona program inaitwa BINOMO nikaidownload kwenye IOS nikaanza kutrade nikawa napata na kukosa inadepend na prediction unazoweka if the price will be up or down then kuna siku nikapata USD 200 kila nikajaribu kutoa inadelay then inabaki kwenye system nikavutiwa kuendelea ikaliwa yote.

Ikabidi niandike complain kwenye page yao ya Instagram maana tangu nimeanza nimepoteza like 500$ then nikaona kuna account imeniadd ya dada inatumia @kelseysabrina1 akanifuata DM akaniambia wana platform yao ambayo unainvest then they trade for you after 7 days unapata profit yako so ukiweka 200$ after 7days u get 2000$ akanishawishi nikajaa nikamtumia 200$ through bitcoins akaniunganisha kwenye platform yao inaitwa 360fxpool nikaona kwenye account yangu trading inaendelea after 7days ikawa 1400$ nikamuuliza mbona sio 2000$ kama tulivyoongea akasema kuna tatizo kwenye system baada ya muda ikabadilika ikawa 2975$ inclusive bonus kwasababu ni end of the year.

Then akaniambia kwenye policy ya kampuni yao imepitishwa withdrawal fee ya 205$ for that amount inabidi ilipiwe before withdrawal kwasababu other customers sio waaminifu wakitoa hawatoi commission nikatuma tena through bitcoins I see alivyopokea akaniblock kila kona nikajua nimepigwa.

Then nikaona jamaa kwenye Instagram Ad anaitwa @Branson_Rodgers akitangaza kufanya trading through bitcoins with nice profit but within 2 days nilivyoona ni ads nikamuamini nikawasiliana nae nikamueleza what happened akasikitika sana na kuniambia hutakiwi kutuma hela kabla hujapata profit yako nikaona huyu ni legit akaniambia initial capital ni 500$ within 2 days unapata 50% profit then unamtumia commision yake 20% nikacheck website anayotumia fxbitcointrade.com nikaona ni legit nikamtumia 500$ baada ya kutuma akaniambia pending withdrawal yangu inaonyesha itakuwa 2,000$ kwahiyo ili aweze kutrade inabidi niongeze 200$.

Ikabidi niongeze katrade 1st day ikawa 854$ 2nd day ikafika 1,400$ 3rd day ikafika 2,550$ kimbembe kikafika wakati wakutoa jamaa anasema nitume 300$ withdrawal fee nikaona ndio yaleyale nikajua nishapigwa tena ikawa ishafika 1,100$ nikajua ni kutokana na kutotoa fungu la kumi nikapiga moyo konde na kuanza moja kuweni makini jamani hakuna easy money wala hakuna mtu atakufanyia trade au kukusaidie upate hela huyu jamaa bado yuko Instagram na anaweka ads angalia msiibiwe jamani.

View attachment 1310298

View attachment 1310301

View attachment 1310302

View attachment 1310303

View attachment 1310304

View attachment 1310305

View attachment 1310306
Wewe NI fala
 
Huo sio uwekezaji mdogo pikipikii 5 kwa m2 sawa na m10 bahaji 5 bajaji moja ni m7 ..bado mgahawa bado saloon.hahaha eti uwekezaji mdogo Nani kasemaaa
1100$ ni kama 2.5 milion ungeweza kuanzisha hata mgahawa wako mdogo amboa ungepata 20000 kama faida kwa siku

Kwa mwaka ungeweza kutengeneza milion 7.2

Vijana tubuni miradi pesa haiji hivi hivi.

Mimi uwa nawekeza kwenye vitu vidago vidogo na napiga pesa kweli nahakikisha hata kama niko kwenye majukumu mengine miradi inajiendesha yenyewe kwa simu.

Ukiwa na mighawa 5, saloon za kiume 5 pikipiki 5 na bajaji 5 kwa siku unatengeneza pesa kama laki3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti tuma withdrawal fee ya $ 2 000 ? Si wakate huko huko wanipe $ 1 700?

Lingine...eti mtu a -trade kwa ajili yangu.

Anisaidie nipate faida kisha nikajichukulie pesa niliyosaidiwa na mtu fulani kuitafuta.

Jiulize kwanini yeye asitrade mwenyewe? Anauhakika hiyo faida yako anaweza kuimake sasa kwanini atafute kidogo kutoka kwako wakati akifanya mwenyewe anapata kingi?

Trade mwenyewe.
Hii haina tofauti na jamaa Fulani wakenya unafungua akaunt sport pesa, kisha, unaweka salio kisha unawapa wao password na pia unawalipa hela ya kukusaidia kucheza, inaitwa Account Management.

Yaani wao kama ni wataalamu zaidi si wajielekeze kwenye kucheza account zao wenyewe badala ya kucheza za wengine??
 
Mpumbavu wa karne huyu. Wewe hujui chochote kuhusu forex na wala ulikuwa hutrade forex bali ulikuwa unacheza mchezo wa upatu.

Yani mfano ingekuwa kwenye kubet, wewe ni sawa na mtu ambaye hajawahi kubet na wala hana idea ya how watu wanabet. Basi utafute mtu akufungulie akaunti na akubetie, then huyo mtu achukue mpunga wako ulowekeza akimbie nao, halafu baada ya hapo uje hapa jf uenze kulaumu eti betting is a scam.

Hapo tatizo sio forex, ni wewe kutokuwa na knowledge ya jinsi forex inavyoendeshwa.

Shubamitt kenge miti[emoji78][emoji82]

Unforgetable
 
Back
Top Bottom