FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #41
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO........
“Ni siku ambayo siwezi kuisahau kwenye yaisha yangu, ni siku iliyo nifanya nikakosa kuwa na familia, ni siku ambayo haikunifanya nikawa na uhakika wa kusimama mbele ya wanawake nikajisifia urijali wangu, wanadamu ni wabaya sana yule mtu alizikata sehemu zangu za siri. Nililia sana ile siku, sehemu za siri kwa mwanaume ni zaidi ya utajiri wowote ule unao ujua wewe hapa duniani, hakuna mwanaume aliyekikosa hicho kiungo akasimama kwa ujasiri na kujisifia mbele za watu kwa sababu anaweza kuishia kwenye michezo mibaya sana, sikuamini nikiwa kwenye kilio kikali niliona amezishika sehemu zangu hizo za siri akazitupa mbali na hapo sikuweza kuelewa kilicho endelea tena” stori ya mzee huyu akiwa anatoa machozi ilimsisimua sana Jamal alikuwa amefumba macho kwa hisia mpaka nayeye chozi lilimtoka, alimfikiria mwanaume huyo amewezaje kuishi akiwa kwenye hali hiyo, kwenye hii dunia yenye masimango makubwa sana ukiwa na matatizo kama haya, alimuonea huruma sana huyo mbele yake kwake alikuwa ni kama baba lakini pia kwa nchi alikuwa ni jasusi hatari mno ila hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba huyo mtu hana hicho kitu.
ENDELEA...........................
“Niko wapi hapa” lilikuwa ni swali langu la kwanza tu baada ya kushtuka kutoka kwenye usingizi wa kifo, macho yangu yalikuwa bado yana ukungu kiasi chake kwa mbali nilikuwa namuona mtu mmoja ambaye alikuwa amenipa mgongo, suti kubwa mwilini mwake ndicho nilicho fanikiwa kukiona kwa wakati ule. Mkono wangu mmoja na sehemu ya bega ulikuwa imejaa bandeji kiasi kwamba hata nyama za mkono zilikuwa hazionekani kabisa, sikuwa nakumbuka chochote nilishangaa nikiwa kwenye hiyo hali, macho yangu niliyageuza pembeni ndipo nilipo ziona mashine kubwa zikiwa zinaonyesha mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kwa utaratibu mzuri kama ilivyokuwa inatakiwa, mikononi kulikuwa na drip mbili ambazo zilinifanya kugundua kwamba nilikuwa mgonjwa na hapo huenda ilikuwa ni hospitalini. Nilitaka kuinuka niliuma meno kwa maumivu makali ya tumbo hiyo sehemu kilikuwa kimezamishwa kisu nadhani bado palihitaji muda wa kutosha ili kuweza kupona na kuwa kwenye hali ya usawa kabisa kama ilivyokuwa mwanzo.
Mguu ulikuwa umepigwa plasta maeneo ya paja ulikuwa hauna nguvu kabisa, nilitulia kidogo ndipo nilipoanza kuvuta kumbu kumbu ya nyuma juu ya matukio yaliyokuwa yamepita ili nielewe kivipi nimeweza kufika ile sehemu nikiwa hata sijitambui kabisa. Nilitoa machozi mengi sana baada ya kukumbuka mpaka muda huo sikuwa na sehemu zangu za siri, nilitamani sana ningeachwa nife pale pale na sio kusaidiwa nikiwa kwenye hali kama hii iliniuma mno, nilikuwa bado hata familia sina kabisa ila ndio hivyo maisha yangu mapema sana yalikuwa yamesha haribika kwa siku moja tu nikiwa kijana mdogo wa miaka ishirini pekee.
“Kwanini umenisaidia kuja kuteseka kwenye huu ulimwengu” mpaka muda huo bado mtu huyo alikuwa amenipa mgongo hivyo sikuweza kujua kabisa kama alikuwa ni nani yupo humo ndani japokuwa nilihisi tu kwamba ni lazima yeye ndiye aliyeweza kunisaidia kwani hakukuwa na mtu mwingine yeyote.
“Hongera sana kwa kuweza kurudi kwenye maisha mengine mr Timotheo Jordan” nilishtuka baada ya kuona mtu huyo alikuwa akinijua kwa usahihi sana, aligeuka kutazama nilipokuwa nilitamani sana ningesimama lakini sikuwa na huo uwezo kabisa, mwanaume huyo ndiye mtu aliyekuwa amesababisha mimi kuwa kwenye hiyo hali Jonson Malisaba ndiye mwanaume aliyekuwa mbele ya macho yangu nilikuwa kwenye ndoto na nilipaswa niamke sasa ndivyo akili yangu ilivyoweza kunidanganya kabisa kwa mara ya kwanza lakini hii haikuwa ndoto kila nilichokuwa nakiona mbele yangu kilikuwa cha kweli kabisa huyo ni mtu ambaye nilihitaji sana kukutana naye tuweze kuongea kwa mapana na marefu leo alikuwa yupo mbele yangu nikiwa kwenye hali ya majuto makubwa sana kwenye maisha yangu.
“Huyu mtu aliye nitendea haya yuko wapi kwa sasa?” niliuliza kwa hasira ni dhahiri nilitamani sana kumuona huyo mwanaume ila hata angekuja kiuhalisia kwa hali niliyokuwa nayo nisingeweza kusimama naye hata kidogo hasira hasara ndicho kilichokuwa kikiniendesha kwa wakati ule.
“Mshukuru sana MUNGU wako umeweza kuamka na kuiona siku nyingine, ni siku saba sasa tangu umelala kwenye hicho kitanda, ukipona utachukua vitambulisho vyako kwenye kabati lililopo pembeni yako hapo na usije ukarudi tena kufanya hicho ulichokuwa unajaribu kukifanya ni hatari sana kwako” alinishangaza maneno yake machache alitaka kuondoka baada ya kumaliza maelezo yake alianza kuondoka mle ndani.
“Ina maana umesha nijua mimi ni nani?”
“Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikusaidie baada ya kukujua kwamba wewe ni mtu wa serikali”
“Wewe ni nani hasa mpaka uweze kunisaidia mimi mtu wa serikali ambaye ulikuwa na mpango wa kuniua na umenifanyia ukatili mkubwa kama huu kwenye maisha yangu?” aligeuka na kutabasamu baada ya kulisikia swali langu
“Dunia imebadilika sana, wanadamu siku hizi ni wajuaji kupitiliza yaani wanaweza kutengeneza stori kukuhusu wewe na watu wa huko nje wakaamini kwamba ni kweli wewe kweli ndivyo ulivyo, mimi nawewe ni watu sawa ila tumepishana tu namna ya ufanyaji wa kazi ndiyo maana wewe uliamua kuhisi unanijua sana ndiyo sababu ukapata mpaka ujasiri wa kunifuata majira yale ya usiku pale kichwani mwako ukiwa tayari una jibu lako kuhusu mimi kitu ambacho sio cha kweli kabisa” maelezo yake kiukweli yaliniacha njiapanda nilidhani labda ni kwa sababu sikuwa na elimu lakini alikuwa mtu wa kutumia akili kubwa sana kwenye kila neno lake ambalo alikuwa analitoa mdomoni mwake.
“Wewe ni nani hasa mpaka useme mimi nawewe ni watu sawa?” nilikuwa na hamu sana ya kuweza kumjua huyu mtu, alijongea taratibu akatoa kitu mfano wa mashine ndogo sana ambayo ni mojawapo ya mashine ambazo huwa zinatumika kukagulia watu kwenye mageti ya sehemu maalumu hasa Ikulu au sehemu kubwa sana za serikali, kwanza nilishangaa kitu kama hicho kakitoa watu, mle ndani ghafla kiza kilitawala zilibaki tu mashine ambazo ndizo zilikuwa zipo pale kuhakikisha maisha yangu yanasalimika kutoka kwenye kifo.
“Mehesh Prakash ndilo jina langu, sijazaliwa India ila maisha yangu nikiwa mdogo nimelelewa na mhindi mmoja ambaye alikuwa mfanya biashara mkubwa sana hapa nchini na ndiye aliyeweza kunipatia hilo jina, Jonson Malisaba ndilo jina langu la kuzaliwa, kwa sababu yule mhindi alinilea kama mwanae baada ya kunichukua kwenye kituo kimoja cha watoto yatima aliweza kunipenda kama mwanae wa kumzaa hivyo alinipa kila kitu nilicho kihitaji kwake nilikuwa mwanae kabisa hivyo namimi nilimzoea kama baba yangu, nilisoma kwenye shule nzuri sana na kufanikiwa kumaliza masomo yangu, nilikuwa nimekuwa kijana wa kujielewa ndipo yule mzee alipoweza kutoweka duniani, kwa sababu kila kitu alinirithisha mimi utajiri wake wote ulikuwa upo mikononi mwangu. Nilikuwa mtu mwenye pesa nyingi nikiwa bado kijana mdogo tu hivyo kuna mtu mmoja kutoka kwenye idara nyeti ya serikali alinifuata na kuniomba nitumie baadhi ya mali zilizopo kuisaidia serikali, kwa sababu ilikuwa ni nia ya kuisaidia nchi yangu mwenyewe nilikubali kuufuata ushauri wake kwa asilimia zote miamoja.
Ilifika siku akawa amenikalisha chini ndipo aliponipa hadithi kamili ya umoja ambao unaitwa M96 OWNER’Z, aliniomba niingie kwenye huo umoja kama moja ya wawekezaji ili nikajue unahusiana na nini hasa kwa sababu walikuwa wamesha utilia shaka mapema. Lilikuwa suala ambalo halikuhitaji mimi kukurupuka sana kulianza lakini nilitolewa wasi wasi baada ya kuweza kukutanishwa na mheshimiwa raisi ambapo yeye kwa mdomo wake aliniomba nifanye hivyo. sikuzubaa tena nilikubali moja kwa moja ilikuwa ni heshima kubwa sana kuweza kuombwa na mheshimiwa raisi. Huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuingia kwenye huo umoja nikiwa bado kijana, watu wale pesa zangu ziliwashawishi sana kuweza kunikubalia haraka kwa mara ya kwanza nilitamani sana kuweza kujua kilichokuwa kinaendelea kwenye kampuni ile iliyokuwa ikijihusisha na usindikaji wa nyama. Pesa nyingi nilizowekeza pale zilinifanya kuwa na nafasi kubwa, kuna siku nikiwa nipo nyumbani baada ya kutoka kwenye kazi zangu walikuja wanaume kumi na mtu mmoja ambaye mpaka leo sijawahi kufanikiwa kumuona sura yake wala kumjua baada ya yeye kufika tu umeme ulizima kila sehemu kwenye ule mtaa hivyo tuliongelea gizani nadhani huyo ndiye kiongozi mkuu wa huu umoja, ni mtu makini, hatari, analindwa kuliko hata ikulu panavyo lindwa, ana watu makini sana kiasi kwamba hata nzi hawezi kuigusa hata kola ya shati lake.
Jadesh Mikasa ndilo jina ambalo aliweza kunitajia kama ni la kwake japo kwenye kufuatilia kote hatukuwahi kulikuta hilo jina kwenye data zozote zile hapa duniani hivyo nilijua huenda ni mtu ambaye utambulisho wake haujulikani kabisa. Kwa mara ya kwanza alinipa mambo machache sana ambayo yanafanyika mle ndani kwa sababu tayari nilikuwa miongoni mwa wawekezeji wakubwa kwenye ile kampuni, mambo niliyokuwa nasimuliwa yalikuwa yanatisha mno ila nilipewa onyo kali sana licha ya kuificha familia yangu mbali watu wale walikuwa na taarifa zangu zote mpaka familia yangu ilipo, ni watu makini kupita kiasi hawafanyi kosa lolote lile kwenye mambo yao ambayo wanayafanya, sikuwa na namna ilinibidi nikubaliane na matakwa yao na kuwaaminisha hilo walianza kunipa mitihani ambayo kuna muda ilinilazimu kumwaga damu zisizokuwa na hatia yoyote ile, ni kazi ambayo nilikuwa nimekabidhiwa na nchi hivyo ilitakiwa niifanye kwa asilimia miamoja. Imani ndicho kitu pekee ambacho kitafanya wanadamu waweze kukupatia kila kitu kwenye maisha yako kama mtu hawezi kukuamini basi hakuna kitu utaweza kuambulia ndio maana waanadamu tunakumbushwa sana kuwa waaminifu kwenye kila jambo tunalo lifanya hasa pale unapokuwa mbele ya watu wanao kuamini sana. ndicho kitu nilichoweza kukifanya ilinibidi kwanza nifanye waniamini ndio maana nilikuwa tayari kufanya kila kitu ambacho wao walihitaji nikifanye ili waniamini” maelezo yake yalinifanya jasho linitoke sikuwahi kufikiria kama huyo mtu alikuwa ni mtu wa serikali na alikuwa pale kutekeleza majukumu ya kitaifa ila nilitatizwa na kitu kimoja ambacho mpaka muda huo sikukielewa kwa mtu huyo. Nilihema kwa nguvu mpaka hasira zangu zote zilikuwa zimeisha kabisa kwa mwanadamu aliyekuwa yupo mbele yangu kitu alichokuwa anakifanya ndicho ambacho hata mimi nilikuwa nakihangaikia kila siku kwa muda huo na ndicho kilinifanya kuwa kitandani kwa wakati huo.
“Sasa kama wewe ni mtu wa serikali kwanini watu wa usalama wakutafute sana namna hiyo na jina lako kule linaonyesha wazi wewe ndiye mtu unaye tafutwa zaidi?” nadhani swali langu lilikuwa mhimu sana kwa wakati ule hata kama ungekuwa ni wewe lazima ungemuuliza iweje mtu wa serikali atafutwe na serikali? Ilikuwa lazima anipe maelekezo ya kutosha kuhusu hilo.
“Serikalini najulikana kwa watu wachache sana hata mkurugenzi wa usalama wa taifa hanijui na ndiyo sababu unaona watu wa usalama wa taifa wananiandama, hata wewe nimekusaidia baada ya kujua unatoka ndani ya idara ya usalama wa taifa” alinieleza kwa kifupi bila wasi wasi
“Kama haupo chini ya idara ya usalama wa taifa sasa unafanya kazi chini ya nani?” swali langu lilimfanya atabasamu sana
“Inakubidi uwe na mdomo mfupi sana kwa maana ukijaribu kuurefusha unaweza kuwa miongoni mwa vijana watakao ingia kwenye historia mbaya ya kuweza kufa mapema wakiwa bado hawajatimiza kabisa malengo yao” aliweka kituo kidogo baada ya kuona siongei chochote aliendelea tena.
“Nafanya kazi na watu wawili, mkuu wa majeshi pamoja na mheshimiwa raisi” maelezo yake yalinishtua sana watu alio wataja walikuwa watu wakubwa mno hapa nchini, nilijikuta naanza kumuogopa mtu huyo baada ya kugundua inawezekana kuna mambo mengi sana ambayo siyajui bado kuhusu yeye
“Kwenye hiyo kazi wewe unasimama kama nani?” nilimuuliza nikiwa natokwa na jasho pale kitandani
“Mimi ni mtoa taarifa za mhimu zaidi ambazo zitaweza kuisaidia nchi kuhusu huu umoja ambao unaonekana ni hatari sana kwa maisha ya baadae”
“Kama walisha ujua kwanini wasiwakamate tu mambo yote yaishe?” niliuliza swali ambalo mimi mwenyewe baadae nililiona kuwa la kijinga sana kwani kama wangekuwa na huo uwezo wa kuwakamata kirahisi wangekuwa wameshafanya hivyo.
“Kwanini wewe umeshindwa kunikamata?” aliniuliza swali ambalo lilinipa mwanga juu ya uhatari wa hilo kundi kama huyu analindwa hivi huyo kiongozi wao itakuaje.
“Na huyo kiongozi wenu uliye mwita Jadesh alikwambia siri gani alipokuja kwako ambayo umesema ilikufanya mpaka uogope sana?” alibadilisha kidogo sura baada ya kumuuliza hilo swali.
“Ukiwa kama mwanaume jifunze namna ya kukitumia kifua chako kwa usahihi vinginevyo kitakuponza, upana wa kifua chako ndio usalama wa maisha yako ukihisi unayajua sana mambo hautafika hata kesho ukiwa bado unahema, ukitoka hapa nitafute kwa hiyo namba 911, hiyo ni namba ya polisi ukipiga we ongea nao kwa kuzuga zuga mpaka mmalize kuongea usitoke hewani hata ikikatwa baada ya dakika tano simu itaita kupitia namba hiyo hiyo ipokee utaongea namimi, tumia simu ya mezani na hakikisha hakuna anaye lijua hili” baada ya kumaliza maelezo yake kwa usahihi aliiweka kola ya shati yake vizuri iliyokuwa ndani ya suti, kiza kilichokuwa humo ndani kilinifanya nisimuone ila hatua za viatu zilinipa taarifa mwanaume huyo alikuwa anatoka humo ndani, dakika mbili baadae umeme uliwaka kama kawaida mle ndani.
Mimi mwenyewe sielewi elewi kinacho endelea kwenye hii hadithi akili yako ndiyo mafanikio yako ya haraka kuielewa.
Niseme tu 26 sina nyongeza tena nadondosha kalamu chini
Bux the story teller
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA.......
Baada ya kumaliza maelezo yake kwa usahihi aliiweka kola ya shati yake vizuri iliyokuwa ndani ya suti, kiza kilichokuwa humo ndani kilinifanya nisimuone ila hatua za viatu zilinipa taarifa mwanaume huyo alikuwa anatoka humo ndani, dakika mbili baadae umeme uliwaka kama kawaida mle ndani.
ENDELEA..................
“Kitu gani kinakufanya mpaka umekuwa mtu wa kuishi kwa kujificha sana namna hii kijana kama wewe” swali la kwanza kabisa kutoka kwa Alexander lilimfanya Ashrafu atabasamu akiwa na glassi yake mkononi anasafisha koo wasi wasi haikuwa sehemu ya maisha yake kijana huyu.
“Dunia hii wanaishi watu mbali mbali na wenye sifa tofauti tofauti, kuishi kwenye huu ulimwengu unatakiwa uwe kama kivuli mbele za nyuso za watu ili upate vitu unavyo vihitaji wewe ila ukiruhusu kila mtu akakujua kwa undani basi sahau kuhusu kila kitu kwenye maisha yako hakuna nafasi utaipata mbele ya dunia ukaweza kutekeleza yale ambayo ulikuwa unataka kuyatimiza kiurahisi. Ninaishi nitakavyo, ninaweza kupata kitu chochote kwa muda wowote ule bila usumbufu wowote ule, sina uhakika sana ila ni miongoni mwa watu wenye usalama mkubwa sana ndani ya mipaka ya nchi hii, maliza maswali yako yote kuniuliza ili nikianza yakwangu usije ukaujutia ulimi wako” kijana mstaarabu kwa mwonekano ila mambo yake yalikuwa ya kutisha mno ndiye aliyekuwa anamwambia Alexander maneno ya kijasiri haya, alijiamini mno Ashrafu Hamad
“Hahahaahahahaahhaahahahah vijana wa siku hizi mnakua vibaya sana labda huenda mmezaliwa nje ya ndoa au kwa sababu mmelelewa na ulimwengu badala ya wazazi wenu ndio maana mnajihisi mnaweza kuropoka chochote kile ambacho kinakuja kwenye vichwa vyenu, yaani kijana kama wewe ndo unaniambia mimi nitaujutia ulimi wangu, hahahahaahahahhahhhhahh……….” Alexander aliona kama kijana huyo hakuwa siriasi kwa alichokuwa anakiongea kwenye mdomo wake haikuwa sawa mtu kama yeye kuweza kutishwa na kijana kama huyo kwake kilikuwa kama kichekesho nadhani hawakuwahi kumfahamu kiundani sana mwanaume huyo lakini alikatishwa kwa ukali na Ashrafu.
“Umemaliza maswali yako” sauti ya ukali wakati huo glasi ilivunjwa kwa mkono ndiyo iliyo mshtua Alexander kwenye kicheko ambacho hakikuwa cha furaha muda wote alikuwa anazipiga hesabu zake kwa usahihi anaweza kutoka vipi kwenye kundi kubwa la watu walio mzunguka mahali hapo wakiwa na silaha.
“ok, nambie wewe ni nani hasa na huyo baba yako ni nani serikalini?” swali la Alexander lilimshtua sana Ashrafu, maisha yake yaliwekwa ya siri kubwa mno hakuna mtu wa nje aliyekuwa anajua kwamba huyo kijana ni mtoto wa mtu kutoka upande wa serikali, hiyo taarifa haikuwa njema kwake hata kidogo japo hakuonyesha mshtuko wa moja kwa moja.
“Hili jambo mnalijua wangapi?” hakuwa na namna ya kupepesa macho kwa namna yoyote ile alijua anajulikana vilivyo na huyo mtu japo kuhusu baba yake ndiye mwanaume huyo alihitaji kumjua kwa usahihi.
“Unapo amua kucheza michezo ya hatari namna hii unatakiwa kuelewa kwamba kuna watu ambao walisha icheza michezo kama hiyo wamekaa pembeni wanakuangalia tu unacho kifanya sasa nao wanapo amua kurudi tena mchezoni inaweza kuwa hatari kubwa sana upande wako,ni vyema ukaitumia nafasi yako kukaa nje na haya mambo ukayaishi maisha yako tu japo umesha chelewa kwani mpaka sasa mafaili yako yapo kwenye mikono ya watu hatari sana na hauwezi kuikwepa hiyo mikono ikiwepo mkono wangu mimi mwenyewe iliniuma sana siku ile napigwa na risasi na kijana wa kawaida kama wewe, nimekutafuta mno kwa miaka kadhaa iliyoweza kupita mpaka nilipo kuja kujua kwamba siku ile ulikuwa kwenye ile hoteli, umekaa na kuwatoa sadaka vijana wa watu wasiokuwa na hatia yoyote ile ili wewe uwe salama nadhani leo utanipa majibu sahihi” Alexander alikuwa akijiamini mno kiasi kwamba aliwashangaza mpaka wao waliokuwa humo ndani ya nyumba hiyo, alijongea bila wasi wasi kabisa akasogea mahali lilipokuwa friji aliitoa moja ya wine iliyokuwepo humo ndani akachukua glass mbili na kwenda nazo mezani, watu wote walikuwa wakimshangaa tu licha ya wanaume wote kuwa na silaha kali haikuwa sababu ya kumfanya awe na wasi wasi. Hayo ni maisha ya viumbe vya kutisha duniani, wanaweza kukifanya chochote kile mahali popote pale na kuondoka bila kuwa na wasi wasi wowote ule, Alexander alimpa ishara Ashrafu akae chini ndipo waongee alionekana kuwa na mazungumzo ya muda mrefu kidogo.
“Tangu nianze kuyaishi haya maisha yangu ya hivi nimekuwa binadamu wa kutisha sana kwenye maisha ya wanadamu wa kawaida, naogopwa mno mtaani, kuna watu hawatamani hata kidogo kukutana namimi kwenye maisha yao lakini wewe unakuja hapa kwenye himaya yangu licha ya kuona aina ya umakini wa watu waliopo hapa ambapo kwa akili ya kawaida tu huna uhakika kama utatoka na nafsi yako ikiwa salama umekuwa mtu wa kujiamini kupita kiasi ni mbaya sana kwa maisha ya mtu kama wewe ambaye kwa sasa ulitakiwa uwe umeoa na una mkeo mnalea watoto wenu na sio kuwafuatilia watu kama mimi japokuwa kwa wewe ilikuwa ni lazima tu kwamba ningekutafuta hata usingekuja siku ya leo” Ashrafu alikuwa amekaa kwenye sofa hapo chini kila mtu akiwa na glasi yake mkononi ya wine wanashushia taratibu, kama ingekuwa ndio mara yako ya kwanza kuwaona watu hawa lazima ungedhani kwamba walikuwa ni watu wenye ukaribu wa hali ya juu kama sio marafiki wakubwa ila hilo halikuwa na ukweli wowote, hao wote wawili walikuwa ni watu ambao walikuwa wanatafutana isivyo kawaida, imani juu ya uwezo wao ndivyo vilivyofanya wakae chini kwanza weweze kuulizana maswali ambayo yangewafaa kwa alfajiri hiyo.
“Mhhhhhhhhhh ni mwanadamu wa aina gani wewe ambaye unaweza kumtisha mwanaume aliyeweza kuingia ndani ya ikulu ambayo ndiyo sehemu inayo lindwa zaidi ndani ya nchi, kuna kila aina ya watu hatari kule, kunalindwa mpaka na mitambo maalumu ya mionzi hata hivyo nilifanikiwa kumuua raisi na kutoweka bila kukamatwa wala kugundulika na binadamu yeyote mpaka leo, vipi naweza nikakuogopa kijana kama wewe ambaye hata uhakika wa maisha yako huna unaishi kwa kujificha ficha tu ukiogopa kwamba huenda maisha yako yakachukuliwa muda wowote ule. Hapa nitaondoka ila sio kwa wewe kuniambia niondoke, nitaondoka kwa kujisikia mwenyewe nitakapo ona nimekipata nilicho kifuata” Tabasanu hafifu ndiyo ilikuwa sehemu ya kuhitimisha maelezo ya Alexander,ni kitu ambacho kilikuwa ni cha kutisha sana, leo Ashrafu alikuwa anaambiwa kwamba mtu ambaye alikuwa naye mbele yake ndiye aliyekuwa amemuua mheshimiwa raisi aliyeweza kupita kwenye madaraka, kumbu kumbu zake zilienda miaka kadhaa nyuma ilikuwa ni kweli kuna raisi alifia madarakani ghafla sana kifo chake kikiwa ni siri kubwa ambayo haikuruhusiwa kutoka nje ya ikulu kwamba chanzo chake ni nini, hakujiuliza mara mbili alihisi huyo mtu anaweza kuondoka na maisha yake humo ndani kizembe sana kama asipo jihami.
Kuingia na kutoka ikulu ukiwa salama tena umefanya mauaji ya mheshimiwa raisi hakikuwa kitu chepesi, kilihitaji binadamu mwenye roho ngumu sana kuweza kufanya hivyo, mguu wake mmoja uliipiga chupa ya wine ambayo ilikuwa mezani, chupa hiyo ilikuwa inaelekea upande wa pili mwa meza hiyo haikuleta madhara yoyote ile baada ya kupokelewa kwa ngumi nzito na kupasukia hewani wine ikasambaa mithili ya maji, risasi mbili zilikuwa zimefyatuliwa kwa spidi kutoka kwenye bastola ambayo ilikuwa ipo kwenye mikono ya Ashrafu, meza ya kioo ilipigwa na teke ambayo ndiyo iliyotumika kuzuia risasi hizo mbili, ni umbali mdogo sana walikuwa wamekaa hao watu ila tukio lililokuwa linatendekea hapo lilikuwa linaleta burudani sana machoni mwa walinzi waliokuwa wako pembeni. Alexander alikuwa amejirushia nyuma ya sofa moja na kuligeuza kwa wepesi, risasi zaidi ya sita ziliishia kunyofoa nyofoa nyama ya sofa hilo kutoka kwenye bastola ya Ashrafu.
Zilipigwa hapo zaidi risasi hamsini kutoka kwa walinzi waliokuwa na silaha za kutisha kwenye mikono yao ikiwa ni kama hatua ya kuweza kumuweka bosi wao kuwa salama, hakutakiwa kuwa hata na kidonda huyo mtu hakuna mlinzi angeweza kutoka salama akiwa hai, sofa lilikuwa limenyofoka nyofoka halikutamanika tena.
“Noooooo stop, he is mine(huyu ni wa kwangu) nahitaji afie kwenye mikono yangu kama hataweza kunijibu maswali yangu”, kitu cha kushangaza Alexander alitokea nyuma ya kabati akiwa hana hata wasi wasi baada ya kusikia kelele za Ashrafu kumhitaji waonyeshane uwezo wao hiyo ndiyo ilikuwa robo tatu ya maisha yake aliipenda michezo ya ngumi kuliko hata alivyo yapenda maisha yake, hawakuelewa kutoka kwenye lile sofa ni muda gani ameutumia kufika kwenye hilo kabati hiyo ndiyo sababu alisema yeye sio mtu wa kawaida walijisumbua tu kupiga risasi zao hapo alikuwa ameondoka muda mrefu sana.
Ashrafu hakuhitaji mtu yeyote aweze kuingilia hilo alihitaji kwa mkono wake kumfanya mwanaume huyo amjibu maswali yake kwa lazima kama sio kumuua, walinzi walisogea nyuma uwanja mkubwa ulikuwa umeachwa kwa sababu ya wanaume hawa wawili. Nguo ya kulalia aliyokuwa ameivaa Ashrafu ilikuwa inakuja usawa wa macho ya Alexander aliipangua kwa nguvu alikutanishwa na teke maeneo ya shingoni alikuwa anaenda kujibamiza ukutani miguu ilitumika kudunda kwenye huo ukuta akatua chini akiwa safi, traki safi ilikuwa mwilini mwa Ashrafu kifua kilichokuwa kimegawanyika kilikuwa kipo wazi kabisa.
Spidi ambazo zilikuwa zinakuja kwa nguvu ya upepo zilitumika ndani ya sekunde chache sana Alexander kuweza kufika sehemu ambayo alikuwepo ashrafu, mwili wa Alexander ulizungushwa kama tairi lililokuwa kwenye mwendo mkali alijigeuzia kwenye mbavu za Ashrafu ambaye alirudi nyuma baada ya mikono iliyo komaa kuzigusa mbavu zake kwa nguvu alikuwa anadondokea kwenye moja ya sofa, mkono wake mmoja aliegamia kwenye pembe ya sofa hilo akajigeuza ila kabla hajakamilisha hilo goti lilikuwa limefika kwenye tumbo lake, Alexander alikuwa anakuja kwa nguvu sana, goti hilo lilimpeleka ukutani sehemu ambapo palikuwa na ala ya upanga ulio onekana kuwa wa muda mrefu kidogo ukiwa upo hapo, mguu uligusa sehemu kilipokuwa kitufe cha kuutolea upanga huo ulidakwa kwa usahihi kwenye mkono wa kulia wa Ashrafu, Alexander alikuwa amefika lakini alirudi nyuma kidogo baada kuzigusa alama za damu kwenye tumbo lake. Alikuwa amekatwa na kijana huyo Ashrafu Hamad ambaye alikuwa mbele yake, alitabasamu uzembe wa sekunde kadhaa tu ulikuwa umefanya ajisahau sana mpaka mpinzani wake akapata sehemu ya kuzigusa sehemu za mwili wake.
“Sasa nahitaji unijibu vizuri, kile mlicho kifuata siku ile ndani ya jiji la mwanza mlikipeleka wapi na kichwa cha yule mzee kipo wapi mpaka sasa?” upanga wake ukiwa na alama za damu alimuuliza mwanaume ambaye alisemekana kuingia ikulu na kumuua mheshimiwa raisi kisha akafanikiwa kutoroka bila kukamatwa na mtu yeyote yule, huyo ndiye Alexander mwenyewe.
“Leo kama utapona siku nyingine unatakiwa ukiniona unikimbie nadhani kwa hiki kinacho enda kutokea hapa leo hata baba yako atajitokeza hadharani akiwalilia watu kwa kitu unacho enda kufanyiwa ni bora ungeendelea kujificha tu, dakika tano ukifanikiwa kuzimaliza sitakuwa na swali la kukuuliza kuhusu maisha yako nitakuacha uende ila kama zitakushinda basi taarifa ya habari ya leo inaenda kuzitangaza habari za kifo chako mtu ambaye kile mtu anajua ulishakufa” kauli ya Alexander ilifuatiwa na uchomolewaji wa visu viwili kwenye kiuno chake.
Atapona nani ataishi nani? tukutane wakati ujao 27 sina la ziada tena
Bux the story teller