STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
TULIPO ISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SABA........
Aliye anzisha ni yule komando ambaye alikuwa nyuma ya kiongozi wake alipiga makelele sana alilalamila kwa maumivu makali ya sikio, sikio lake halikuwepo sehemu ambapo lilitakiwa kuwa lilikuwa lipo chini kisu kikali sana kilipita na sikio hilo haikujulikana ilikuwaje na kwa muda gani, kwa kiongozi wa hawa makomando alikuwa anavuja damu nyingi sana kwenye tumbo lake, alikuwa amecharangwa mithili ya mishikaki MUNGU wake utumbo haukuguswa japokuwa tumbo lilikuwa linahitaji apewe matibabu ya haraka sana vinginevyo lingemletea madhara makubwa, kwa Jamal alitaka kitingisha hata mkono wake lakini alishindwa, alihisi labda hakufanya vizuri alijaribu tena lakini ilikuwa ni vile vile tu hakuna kiungo chochote kwenye mwili wake ambacho kilikuwa kinaweza kusogea hakuelewa imekuaje, uso wake ulianza kukumbwa na usingizi ambao hata yeye mwenyewe hakuelewa umetokea wapi alianza kukakamaa mwili mzima, mwili wake ulilegea sana alidondoka chini na kuyafumba macho yake.
ENDELEA........................
Wakati makomando wawili wale wanakuja Jamal alikuwa na kisu mkononi mwake, kiongozi wao alivyorusha mikono yake alikuwa ameshika sindano zenye sumu kali sana mkononi mwake ndizo ambazo aliziachia wakati ule anairusha mikono yake kwa nguvu ilikuwa ni kazi ngumu sana kuweza kuziona kiurahisi ndio maana Jamal hakuweza kulitambua hilo mpaka zinazama mwilini mwake, sumu iliyokuwa ndani ya sindano hizo ilikuwa ikimaliza nguvu zote za mwili na kuufanya mwili uweze kukakamaa na kama zikiachwa kwa zaidi ya dakika tano bila kutolewa basi huwa ni lazima mtu aliye chomwa apoteze maisha.
Kitendo cha kumkwepa kiongozi huyo wa hao makomando mwanume aliinama kidogo na kupitisha kisu hake kidogo hicho kwenye tumbo la mwanaume mkomavu huyo na kulifanya lichanike hovyo hovyo baada ya hapo kisu kilirushwa kwa nguvu kwa komando wa nyuma ambaye alikuwa amebakiza hatua mbili tu amfikie Jamal.
***************************
Kukamatwa kwa gaidi aliyehusika kumuua mheshimiwa makamu wa raisi wa nchi ambaye alisemekana kuwa komando mkubwa sana ndiyo habari ambayo ilikuwa ikizungumziwa kila pande ya Tanzania, Afrika pamoja na dunia kwa ujumla, hakuna sehemu ambayo habari hiyo haikufika. Watu wana siri sana ila sio kwa utandawazi mkubwa uliopo kwa sasa hasa pale Jambo linapofika kwenye mkono wa mitandao ya kijamii, kila sehemu hiyo ndiyo iliyokuwa topic bora zaidi ndani ya nchi ya Tanzania, watu walikuwa wapo busy sana kuzungumzia jambo hili huku habari za chini chini ikisemekana kwamba mtu huyo alikuwa akifikishwa mahakamani siku ya mchana huo na kesi yake ilikuwa inasomwa siku hiyo hiyo watu walikuwa wapo makini sana kufuatilia kila hatua ili waweze kuujua mwafaka wa mwanaume kijana mdogo sana ambaye alikuwa amefanya tukio la kihistoria tangu nchi hii iweze kupata uhuru.
Moyo huwa ni kitu cha hovyo na cha ajabu zaidi kuwahi kutokea kwenye maisha ya mwanadamu yeyote yule, moyo ndicho chanzo cha lawama zote ambazo wanazitoa wanadamu kwa sababu walishajihalalishia kwamba moyo kazi yake kubwa ni kupenda kitu ambacho huwa kinakuja kuwaletea maumivu mazito sana baadaye na huwa wanakosa kabisa msaada kwa sababu wanatengeneza imani kwa wanadamu ambao wamekutana nao ukubwani tu na hawakuwahi hata kujuana huko nyuma.
Nimeuita ni kitu cha hovyo kwa sababu ukitoa umaskini moyo ndicho kitu ambacho kinaongoza kuleta maafa mengi duniani, unapo bahatika kuwa mbali na magonjwa ya moyo yanayo sababishwa na mapenzi basi unatakiwa umshukuru sana MUNGU kukuepusha na kikombe cha mwana haramu mapenzi.
Ndani ya nchi ya Cuba Catheline Yudel mtoto wa mr Yudel ambaye alikuwa ni kiongozi mkuu wa kambi kubwa zaidi ya kikomando ndani ya nchi hiyo alikuwa ametoka kuoga wakati anafika chumbani kwake baada ya kuvaa nguo yake laini ili aweze kumpumzika aliweza kuiona taarifa ya habari ya mheshimiwa raisi wa Tanzania kuhusu mtu mmoja ambaye alijulikana kwa jina la LENOVATUS kutafutwa baada ya kumuua makamu wa raisi wa nchi, picha aliyo iona ndicho kitu kilicho mshtua alikuwa ni mpori pori wake Jamal ambaye siku ya mwisho alimuahidi atakuwa naye kwenye sehemu yoyote ile duniani na popote pale atakapokuwa, hakuamini hicho kitu alikuwa amepanga kukikucha aanze rasmi kulifuatilia hilo jambo lakini baada ya asubuhi kukucha alijutia sana kuchelewesha maamuzi yake.
Alikuwa akitokwa na machozi mengi sana muda huo kwani baada ya kuwasha simu yake na kuingia kwenye mitandao ya kijamii taarifa za kukamatwa kwa mtu huyo ambaye alipewa jina la gaidi zilisambaa mno na mchana wake ilisemekana ndio muda ambao kesi yake ilikuwa inaenda kusomwa mahakamani.
Ilimhitaji sio chini ya masaa 23 kuweza kufika kwenye nchi ya Tanzania maana yake hakuwa na uwezo wa kuwahi mahakamani kwa sababu ilikuwa ni siku nzima kuweza kufika Tanzania hata hivyo hakukata tamaa mwanadada huyu mrembo ambaye alikuwa jasusi wa nchi ya Cuba, alipanga vitu vyake vya mhimu na kutoka ndani kwake, alikuwa anakuja Tanzania kulipigania penzi la mwanaume wa kwanza kwenye maisha yake ambaye ndiye aliye mtoa bikra yake hawezi kuusahau usiku ule hata siku moja ilikuwa ni miongoni mwa siku bora sana yeye kuwahi kuipitia. Alijisahau kabisa kwamba yeye ni komando wa nchi na hakuruhusiwa kabisa kwenda popote bila ruhusa ya mkubwa wake, mapenzi yalimchanganya hakuna kitu ambacho angeweza kuelewa kwa mtu ambaye angehitaji kumzuia.
*****************
Muda na umri ndivyo vitu pekee duniani ambavyo huwa havisimami kabisa hilo unatakiwa kulielewa kwa umakini sana, unavyo yaishi maisha yako inabidi uende kwa usahihi na hizo hesabu mbili kama ukiikosea hata moja basi utayaishi maisha yako kwa majuto sana. Mchana ulikuwa umefika jua kali sana la jiji la Dar es salaam haikuwa sababu ya kuwafanya watu washindwe kufika kwenye mahakama kuu ya nchi inayo husika na makosa ya jinai hapo ndipo palipo amuliwa kwenda kutoa hatima ya kesi ya kijana Jamal, kila kituo cha habari siku hiyo kilikuwa na soko sana waliuza mno walitamani habari za aina hiyo ziwe zinatokea kila siku kwani habari mbaya ndizo huwa zinauza sana, mchana huo hakuna hata mwananchi mmoja ambaye alikuwa akizurura mtaani, watu walikuwa wameyakaza macho yao kwenye kila runinga zao mtaani majenereta yaliandaliwa ili kama ikitokea umeme ukikatika kusiwe na tatizo lolote lile la umeme kukatika wasiweze kuikosa hiyo kesi, ndiyo ilikuwa kesi ya kwanza ya mauaji kuweza kuonyeshwa laivu ikiwa ni kama onyo kali kwa watu ambao walikuwa na tabia za hovyo kama za Jamal kwa kuziasi nchi zao kitu ambacho sheria ilikuwa hairuhusu kabisa.
Watu walijazana nje ya mahakama kumshuhudia kijana huyo ambaye wengi wao walishangaa sana kwani alionekana bado ni mdogo sana hakuna ambaye alitegemea kwamba anaweza kufanya tukio kama hilo la kutisha, watu walikuwa na simu zao wakirekodi tukio hilo moja kwa moja ili wakasambaze kwenye mitandao kama ilivyokuwa kawaida yao watu wengi kuliko kuwaza mambo ya maendeleo kwao mitandao ndilo chaguo sahihi zaidi kwa maisha yao, mwanaume alikuwa amechakaa damu kwenye mwili wake kuonyesha wazi alipigwa vikali mno ni shehemu ya uso tu ndiyo ilikuwa inatazamika hakuwa kwenye hali nzuri kitu ambacho hata wananchi kiliwatisha kwani hata kama alifanya makosa basi hakustahili kufanyiwa hivyo kwa kuzingatia haki za binadamu.
***************************
“Ndugu Jamal umahusishwa na kesi ya mauaji ya mheshimiwa makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania, je kuna ukweli gani wa hili tukio ni kweli wewe ndiye uliye lifanya kwa mikono yako na ukiwa timamu kabisa kichwani?” ilikuwa ni sauti ya jaji baada ya kuingizwa ndani ya mahakama.
“Sijaua” ni sauti nzito sana yenye mkwaruzo kutoka kwa Jamal akiwa kwenye pingu pale kizimbani ambapo alikuwa amesimama
“Kama hujaua wewe kwanini wewe ndiye ukamatwe?”
“Nadhani hilo swali ungewauliza walio nikamata”
“Ninavyo kuuliza swali Mr Jamal unatakiwa kutoa ushirikiano na sio kunijibu jeuri utakuwa unaenda kinyume na sheria za mahakama kitu ambacho ni hatari sana”
“Sawa”
“Sasa kwanini tuamini kwamba wewe haujaua?” sauti ya jaji ilisikika na ndiyo iliyo mfanya atabasamu japo alikuwa na maumivu makali sana
“Wewe kama jaji una ushahidi gani wa kujihakikishia kama mimi ndiye niliye ua?” swali la Jamal lilimfanya jaji mkuu amkazie macho Jamal
“Vipi kama ushahidi ukiletwa mbele ya mahakama utafanyaje”
“Kama ni hivyo kweli basi nataka kufa hakimu (I WANT TO DIE JUDGE) niue nitaipokea adhabu ” mwanaume aliongea akiwa hana hata tone la wasi wasi watu walikuwa kimya wakimshangaa kijana huyo alivyokuwa anajiamini sana kwenye sehemu ambayo binadamu wengi huwa wanaiogopa mno, Mahakama sio sehemu ya kuombea kupelekwa panatisha sana hususani kama unapelekwa kwa makosa ya jinai, kama ni kijana hakikisha unayaishi maisha kwa usahihi kukwepana na dhahama hii ya kwenda mahakamani ni hatari sana jela sio sehemu nzuri kwa mtu mwenye ndoto. Mheshimiwa jaji alinyoosha mkono wake kama ishara ya kuweza kumuita mtu, kuna mwanaume mrefu alikuwa akiingia hapo ndani akiwa na miwani yake safi usoni hakuwa hata na presha, nguo zake tu zilitosha kumuaminisha mtu yeyote mwenye macho kwamba huyo ni mwanasheria lakini aina ya vazi lake lilikuwa ni tofauti sana na ya wanasheria wengine.
Nicolous Philemone ndilo lilikuwa jina halisi la mtu huyo ambaye ndiye mwana sheria mkuu wan nchi ya Tanzania, alikuwa yupo hapo baada ya Jamal kugoma kabisa kwamba yeye hakuhusika kabisa kwenye hayo mauaji ambayo walisema ameyafanya, aliulizwa kama akikutwa na hatia wamfanye nini alisema mwenyewe kwamba wamuue sasa huyu aliyekuwa amekuja hapa alikuwa yupo kwa ajili ya kulithibitisha hilo, aliijua sheria kuliko hata jina lake na ndiye aliyekuwa akizisimamia sheria zote za nchi kazi ilikuwa ipo kwake.
“Mr Jamal umesema sio wewe uliye husika na hili tukio na mbele ya mahakama umekana kabisa huku ukidai kwamba kama ukikutwa na hatia basi upo tayari kupokea adhabu yoyote hususani ukidai kufa una uhakika na maamuzi yako na hauta yajutia?” wanasheria ni watu hatari sana maelezo yako ndiyo yanayo kufunga ukiwa mbele ya hao watu angalia kila aina ya neno ambalo linakutoka kinywani kwani linaweza kukuharibia kila kitu ndicho alichokuwa anakifanya mwanaume huyu kesi kwake ilikuwa ni rahisi sana kupitia tu maelezo yake ndiyo aliyokuwa anaenda kuwashangaza mamilioni ya watanzania ambao walikuwa wakishuhudia kila kitu.
“Yes, nipo tayari”
“Sawa” hakuongea sana kuna frashi ndogo alienda kuichomeka kwenye skrini kubwa iliyokuwa ikitumika kutolea ushahidi wa video pamoja na sauti za mfumo wa audio pale inapo hitajika, kilichokuwa kinaonekana kwenye hiyo video kiliwashangaza watu wengi sana kila aliyekuwa anaangalia alimfumba mtoto wake macho, unyama ambao ulikuwa unafanyika ndani ya hiyo video ulikuwa unatisha sana sura ya Jamal ilikuwa inaonekana kwa usahihi akiwa ndani ya gwanda ambalo huwa linavaliwa na makomando tu pekee hata mwanajeshi wa kawaida haruhusiwi kabisa hata kuligusa.
Silaha nzito ya maangamizi aliyo itumia kuvamia msafara huo ilitisha namna alivyokuwa akiwatoboa maaskari kwa risasi, aina ya kisu ambacho alikitumia kukata baadhi ya shingo za watu hao namna kilivyokuwa kinazungushwa kiliwatisha watu wenye roho nyepesi waliyafumba macho yao hakuna ambaye aliamini binadamu anaweza kuwa na roho ngumu kiasi hicho kiasi kwamba anachinja wenzake mithili ya kuku.
Tukio lililo leta msisimko zaidi ni pale wakati mtu huyo amemfikia makamu wa raisi namna mzee huyo alivyokuwa anaomba msamaha akitoa kilio kiliwafanya wengi wamuonee huruma sana hata hivyo hakuna ambacho kilisaidia kwani ilikuwa ni tayari alishakufa alimmiminia risasi nyingi sana mtu huyo alikufa hapo hapo kisha mwanaume akapotelea kwenye vichochoro na kutokomea huko. Video hiyo ilizalisha minong’ono mingi sana hiyo sehemu wenye roho nyepesi walibaki wanaangua kilio mahakamani na hata wale ambao walikuwa wanaangalia kwenye video zao nchi ilikuwa imefikia sehemu mbaya sana matukio kama hayo kuweza kufanyika.
Nisiwe muongeaji sana mtuhumiwa alitaka kuuawa, ushahidi upo wazi ni yeye kweli ndiye aliyeua hukumu mikononi mwa jaji, Mr mind mwanasheria mkuu ameshamaliza kazi yake nini kinatokea?.......48 naweka nukta hapa tukutane tena wakati ujao[emoji3578]
Bux the story teller
Sent from my TA-1053 using
JamiiForums mobile app