I want to die a judge

STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA.......

Baada ya kumaliza maelezo yake kwa usahihi aliiweka kola ya shati yake vizuri iliyokuwa ndani ya suti, kiza kilichokuwa humo ndani kilinifanya nisimuone ila hatua za viatu zilinipa taarifa mwanaume huyo alikuwa anatoka humo ndani, dakika mbili baadae umeme uliwaka kama kawaida mle ndani.

ENDELEA..................

“Kitu gani kinakufanya mpaka umekuwa mtu wa kuishi kwa kujificha sana namna hii kijana kama wewe” swali la kwanza kabisa kutoka kwa Alexander lilimfanya Ashrafu atabasamu akiwa na glassi yake mkononi anasafisha koo wasi wasi haikuwa sehemu ya maisha yake kijana huyu.

“Dunia hii wanaishi watu mbali mbali na wenye sifa tofauti tofauti, kuishi kwenye huu ulimwengu unatakiwa uwe kama kivuli mbele za nyuso za watu ili upate vitu unavyo vihitaji wewe ila ukiruhusu kila mtu akakujua kwa undani basi sahau kuhusu kila kitu kwenye maisha yako hakuna nafasi utaipata mbele ya dunia ukaweza kutekeleza yale ambayo ulikuwa unataka kuyatimiza kiurahisi. Ninaishi nitakavyo, ninaweza kupata kitu chochote kwa muda wowote ule bila usumbufu wowote ule, sina uhakika sana ila ni miongoni mwa watu wenye usalama mkubwa sana ndani ya mipaka ya nchi hii, maliza maswali yako yote kuniuliza ili nikianza yakwangu usije ukaujutia ulimi wako” kijana mstaarabu kwa mwonekano ila mambo yake yalikuwa ya kutisha mno ndiye aliyekuwa anamwambia Alexander maneno ya kijasiri haya, alijiamini mno Ashrafu Hamad

“Hahahaahahahaahhaahahahah vijana wa siku hizi mnakua vibaya sana labda huenda mmezaliwa nje ya ndoa au kwa sababu mmelelewa na ulimwengu badala ya wazazi wenu ndio maana mnajihisi mnaweza kuropoka chochote kile ambacho kinakuja kwenye vichwa vyenu, yaani kijana kama wewe ndo unaniambia mimi nitaujutia ulimi wangu, hahahahaahahahhahhhhahh……….” Alexander aliona kama kijana huyo hakuwa siriasi kwa alichokuwa anakiongea kwenye mdomo wake haikuwa sawa mtu kama yeye kuweza kutishwa na kijana kama huyo kwake kilikuwa kama kichekesho nadhani hawakuwahi kumfahamu kiundani sana mwanaume huyo lakini alikatishwa kwa ukali na Ashrafu.

“Umemaliza maswali yako” sauti ya ukali wakati huo glasi ilivunjwa kwa mkono ndiyo iliyo mshtua Alexander kwenye kicheko ambacho hakikuwa cha furaha muda wote alikuwa anazipiga hesabu zake kwa usahihi anaweza kutoka vipi kwenye kundi kubwa la watu walio mzunguka mahali hapo wakiwa na silaha.

“ok, nambie wewe ni nani hasa na huyo baba yako ni nani serikalini?” swali la Alexander lilimshtua sana Ashrafu, maisha yake yaliwekwa ya siri kubwa mno hakuna mtu wa nje aliyekuwa anajua kwamba huyo kijana ni mtoto wa mtu kutoka upande wa serikali, hiyo taarifa haikuwa njema kwake hata kidogo japo hakuonyesha mshtuko wa moja kwa moja.

“Hili jambo mnalijua wangapi?” hakuwa na namna ya kupepesa macho kwa namna yoyote ile alijua anajulikana vilivyo na huyo mtu japo kuhusu baba yake ndiye mwanaume huyo alihitaji kumjua kwa usahihi.

“Unapo amua kucheza michezo ya hatari namna hii unatakiwa kuelewa kwamba kuna watu ambao walisha icheza michezo kama hiyo wamekaa pembeni wanakuangalia tu unacho kifanya sasa nao wanapo amua kurudi tena mchezoni inaweza kuwa hatari kubwa sana upande wako,ni vyema ukaitumia nafasi yako kukaa nje na haya mambo ukayaishi maisha yako tu japo umesha chelewa kwani mpaka sasa mafaili yako yapo kwenye mikono ya watu hatari sana na hauwezi kuikwepa hiyo mikono ikiwepo mkono wangu mimi mwenyewe iliniuma sana siku ile napigwa na risasi na kijana wa kawaida kama wewe, nimekutafuta mno kwa miaka kadhaa iliyoweza kupita mpaka nilipo kuja kujua kwamba siku ile ulikuwa kwenye ile hoteli, umekaa na kuwatoa sadaka vijana wa watu wasiokuwa na hatia yoyote ile ili wewe uwe salama nadhani leo utanipa majibu sahihi” Alexander alikuwa akijiamini mno kiasi kwamba aliwashangaza mpaka wao waliokuwa humo ndani ya nyumba hiyo, alijongea bila wasi wasi kabisa akasogea mahali lilipokuwa friji aliitoa moja ya wine iliyokuwepo humo ndani akachukua glass mbili na kwenda nazo mezani, watu wote walikuwa wakimshangaa tu licha ya wanaume wote kuwa na silaha kali haikuwa sababu ya kumfanya awe na wasi wasi. Hayo ni maisha ya viumbe vya kutisha duniani, wanaweza kukifanya chochote kile mahali popote pale na kuondoka bila kuwa na wasi wasi wowote ule, Alexander alimpa ishara Ashrafu akae chini ndipo waongee alionekana kuwa na mazungumzo ya muda mrefu kidogo.

“Tangu nianze kuyaishi haya maisha yangu ya hivi nimekuwa binadamu wa kutisha sana kwenye maisha ya wanadamu wa kawaida, naogopwa mno mtaani, kuna watu hawatamani hata kidogo kukutana namimi kwenye maisha yao lakini wewe unakuja hapa kwenye himaya yangu licha ya kuona aina ya umakini wa watu waliopo hapa ambapo kwa akili ya kawaida tu huna uhakika kama utatoka na nafsi yako ikiwa salama umekuwa mtu wa kujiamini kupita kiasi ni mbaya sana kwa maisha ya mtu kama wewe ambaye kwa sasa ulitakiwa uwe umeoa na una mkeo mnalea watoto wenu na sio kuwafuatilia watu kama mimi japokuwa kwa wewe ilikuwa ni lazima tu kwamba ningekutafuta hata usingekuja siku ya leo” Ashrafu alikuwa amekaa kwenye sofa hapo chini kila mtu akiwa na glasi yake mkononi ya wine wanashushia taratibu, kama ingekuwa ndio mara yako ya kwanza kuwaona watu hawa lazima ungedhani kwamba walikuwa ni watu wenye ukaribu wa hali ya juu kama sio marafiki wakubwa ila hilo halikuwa na ukweli wowote, hao wote wawili walikuwa ni watu ambao walikuwa wanatafutana isivyo kawaida, imani juu ya uwezo wao ndivyo vilivyofanya wakae chini kwanza weweze kuulizana maswali ambayo yangewafaa kwa alfajiri hiyo.

“Mhhhhhhhhhh ni mwanadamu wa aina gani wewe ambaye unaweza kumtisha mwanaume aliyeweza kuingia ndani ya ikulu ambayo ndiyo sehemu inayo lindwa zaidi ndani ya nchi, kuna kila aina ya watu hatari kule, kunalindwa mpaka na mitambo maalumu ya mionzi hata hivyo nilifanikiwa kumuua raisi na kutoweka bila kukamatwa wala kugundulika na binadamu yeyote mpaka leo, vipi naweza nikakuogopa kijana kama wewe ambaye hata uhakika wa maisha yako huna unaishi kwa kujificha ficha tu ukiogopa kwamba huenda maisha yako yakachukuliwa muda wowote ule. Hapa nitaondoka ila sio kwa wewe kuniambia niondoke, nitaondoka kwa kujisikia mwenyewe nitakapo ona nimekipata nilicho kifuata” Tabasanu hafifu ndiyo ilikuwa sehemu ya kuhitimisha maelezo ya Alexander,ni kitu ambacho kilikuwa ni cha kutisha sana, leo Ashrafu alikuwa anaambiwa kwamba mtu ambaye alikuwa naye mbele yake ndiye aliyekuwa amemuua mheshimiwa raisi aliyeweza kupita kwenye madaraka, kumbu kumbu zake zilienda miaka kadhaa nyuma ilikuwa ni kweli kuna raisi alifia madarakani ghafla sana kifo chake kikiwa ni siri kubwa ambayo haikuruhusiwa kutoka nje ya ikulu kwamba chanzo chake ni nini, hakujiuliza mara mbili alihisi huyo mtu anaweza kuondoka na maisha yake humo ndani kizembe sana kama asipo jihami.

Kuingia na kutoka ikulu ukiwa salama tena umefanya mauaji ya mheshimiwa raisi hakikuwa kitu chepesi, kilihitaji binadamu mwenye roho ngumu sana kuweza kufanya hivyo, mguu wake mmoja uliipiga chupa ya wine ambayo ilikuwa mezani, chupa hiyo ilikuwa inaelekea upande wa pili mwa meza hiyo haikuleta madhara yoyote ile baada ya kupokelewa kwa ngumi nzito na kupasukia hewani wine ikasambaa mithili ya maji, risasi mbili zilikuwa zimefyatuliwa kwa spidi kutoka kwenye bastola ambayo ilikuwa ipo kwenye mikono ya Ashrafu, meza ya kioo ilipigwa na teke ambayo ndiyo iliyotumika kuzuia risasi hizo mbili, ni umbali mdogo sana walikuwa wamekaa hao watu ila tukio lililokuwa linatendekea hapo lilikuwa linaleta burudani sana machoni mwa walinzi waliokuwa wako pembeni. Alexander alikuwa amejirushia nyuma ya sofa moja na kuligeuza kwa wepesi, risasi zaidi ya sita ziliishia kunyofoa nyofoa nyama ya sofa hilo kutoka kwenye bastola ya Ashrafu.

Zilipigwa hapo zaidi risasi hamsini kutoka kwa walinzi waliokuwa na silaha za kutisha kwenye mikono yao ikiwa ni kama hatua ya kuweza kumuweka bosi wao kuwa salama, hakutakiwa kuwa hata na kidonda huyo mtu hakuna mlinzi angeweza kutoka salama akiwa hai, sofa lilikuwa limenyofoka nyofoka halikutamanika tena.

“Noooooo stop, he is mine(huyu ni wa kwangu) nahitaji afie kwenye mikono yangu kama hataweza kunijibu maswali yangu”, kitu cha kushangaza Alexander alitokea nyuma ya kabati akiwa hana hata wasi wasi baada ya kusikia kelele za Ashrafu kumhitaji waonyeshane uwezo wao hiyo ndiyo ilikuwa robo tatu ya maisha yake aliipenda michezo ya ngumi kuliko hata alivyo yapenda maisha yake, hawakuelewa kutoka kwenye lile sofa ni muda gani ameutumia kufika kwenye hilo kabati hiyo ndiyo sababu alisema yeye sio mtu wa kawaida walijisumbua tu kupiga risasi zao hapo alikuwa ameondoka muda mrefu sana.

Ashrafu hakuhitaji mtu yeyote aweze kuingilia hilo alihitaji kwa mkono wake kumfanya mwanaume huyo amjibu maswali yake kwa lazima kama sio kumuua, walinzi walisogea nyuma uwanja mkubwa ulikuwa umeachwa kwa sababu ya wanaume hawa wawili. Nguo ya kulalia aliyokuwa ameivaa Ashrafu ilikuwa inakuja usawa wa macho ya Alexander aliipangua kwa nguvu alikutanishwa na teke maeneo ya shingoni alikuwa anaenda kujibamiza ukutani miguu ilitumika kudunda kwenye huo ukuta akatua chini akiwa safi, traki safi ilikuwa mwilini mwa Ashrafu kifua kilichokuwa kimegawanyika kilikuwa kipo wazi kabisa.

Spidi ambazo zilikuwa zinakuja kwa nguvu ya upepo zilitumika ndani ya sekunde chache sana Alexander kuweza kufika sehemu ambayo alikuwepo ashrafu, mwili wa Alexander ulizungushwa kama tairi lililokuwa kwenye mwendo mkali alijigeuzia kwenye mbavu za Ashrafu ambaye alirudi nyuma baada ya mikono iliyo komaa kuzigusa mbavu zake kwa nguvu alikuwa anadondokea kwenye moja ya sofa, mkono wake mmoja aliegamia kwenye pembe ya sofa hilo akajigeuza ila kabla hajakamilisha hilo goti lilikuwa limefika kwenye tumbo lake, Alexander alikuwa anakuja kwa nguvu sana, goti hilo lilimpeleka ukutani sehemu ambapo palikuwa na ala ya upanga ulio onekana kuwa wa muda mrefu kidogo ukiwa upo hapo, mguu uligusa sehemu kilipokuwa kitufe cha kuutolea upanga huo ulidakwa kwa usahihi kwenye mkono wa kulia wa Ashrafu, Alexander alikuwa amefika lakini alirudi nyuma kidogo baada kuzigusa alama za damu kwenye tumbo lake. Alikuwa amekatwa na kijana huyo Ashrafu Hamad ambaye alikuwa mbele yake, alitabasamu uzembe wa sekunde kadhaa tu ulikuwa umefanya ajisahau sana mpaka mpinzani wake akapata sehemu ya kuzigusa sehemu za mwili wake.

“Sasa nahitaji unijibu vizuri, kile mlicho kifuata siku ile ndani ya jiji la mwanza mlikipeleka wapi na kichwa cha yule mzee kipo wapi mpaka sasa?” upanga wake ukiwa na alama za damu alimuuliza mwanaume ambaye alisemekana kuingia ikulu na kumuua mheshimiwa raisi kisha akafanikiwa kutoroka bila kukamatwa na mtu yeyote yule, huyo ndiye Alexander mwenyewe.

“Leo kama utapona siku nyingine unatakiwa ukiniona unikimbie nadhani kwa hiki kinacho enda kutokea hapa leo hata baba yako atajitokeza hadharani akiwalilia watu kwa kitu unacho enda kufanyiwa ni bora ungeendelea kujificha tu, dakika tano ukifanikiwa kuzimaliza sitakuwa na swali la kukuuliza kuhusu maisha yako nitakuacha uende ila kama zitakushinda basi taarifa ya habari ya leo inaenda kuzitangaza habari za kifo chako mtu ambaye kile mtu anajua ulishakufa” kauli ya Alexander ilifuatiwa na uchomolewaji wa visu viwili kwenye kiuno chake.


Atapona nani ataishi nani? tukutane wakati ujao 27 sina la ziada tena

Bux the story teller
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA.......

“Leo kama utapona siku nyingine unatakiwa ukiniona unikimbie nadhani kwa hiki kinacho enda kutokea hapa leo hata baba yako atajitokeza hadharani akiwalilia watu kwa kitu unacho enda kufanyiwa ni bora ungeendelea kujificha tu, dakika tano ukifanikiwa kuzimaliza sitakuwa na swali la kukuuliza kuhusu maisha yako nitakuacha uende ila kama zitakushinda basi taarifa ya habari ya leo inaenda kuzitangaza habari za kifo chako mtu ambaye kile mtu anajua ulishakufa” kauli ya Alexander ilifuatiwa na uchomolewaji wa visu viwili kwenye kiuno chake.

ENDELEA...................

Visu viwili mkononi ndizo silaha ambazo alikuwa akiziheshimu sana Alexander akiwa kwenye sehemu yoyote ile ya hatari kwenye maisha yake, licha ya kukatwa na kisu kwenye sehemu yake ya tumbo bado mwili wake ulikuwa una joto la kutosha kuhitaji mapigano, ni dakika tano tu pekee ambazo ndizo alikuwa amezitoa kwa Ashrafu kama angefanikiwa kuzimaliza angeweza kumuacha akiwa hai kabisa na akaenda mbali ila kama angeshindwa kuzimaliza basi alitakiwa kuyajibu maswali yote aliyo ulizwa kwa usahihi ambayo ni mawili tu pekee yeye ni nani na ni mtoto wa nani serikalini hata hivyo kuachwa kwake ilikuwa ni ngumu sana kwani aliahidiwa kuuawa kikatili sana kiasi kwamba baba yake mzazi angejutia sana kwenye taarifa ya habari ya kifo cha kijana huyo. Hakuwahi kumuogopa binadamu yoyote yule Ashrafu lakini kwa siku hiyo kwa mara ya kwanza kabisa aliingiwa na hofu kwenye maisha yake mpaka muda huo mbavu zake zilikuwa kwenye hali mbaya sana ya maumivu ni mazoezi makali mno ndiyo yalikuwa yakimlinda mpaka muda huo ila kama angekuwa ni mtu wa kawaida asingeweza hata kumeza mate wala kuongea kwa usahihi.

Kisu kimoja kilikuwa kinakuja kwenye kifua cha Ashrafu, kilipanguliwa na upanga wake alijikuta yuko mbali sana baada ya kudondokea miguuni mwa moja ya walinzi wake, ujio wa kisu ulikuwa uko sambamba kabisa na spidi alizokuwa anakuja nazo Alexander mtu wa Kagera, Ashrafu alijinyanyua kwa maumivu akiwa haelewi mtu huyo alikuwa anapiga vipi dakika tatu ndizo zilikuwa zinamfanya ayasaidie maisha yake alijinyoosha na upanga wake akisukumizia na mateke yote mawili ambapo moja lilifanikiwa kumugusa Alexander kwenye paji la uso, alihisi pamechanika lakini alitikisa kichwa chake na kukiweka sawa, alijinyoosha akakiokota kisu chake kimoja ambacho kilipanguliwa na upanga wa Ashrafu, aliuma meno kwa hasira sana hakuamini kama mtu huyo angeweza kumsumbua sana namna hiyo, Ashrafu alibetuka tiktaka moja safi sana ili kuitegua shingo ya Alexander mwanaume aliinama chini kidogo akapitiliza Ashrafu wakati anageuza kichwa chake alikutana na teke la uso hakuamini kama ni teke limempiga ilikuwa ni mithili ya jiwe la chuma ndilo alikutanishwa nalo kwa mawazo yake yalivyo mtuma, alipoteza kabisa uwezo wa kuona alianza kupiga kelele kwa kupoteza uwezo wa kuona, kichwa kilikuwa kinauma na macho yalikuwa yanauma, alianza kurusha upanga bila mpangilio akipiga makelele.

Alexander aliangalia saa yake dakika moja ilikuwa imebaki zikamilike tano, alizungusha ngumi yake kwa hasira na kuituliza kwenye kifua cha Ashrafu ambaye alicheua damu, visu viwili vilipita kwenye bega lake mkono mmoja haukuwa na kazi tena ulichanika vibaya sana, alipiga kelele za kutisha zilizowafanya walinzi wake waingilie sasa baada ya kuona bosi wao amezidiwa hana uwezo wa kujilinda tena mbele ya mwanaume mkatili mno aliyekuwa yupo mbele yake. Alexander hakuwa na muda wa kupoteza humo ndani alikuwa anaenda kufa kwa spidi alijipindua na kumdaka Ashrafu ambapo mwili wa kijana huyo aliutumia kama kinga ya kujilindia baada ya kukoswa na risasi kadhaa kutoka kwa hao watu, aligeuza macho ule upande ambako walikuwa wale vijana wawili wenye kufanana na Ashrafu Hamad hakuona kitu chochote kile aligundua tayari walishakimbia, mkononi mwake alikuwa ameshika kitu kama bomu alilifungua juu yake moshi mwingi sana ulitanda humo ndani walinzi wote walianza kukohoa na kuishiwa nguvu hatimaye wakadondoka chini kabisa baada ya kukosa pumzi haikujulikana kama Alexander alipona kwenye huo moshi mkali au alipatwa na nini.

Mheshimiwa makamu wa raisi alikuwa ndani ya ofisi yake akiwaza mambo mengi sana ambayo yalikuwa yanaendelea kwenye maisha yake, stori ya maisha yake ndiyo iliyokuwa ikimfanya awe na mawazo mengi sana kichwani mwake, miaka kadhaa nyuma alikumbuka alikuwa mtu mwenye furaha kubwa sana wakati alipokuwa akiishi na mwanamke aliyekuwa akimpenda sana, alimshukuru MUNGU kwa kumpa zawadi hiyo ya pekee kabisa kwenye maisha yake, ni mwanamke ambaye hakuwa na uwezo wa kuelezea ni namna gani aliweza kumpata.

“Mbali na siasa ni kitu gani ambacho ndicho unakipenda sana kwenye maisha yako?”
“Kama ningeambiwa nichague maisha na mapenzi basi mapenzi kingekuwa kitu ambacho nisingekosa kukitaja, hakuna maisha bila mapenzi niamini mimi ila kunaweza kuwa na mapenzi bila maisha, kauli yangu inaweza kuwa tata na nisieleweke kirahisi hususani kwa binadamu wa sasa ambao wamepoteza imani kabisa ila ina maana kubwa sana, nakumbuka kwenye maisha yangu nilifanikiwa kukisoma kitabu kimoja kizuri sana cha mapenzi kinacho wahusu Romeo and Juliet tangu siku ile nilijifunza kwamba hakuna maisha bila mapenzi ila kuna mapenzi bila maisha kwa sababu watu wawili wapendanao waliamua kuyatoa maisha yao kwa sababu ya mapenzi ila hawakuwa tayari kuwa na maisha bila mapenzi. Tumeumbwa ili tuishi kwenye kuishi ni lazima upate mtu wa kuishi naye kwa wakati wako ambao MUNGU amekupendelea, mimi ni moja ya watu ambao nimebahatika kuishi kwenye maisha ambayo kila mwanaume anayatamani. Kukupata mwanamke kama wewe najihisi naweza kuufundisha ulimwengu juu ya nini maana ya mapenzi yalivyo, Asiana ni jina la mwanamke ambaye ninampenda sana kwenye maisha yangu, ni mwanamke ambaye kila nikimuona naelewa maana halisi ya mapenzi, nampenda sana huyo mpori pori wangu, na sio siasa tu hata ningeambiwa kwenye vitu vyote ambavyo vipo chini ya ulimwengu huu nataka nini, penzi la huyu mwanamke kwangu ni zawadi kubwa sana kwenye bustani nzuri ya huba la moyo wangu” sio wimbo wala hadithi ya kwenye kitabu ni maneno adhimu yalikuwa yakimtoka kijana mmoja pembezoni ya mto mdogo maeneo ya Kibiti akiwa kando ya mwanamke aliyekuwa akimpenda sana.

Hamad Hamad ndiye kijana aliyekuwa akielezea namna alivyokuwa akimpenda mwanamke wake huyo aliyepatwa kuitwa Asiana, mara ya kwanza mwanamke huyo alikuwa akijisikia vibaya sana kwa kuhisi mwanaume aliyekuwa akimpenda sana alikuwa akiipenda siasa kuliko anavyo mpenda yeye lakini hicho kitu kilikuwa ni cha tofauti kabisa na mawazo yake leo mwanaume alikuwa akimpa tasnia ya tungo nzuri zilizopo kwenye mdomo wake kuelezea namna anavyo mpenda, ni jambo lililompa furaha ambayo asingeweza kuielezea mwanamke huyo kwa namna alivyo kuwa amefurahi kupitiliza, kicheko ndiyo ilikuwa sehemu ya kuupamba uso wake mpana majira ya jioni maeneo ya Kibiti kwa walima mihogo huko.

Makamu wa raisi alishtuka kutoka kwenye hayo mawazo ambayo alitamani yasingekuwa yanaisha kirahisi sana namna hiyo, ule ulikuwa ni wakati sahihi sana wa yeye kuyaishi maisha hayo aliona kabisa alistahili kuipata furaha hiyo kwenye maisha yake yote lakini liwalo na kicheko leo basi kilio chaliita kesho yake ni tamathali ambazo baadhi ya watu wenye maarifa waliwahi kuzitamka na makamu huyo alikuwa akizikumbuka kwa usahihi sana. machozi yalimtoka kwenye macho yake usingeweza kuamini kama mwanaume wa aina hiyo alikuwa akililia mapenzi ni jambo la kuchekesha sana ila kama unalishuhudia upande wa pili, ni ugonjwa ambao hata wanao yachambua mapenzi kwa usahihi hawawezi kujitibu wenyewe, alisimama hapo alipokuwa amekaa akaenda kwenye kabati moja kubwa sana ambalo lilikuwa pembeni yake kidogo, aliingiza nywila hapo akatoka na Album moja nzuri sana ya picha, aliufungua ukurasa wa kwanza wa album hiyo kulikuwa na picha za watu watatu, picha moja alikuwa anaonekana yeye wakati akiwa kijana, picha ya pili kulikuwa na mwanamke mmoja mrembo sana lakini katikati ya picha hizo alikuwa amekaa mtoto mdogo sana mchanga tabasamu likiwa limeiangaza nuru ya uso wake. Alitoa kitambaa baada ya chozi lake kudondokea kwenye hiyo picha akajifuta kwa uchungu mkubwa.

“Mlinde mwanangu kwa namna yoyote ile huyo ndiyo alama ya uwepo wangu duniani hakuna mwingine zaidi yake, ukimuona yeye ni sawa na kwamba umeniona mimi” ni sauti ya mwanamke ambayo ilijirudia kichwani kwake, aliiheshimu mno hiyo sauti, alikurupuka humo ndani akatoka nje kwa kasi.

“Bosi kuna nini mpaka upo kwenye hiyo hali saivi?” mlinzi wake wa karibu sana aliweza kumuuliza bosi wake baada ya kumuona kama hakuwa sawa kabisa.
“Andaa msafara nahitaji kwenda kumuona mwanangu sasa hivi” aliitamka sentensi yake kwa jazba kiasi kwamba hakuhitaji maelezo mengi kutoka kwa hao watu.
“Sawa bosi lakini inadaiwa kwamba nyumbani kwake hayupo jana ameaga anaenda kwenye nyumba ndogo Kinondoni”
“Alienda kufanya nini huko bila mimi kujua”
“Sijui bosi ni tarifa ambayo nimeipata usiku wa leo kabla hakujapambazuka”
“Nahitaji kwenda huko haraka sana huyo mtoto kwangu ni mhimu sana andaa kila kitu nahitaji kufika huko haraka sana kwa muda mfupi” kauli yake ilikuwa ni amri na ilitekelezwa mara moja safari ya kuelekea Kinondoni ilianza mara moja. Dakika thelathini hakukuwa na foleni sana alfajiri hiyo na mapema walikuwa wamefika nje ya geti la nyumba hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na Ashrafu Hamad mtoto wa mheshimiwa makamu wa raisi walishtuka kidogo baada ya kukuta nje kulikuwa na pikipiki ambayo ilionekana imetoka kulipuliwa muda sio mrefu sana kwani bado ilikuwa na mto unawaka. Mzee huyo alifika getini na kuingiza namba kadhaa geti likafunguka kwanza walistaajabu kuona kuna vijana wawili wameuawa kikatili mno hapo nje, makamu wa raisi alikimbilia ndani ya nyumba hiyo wakati huo moshi ulikuwa umeisha ila humo ndani kulikuwa na harufu kali ya kutisha. Aliangaza huku na huku kama ataona mtu lakini hakuona chochote kile wakati anageuza macho yake aliona alama za damu chini na mfumuko wa sofa ambao alijua wazi ni risasi zilipita hapo, hofu iliongezeka kwenye moyo wake sana.

Nyuma yake kulikuwa na miili ya wanaume kama kumi na wawili ambao walikuwa wapo chini wamelala, hakuelewa sababu ni nini aliinama ili kuwagusa na kuwageuza lakini alizuiwa na mlinzi wake ambaye alimuonyeshea alama ya kukataa kwa kichwa.

“Hii ni sumu kali sana ambayo huwa inamlevya kwanza mtu, anakosa nguvu kabisa kisha baada ya dakika thelathini kama atakosa matibabu basi hawezi kupona tena ataanza kubadilika taratibu” Mlinzi wa mzee huyo alikuwa anaongea huku akumvalisha bosi wake usoni mashine ya kuvutia hewa safi kwa sababu mazingira ya humo ndani hayakuwa rafiki kabisa kwa afya ya mtu wa kawaida.
“Atakuwa ni nani huyu mwenye ujasiri wa kuingia kwenye nyumba ya mwanangu bila wasi wasi wowote akatenda haya kwa wepesi sana namna hii?” swali kidogo lilikuwa gumu kwani wote ndo walikuwa wanafika muda huo hakuna mtu ambaye angeweza kujua kama nini kilitokea bila kuwa na ushahidi. Kabla hajajibiwa ili miili ya wale walinzi wa Ashrafu Hamad pale chini ilianza kubadilika rangi na kuwa myeusi.

“Huyu mtu anaonekana sio wa kawaida kwa sababu kuu mbili, yakwanza sio rahisi kumuingilia Ashrafu kwa ninavyo mjua mimi ni mtu wa kutisha sana kwenye mapigano ina maana kama huyu mtu amevamia na kumpata hapa akapata mpaka ujasiri wa kuyafanya haya basi ni mtu hatari mno, lakini sababu ya pili hii sumu iliyo tumika huwa inapatikana ndani ya nchi ya Urusi tu pekee duniani na haijawahi kuruhusiwa kusambaa kwenye nchi yoyote duniani kwa kuhofia usalama wa binadamu, hapa ndani ya saa moja lijalo hakuna kiumbe ambacho kimeivuta hiyo hewa kwa muda mrefu kitakuwa hai mpaka kwa muda huo” maelezo ya mlinzi wake yalimpa wasi wasi sana makamu wa raisi, hii nyumba aliijenga mwenyewe hivyo aliijua vyema sana aliingia mpaka kwenye chumba ambacho kilikuwa kinatumika kwa ajiri ya kamera za ulinzi zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.

Mjongeo wa kamera hizo uliionyesha sura ambayo baada ya kuiona tu mbele yake alionekana kuogopa mno hakutegemea hicho kitu kabisa kwenye maisha yake kama kinawezekana, hakuwa na nguvu tena za kusimama mzee huyu alilegea kiasi kwamba alidondokea kwenye kiti.

“Nooooo haiwezekani haiwezekani, imewezekanaje yupo hai mpaka leo nooooooooooo” aliongea kwa hasira akiinuka na kupiga ngumi kwenye ukuta kwa hasira kali, akiwa kwenye huo mshtuko na hasira simu ya kwenye hicho chumba cha kamera ilianza kuita kwa fujo, ni kitu ambacho hawakukitegemea hata kidogo ni vipi mpigaji aliweza kujua kwamba huo muda wangekuwa hapo alfajiri hiyo na mapema sana, aliinua na kuipokea simu yake midomo yake ikiwa inatetemeka sana, hakuwa na imani na usalama wa hiyo simu.

Nani kaanza kumgusa sehemu mbaya makamu wetu wa raisi? Hatima ya Alexander na Ashrafu ni ipi? Unadhani mpigaji wa simu atakuwa nani?...........

Naachia kalamu 28, tukutane sehemu ijayo baada ya Jamal kuujua ukweli wa maisha yake, unadhani anaenda kufanya nini?

Bux the story teller
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE.......
“Nooooo haiwezekani haiwezekani, imewezekanaje yupo hai mpaka leo nooooooooooo” aliongea kwa hasira akiinuka na kupiga ngumi kwenye ukuta kwa hasira kali, akiwa kwenye huo mshtuko na hasira simu ya kwenye hicho chumba cha kamera ilianza kuita kwa fujo, ni kitu ambacho hawakukitegemea hata kidogo ni vipi mpigaji aliweza kujua kwamba huo muda wangekuwa hapo alfajiri hiyo na mapema sana, aliinua na kuipokea simu yake midomo yake ikiwa inatetemeka sana, hakuwa na imani na usalama wa hiyo simu.

ENDELEA.....................


“Muda huwa unaenda kwa kasi sana hapa duniani kama ilivyokuwa kawaida hauwezi kusimama, wiki tatu zilipita nikiwa napatiwa matibabu pale kitandani hatimaye niliweza kunyanyuka nikiwa kamili , yule mtu alitumia pesa nyingi sana kuhakikisha nasimama tena maana waliletwa madaktari bingwa kutoka nje za nchi ambao walinishughulikia wakati huo kiongozi wangu hakuwa akijua lolote kuhusu hayo ambayo yalikuwa yamenitokea kwa muda huo. Huenda ni miongoni mwa wanadamu ambao nilikuja kuwaheshimu zaidi kwenye maisha yangu yote, kwanza alinilindia siri kwa wenzake kwamba mimi ni usalama wa taifa kwa sababu kama wangejua basi wangenitafuta sehemu yoyote ile waweze kuniua, mpaka muda huo sikuwa na uwezo wa kumpatia mwanamke yeyote mimba kwa sababu sikuwa na sehemu ambazo zingenipa huo uwezo kwenye maisha yangu lakini sikuwa mchoyo wa fadhila kwa mwenyezi MUNGU kwa kunipendelea nafasi nyingine ya kuendelea kushuhudia ubaya wa ulimwengu, pumzi ndicho kiburi kikubwa sana kwa mwanadamu yeyote yule, ndiyo huwa inawafanya wanadamu wanakuwa jeuri mno ila ikifika siku ukiwa huna uwezo wa kuivuta hiyo pumzi vizuri upo kitandani malaika wa kifo anakung’ang’ania uondoke naye ndipo utakapo elewa thamani ya maisha ambayo unayachezea kwa sasa hapa duniani. Baada ya kuweza kusimama kwa mara nyingine tena nilifanya mazoezi kwa nguvu sana sikuhitaji kukutana na mkuu wangu kwa hali niliyokuwa nayo isingekuwa vyema kukaa naye kuongea ningeonekana mwanadamu dhaifu sana.

Wiki moja baadae nilijihisi kuwa vizuri sana hivyo nilifanikiwa kutoka kwenye hospitali ambayo nilikuja kugundua baadae kwamba ilikuwa ni nyumba ya mtu binafsi ambayo ilikuwa nje ya jiji kabisa, gari moja nilipewa na wale madaktari ambao walihakikisha usalama wangu, nikiwa ndani ya suti yangu nilirudi ndani ya jiji la Dar es salaam bila wasi wasi, mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa ni mkurugenzi wa usalama wa taifa baada ya kupotea kwa zaidi ya mwezi mzima nilijua lazima watakuwa wamenitafuta sana.
“Ni mwezi sasa umepita haupo wala hauonekani ni kipi kimetokea huko ulikokuwa” baada ya kukutana na mzee yule hakuihitaji hata salamu yangu swali lake ndiyo ilikuwa salamu. Nilimsimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea mpaka wakati huo, alinisikitikia sana mambo yaliyonikuta yalikuwa yanatisha sana ilihitaji moyo kuweza kuyamudu. Alishtuka sana baada ya mimi kumwambia Jonson Malisaba alikuwa akifanya kazi chini ya viongozi wakubwa wa serikali, ni kitu ambacho ilikuwa ni ngumu sana kwake kukiamini lakini ndio ulikuwa ukweli wenyewe alitamani sana akutane na Malisaba mwenyewe. Baada ya kutoka hapo maisha yaliendelea bila kuweza kuongea na baba yako ni mwaka mmoja ulikuwa umeisha, siku moja saa sita za usiku niliamua kuipiga ile namba ambayo alikuwa amenipa kwamba nikimhitaji muda wowote nitampata 911 niliipiga bila kusita kwa kutumia simu yangu ya mezani, simu moja kwa moja ilipokelewa kituo cha polisi sikuogopa kwa sababu hilo nilikuwa nikilijua mapema sana yalifuata maongezi ya kawaida tu kisha ikakatwa, dakika zaidi ya tano zilipita kukiwa kimya lakini haikuchukua muda simu yangu iliita niliipokea kwa wepesi mno.
“Hello” sauti yenye mgandamizo kutoka upande wa pili niliisikia majira hayo ya usiku wa manane kwa usahihi kabisa.
“Naomba tuonane” nilimjibu kwa ufupi kwa sababu ilikuwa ni hatari sana kuanza kutambulishana kwenye simu ni kitu cha hatari sana unaweza kukamatwa muda wowote ule.
“Toka nje ndani ya dakika saba kuna gari inakuja kukuchukua hapo” aliongea kwa msisitizo ila nilishangaa kwani nilikuwa naishi sehemu ya siri sana sasa sikujua amepajuaje
“Unajua nilipo mpaka useme nakuja kuchukuliwa” swali langu lilionekana la kipuuzi kwani alikata simu, nilitoka nje ili nijue kama hicho kitu ni cha kweli au alikuwa ananitania tu, nilishuka ngazi kwa wepesi nikatoka nje kweli sio muda niliona kuna gari nyeusi inafika hapo sikuwa na shaka niliingia ndani. Tulizunguka nyuma tu ya mtaa huo gari ikasimama kwa mbele alikuwa amesimama mwanaume ambaye alinipa mgongo ila nilimfahamu vyema nilitabasamu tu.
“Unaonekana kuwa mtu wa kutisha sana kama umefanikiwa kuweza kuijua sehemu ambayo ninaishi mtu kama mimi” niliongea huku nikiwa nasogea mahali alipokuwa akiendelea kuivuta sigara yake kubwa
“Haya maisha ni wajinga tu pekee ndio huwa wanajihisi wao wana akili kupita kiasi hasa pale wanapokuwa kati kati ya wajinga wenzao ila huwa ni tofauti kwa watu wenye akili sana kwao mjinga ndiye huwa anatumika kurahisisha kazi zao kupitia kujisifia kwake hivyo usije ukakaa ukajiona kwamba wewe unaishi kwa siri hata kidogo ni wajinga tu ndo wanajua hivyo ila kuna watu tunaweza kukupata muda wowote ule ambao tunataka sisi na hii ndiyo dunia tunayo iishi leo kila kitu kipo mkononi” alimaliza maelezo yake akinirushia kichupa cha pombe kali ambacho kwa kiasi fulani kingenipatia joto kutokana na upepo wa bahari uliokuwa ukivuma mpaka hayo maeneo.
“Hii ndiyo sababu serikali haiwezi kuwapata kirahisi sana watu kama nyie mna kila kitu cha kuwafanya muwe salama muda wote, kwa nchi hili jambo ni la kutisha kupita kiasi kama kuna raia tu wa kawaida wanaweza kuyafanya haya mambo bila vyombo vya usalama kujua inatishia amani ya nchi” nilimjibu huku nikikunja ndita kwa ukali wa pombe niliyokuwa nimepewa.
“Tatizo ni pesa, inapokuwepo pesa basi hakuna haki wala hakuna uzalendo, nchi haina pesa wanazishikilia watu wachache tu ambao wanafanikiwa kupata nafasi za juu unadhani kinatokea nini hapo, sisi tuna pesa nyingi sana, serikalini tuna watu wengi mno ambao ndio hao mnategemea waitengeneze nchi, mimi ukinikamata saivi baada ya saa moja tu baadae natoka nawewe unauawa unadhani ni kitu gani nchi itatufanya? Ujio wa pesa umebadilisha aina ya maisha ambayo wanadamu wa kawaida walitakiwa kuyaishi hivyo usipoteze muda sana kuwaza hilo jambo. Kesho ni siku ambayo unaenda kukutana na ndugu yako kwa mara ya kwanza tangu utoke nchini ni miaka sita nadhani imepita sasa, ni mwanajeshi sasa na ana nyota tatu kwa sababu yako tu kukubali kufanya kazi na serikali basi mwenzako naye anaishi vizuri kwa sasa, usijiulize nimejuaje nimekwambia hii nchi ipo kwenye mikono ya watu ambao wana uwezo wa kufanya jambo lolote lile na asiwepo mtu yeyote yule wa kuwazuia.

Hiyo siku ya kesho una kazi kubwa ya kulikomboa taifa lako kama ukishindwa basi hii nchi mtakuwa mmeikabidhi rasmi kwenye mikono ya watu ambao ninafanya nao kazi kwa sasa” maelezo yake yalikuwa yakinichanganya sana sikumuelewa vitu vyangu vingi namna ile ameweza kuvijua vipi ila nilifurahi sana moyoni kusikia ndugu yangu alikuwa na nyota tatu mpaka wakati huo ulipita muda mrefu sana bila kumuona wala kupata taarifa zake lakini hilo sikuliwaza sana kitendo cha kuniambia kwamba nilikuwa na kazi kubwa sana ya kulilinda taifa langu ndicho hicho kilichoweza kuniumiza kichwa sana huku yeye akiwa hana hata wasi wasi kwenye uso wake.
“Una maanisha nini kusema kwamba natakiwa nilikomboe taifa kwa mikono yangu mwenyewe?”
“Kesho raisi wa nchi anaenda kuuawa”
“Raisi anaenda kuuawa? Kivipi? Na nani anaenda kufanya hilo tukio?” maswali yalinitoka kwa mkupuo jasho likiwa linanitoka kwa kasi lakini yeye alikuwa anacheka sana
“Vipi unaogopa sana?” aliniuliza akiitupa sigara yake chini
“Unajua mimi nashindwa kabisa kukuelewa, uliniambia mheshimiwa raisi ndiye aliyekupa kazi ya kuisaidia nchi leo unaniambia raisi anaenda kuuawa nitakuamini vipi kwa hayo yote unayo yaongea?” nilimuuliza kwa hasira jina raisi huwa linapaswa kutajwa kwa heshima sana tofauti nayeye alivyokuwa akilitaja kiwepesi mno tena akisemea kifo cha mheshimiwa kwa urahisi sana namna hiyo
“Nadhani uliwahi kuathirika sana na madhara ya upigaji wa punyeto kwenye ukuaji wako hiyo michezo ni hatari kwenye kuwafanya watu kupoteza sana kumbu kumbu, kazi nilipewa na mkuu wa majeshi na ndiye aliye nikutanisha na mheshimiwa raisi ila hata hivi hilo halihusiani na kufa kwake” wakati huu sasa alinigeukia akionekana sura yake kuiweka kwenye hali ya usiriasi sana.
“Unamaanisha nini kuniambia hivyo”
“Nilikwambia unitafute mapema ukitoka kitandani lakini wewe ukapuuzia ni mwaka sasa ndo umenitafuta muda ukiwa umeenda sana, ungenitafuta mapema huenda hili ungekuwa umelizuia mapema sana kwa sasa sina imani sana kama utafanikisha ila jaribu kila linalowezekana kama utaweza kuifanya hiyo kazi. Huyu raisi aliyepo madarakani ni mtu ambaye anafanya baadhi ya mambo yetu kukwama hivyo kinacho fanyika ni kumtoa kwenye kile kiti na kumtoa kwake ni kumuua tu hakuna njia nyingine. Kesho majira ya saa nane usiku ndio muda ambao anatakiwa kufa kwahiyo kama mkishindwa kumsaidia mpaka muda huo keshokutwa asubuhi taifa litapokea taarifa mbaya sana hivyo ni kazi kwako wewe pamoja na wenzako wahini mapema kama mtalifanikisha hilo ila kumbuka tu kwamba wanao kuja kuifanya hii kazi ni watu wa kutisha na ni hatari mno” baada ya maelezo yake alianza kuondoka.
“Itakuaje kama hilo jambo litafanikiwa kukamilika?” swali langu lilimfanya akageuka tena pale nilipokuwa.
“Vyombo vya usalama mtakuwa kwenye hatari kubwa sana kwa sababu mtaonekana hampo makini na kazi yenu mpaka mheshimiwa raisi anauawa mkiwa mpo jiandaeni kwa hilo”
“Hili tukio limepangwa kufanyikia wapi? ili ikiwezekana ratiba zote za mheshimiwa ziweze kuvunjwa hiyo kesho”
“Bahati mbaya sana hata kama ungeipata nafasi huna hiyo nguvu ya kuweza kuzifuta ratiba za mheshimiwa raisi kwa nafasi uliyo nayo kumbuka umeingizwa kwenye usalama kiholela hivyo haujulikani. Hilo tukio linaenda kufanyikia ikulu”
“Haiwezekani, hakuna binadamu anayeweza kulifanya hilo tukio ndani ya ikulu hata kama angekuwa nani, hiyo ndiyo sehemu inayo lindwa zaidi kwenye ardhi hii inawezekana vipi raia afanye hilo tukio kule”
“Mhhhhhhhhh, hauna hata miaka mingi kwenye hiyo kazi ndo kwanza unaanza hiyo jeuri ya kupinga hicho kitu unaitolewa wapi? watu wanaiba mpaka benki kuu ya dunia ambayo ndiyo sehemu unapo hifadhiwa utajiri wa dunia nzima sasa kwenye nchi moja watashindwa? Usipende kukurupuka sana hasa kwa watu ambao huwajui, mna masaa ishirini na manne pekee ya kumkomboa kiongozi mkuu wa nchi. Kesho mchana kaonane na ndugu yako ukiwa kwenye sura tofauti na hiyo hautakiwi kujulikana kabisa kwa watu halafu baada ya kesho nitafute ni mhimu sana” alimaliza maelezo yake kisha akaangalia saa yake na kuingia kwenye gari ambayo ndiyo iliyokuja kunichukua kwangu na kupotea hayo maeneo.

Niliishia tu kuishuhudia gari hiyo ikipotelea kwenye barabara kuu, midomo yangu ilikuwa mizito kupita kiasi, mbele yangu nilikuwa nimepewa kazi ngumu mno ya kuweza kumlinda mheshimiwa raisi wa Tanzania ambaye sikujua nitamlinda vipi na kwa bahati mbaya sana tukio lilikuwa linaenda kufanyikia Ikulu, hakuna mtu ambaye ningemwambia hicho kitu akaniamini kabisa kwenye maisha yangu, nilitoa machozi na kukaa chini nilitamani sana kumsaidia raisi wangu mtu ambaye usalama wa nchi upo kuhakikisha yeye ndiye mtu wa kwanza anayekuwa salama kwa gharama yoyote ile na ndipo wangefuata wananchi.

Raisi atakufa kweli? Na mtekelezaji wa hilo tukio ni nani mwenye ujasiri wa kwenda kufanyia hilo tukio ndani ya Ikulu sehemu inayo lindwa kuliko kitu chochote kile kwenye nchi?.............29 natundika daruga uwanja umejaa maji ungana nami wakati ujao tena.

Bux the story teller
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA THELATHINI

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA..........

Niliishia tu kuishuhudia gari hiyo ikipotelea kwenye barabara kuu, midomo yangu ilikuwa mizito kupita kiasi, mbele yangu nilikuwa nimepewa kazi ngumu mno ya kuweza kumlinda mheshimiwa raisi wa Tanzania ambaye sikujua nitamlinda vipi na kwa bahati mbaya sana tukio lilikuwa linaenda kufanyikia Ikulu, hakuna mtu ambaye ningemwambia hicho kitu akaniamini kabisa kwenye maisha yangu, nilitoa machozi na kukaa chini nilitamani sana kumsaidia raisi wangu mtu ambaye usalama wa nchi upo kuhakikisha yeye ndiye mtu wa kwanza anayekuwa salama kwa gharama yoyote ile na ndipo wangefuata wananchi.

ENDELEA...........................


“Nina imani tayari ulishanijua na unanisikia vizuri sana mzee hivyo haina haja ya kuzunguka sana kwenye hili, mwanao yupo kwenye mikono yangu sina shida naye sana japokuwa dharau zake ndizo zimemponza mpaka yamemptokea haya, miaka kadhaa nyuma alionekana kunitafuta sana kitu ambacho kilifanya mpaka amuue rafiki yangu na kufanikiwa kunipiga risasi moja kwenye mwili wangu, sikuwahi kumuona baada ya hiyo miaka miwili nimemtafuta sana na kwa bahati mbaya alikuwa akitumia miili ya vijana wenye njaa wa mtaani kwa kuwatengenezea sura za bandia ili yeye awe salama, kushindwa kwake kunijibu maswali yangu marahisi sana ndiko kumempelekea yeye kuishia kuwa kwenye hii hali ambayo sikupenda sana tufikie huku lakini nimekuwa sina namna zaidi ya kuyafanya haya kwa mtu ambaye ameonekana kuwa hatari sana kwangu. Sasa mimi nahitaji tuonane ndani ya dakika tano zijazo maswali yake uyajibu wewe hapo vinginevyo likiisha lisaa limoja kabla hajapatiwa matibabu hatakuwa na nafasi ya kuwa hai tena kwa hali aliyokuwa nayo mpaka sasa, uamuzi ni wako kuamua kuyaokoa maisha ya mwanao au kuyaacha yateketee ndani ya dakika tano naisubiri simu yako baada ya hapo hautanipata hewani tena nadhani umenielewa vizuri sana” sauti nzito ndiyo iliyokuwa inasikika kwenye simu ambayo ilikuwa ipo mkononi mwa waziri mkuu akiwa anatetemeka sana, alibahatika kupata mtoto mmoja tu kwenye maisha yake, mkewe alikuwa amemuusia sana kumtunza mtoto huyo kwa nguvu zake yote na kwa gharama yoyote ile.

“Pumbavu sana, hivi ni nani ambaye kwenye hii nchi anaweza kuwa na huo uwezo wa kujiamini mpaka kufikia hatua ya kunitishia mimi bila kuwa na uoga wowote ule juu ya kile ambacho kinaweza kumtokea yeye na familia yake? Kama nikimkamata hakuna hata chembe ndogo ya familia yake itabaki hai amepita kwenye mikono yangu mwenyewe leo hii anakuja kunitishia hadi mimi hahahahaha nitamfanyia kitu kibaya sana” makamu wa raisi alikuwa anaongea kwa hasira sana akiwa ameikunja sura yake baada ya simu kukatwa, alichukia sana kijana ambaye hakuwa mgeni kwake kuwa na ujasiri wa kuweza kumpigia simu na kumtisha huku akimpa dakika kadhaa za kuweza kufanya maamuzi ya kukutana nae vinginevyo alikuwa anaenda kumpoteza mwanae wa pekee Ashrafu Hamad, alikuwa mwenye hasira mno alirudi kwenye marejeo ya zile video akihitaji kujua ni kipi kilikuwa kimetokea mpaka mtoto wake akamatwe kizembe sana namna hiyo. Video ilikuwa inaonyesha kwa usahihi tukio tangu Alexander anaingia humo ndani mpaka muda ambao Ashrafu aliwakataza walinzi wake kuingilia huo ugomvi alisikitika sana mzee huyu kwa sababu mtu ambaye mwanae alikuwa anang’ang’ania kupigana naye yeye alimjua vyema sana hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo na mpaka muda huo alikuwa anashangaa imekuaje mpaka mtu huyo yuko hai na anaishi.

Mapigano ambayo yalifanyika hapo ndani na namna mwanaume huyo alivyofanikiwa kukwepa risasi za zaidi ya walinzi 12 iliwafanya hata mlinzi wa makamu wa raisi mwili kumsisimuka, mwanaume huyo alikuwa anayajua mapigano kama aliyatengeneza yeye hakuwa na roho ya huruma kabisa kwenye mishipa yake tukio la kutisha lilipita kwenye macho ya makamu wa raisi wakati visu viwili vikipitishwa kwenye mkono wa mtoto wake na kumfanya kupiga kelele sana akihitaji msaada lakini hata walinzi wake hawakuwa na msaada tena baada ya kuweza kuachiwa sumu kali moshi ulijaa humo ndani kiasi kwamba hata kamera hazikuwa na uwezo wa kuchukua matukio hayo tena moshi ulipokuja kuisha hapakuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akionekana hapo. Makamu wa raisi aliipiga kwa ngumi skrini ndogo ambayo ilikuwa inasaidia kuonyesha matukio yote kwenye hizo kamera za ulinzi humo ndani kwa hasira na kuipasua.

“Bosi kwani huyu mtu unamjua?” swali lilitoka kwa mlinzi wake baada ya kuhisi kama hao watu walikuwa wanajuana hivi
“Huyu tumemtengeneza mwenyewe kwa mikono yetu, sio mtu wa kuombea kukutana naye kirahisi sana kwenye maisha yako hana ubinadamu pale alipo, mpaka sasa huwa tunajua alishakufa kwa sababu aliuawa nikiwa naona kwa macho yangu sasa mpaka leo nashangaa yupo hai ni kitu ambacho kinanipa wakati mgumu sana kuamini hili tukio kama ni la kweli au mimi ndiye nipo ndotoni” maelezo yake yalimfanya mpaka mlinzi wake ahisi kuchanganyikiwa inakuaje mtu ambaye umemshuhudia anauawa leo hii umshuhudie yupo hai tena wa afya tele hiki kitu huwa kinatisha sana na kwa mwanadamu mwenye roho nyepesi ya kawaida huwa hawezi kuhimili haya mambo. Aliinyanyua simu na kupiga hiyo namba ambayo muda sio mrefu alitoka kuongea nayo.

“Nije wapi?” aliongea kwa jazba akiwa na hamu ya kumtia Alexander kwenye mikono yake ili aweze kujua aliponaje na aweze kumuonyesha ni wapi ambako alikuwa amemhifadhi mtoto wake.
“Ukitoka nje ya huo mlango wa hiyo nyumba piga hesabu hatua tano kisha kunja kulia ukitembea hatua kumi simama nitakufuata ulipo, hakikisha unakuja wewe mwenyewe nataka tuzungumze kwa kina tukiwa wawili tu ukienda kinyume na hilo utakikuta kichwa cha mtoto wako” maelekezo hayakuhitaji kuelezewa sana moja kwa moja yalikuwa yanaeleweka kwa usahihi sana. Mheshimiwa makamu wa raisi alianza kutoka nje ya hicho chumba kwa mwendo wa haraka sana alihitaji kuyasaidia maisha ya mwanae kwa namna yoyote ile, mlinzi wake hakuwa tayari kuona hilo jambo linatokea kwa sababu kama mtu huyo angepata tatizo yeye ndiye ambaye angepaswa kuieleza serikali ni kipi kimetokea alianza kumfuata nyuma lakini alipewa ishara ya kuto mfuata mzee huyo.

“Mzee ni hatari sana kirahisi namna hiyo kwenda kwa mtu ambaye tayari alisha onyesha kila dalili za kuwa sio salama kwa maisha yako mimi siwezi kuruhusu hilo” mlinzi wake aliongea kwa msisitizo akionekana wazi hakuwa tayari kuruhusu hilo jambo lifanyike lakini alikatwa jicho kali mno na mzee huyo ambaye aligeuka na kuanza kutoka humo, mlinzi wake alikimbia kwa spidi akauweka mkono wake mbele ya makamu wa raisi huyo

“Bosi hatuwezi kukuruhusu kwenda huko nje bila kuhakiki usalama ambao utakuwepo huko hata kama ukit….” Hakumalizia sentensi yake alipigwa kofi moja kali kwenye shavu lake hata hivyo hata hakutikisika kilikuwa kitu cha kawaida mno kwake.

“Hivi wewe mpuuzi unaelewa hata nini maana ya familia wewe? ulishawahi kuwa na mtoto wewe? au unaropoka tu hapa vitu ambavyo huvielewi, hujui lolote kuhusu uchungu wa familia hapo ulipo unawaza tu ukidhani hayo mabunduki kila muda yanaweza yakatatua kila tatizo, huyo mtu mwenyewe ambaye yupo huko unamjua au unaropoka tu, nitokee mbele yangu nisije nikakupiga risasi bure unahisi mimi naweza kuuawa kirahisi sana kama unavyo fikiria hivyo mpuuzi wewe” aliongea kwa hasira sana mheshimiwa baada ya kuona mlinzi wake huyo haelewi maumivu yoyote yale pale mtu anapogusiwa familia yake anayo ipenda sana, aliyafuata maelekezo kwa usahihi sana na hatimae alifanikiwa kufika alipokuwa ameambiwa. Mbele yake chini ya mti ambao ulikuwa una majani marefu kiasi kwamba ukiwa mbali huwezi kuona kilichopo hapo chini ndani ya geti la nyumba ya mwanae ndipo alipo muona mtu akiwa anakizungusha kisu chake, Alexander alijisogeza mbele kidogo alicho kiona hakuamini hata kidogo hakuwahi kufikiria kama huyo mtu ndiye baba wa huyo mtoto ambaye mpaka muda huo alikuwa mkononi mwake, ni muda mrefu sana amemtafuta mtu huyu na hakujua ni lini atapata bahati ya kukutana naye maana moyoni alikuwa na kisasi naye kizito sana ila leo alikuwa yupo mbele yake uamuzi ulikuwa ni wake ni nini akifanye kwa mtu huyo japo sio kazi nyepesi kama inavyoweza kufikirika kirahisi.


Nilichanganyikiwa sikujua ni nani nitamfikishia ile habari akawa na uwezo wa kunisikiliza, hakuna mtu ambaye ungemwelekeza kwamba raisi anakuja kufia Ikulu akakuelewa kirahisi, sikuwa na namna nilienda kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa ambaye ndiye alikuwa mlezi wangu nilikuwa nina imani kwamba ndiye mtu ambaye angeweza kunisikiliza. Nilikutana naye na kumweleza kile kitu kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu niliona mzee yule akiyapuuzia maneno yangu nilimsisitiza sana kwamba hicho kitu kilikuwa cha kweli aliishia tu kuniambia kwamba nikapumzike tu hakuna binadamu ambaye alikuwa na huo uwezo wa kufanya tukio kama hilo, sikuwa na cha kufanya ukizingatia kwa wakati ule hakuna watu wengi ambao walikuwa wananifahamu nilikuwa agenti wa siri sana nilirudi nyumbani kwangu kinyonge sana nikiwa najua wazi mheshimiwa raisi alikuwa na maisha mafupi sana maana nilisisitiziwa kwamba kama tungepuuza ilikuwa ni lazima afe.

Jioni ile nilikuwa nimekaa kwangu nikiwa naangalia televisheni yangu wakati huo raisi huyo alikuwa ana mkutano na waandishi wa habari kuweza kuongea na wananchi wake kwani ulikuwa umepita muda mrefu sana bila kuongea na watu wake hao, alikuwa kipenzi cha watu na wengi walikuwa wakimtakia maisha mema kiongozi yule niliamua kuizima na kwenda kujipumzisha kitandani kwangu machozi yalikuwa yananitoka, nilijua wazi tunaenda kumpoteza mheshimiwa raisi kizembe sana kwa sababu hakukuwa na mtu ambaye aliyachukulia maanani maneno yangu, niliinua simu yangu na kumpigia tena simu mkurugenzi lakini jibu lake lilikuwa ni lile lile, nilichanganyikiwa siku hiyo sikukumbuka hata kwenda kumuona ndugu yangu ambaye ilikuwa imepita miaka sita bila kuonana. Nilipitiwa na usingizi nilikuja kushtuka majira ya saa tisa na nusu usiku moyo ulinienda mbio sana baada ya kukumbuka saa nane ndio muda ambao mheshimiwa raisi alikuwa anatakiwa kuuawa, nilikurupuka kitandani nikaiwasha televisheni yangu ila nilisikia milio ya gari za polisi nje zikiwa zinapishana kwa kasi sana, niliiangalia simu yangu ilikuwa na simu nyingi sana ambazo zilikuwa zimeingia kutoka kwa kiongozi wangu huyo niliinyanyua na kuipiga ambayo haikuchukua muda ilipokelewa nilikuwa nikitetemeka kwani sikuhitaji kukisikia kile ambacho nilikuwa nikikifikiria kwenye maisha yangu, alipokea simu akionekana wazi ni mtu aliye changanyikiwa sana alinihitaji nifike ikulu mara moja nilishituka sana kuambiwa hivyo kwa mara ya kwanza nilikuwa naenda kutia mguu wangu kwenye sehemu takatifu zaidi ndani ya nchi.

“Nilitoka nje haraka sana sikutaka kutumia gari yangu nilitembea kwa mguu kwa mbele kidogo nilibahatika kupata boda boda ambayo ilibidi nimuelekeze kupitia vichochoroni ili kuweza kutokea ilipokuwa ikulu hiyo ya nchi, alikuwa na wasi wasi alitulia baada ya mimi kumuonyesha kitambulisho safari ikaanza, wakati tunakaribia kufika karibu na maeneo ikulu ilipo tulipishana na msafara wenye gari zaidi ya ishirini za ikulu zikiwa kwenye mwendo mkali mno njia zote zilizuiliwa hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa anaruhusiwa kukatiza popote pale. Nilishuka na kumsihi boda boda yule atafute sehemu ya kujihifadhi asije akaonekane muda huo ingekuwa ni hatari sana kwake ule muda, nilimlipa pesa ngingi sana kisha nikaondoka, kwenye geti kuu la kuingilia Ikulu kulikuwa na ukaguzi wa kutisha ila kwa mimi nilishangaa baada ya kuonyesha tu kitambulisho sikukaguliwa kabisa nadhani taarifa yangu ilikuwa imefika kule mapema, kuna mtu alinipa ishara ya kidole nimfuate basi nilinyoosha kwenye jengo moja kubwa sana ambalo lilikuwa limejengwa kwa ustadi mno nilikuwa naishangaa sana ikulu ilivyokuwa sehemu nzuri mno, panalindwa sana kiasi kwamba hata sisimizi hawezi kukatiza bila kuonekana, tuliipita kordo moja ambapo ndani watu walikuwa na heka heka kibao wakiwa wamevaa nguo za usalama, tulipishana na mrembo mmoja ambaye alikuwa mapokezi aliniangalia sana lakini sikuwa na muda naye nilielekezwa mlango wa kuingilia kwenye chumba kimoja.

Baada ya kuingia nilifanikiwa kumuona kiongozi wangu ambaye alikuwa kama vile amechanganyikiwa, vitu vilikuwa vimevurugwa sana mle ndani
“Mzee” alishtuka baada ya mimi kumuita na kumpa heshima kwa kuinama sikuwa nikijua chochote mpaka muda huo aligeuka machozi yakiwa yamejaa kwenye macho yake.

“Ooooh damn it…. Mr President…… oooh my God” aliongea kwa sauti ya ukali akikaa chini, sikuwahi kumuona kwenye hali kama hiyo hata siku moja nilijua kutakuwa na tatizo kubwa sana

“What happened to Mr President (nini kimetokea kwa mheshimiwa raisi)?” swali langu lilikuwa zito sana kunijibu alitumia zaidi ya dakika tano ndipo akaufungua mdomo wake.

“He is no more (amekufa)” ……… Nani ameweza kufanya hili tukio sehemu yenye ulinzi kama hii kirahisi sana namna hiyo kumuua kiongozi mkubwa zaidi wa nchi tena akiwa ikulu?........ Alexander alifanikiwa kulipa kisasi chake kwa makamu wa raisi na kisasi chake kimetokana na nini?

Binafsi sina la ziada kwenye sehemu ya 30 sehemu zifuatazo zitatupa majibu zaidi ya nini kinajiri kwenye tamthilia moja nzuri sana ya kusisimua.

Langu jina naitwa Bux the

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Kwa shilingi 5000 tu isome hadithi hii mpaka mwisho kabisa sehemu ya 100 uweze kuiburudisha akili vya kutosha.

Namba za malipo ni

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

Ukituma pesa unatumiwa muda huo huo[emoji3578]

Wako

Bux the story teller

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Kwa shilingi 5000 tu isome hadithi hii mpaka mwisho kabisa sehemu ya 100 uweze kuiburudisha akili vya kutosha.

Namba za malipo ni

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

Ukituma pesa unatumiwa muda huo huo[emoji3578]

Wako

Bux the story teller

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Ofa ya leo tu kwa sababu ya kumuenzi Baba yetu wa taifa vipande vilivyobaki 62 ili kufika final sehemu ya 100 nakupatia kwa shilingi 4500 tu pekee.

Hivyo usijisikie unyonge kukaa mwenyewe nyumbani siku ya leo wakati Bux the story teller yupo kwa ajili yako.

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

lipia kwa hizo namba jina FEBIANI BABUYA.

Unapewa hadithi muda huo huo ili siku yako iishe vyema ukiupa ubongo burudani ya madini ya kutosha

Bux the story teller
 
Imalizie hadithi hii mpaka sehemu ya 100 kwa shilingi 4000 tu mpaka mwisho.

Hivyo usijisikie unyonge kukaa mwenyewe nyumbani siku ya leo wakati Bux the story teller yupo kwa ajili yako.

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

lipia kwa hizo namba jina FEBIANI BABUYA.

Unapewa hadithi muda huo huo ili siku yako iishe vyema ukiupa ubongo burudani na kupata madini ya kutosha
 
Kwa shilingi 4000 tu unaisoma yote mpaka mwisho sehemu ya 100.

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Jina

FEBIANI BABUYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…