I want to die a judge

I want to die a judge

Kwa
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE.......

Ni mkuu mpya wa magereza Lunyika Mwita ambaye alikuwa akimpa utaratibu wa kuishi ndani ya hilo gereza ambalo alikuwa amekabidhiwa na Denis Manoti, ni maelezo ambayo yalimfahamisha kwa usahihi ni namna gani anapaswa kuliishi hilo gereza ambalo mpaka muda huo alikuwa kwenye mshangao mkubwa hakujua lipo sehemu gani licha ya kujiuliza sana imewezekana vipi yeye kupatikana na kesi ya mauaji kwenye kesi ambayo hata hakuwa akihusika kwa namna yoyote ile na ndio hiyo ilikuwa imemfikisha pabaya ikiwa ndio kwanza alikuwa ameanza kazi yake ya kuitafuta haki yake ambayo ilikuwa imepotea.

ENDELEA..............................

Hakukuwa na cha nyongeza alivuliwa nguo zake zote na kupewa nguo mpya za pale ambazo zilichoka sana na hazikuwa nguo za kawaida bali yalikuwa ni magunia kabisa ambayo mara nyingi kwa nchi ya Tanzania huwa yanatumika sana kubebea zao la kahawa, namba 49 ndiyo ilikuwa namba yake ya hapo jela ni rahisi tu alielewa hiyo ndiyo idadi ya watu waliokuwa wanaishi ndani ya gereza hilo, komando mmoja alimfunga tena minyororo na kuanza kumuongoza kwenye selo ambayo ndicho kingekuwa chumba cha maisha yake yote ambayo alikuwa anaenda kuyatumikia hapo. Kulikuwa kimya sana humo ndani taa kali zikiwa zimewaka kila sehemu na kila mahali na kufanya kila sehemu kuwa kama mchana tu, upande wake wa kulia alisikia kilio kikali kwenye masikio yake aligeuka kuweza kujua ni kitu gani hasa ambacho kilikuwa kinaendelea humo ndani, kuna mwanaume alikuwa anakatwa mguu wake na msumeno alipiga sana kelele lakini hakuna aliyemsikiliza mpaka mguu wake ulipo maliziwa kukatwa, Jamal mwili ulimsisimka sana dunia aliyokuwa ameletwa ilikuwa inatisha mno tofauti na huko alikokuwa anatoka yeye alizoea kuona watu wakiwa wababe sana mtaani ila huku hakukuwa na mbabe ubabe wako ulikuwa unakupatia mateso ya kutisha na kukukatishia ndoto zako za kuwa mtu ambaye umeishi maisha marefu sana hapa duniani.

“Huyo alikuwa amemjibu msimamizi wake matusi ndiyo sababu amekatwa huo mguu wake kwahiyo hata wewe ukifanya kosa kama hilo lazima hayo yote yakukute” ni maelezo ya mwanaume aliyekuwa anamsisindikiza kwenye selo yake kwake aliongea jambo hilo kiwepesi mno na kulifanya la kawaida ila hata Jamal aliingiwa na uoga mno watu hao hawakuwa hata na chembe ya huruma aliona mtu yule anamwagia chumvi kwenye kidonda ili kuzuia damu isiendelee kutoka alimuonea sana huruma mfungwa mwenzake huyo ila hakuwa na kitu chochote kile ambacho alikuwa ana uwezo wa kukifanya.

Aliongozwa mpaka kwenye chumba ambacho alikuwa anatakiwa kuingia alionyeshewa tu ishara ya sehemu ambayo alikuwa anatakiwa kuingia kisha mwanaume huyo aliyekuwa anamsindikiza akageuza na kuanza kuondoka hiyo sehemu, chumba kidogo kiasi ndicho kilikuwa kwa ajili yake alisogea taratibu ili kuingia kwenye makazi yake mpya ila kabla hajafika hapo alisikia kwa pembeni kidogo mtu anaguna ilimbidi kugeuka alimuona mzee mmoja ambaye alikuwa amedhoofu sana maisha yake yalionekana kabisa kuwa ya wasiwasi mno, mzee huyo alibaki anamshangaa Jamal kwa muda mrefu kana kwamba ni mtu ambaye alikuwa anamfananisha kama sio kumjua, aliangalia huku na huko hakuona mtu yeyote yule akazamisha mkono wake kwenye gunia lake akatoa kalamu na kikaratasi kidogo aliandika kwa shida japo alifanikiwa kukimaliza pingu zikiwa mkononi mwake alikirusha kikaratasi hicho sehemu ambayo Jamal alikuwa amesimama ni wazi selo zao zilikuwa zinafuatana Jamal alielewa kwamba maeneo yanaweza yasiwe rafiki sana hivyo alikiokota kwa mguu wake kwa kutumia vidole vya mguuni kisha taratibu akaanza kuelekea pale palipokuwa na chumba chake huku akiwa haelewi mzee huyo kamjuaje.

Alisogelea nondo kali ambazo ndizo zilikuwa ni mlango hapo alishangaa wakati anaendelea kusogelea nondo hizo palijifungua penyewe na kujifunga tena baada ya yeye kuingia ndani, alirudi aone kama patajifungua tena lakini mlango haukufanya hivyo akajua basi ni lazima ni mifumo ambayo tayari ilishawekwa ambayo ilikuwa inaongozwa kwa umeme. Alikaa chini na kukitoa kikaratasi ambao alikuwa amepewa na mzee huyo ili ajue kimeandikwa nini “KESHO NI SIKU YA KUTOKA NJE YA VYUMBA VYETU KUNA SEHEMU HUWA TUNAENDA KUKAA HIVYO KESHO TUNAVYOTOKA HAKIKISHA UNASUBIRI KWANZA MIMI NITOKE KISHA NAWEWE UTATOKA UKIWA UNANIFUATA NYUMA KWA UMAKINI NA UJE KUKAA SEHEMU NITAKAYOKUWA NIMEKAA, HAKIKISHA HAUKOSI NAFASI HII NI YA KIPEKEE UNATAKIWA KUTOLEWA UPOFU AMBAO UPO KWENYE MACHO YAKO KUHUSU MAISHA YAKO” japo maneno yalikuwa hafifu sana ila alisoma na kuelewa vizuri sana, ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa kwenye hicho kikaratasi kitu ambacho kilimfanya ashangae mtu huyo yupo ndani ya jela na inaonekana ni muda mrefu sana yupo hapa sasa yeye kamjulia wapi? hivi vitu vya kuandikia anavitoa wapi wakati jela hatakiwi mtu yeyote yule kuweza kumiliki hivyo vitu alichoka sana hakuelewa ni kitu kipi alitakiwa kukifanya kwa muda huo ila aliamua kuwa mvumilivu kesho yake ifike akamuulize hayo maswali huyo mzee. Chumba alichokuwa kilikuwa na joto kali sana kitu ambacho kilimpelekea yeye kuweza kukosa kabisa usingizi asingeweza kulala kwenye chumba kama hicho ambacho kilikuwa kama kuna mtu anakoleza moto ndani yake.

Uwanja wa taifa ulikuwa umetengwa maalumu kwa ajili ya kuweza kuuaga mwili wa mheshimiwa makamu wa raisi, watu kutoka nchi za mbali pamoja na kutoka sehemu mbali mbali ndani ya nchi walikuwa wamehudhuria kuweza kumuaga mpendwa wao, taarifa ya mhusika kukamatwa kidogo ilileta faraja sana kwenye nyoyo za watanzania, wengi walisifia sana mtu huyo kuhukumiwa kifungo kikali cha mateso makali pamoja na kunyongwa baadae huku wengine wakisema alitakiwa anyongwe hadharani ili kuweza kukomesha matukio ya kigaidi ndani ya nchi hii yenye amani kubwa sana. Kwenye msiba huo hata Catherine alikuwa amehudhuria akiwa na nguo zake nyeusi sana ambazo ndizo huwa sare nyingi kwenye sehemu ya misiba hasa ile ya watu wakubwa, akiwa anaingia ndani kabisa ambako kulikuwa na foleni ya watu wengi sana aliiona sura ambayo bila shaka alikuwa akiijua japokuwa hakuwahi kuonana nayo kwenye maisha yake yote.

Upande wa pili alikuwa Rashid akiwa kwenye foleni akiwa kama mmoja ambaye alikuwa anaenda kuuga mwili huo wa mheshimiwa, suti yake na miwani ilikuwa ni ngumu sana kwa mtu yeyote yule kuweza kuugundua uwepo wa huyo mtu mahali hapo, kwenye mkono wake wa kulia alikuwa amevaa saa ndogo ambayo ilionekana kuwa ya gharama sana, huyo ndiye mtu ambaye Catherine alikuwa amemuona kwenye hiyo sehemu kwa mara ya kwanza aliona picha zake pale alipokuwa anatolewa na Jamal kwenye kituo kikubwa cha polisi cha OSTERBAY, ni mtu makini mno mwanamke huyu kwenye majukumu yake ya kikazi na ndiyo sababu kubwa sana ambayo ilimfanya baba yake aweze kumtumia kwenye kazi nyingi sana za siri za jeshi la nchi ya Cuba pale inapohitajika. Kwa kupitia miwani yake ambayo ilikuwa kwenye macho yake aliweza kukiona kioo kidogo kwenye saa ya Rashid ni kamera ndiyo iliyokuwa hapo hizo huwa zinatumiwa sana na majasusi wa usalama wa taifa kwa siri sana hata jeshi huwa halina taarifa kuhusu vifaa hivyo vya kutisha sana, alielewa kwamba mwanaume huyo hapo alikuwa kikazi alikuwa na kazi ya kumpata mtu huyo bila kumpoteza hapo uwanjani ambapo palikuwa na watu wengi sana. Alikuwa makini sana kumfuatilia huyo mtu kwa kila hatua Rashid alifika sehemu ambapo ulikuwa umelazwa mwili wa makamu wa raisi aliuangalia kwa umakini ni kweli alikuwa ni yeye mwenyewe hivyo alijifanya kama anajifuata machozi kwa kutoa miwani yake kumbe mwanaume alikuwa anaigeuzia kamera ya saa yake ambayo ilipiga picha za kutosha kwenye ule mwili kwa sekunde za kuhesabu tu, Catherine naye alipita haraka haraka miwani yake ikichukua picha za kutosha na kurekodi kila tukio lililokuwa linaendelea hapo ila akili yake kubwa sana ilikuwa inawaza asije akampoteza Rashid kwake alikuwa ni mtu wa mhimu sana kuliko hata ilivyokuwa kawaida.

Rashidi baada ya kufanikisha kile ambacho alikuwa amekifuata hapo alielekea moja kwa moja chooni na kupitiliza mbele ambako kulikuwa hakuna kitu kabisa na ndipo ulipokuwa uwanja wa uani kutokana na tukio lililokuwepo mlango huo ulikuwa wazi wakionekana tu maaskari akipita mmoja mmoja kuweza kudumisha ulinzi eneo hilo, alihisi kama kuna mtu anamfuata aligeuka kwa machale lakini hakuona mtu yeyote yuule hata hivi roho yake ilikataa kabisa aliamua kuingia sehemu na kujibanza, dakika moja baadae aliona kuna kivuli cha mtu alivyo ona kimesogea alijitokeza ili amshambulie mtu huyo ni kama yeye ndiye aliyeingizwa mtegoni alikutanishwa na goti la tumbo kisha akatupwa mbali na teke ambalo bila shaka mchongoko wa kiatu cha kike ulimchoma kifuani kwake, alijizungusha na kusimama mbele yake alikuwa amesimama mrembo mmoja ambaye asili yake alikuwa kama mweusi lakini weusi wake ulichanganyika na weupe kitu kilicho pelekea kuwa na rangi moja nzuri sana, maelezo huwa sio ya mhimu sana unapovamiwa na mtu ambaye humjui kujikusnya kwake nguvu alikuwa amepania kumuumiza mtoto mrembo sana namna hiyo, hii dhambi alikuwa anaenda motoni moja kwa moja ila cha ajabu alikuwa amdhaniye hakuwa ndiye mwanamke huyo alikuwa ana spidi ambazo kwa binadamu wa kawaida ni za kutisha mwanaume alikunjwa kama mtoto mdogo na mafunzo yake yote mwanamke huyo alikuwa hapigiki kabisa.

“Usipoteze nguvu zako bure kuna kazi nzito sana ya kuifanya unamjua Jamal?”

“Who are you? (wewe ni nani?)”

“Im Catherine from Cuba (naitwa Catherine kutoka Cuba)”

“What do you want from him? (unahitaji nini kwake?)” swali la Rashid lilifuatiwa na vitendo Catherine alitoa simu yake na kumuonyesha picha ambayo yeye alikuwa amekumbatiana na Jamal huku mwanaume akiwa kifua wazi, mwanaume alishtuka sana hakuwahi kabisa kwenye maisha yake ambayo alisimuliwa kuhusu Jamal kusikia ana mwanamke wakati huo alikuwa anaachiwa shingo yake ambayo ilikuwa imekunjwa sana na kumfanya aheme kwa taabu mno.

“What are you to him? (wewe ni nani kwake?)” hilo ndilo lilikuwa swali mhimu zaidi kutoka kwa Rashid

“Im his future wife (mimi ni mkewe mtarajiwa)” Rashid hakuamini hicho kitu ila hakuwa na namna kwa sababu mpaka picha alikuwa ameonyeswa maana yake mtu aliyekuwa amesimama mbele yake alikuwa ni shemeji yake na alipaswa kumheshimu sana, Rashid alimkadiria sana mwanamke huyo maana alikuwa ni mrembo mno hata yeye alikuwa na maswali mengi sana ya kuweza kumuuliza huyo mwanamke ila sehemu ambayo walikuwepo haikuwa salama sana kufanya mazungumzo ya siri

“Nifuate” ni kauli yake moja ambayo aliitamka huku akimrushia shemeji yake mpya mjini huyo kitambaa ambacho alitakiwa kujifunga usoni baada ya hapo walipanda kwenye ukuta na kutokezea barabarani, walivuka mpaka ng’ambo na hapo kulikuwa na pikipiki moja kubwa sana ambayo alikuwa amekuja nayo Rashid walipanda na kutoweka kwenye hilo eneo haraka sana.

Mtoni Kijichi ndiko safari yao ilikokuwa imeenda kuishia kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ni kubwa na ina geti refu sana, hawakupita getini walizunguka nyuma ya hiyo nyumba huko kulikuwa na mlango mdogo, Rashid aliweka jicho lake hapo mlango ukafunguka waliingia mpaka kwenye nyumba kubwa ambayo ndani yake ilikuwa na vitu vya thamani mno.

Ni kipi viumbe hawa walikuwa wamekifuata pale uwanja wa taifa na watagundua nini kwenye picha ambazo wamempiga makamu wa raisi?...... mchezo bado mbichi sana 55 niseme sina la nyongeza.

Bux the story teller
Kwa shilingi 2500 tu unaweza kuisoma hadithi hii mpaka mwisho sehemu ya 100.

lipia kupitia namba
0621567672 ( WhatsApp)
0745982347

zote jina FEBIANI BABUYA unaipata muda huo huo
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO.......

Mtoni Kijichi ndiko safari yao ilikokuwa imeenda kuishia kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ni kubwa na ina geti refu sana, hawakupita getini walizunguka nyuma ya hiyo nyumba huko kulikuwa na mlango mdogo, Rashid aliweka jicho lake hapo mlango ukafunguka waliingia mpaka kwenye nyumba kubwa ambayo ndani yake ilikuwa na vitu vya thamani mno.

ENDELEA.........................

“Is this your house? (hii ni nyumba yako?)” lilikuwa ni swali kutoka kwa shimeji yake, alitabasamu tu

“Welcome” alitamka kiufupi huku akiwa anaenda nje ambako bila shaka alikuwa anaenda kuichukua piki piki yake ili aweze kuiingiza ndani.

“Umewezaje kujua kama nipo pale na umenijulia wapi” swali la Rashid lilikuwa likakamilishwa na utoaji wa wine kali sana kwenye friji yake kubwa.

“Teknolojia ni kitu kilicho rahisisha mambo sana japo ndicho kitu cha hatari sana kwenye hii dunia ya leo inaweza kuondoka na maelfu ya watu, niliweza kuzipata picha ambazo mlipiga wakati unachukuliwa pale kituo cha polisi hivyo sura yako ilikuwa kichwani leo nilivyokuona tu pale nikawa nimekujua japo sikuwa na uhakika sana ila niliamua kuyaamini macho yangu na hisia zangu”

“Mhhhhhh upo makini sana kwenye kazi zako, nahitaji unijibu maswali matatu tu wewe ni nani? Tanzania umekuja kufanya nini na pale uwanjani umefuata kitu gani hasa?” kabla ya kujibu chochote Catherine kwanza alimimina wine kwenye glasi na kubugia yote huku akikunja ndita zake kuonyesha ilikuwa ni kali sana.

“Unamwamini sana Jamal? Mpaka umefika hatua ya kuniamini na kunileta kwenye makazi yako”

“Yule ndiye ndugu pekee ambaye kwa sasa naweza nikasema ninaye, mtu aliye tukutanisha na kutuweka pamoja ni mtu ambaye nilikuwa namwamini sana kuliko kiumbe chochote kile ambacho kimewahi kuzaliwa kwahiyo hata yeye namuamini sana kwa sababu ameishi kwenye mikono ya huyo mtu ambaye pia kanilea mimi”

“Naitwa Catherine mimi ni mchumba wake na Jamal nimeingia hapa siku ya jana baada ya kuzipata habari kwamba ameweza kukamatwa hivyo kuja kwangu hapa nilihitaji kujua nini chanzo cha haya yote kwa sababu hakuwahi hata siku moja kunipa baadhi ya taarifa ambazo nilianza kuzijua jana, kwa pale uwanjani nilikuwa nahitaji kuzipata picha za yule mzee ambaye inasemekana kwamba amekufa nahisi kuna mchezo unaendelea chini chini na ndicho kitu ambacho hata wewe nimeona unakifanya”

“Umejuaje kama nimekifanya hicho kitu?”

“Mwili wangu una silaha kila mahali hiyo saa yako sio saa ni kamera japo kwa nchi hii ni watu wachache sana wanaweza kulijua hilo”

“Naitwa Rashid mimi ni jasusi kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa la Tanzania” maelezo yake yalionekana kumshtua sana Catherine hakuwa na habari kama mtu huyo alikuwa ni mtu wa usalama

“Jamal anajua kuhusu hili?”

“Yes, anajua vipi kwani mbona umeshtuka hivyo?”

“Nimeshangaa mtu wa usalama unawezaje kukamatwa kirahisi sana namna ile na kupelekwa kituoni ambapo uliadhibiwa vikali sana maana nilikuona ukiwa na majeraha kwenye video ambayo niipata wakati unatolewa pale”

“Yes, mimi ni mtu wa siri sana na ndiyo maisha yetu ambayo huwa tunyaaishi kila siku ili kuhakikisha nchi inakuwa salama, sisi huwa tunatambulika kwa watu wachache sana na ndiyo sababu hata kutujua ni vigumu sana labda mimi ndo niamue kukwambia kama nilivyo kwambia wewe hapa. wengi mtaani ninakoishi wanajua mimi ni kijana ambaye napenda sana wanawake wenye pesa na ndio wanao nilea mjini, wanajua mimi ni kijana ambaye sipendi kabisa kazi wengine wananiita marioo na hayo ndiyo maisha yanayo nifanya nifanye kazi zangu bila kubughudhiwa kila mtu akinijua itakuwa ni hatari sana maana yake hata taarifa za siri zinaweza kuvuja kirahisi sana nje” alitulia kidogo na kuendelea.

“Jamal wakati yupo kupata mafunzo yake hakuwa Jamal wa sasa baada ya familia yake kuuawa yeye pekee ndiye aliyeweza kupona hivyo ili kumtengenezea mazingira ya kuto iumiza akili yake alichomwa sindano akiwa amezimishwa ambayo ilienda kumpotezeshea kumbukumbu zake zote za nyuma na kuenda kuyaanza maisha mapya kabisa mbali na jiji hili, huko siku ya mwisho ambayo alikuja kuambiwa ukweli aliambiwa kwamba ameishi miaka mitano tu pekee kitu ambacho hakikuwa kweli huko alikuwa ameishi kwa miaka saba aliondoka akiwa ana miaka 14 alirudishwa hapa mjini akiwa na miaka 21 na ndio muda ambao aliletwa huko Cuba kwa miaka miwili lakini wakati anakuja huko alikuwa tayari amefundishwa kila kitu kwa hiyo miaka saba ambayo aliishi milimani”

“Ni nani huyo ambaye aliweza kuondoka naye kwa miaka yote hiyo na kumpa hayo mafunzo?” Rashid alitikisa kichwa kuonyesha alikuwa akisikitika

“Huyo kwetu ni zaidi ya baba ndiye binadamu bora sana kwenye maisha yangu ila bahati mbaya sana hivi tunavyo ongea mimi nawewe ana siku kadhaa tangu azikwe, aliuawa kwa sumu kali sana mpaka sasa bado hatujajua ni nani aliye muua hilo litafanyiwa uchunguzi muda sio mrefu, huyu mtu alikuwa ni jasusi mkubwa sana ndani ya usalama wa taifa na ndiye aliyenilea na kuniingiza huko, huyu mtu alikuwa ndiye mlinzi mkuu wa familia ya Jonson Malisaba ambaye ndiye baba mzazi wa Jamal na yule haitwi Jamal jina lake halisi la kuzaliwa anaitwa Lenovatus Jonson hilo la Jamal alipewa baada ya kuondolewa kumbukumbu zake kichwani amekuja kujijua siku chache sana zilizopita”

“Daaah poleni sana nadhani mtakuwa watu wenye maumivu makali sana mpaka sasa”

“Yes, kila kitu huwa kinapangwa na MUNGU kwa kupitia wanadamu hata sisi ipo siku itafika tutakufa tu” Rashid alijibu akionekana wazi kutopendezwa na hiyo maada ambayo ilikuwa ikiendelea hapo, safari yake ilikuwa kwenda chumbani ambako alirudi na laptop yake ndogo.

“Jamal aliweza vipi kujulikana alipo? Na nani alimkamata?”

“Kwa taarifa ambazo nimepata kwa wenzangu wa usalama inasemekana kuna simu alipigiwa kwa mara ya mwisho kupewa maelekezo ya kutoroshwa nchini lakini kabla ya kufanikiwa kuondoka alitumiwa makomando kumi ambao wote walikutwa wakiwa kwenye hali mbaya sana hata yeye alikuwa kwenye hali mbaya mno inasemekana alichomwa na sindano zenye sumu kali sana kwenye kifua chake ndio ilikuwa pona pona yao baada ya yeye kulegea vinginevyo hakuna komando hata mmoja ambaye angeweza kutoka pale akiwa yupo salama”

“Nchi hii mmebahatika sana kupata mtu kama yule kama mngeweza kumtumia vizuri basi angewasaidia kwenye mambo mengi sana ila bahati mbaya naona hata kumtumia hamuwezi kabisa”

“Yaah unajua kwenye ulimwengu huu wa mashujaa kuna watu huwa moja kwa moja wanachaguliwa na MUNGU na yule jamaa nadhani ni miongoni mwa watu wachache sana ambao walitumwa duniani, ana kipaji kikubwa sana sijawahi kuona binadamu akipigana namna ile, nilibahatika kumuona siku amekuja kunichukua pale kituoni namna alivyo na kasi na uzito wa ngumi yake ilinifanya mpaka mimi nianze kumuogopa sana yule siyo mtu wa kupigana naye kama hauna watoto unaweza ukapotezewa kizazi kama atakupiga hata ngumi yake moja tu kwenye eneo la kiuno chako lazima itakuwa ni hatari kubwa sana kwa maisha yako na hao wanadamu wa hivyo wapo wachache sana ingekuwa huko kwenu basi yule angelinufaisha sana taifa ila huku kwetu ndiye mtu ambaye amepewa kesi ambayo ni wazi naona haina ukweli wowote ndiyo sababu nimeingia kazini nataka niutafute ukweli na nijue kuna nini kimetendekea hapa siwezi kukaa bora nife nikiwa nampambania mtu ambaye amejitoa kwa ajili yangu, na ana kazi nzito sana ya kumlinda dada yake” maelezo ya Rashidi yalimgusa sana mwanadada huyu japo ni kama kuna sehemu yalimchanganya hivi.

“Samahani umesema familia yake yote iliuawa sasa vipi tena unasema ana kazi ya kumlinda dada yake mbona sijakuelewa?”

“Yule hajazaliwa mwenyewe wapo wawili ni mapacha ukiacha dada yao Cleopatra ambaye hakuweza kupona siku ya mauaji, yeye anaitwa Lenovatus ila pacha wake anaitwa Octavian na ndiye huyo ambaye yeye yupo tayari kufanya lolote ili aweze kumlinda, hicho kitu hata yeye kiliwahi kumchanganya sana kwa sababu alikuwa anajua kwamba yuko pekeyake ila kwenye lile tukio dada yake alipona hakuweza kufa kama ilivyo semekana mwanzo” leo hii Catherine alikuwa anayajua mambo ambayo aliamini kweli ulimwengu una mambo mengi sana ya siri ambayo binadamu huwa hawajui na wanahisi wanayajua kwa usahihi sana kumbe wanaishia kujifariji tu.

“Huyo dada yake yuko wapi?”

“Yupo chini ya mikono ya muu wa majeshi”

“Whaaatttttttttttt?”

“Yes, ni jambo la kushangaza kidogo ila huo ndio uhalisia wenyewe, mtu ambaye amenilea mimi na kumsaidia Jamal ni pacha wa kuzaliwa kabisa wa mkuu wa majeshi”

“How is that possible? (hilo linawezekanaje?)”

“Hii ndiyo dunia ambayo tunaiishi wanadamu kuna baadhi ya watu wanaweza kufanya chochote wanacho kitaka na upo nao hapo hapo na huwezi kujua hili huwa ni jambo la siri sana na baba yake Jamal ndiye aliyefanikisha hilo jambo la kumfanya mtu huyo kuwa mkuu wa majeshi baada ya ndugu yake kujitolea kuweza kuilinda familia yake kwa maisha yake yote”

“Nadhani inatakiwa tumpate kwanza huyo ndugu yake ili tujue cha kufanya”

“Usiumize kichwa kwa hilo jambo huwezi kumpata hata ufanyaje”

“Kwanini?”

“Hiyo sehemu aliyopo inadaiwa kuwa salama zaidi kama kuna mtu yeyote yule akaweza kumtambua basi lazima atauawa”

“Sasa kama mkuu wa majeshi ni mtu wenu wa karibu hivyo kivipi uniambie kwamba Jamal alikamatwa na makomando, maana makomando hawawezi kufanya kazi bila amri ya mkuu wa majeshi na ndiye pekee anaye wajua sasa hili linawezekanaje?”

“Hata mimi nimejiuliza sana hilo swali ninaanza kuwa na mashaka sana na yule mtu maana hata siku tumetoka kwake ambayo ndiyo siku tuliyo toka kumzika ndugu yake ndiyo siku ambayo nilikamatwa kupelekwa kituoni maana yake hao watu walijua wazi sehemu ambayo nilitoka”

“Hii ni hatari mno Octavian inabidi atafutwe kwa namna yoyote ile huenda huko aliko hakuna kabisa usalama wowote ule na anaweza kupotea kizembe sana kama suala hili likichukuliwa kawaida" Mezani kulikuwa na picha kubwa sana kwenye laptop ambayo ilikuwa ikimuonyesha makamu wa raisi akiwa ndani ya jeneza lake, picha ilikuzwa vizuri sana kwa kutumia miwani yenye lenzi kali sana aliyokuwa nayo Catherine alimpatia na Rashidi aweze kuangalia, mwanaume bila kuuliza aliichukua na kuiweka machoni pake kitu ambacho alikiona kilimshangaza mno, alilegea sana mdomo wake ukiwa wazi ni wazi wazi dunia ambayo alikuwa anaishi ilimtisha sana na alijiona hakuna kitu chochote ambacho anakijua kuhusu huu ulimwengu dunia ni chumba chenye siri kali mno funguo za chumba hiki wanazo wanadamu wachache sana wenye nguvu kubwa ya pesa na michezo ya akili.

Kipi kimemtoa macho kijana mdogo kama huyu kwenye huu ulimwengu wa wajuaji??.....56 inafika mwisho ungana namimi wakati ujao.

Bux the story teller
Leo tunasoma viwili so naongeza kingine hapa saivi
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA SABA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SITA.......

“Hii ni hatari mno Octavian inabidi atafutwe kwa namna yoyote ile huenda huko aliko hakuna kabisa usalama wowote ule na anaweza kupotea kizembe sana kama suala hili likichukuliwa kawaida" Mezani kulikuwa na picha kubwa sana kwenye laptop ambayo ilikuwa ikimuonyesha makamu wa raisi akiwa ndani ya jeneza lake, picha ilikuzwa vizuri sana kwa kutumia miwani yenye lenzi kali sana aliyokuwa nayo Catherine alimpatia na Rashidi aweze kuangalia, mwanaume bila kuuliza aliichukua na kuiweka machoni pake kitu ambacho alikiona kilimshangaza mno, alilegea sana mdomo wake ukiwa wazi ni wazi wazi dunia ambayo alikuwa anaishi ilimtisha sana na alijiona hakuna kitu chochote ambacho anakijua kuhusu huu ulimwengu dunia ni chumba chenye siri kali mno funguo za chumba hiki wanazo wanadamu wachache sana wenye nguvu kubwa ya pesa na michezo ya akili.

ENDELEA...........................

Masaa yalikuwa yanaenda taratibu sana kwa upande wa Jamal lakini hata hivyo asubuhi ya siku ya pili yake ilifika, hamu kubwa ambayo alikuwa nayo moyoni mwake ilikuwa ni kwenda kumuuliza mzee huyo ili ajue ni kipi hasa ambacho yeye anakijua kwenye maisha yake kama alivyoweza kuandikiwa kwenye karatasi ambayo alipewa. Ni muda ambao hata hakujua ni saa ngapi kwani hilo eneo ilikuwa huwezi kujua kama ni usiku au ni mchana kiufupi ni kwamba walikuwa wapo kwenye dunia yao wenyewe watu hawa, alisikia milio ya milango hiyo ya chumba ikifunguka alichungulia hakuona mtu alisogea mlangoni alishangaa unafunguka aliangalia pande zote hakuona mtu dakika moja baadae aliweza kumuona yule mzee ambaye jana yake alimpatia kikaratasi, alikuwa amechoka sana inaonekana ni uimara wa mifupa yake ndio uliokuwa unafanya anatembea mpaka muda huo, basi taratibu alianza kumfuata kwa nyuma mpaka sehemu ambayo ilikuwa na chumba kikubwa kilichokuwa na sehemu yenye maji yaliyokuwa yamezungushiwa vioo vigumu sana ndani yake walikuwa wakifugia samaki humo ndiyo sehemu ambayo kidogo huwa wanakuja kuzipumzisha akili zao japo hakuna cha maana chochote ambacho huwa wanakiwaza pindi wanapokuwa humo ndani zaidi ya kusubiria kufa tu.

“Kila nikikuangalia nakumbuka mbali sana, umri unazidi kwenda miaka inazidi kukatika na binadamu ndivyo wanavyozidi kubadilika kila inapo itwa leo, pole sana na karibu kwenye hii dunia ya ulimwengu mwingine ukiwa bado ni mdogo sana” ni sauti ya mzee huyo ambaye ndiye aliyeweza kumuandikia ile karatasi siku ya jana na kwa wakati huo walikuwa wamejitenga kwenye moja ya kona ya hicho chumba kikubwa ambamo walikuwa wamekusanyika wote.

“Mzee kwani mimi unanifahamu?”

“Ndiyo” jibu la yule mzee lilimshitua sana Jamal hakuamini mtu huyo yupo huku ndani na anasema anamjua vizuri.

“Umekaa huku kwa miaka mingapi?”

“Keshokutwa natimiza miaka ishirini na minane ndani ya hili gereza bila kuuona mwanga wa jua wala kuona namna dunia inavyo enda huko nje”

“Mzee mbona unanichanganya, hivi unajua mimi nina miaka mingapi?”

“Kwa sasa ndo unaelekea kutimiza miaka ishirini na minne” Jamal alishtuka na kutaka kuondoka hiyo sehemu alianza kumuogopa huyo mzee haiwezekanai mtu awe ndani ya jela kwa miaka ishirini na minane halafu leo anamjua yeye kwa kila kitu mwanadamu wa hivyo hata uwe jasiri vipi hauwezi ukakubali kabisa kuwa naye karibu ni watu hatari mno.

“Kaa chini hicho unachotaka kukifanya kitakufanya ujutie sana hapo baadae hao watu ni wabaya sana ambao wanatulinda humu ndani ukionekana ni mtu mwenye mashaka mashaka nadhani jana umeona mwenzako anatolewa mguu hicho ndicho kitu ambacho kitakukuta” hakuwa na haraka kabisa mzee wa watu Jamal alikaa chini huku akitetemeka alikuwa hajiamini tena mbele ya mtu huyo.

“Wewe ni nani mzee?” aliuliza midomo yake ikiwa bado ni mizito sana.

“Baba yako ni moja kati ya watu wenye bahati sana kuwahi kuishi kwenye uso wa dunia hii, kupotea na kuacha damu ambayo inafanana naye ni jambo la kumshukuru sana MUNGU”

“Baba yangu alishakufa sasa unasemaje alikuwa ana bahati kubwa?”

“Yes, najua ndiyo kwamba amekufa unahisi sijui? dunia imegawanyika sehemu mbili kuna sehemu ambayo wanaishi matajiri na sehemu ambayo wanaishi maskini lakini hawa wote huwa wanaunganishwa hapa katikati na watu hatari sana kuwahi kuishi kwenye ulimwengu huu hapa nawazungumzia watu wenye akili, hawa ndio watu hatarishi duniani hapa kuwahi kuishi wanatisha sana wakiamua kulifanya jambo lao, wanaweza kukipata kitu chochote kile ambacho wao wanakihitaji na wengine wamebahatika sana wamepewa akili nyingi mno pamoja na utajiri wa kutisha hili ndilo jambo linalo itishia dunia kwa sasa, ila pole sana nasikitika tangu umerudisha kumbukumbu zako hujawahi hata kumuona dada yako” Jamal alikuwa akiyapima maneno ambayo mzee huyu alikuwa akiyaongea lakini hakumuelewa kabisa kichwa chake kilikuwa kinauma sana alishindwa kutambua huyu ni mtu wa aina gani kwake.

“Tangu lini umejua kuhusu sasa dada yangu mzee?”

“Mhhhhhhhh kwani wewe unajua dada yako alipo?”

“Hapana”

“Sasa kwanini unaniuliza swali la kijinga sana namna hii? kama nimeweza kujua miaka ambayo nimeishi kwenye eneo kama hili ambalo halina hata mwagaza wa jua kujua leo ni lini, hujiulizi kwanini namiliki kalamu na naandika vizuri tu ndio maana hata wewe umeweza kuupata ujumbe wangu. Pesa ni kitu cha ajabu sana kuwahi kukishuhudia kwenye maisha yangu, watu wengi sana huwa wanafarijiana kuhusu hili jambo ila kiuhalisia kwenye maisha ya leo hakikisha unaimiliki hata ya kukutosheleza wewe na familia yako na ukaweza kukidhi mahitaji ya kifamilia na ya kwako pia. Kwenye chumba changu huwa ninachora kila muda na kwa umakini sana ambao hakuna mtu anaweza kujua, walisha nifuatilia mara nyingi sana wakaja kugundua hakuna cha maana zaidi ya kunidhihaki kwamba nina ugonjwa wa akili ndiyo sababu huwa naishia kuwacheka sana moyoni kwa sababu ule ukuta nimeandika mambo yangu ya mhimu yote na kila tarehe ya kila siku huwa naiandika ndiyo sababu mimi ndiye mtu pekeyangu humu ndani ninaweza kujua kwamba leo ni jumatatu, kesho ni jumanne hakuna mwingine yeyote ambaye anaweza kukupa hilo jibu. Sasa nataka uniambie umekamatwa vipi mpaka uweze kuletwa huku” Jamal leo alikuwa amekutana na kichwa ambacho hata moyo wake ulikiri kwamba kama angekuwa anasoma mtu huyo basi kwa dunia hii ya leo angekuwa miongoni mwa watu wenye akili zaidi kuwahi kutokea duniani ila bahati mbaya sana akili kubwa kama hii ambayo ilitakiwa moja kwa moja kuweza kutumiwa na taifa ilikuwa ipo kwenye sehemu kama hii.

“Nimepewa kesi ya kuweza kumuua makamu wa raisi wa nchi, sikufanya tukio lolote ila nilishangaa tu mahakamani naonyeshwa video ambayo inanionyesha mimi kufanya tukio kama hilo ambalo hata halikuwahi kutokea kabisa nimeogopa sana” Jamal alijibu huku akitokwa na jasho usoni.

“Yes, ilikuwa ni lazima iwe hivyo ndiyo sababu nimekwambia kuna viumbe ni hatari sana kuwahi kuishi kwenye huu ulimwengu ila kuna mtu mmoja pekee ndiye anaye nufaika na hiki kitu kuna wengi sana wanaingizwa sehemu mbaya bila wao kujijua na hapo baadae wao wenyewe wataanza kugeukana”

“Unamaanisha akina nani?”

“Achana na maswali ya kitu ambacho unakijua, mkufu wako uko wapi?” Jamal ni kama alihisi hakusikia vizuri ila alishangaa mzee huyo alikuwa amemkazia macho kumaanisha alicho kiongea alikuwa anamaanisha sana

“Mkufu, umejuaje kuhusu kuhusu hili?” alishangaa mzee huyo alionekana kumjua kupita kiasi kuliko hata yeye alivyokuwa anafikiria

“Haujanijibu nilicho kuuliza”

“Mkufu upo ila nimeuficha mahali salama sana ambapo hakuna mtu anaweza kuuona”

“Unajua kwanza hata kilichopo ndani ya ule mkufu?”

“Hapana”

“Ule mkufu ndicho chanzo cha mambo yote haya ambayo unayaona yanatokea”

“Kivipi?”

“ Ile ni funguo ya sehemu moja nyeti sana japo hiyo sehemu kama ikifunguka itategemea na mtu atakaye kuwa wakwanza kuifungua, kama hao wanao utafuta sana watawahi kuufungua kabla yako basi nchi hii itakuwa kwenye mkono wao na wataweza kuiendesha vile wanataka wao ila kama wewe ndiye utakaye wahi kufungua hiyo sehemu basi hii nchi itakuwa salama sana kwa asilimia miamoja” leo kwa mara ya kwanza alisikia neno kubwa sana likitamkwa kitu alichokuwa anashinda nacho kwenye shingo yake ndiyo iliyokuwa funguo ya sehemu ambayo ilikuwa ni mhimu sana na ndicho chanzo cha hayo mauaji ambayo yalikuwa yanatendeka ndani ya nchi hii.

“Ni watu wangapi ambao wanajua kuhusu hili jambo?”

“Walikuwa wanne ila kwa sasa wamebakia watu wawili tu pamoja namimi ni wa tatu kuna baba yako na Timotheo Jordan ambao wote kwa sasa hawapo duniani, kwa waliobaki ukinitoa mimi mmoja wao ni mmiliki wa kampuni kubwa ya M96OWNER’Z huyu hajulikani kabisa kwenye macho ya watu huwa anawatumia watu wengine kabisa kwnye nafasi yake anaye mjua mtu huyu ni makamu wa raisi peke yake sijamfuatilia sana ila ni mtu ambaye ameishi sana ndani ya nchi ya Japan kwa muda mrefu sana japo ni mtanzania kwa kuzaliwa na mwingine ndiye binadamu hatari zaidi ambaye anaishi kwenye nchi hii anamiliki karata tatu nadhani kwenye mkono wake, huyu hautakiwi kukutana naye kwenye maisha yako yote akiwa kwenye sura yake halisia ni mtu ambaye kwenye nchi hii hakuna binadamu hata mmoja ambaye anaweza akasimama naye kwenye suala la mapigano, ni mwanadamu hatari sana ila anaishi kwenye sura nyingi sana nadhani zipo tatu na pia ndiye mwanadamu mwenye akili zaidi kuwahi kuzaliwa kwenye nchi hii, ni mtu ambaye hata wewe huwezi kumdhania kabisa na ni mtu anaye julikana nchi nzima” vitu vipya alikuwa anavisikia leo Jamal kwenye masikio yake vilikuwa vikimchanganya mno bado mpaka muda huo alikuwa ana maswali mengi sana kwa mzee huyu hakumjua ni nani mpaka sasa lakini alikuwa akimpa siri za mambo makubwa sana ambayo hata yeye aliyekuwa anapigana hiyo vita yake hakuwahi kuyajua kabisa.

“Ni nani huyo mtu”

“Nicolous Philemone ndilo jina lake, huko nje mnamjua kama mwanasheria mkuu wa nchi ya Tanzania”

“Hapanaaaa, hapaaana hapana hapana umekosea sio yeeye sio yeye na hawezi kuwa yeye, licha ya mimi kuishi kwenye sehemu za hovyo sana wakati nakua na nilikuwa nimepoteza kumbukumbu lakini huyo mtu namjua sana na jana tu alikuwepo mahakamani kwenye kesi yangu, ni mdhaifu mno huyo mtu hawezi kuwa yeye” Jamal aliona kama ni kichekesho mwanaume aliyekuwa akizungumziwa kwenye macho yake alikuwa ni mdhaifu sana aliamini kabisa mtu kama yule hawezi kuwa hatari kwa namna yoyote ile hata iweje ilikuwa ni kitu ambacho hakikuwezekana kabisa.

Hii ni dunia ambayo wanaishi wanadamu wanaotisha sana ndani yake naogopa hata kuendelea kuandika[emoji22]

57 niweke nukta nimeshindwa kabisa kuendelea[emoji2768]

Bux the the story teller

Ahsante sana Kazi nzuri Bigup
 
Hii ni dunia ambayo wanaishi wanadamu wanaotisha sana ndani yake naogopa hata kuendelea kuandika😢

57 niweke nukta nimeshindwa kabisa kuendelea🖊️

Bux the the story teller
Hello fam, najua mna arosto za kutosha tusameheane sana nilikuwa offline kwa siku mbili hatuja isoma kabisa hivyo kaa mkao wa kula sio muda inakuja naleta kurasa mbili kufidia juzi na jana. Lakini pia kwa ofa ya christimas unaweza kuisoma kwa 2000 tu yote mpaka mwisho kwa siku ya leo.

Mery christmas
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA.......

“Hapanaaaa, hapaaana hapana hapana umekosea sio yeeye sio yeye na hawezi kuwa yeye, licha ya mimi kuishi kwenye sehemu za hovyo sana wakati nakua na nilikuwa nimepoteza kumbukumbu lakinu huyo mtu namjua sana na jana tu alikuwepo mahakamani kwenye kesi yangu, ni mdhaifu mno huyo mtu hawezi kuwa yeye” Jamal aliona kama ni kichekesho mwanaume aliyekuwa akizungumziwa kwenye macho yake alikuwa ni mdhaifu sana aliamini kabisa mtu kama yule hawezi kuwa hatari kwa namna yoyote ile hata iweje ilikuwa ni kitu ambacho hakikuwezekana kabisa.

ENDELEA.....................

“Hiyo ndiyo sababu kubwa niliyo kwambia huyo ndiye binadamu mwenye akili zaidi kuwahi kuishi kwenye nchi hii, ni mtu mkatili na hatari sana ni bora ukutane na risasi hata kumi mwilini mwako unaweza ukabahatika kupona ila sio kukutana naye huyo mwanadamu akiwa kwenye uhalisia wake ni kiumbe wa kutisha mno mimi huwa namuogopa kuliko kitu chochote kile, huyu ndiye yupo nyuma ya michezo yote inayo endelea na hakuna mtu yeyote anaye jua, na kama unasema kwamba yeye alikuwepo mahakamani basi huo ushahidi uliokufunga lazima ameutengeneza yeye mwenyewe” Jamal alitoa macho sana, umdhaniae kumbe ndiye siye, wanadamu ni watu wa kuwaogopa sana, wanatisha sana na ni hatari kupita kiasi. Watu wanazizika siri kwenye mioyo yao na hakuna mtu anaweza kuzipata hakuna mtanzania ungeweza kumwambia akakuamini kwamba huyo mvaa miwani huyo ni mtu hatari sana dunia imebadilika sana siku hizi.

“Huyu mtu haya mambo amejifunzia wapi?”

“Siku ukitoka humu ndani unatakiwa umtafute mtu mmoja ambaye ndiye anaishi na dada yako”

“Hey hey sorry umesema mtu anayeishi na dada yangu kivipi wakati dada yangu yupo kwenye mikono ya mkuu wa majeshi”

“Daaah pole sana ulikuwa unaenda kuteketea vibaya sana bila kujua, tuna muda mchache wa kuendelea kukaa hapa uchague moja nikupe hadithi ya maisha ya dada yako au yakwangu mimi” swali alilo ulizwa lilikuwa kama mtihani kwake alihitaji kujua vyote lakini muda haukuwa rafiki kabisa kwao hivyo suala la dada yake ndilo lililokuwa la mhumu zaidi hapo.

“Nahitaji kujua hicho ambacho sikijui kuhusu dada yangu”

“Ule usiku ulikuwa ni usiku wa kutisha sana kwenye familia ya mzee yule ambaye alijulikana kama Jonson Malisaba, baada ya familia nzima kuuliwa nawewe ukachukuliwa na Timotheo Jordan pale kwenye familia yenu hakuna hata mmoja ambaye alipona zaidi yako wote walikufa kitu ambacho wewe ulienda kuambiwa kwamba dada yako amepona pale ni uongo mkubwa sana na ni kitu ambacho kilitengenezwa tu kukuaminisha vitu ambavyo havipo hapa duniani”

“Unajaribu kumaanisha nini mzee kwamba dada yangu alishakufa?” joto lilikuwa limempanda sana Jamal machozi yalianza kumshuka tena kwenye macho yake hadithi ilikuwa inabadilika kila dakika saivi tena alikuwa anaambiwa kwamba dada yake hakupona siku ile alikufa pale pale

“Mkiwa na siku mbili tangu mzaliwe dada yako aliondolewa kabisa pale kwenu ila kilicho fanyika alichukuliwa mtoto mwingine hospitalini akawekwa kwenye nafasi ya dada yako”

“Whaaaaaaat? Kwanini ifanyike hivyo na dada yangu yuko wapi?”

“Dada yako yupo kwenye mikono yangu ambayo na yule ambaye uliambiwa ni dada yako ni uongo kwa sababu wote walikufa ile sehemu pale”

“Where is my sister (dada yangu yuko wapi?)”

“Wakati mnazaliwa kwa kazi ambayo baba yako alikuwa akiifanya ya kuisaidia serikali ilikuwa ni hatari sana hususani kwa mtu mwenye familia kama yeye hivyo alijua wazi ipo siku moja watu watakuja kuiua familia yake yote kitu kitakacho pelekea yeye kukosa kabisa familia kwa baadaye, kwa sababu mimi ndiye mtu ambaye nilimshauri kwa siri sana aweze kulisaidia taifa namimi ndiye niliyeweza kumshawishi mheshimiwa raisi aweze kumuomba Jonson kwa pesa ambazo aliachiwa na yule baba yake mlezi wa kihindi aweze kulisadia taifa lake kweli hakuweza kupinga kabisa kuhusu hilo alikubali na wakati huo nyie kabla hata hamjazaliwa alikuwa ana mtoto mwingine ambaye aliuawa baadaye ndipo alipokuja kukutana na mama yenu haya mambo ni siri kubwa sana ndio maana kwenye historia yake hakuna anayejua kwamba mimi ndiye niliye enda kumuomba aweze kulisaidia taifa wanajua ni mkuu wa majeshi na mheshimiwa raisi wa wakati ule. Ni mtu ambaye nilikuwa nakutana naye kwa siri sana kiasi kwamba raisi pekee na mkuu wa majeshi ndio waliokuwa wanajua hiyo siri hata kijana wangu mwenyewe Timotheo hakuwahi kabisa kujua hiki kitu, kulingana na hiyo kazi ambayo alikuwa akiifanya aliniomba kwamba kama ingetokea akapata watoto basi mtoto mmoja sisi ndio tumlee ili asije baadaye akakosa familia nzima. Akiwa kwenye hilo kampuni ambalo mimi ndiye niliye mpelekea hilo wazo la kujiunga nalo ili kuokoa kizazi hiki ndio muda ambao ulipangwa mpango wa kuweza kumuua mheshimiwa raisi aliyekuwa madarakani kwa wakati ule” ni siri nzito sana ambazo siku ya leo Jamal alikuwa anazijua alikuwa akitetemeka sana hakuyaamini macho yake.

“Unamaanisha ulikuwa ukijua kwamba raisi atauawa?”

“Yes, nilikuwa najua na ndio maana kama kiongozi mkuu wa usalama sikuweza kuweka ulinzi wa kutisha sana siku ile”

“Kipi kilikufanya uyatoe maisha ya raisi sadaka kirahisi sana namna hiyo”

“Raisi ilikuwa ni lazima afe ili siri iendelee kuwepo, baadaye walikuja kumpata mtoto wake ambaye alizaa nje ya ndoa na ndiye huyo huyo aliyekuwa amempata, watu hao walimshika mtoto huyo na kutishia kumuweka hadharani kwa kutoa taarifa kwamba raisi amezaa nje ya ndoa hicho kitu kingemharibia sana sifa yake mzee yule hivyo alikuja kuwa tayari kuwapa taarifa zote, kumbuka kulikuwa na watu wawili kwenye hilo kampuni ambao walikuwa wanahitaji maslahi tofauti bila kujuana, mmoja alivyo ona wenzake wanaweza kumzidi ndiye aliyefanya maamuzi ya kumuua raisi, hivyo nilivyojua hicho kitu nilikubali raisi afe na lawama zote nikakubali kuzibeba. Asingekufa maana yake siri zote zingejulikana na baba yenu angeuawa kabla hata nyie hamjazaliwa. Baada ya nyie kuzaliwa mtoto mmoja alichukuliwa ambaye ni wa kike wakati huo mimi nilikuwa nipo jela kwa miaka minne ila kila kitu nilikuwa nakipanga vizuri sana mtaani kinafanyika, baada ya nyie kuzaliwa mapacha mmoja wa kike ambaye ndiye dada yako tulimchukua na huyo mwingine ndiye akaingizwa pale, hata mama yako mzazi amekufa akiwa halijui hili zaidi ya baba yako tu ambaye amekubari kufa na siri yake moyoni. Hivyo siku watu wale wanakuja kufanya mauaji kwenye familia yako pale hakuna hata mmoja ambaye aliopona wote walifia pale pale.

Dada yako mimi sijawahi kumuona kwa macho yangu zaidi ya kuonyeshwa picha zake tu ila anaishi kwa kutumia pesa zangu mimi, kila kilichokuwa changu nimemmilikisha huyo mtoto, sijawahi kumuona ila ninampenda kuliko kitu chochote kile kwangu ni zaidi ya mwanangu na sina mtu mwingine yeyote kwenye nchi hii zaidi yake, kwa sasa amemaliza masomo yake ya chuo kikuu kwenye chuo cha KENYATA UNIVERSITY nchini Kenya jina lake anaitwa Dinorious au Natasha ukipenda waweza kumuita hivyo” Jamal hakuelewa kama amshukuru huyu mzee au afanye nini alikuwa ni mtu mhimu sana kwenye maisha yake hapa ndipo alikuja kuelewa kwamba huyu ni miongoni mwa wale watu watatu ambao aliachiwa maagizo na Timotheo Jordan kwamba awatafute mtu ambaye alikuwa ndani ya gereza alilowahi kuambiwa alifungwa kwa sababu ya uzembe wa kusababisha kifo cha raisi alikuwa ndiye huyu mzee aliona kabisa hakuwa na cha kumlipa mzee huyo.

“Sasa kama ni hivyo mkuu wa majeshi ni nani?”

“Yule anaitwa Antony Mlipa ni mtu wa Sumbawanga huko, moja kati ya makosa ambayo Timotheo Jordan aliyafanya ni kuweza kuaminishwa uongo, ndugu yake baada ya kuipata nafasi kutoka kwa baba yako ni kweli alikuwa ni mkuu wa majeshi lakini aliuawa muda mrefu sana, yule pacha wake ambaye yeye alidhani anamuona alikuwa ni mtu wa kutengenezwa tu kwa akili ya kawaida ya mwanadamu na walikuwa wanasema kwamba wamemhifadhi dada yako ili wakipate wanacho kihitaji, bahati kubwa sana kwa Timotheo aliweza kuificha hiyo siri ya kuwa na huo mkufu mpaka siku anakukabidhi vinginevyo angeingia kichwa kichwa sana, huyo mtu pale aliwekwa tu na huyo mwanasheria ambaye wewe umesema ni mlaini sana na ndiye mtu anaye icheza hii michezo, yule siyo mkuu wa majeshi ambaye mnamdhani nyie huyo alishakufa muda mrefu sana, ila hakikisha ukitoka hapa unaenda kumuona mdogo wako atakuwa mpweke sana tukionana siku nyingine utaweza kuniuliza tena pale ambapo unahisi patakuwa pamebakia wewe kuweza kupajua” mzee wa watu alikuwa amekaa sana alinyanyuka taratibu akamdondoshea Jamal kikaratasi ambayo kilionekana kuwa kigumu kwa namna ambayo hakuna mtu yeyote yule angeweza kujua wala kugundua na kuanza kuelekea mahali ambako ilikuwa ipo selo yake wakati huo Jamal alibaki anamwangalia mzee huyo bila kummaliza kabisa kama alikuwa ni binadamu wa aina gani, alikumbuka siku anakutana na wale makomando simu ya mwisho alipigiwa na mkuu wa majeshi na alimwambia asizime simu wala kuondoka bila yeye kumruhusu wakati anapanga kumtorosha nchini kumbe alikuwa anajua kila alichokuwa anakifanya na ndiye aliyewatuma hao watu waweze kumkamata, alikumbuka vyema hata pale mahakamani mzee huyo alikuwa akiongea na simu huku akifurahi sana wakati huo yeye anapelekwa gerezani, uchungu ulimjaa sana kwenye moyo wake aliapa kama angeweza kumkamata huyo mzee basi angemfanya kitu ambacho hakuna mwanadamu angetamani kukiona kwa mwanadamu mwenzake, aliokota kile kikaratasi kigumu na kukikunja kwenye gunia lake akisubiri afike kwenye selo yake ili aweze kujua kama hicho kitu kilikuwa ni nini hasa.

“Nooooooooooo hili ni jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye maisha yangu sijawahi kupigwa hata na mtu mmoja mimi ndiye mtu pekee ambaye niliweza kuingia kwenye Ikulu ya nchi mpaka nikatoka salama bila mtu yeyote yule kuweza kuniona au kunijua inakuaje leo nifanyiwe kitu kama hiki na binadamu wa kawaida sana hapaaaaaaanaaaaaaaaaa” ilikuwa ni sauti kali ya uchungu kutoka kwa Alexander alikuwa na hasira laiti kama kuna mtu angetokea karibu yake basi asingeweza kumuacha salama lazima angemuua, kwenye maisha yake hakuwahi kupigwa hata siku moja yeye ndiye mtu ambaye alikuwa akiogopeka sana kwa kuyatenda matukio ya kutisha mno leo alikuwa amepigwa kizembe sana tena na mtu ambaye yeye mwenyewe alisadiki kumuita ni mtu wa kawaida sana mbele yake sasa aliwezaje kumpiga? Ni swali ambalo yeye mwenyewe alikuwa anajiuliza hapati jibu, alikipasua kioo kwa hasira ambacho ndicho kilikuwa kinaonyesha alama yake ambayo alikuwa nayo kwenye paji la uso wake kushuka mpaka kwenye shavu lake la upande wa kulia likiwa na damu nyingi sana, hakuwa na uhakika kama watu wataweza kumchukulia kama kiumbe wa kawaida sura yake ilikuwa imeharibika sana, moyo wake ulikuwa unamuenda mbio mno unaweza ukadhani kuna mtu anakoleza moto ndani yake alikuwa na hasira kali.

“Nitabaki hivi hivi mpaka siku namuua huyu mwanaharamu” alijiongelesha tena mwenyewe kisu chake kikali akikizamisha kwenye ukuta ambao ulikuwa ni mgumu mno lakini kilizama bila wasi wasi wowote ule kuonyesha ukamilifu wa nguvu nyingi ambazo alikuwa nazo kwenye mkono wake kiumbe huyu. Kumbukumbu zake zilirudi siku kadhaa nyuma ambapo alifika kwenye nyumba ambayo alikuwa anaishi Deodata waweza kumuita Black Widow na kukuta mauaji yamefanyika hapo akaamua kummalizia Ashrafu Hamad kwa risasi tano za kichwa wakati huo alikuwa na uchungu sana wa kuchukuliwa dada yake, alichukua gari na kuondoka kwa ghadhabu akiwa njiani kwenye simu yake uliingia ujumbe “NJOO MACHINGA COMPLEX HAPA KARUME KWENYE GHOROFA LA JUU KABISA SAA 4 USIKU UKIKOSA DADA YAKO UMEMKOSA” maneno yalikuwa yameandikwa kwa herufi kubwa kuonyesha msisitizo wa hicho kilichokuwa kinaongelewa hapo na namba iliyokuwa imemtumia ujumbe huo ilikuwa ni ngeni kabisa kwake hakuwahi kuwa nayo wala kuiona, alipiga usukani wa gari yake kwa hasira sana baada ya kujaribu kupiga simu mara kadhaa lakini namba hiyo haikuweza kupatikana.

Wasakana kuonana?.....sina usemi nakuachia wewe ndo unipe comment yako....

58 ngoja nipumzike kwanza...sina lingine 59 tukutane

Bux the story teller
59 inakuja now then tuelekee kwenye mialiko, enjoy

Wasalaam

Bux the storyteller
 
Dah...umetuachia maswali zaidi...inawezekanaje akawa gerezani kisha akawa ana Alex kwenye mtanage ama ni flashback kabla hajenda gerezani? Tusanue FEBIANI BABUYA hapo kesho kwenye kufungua mabox[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuwa mvumilivu mkuu utaelewa kila kitu na hilo tukio kumbuka Alexander anakumbuka akiwa mbele ya kioo akiwa na alama ya bisu usoni ndo anakumbuka kilicho mkuta, umakini unahitajika mkuu utaachwa
 
Tukutane baadae sehemu ya 63, ni kali mnooooooo kuna mkono wa kufa raia, ni hatari sanaaaaa, vuta kiti tupate kidogo chakula cha ubongo hiki. I'll be back.

Wasalaam

Bux the storyteller
 
Shukrani [mention]FEBIANI BABUYA [/mention] kazi nzuri…Ila umetusahau kidogo
 
Back
Top Bottom