I want to die a judge

I want to die a judge

STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA SITINI NA TATU

TULIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA MBILI.........

Alifumba macho yake na kutulia ili kuuweka mwili sawa kwa utulivu masikio yake akitulia yalikuwa yanaweza kusikia vitu vingi sana kuna sauti alianza kuzisikia hazikuwa za kawaida hata kidogo usalama wa hilo eneo ulionekana kuwa mdogo sana, aliyafumbua macho yake na kujaribu kuchungulia nje kulikuwa na kiza kikali ambacho kwa siku kadhaa tangu afike hapo hakuwahi kukishuhudia na aliambiwa hiyo sehemu taa huwa hazizimwi hata sekunde moja kwanini umeme uzime muda kama huu akili yake iligoma kabisa kuweza kukubaliana na jambo kama hilo alisimama taratibu hatua za ujio wa watu wakiwa wananyata aliweza kuzisikia vizuri sana japo alishindwa kutambua wapo wangapi. Mlango wa chumba alichokuwepo ulisikika kwa mbali ukionekana unajivuta kufunguka hakuelewa imewezekanaje kwa maana unatumia umeme na kwa muda huo umeme ulikuwa umekatika.

ENDELEA..............................

“Una machaguo mawili hapa utuelekeze hicho kitu umekiweka wapi au tukutie ukilema uweze kutueleza kwa lazima” ni wanaume watatu ambao walikuwa wameingia kwenye hicho chumba mmoja wao alisikika kwa usahihi akiwa anaongea hiyo kauli mikononi mwao wawili walikuwa na vishoka na mmoja alikuwa ameshika upanga mkali ambao hata kizani ulikuwa unang’aa sana, hakuna jibu walilo lipata humo ndani.

“Hayupo mbali naisikia harufu ya jasho lake lazima yupo karibu sana hapa hapa” mmoja wao aliongea huku akiwa yupo makini kuchungulia kwenye kila pembe ya hicho chumba ila alihisi kama kuna mtu nyuma yake aligeuka kwa nguvu akiwa anaulazimisha mkono wake ambao ulikuwa na uzito kazaa aliirusha shoka yale ulisikika mlio mkali ikonekana kuna chuma kinakatika wenye meno madhaifu lazima wangehisi meno yao yanauma kwa kelele ya kuburuza chuma ambayo ilisikika, shoka hilo lilimkosa Jamal kwenye paji lake la uso na tumboni lilienda kukata minyororo ambayo ilikuwa ipo kwenye miguu yake mpaka ikakatika inamaanisha kama hiyo shoka ingetua hata mguuni basi huo mguu ungeweza kuokotwa vipande vidogo vidogo. Kamali ambayo Jamal aliicheza ilihitaji binadamu wajasiri kupindukia alisikia minyato ya hao watu alijirusha akajiviringisha na kwenye kunasa kwenye ukuta wa juu ndani ya selo wakati wanafika aliamua kutua nyuma ya mtu wa mwisho kabisa ambaye bado alikuwa yupo karibu na mlango akijua wazi mtu huyo atageuka kwa nguvu na silaha yake mkononi kama akigeuka kwa nguvu atamsaidia kupunguza hizo nyororo na hesabu zake zilifanikiwa kwa asilimia kadhaa.

“Mbona na usiku ndugu zangu mnataka nini mpaka mnawinda roho ya kijana mdogo kama mimi kwa mambo ambayo yanaweza kuzungumzika?” Jamal alikuwa akiwaongelesha ili kujipanga na kuwasoma vizuri kwani hakuwa na uwezo wowote ule wa kuweza kuwajua kwenye hilo giza japo alihisi ni wale watatu ambao kuna muda waliingizwa kama wafungwa wapya gerezani hapo.

“Fuata kile ulicho elekezwa kwa mara ya kwanza unaweza ukaipata nafasi ya kuishi tena” sauti moja ambayo ilitoka kwenye mdomo ambao ilipita zaidi hata ya mwezi bila kuujua mswaki ilitamka na kuacha harufu mbaya humo ndani.

“Huo mdomo wako unanuka sana ni vyema ukatafuta mwanamke wa kukufanya ukumbuke namna mwanaume anavyotakiwa kujiweka, hicho mnacho kitafuta mpaka kukipata inabidi watolewe sadaka watu wengi sana ndipo kipatikane hata nyie najua mmetumwa na hamna uwezo wa kuniua kwani na nyie mtauawa hahahahhaahahah” Jamal alikuwa ananunua muda kwa hao wanaume ili awasome aligundua hakuna aliyekuwa na wasiwasi hata mmoja. Ngumi ilitoka gizani aliiona bila shaka kwa mwanaume ambaye yeye alimpa kauli mbaya sana kumwambia atafute mwanamke ikiwa inakaribia kwenye uso wake aliikwepa kwa kurukia pembeni ambayo ilienda kugonga kwenye nondo na hakuwa na imani kama mkono ndio umevunjika au nondo kwenye mkono wake alikuwa bado ana minyororo ni miguu pekee ndiyo ilikuwa imefunguliwa hakupewa nafasi pale aliporukia alipigwa na kisigino ambacho kilimzoa mpaka ukutani alidondoka chini akiwa anatoka damu mdomoni. Hakuelewa ngumi zinapigwa muda gani alikuwa amepokea ngumi zaidi ya sita kwenye hilo giza ambazo zilimfanya ahisi nafsi inamtoka matokeo yake hakufa ila maumivu ndiyo aliyapata vya kutosha mpaka alijuta kuongea jeuri mbele ya wanaume wa kazi. Mwanaume mmoja alimbeba kwa nguvu na kumrusha juu sarakasi za kuvutia kwenye giza zilichezwa na wanaume wawili ambao walimbamizia ukutani na wateke yao manne ya pamoja, kifua chake kilikuwa kinawaka moto watu ambao alikutana nao walikuwa wana roho mbaya unaweza ukadhani hawakuzaliwa na binadamu wenzao.

“This is my time (huu ni muda wangu)” ni sauti ambayo ilionyesha wazi mtu huyo alikuwa kwenye maumivu makali ilisikika wakati wanaume hao wakiwa wanapongezana kwa kupeana tano kazi yao ilikuwa nyepesi kupitiliza, wote walishangaa walihisi huenda wamesikiana vibaya wenyewe ila kwa mbele walihisi kabisa kuna mtu ambaye amesimama. Mwenye upanga ndiye aliyetangulia upanga ukiwa umetangulizwa mbele paja lake lilipokea maumivu ya kutisha ambayo hakuweza kuyakabili aliunguruma akigugumia kwa maumivu hilo lilienda sambamba na kuinama chini kidogo mguu ulikosa balansi hesabu yake ilimalizwa na mguu uliokuwa peku ulikomaa kama mawe ya mlimani hakuongea neno lolote tena aling’ata ulimi wake huyo hata kuongea tena kwenye maisha yake ilikuwa kama ndoto alibaki anajirusha rusha pale chini hatimaye alitulia. Shoka ilikuwa inakuja kwa spidi, ukali wake uliifanye itoe mwanga mweupe kiasi Jamal aliiweka mikono mbele ili kama inamkata uso wake uwe salama MUNGU alikuwa upande wake shoka iliishia kwenye minyororo ambayo ilikuwa mkononi ilikuwa ni bahati mbaya kwa hawa wanaume ambao walikuwa wamebaki wawili humo ndani sasa alikuwa yupo huru kabisaaa mikono na miguu yake alijinyoosha kidogo kisha akainama na kuishika hiyo shoka.

Mmoja wao alisikika akitoa kilio kikali sana ndani ya hicho chumba hali iliyopelekea wafungwa wote kuweza kushtuka humo ndani shoka ilikuwa imepasua mguu wake sehemu ya goti na kuwa vipande viwili, umeme ulirudi ghafla sana kutokana na hizo kelele mwanaume alisogea kwa yule aliyekuwa chini analia kwa maumivu ya kupasuliwa mguu wake kama kuni mwenzake alikuwa ameyatoa macho akiwa pembeni bila kuongea wala kusogea shoka ilichomolewa maamuzi ya haraka sana Jamal aliinyanyua juu na kuukata huo mguu maeneo ya juu ya goti ukilema wa maisha ulikuwa umemvaa huyo mwanaume nadhani alijutia sana kuwafahamu wanadamu halafu anacheza nao vibaya. Shoka ilirushwa kwa yule mmoja aliyekuwa amebaki ilimkosa shingo na kwenda kukita kwenye ukuta alitetemeka mpaka shoka ambayo yeye ndiyo aliyokuwa ameishika kwenye mkono wake ilimdondoka aliinama na kuokota upanga wa mwenzake wa kwanza ambaye alipigwa kikatili kwenye kiza na kujing’ata ulimi akafia hapo hapo, aliokota upanga huo na kujizamishia kwenye tumbo lake yeye mwenyewe mpaka makomando ambao walifika hapo baada ya kusikia zile kelele walibaki wanashangaa baada ya kufika ndani ya hiyo selo, haikuwa kawaida mwanaume imara kama huyo aweze kuchukua maamuzi ya kujiua kirahisi sana namna hiyo walijiuliza sana ila wakati wanageuza macho yao mmoja alikuwa yupo chini amekufa, mmoja mguu ulikuwa kando ya mwili wake na alionekana anahema kwa mbali huyu ambaye alijichoma na kisu tumboni alikufa baada ya dakika moja. Jamal alikuwa ameiweka mikono yake nyuma akiwa hana mnyororo hata mmoja.

“Huyu kilicho muua ni hofu, hofu ndio udhaifu mkubwa sana kwa mwanadamu ukiwa sehemu yoyote ile halafu hofu ikakuingia hauwezi kufanya kitu chochote kile kama upo ni kwenye uwanja wa vita basi tafuta nafasi ya kuweza kukimbia kwa sababu vinginevyo lazima utajikuta unakufa kizembe sana mpaka wewe mwenyewe baadaye unaweza ukaanza kujilaumu na kujiona kama vile umekuwa mjinga. Mtu hatari kama huyu mpaka kachukua haya maamuzi maana yake ameshuhudia mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyafikiria kwenye maisha yake kabisa Professor Daniel alitueleza kwa undani sana wa hili jambo nilipokuwa kwenye chuo kimoja cha siri cha kiintelijensia huko Florida Marekani wakati tunafundishwa kuhusu saikolojia ya mwanadamu” ni mmoja wa makomando aliyekuwepo alikuwa anawaambia wenzake wakati ametoka kumpima mwanaume huyo na kumkazia macho Calvin wote walibaki wanamshangaa yeye alikuwa amefumba macho yake, hakuna aliye muongelesha wala kufanya chochote walimuacha huru na mikono yake alikuja kushtuka na kufumbua macho baada ya kusikia sauti ya nondo zikijifunga watu watatu waliokuwa wamekuja humo ndani na akafanikiwa kutoka salama mmoja ambaye alikatwa mguu na shoka miili yao ilikuwa imetolewa, Jamal hakuweza kuamini aliachwa bila kufungwa alikaa chini na kuwaza sana mpaka pale alipokuja kupitiwa na usingizi kwa mara nyingine tena.



Ilikuwa imepita siku moja tangu mwili wa mheshimiwa makamu wa raisi uweze kupumzishwa, watu walikuwa bado hawajamaliza stori za taarifa hizo mitandaoni zilianza kuzagaa tena habari nyingine za kuweza kupotea kwa manasheria mkuu wa nchi, KIZINGITI CHA KUTISHA CHAITIKISA SHERIA TANZANIA hilo ni gazeti moja lilikuwa limeupamba ukurasa wake siku ya asubuhi kama kawaida ya magazeti yetu jinsi yanavyopenda kuzipamba habari ili kuweza kuwavutia wasomaji. Watu walikuwa wanashangaa imekuwa vipi mtu juzi tu hapo wamemuona kwenye kesi ambayo ndiyo ilikuwa inatikisa nchi nzima leo awe ametekwa, waunganisha nukta za mistari na kuweza kutunga hadithi zao walikuwa tayari wameshayaunganisha matukio moja kwa moja walihusisha kukamatwa kwa Jamal pamoja na tukio hilo wengi wakidai kwamba lazima ni kundi la Kigaidi ambalo linashirikiana na Jamal ndilo lililoweza kumteka mwanasheria wao, wengi walilaani sana wakidai ni vyema Jamal atolewe jela aje auawe hadharani mbele ya watu wote au vinginevyo aeleze mwanasheria wao yuko wapi.


Raisi alikuwa amewaka sana hilo jambo lilikuwa linaenda kumharibia sana jina lake mtu huyo alikuwa mkubwa sana ndani ya taifa hili ilikuwa ni lazima apatikane ili aendelee kujisafishia njia ni siku mbili tu nyuma watu wametoka kumsifia baada ya kuweza kumkamata gaidi mkubwa ambaye aliweza kuondoka na maisha ya makamu wa raisi leo alihitaji kuendelea kulipata jina zaidi kwa kuwapofua macho wananchi wake wasiweze kuujua uhalisia na Ngozi yake halisi yeye yupoje.

“Umesema Colombia?”

“Ndio mkuu”

“How?”

“Hata sisi tumeshangazwa sana na hilo jambo mpaka sasa hatujajua imekuaje”

“Hizo taarifa mmezipatia wapi?”

“Ndani ya usalama wa taifa vijana wangu wameweza kutumiwa hizo taarifa na picha ambazo zinaonekana namna alivyoweza kupigwa huko aliko” mheshimiwa raisi alikuwa kwenye chumba chake cha mkutano akiwa na mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa aliongea huku akiwa anamuonyesha mheshimiwa picha hizo pamoja na video ambazo zilirekodiwa kwa lugha ya kikolombia video ikionyesha namna upanga ulinyofoa vidole viwili vya mwanasheria mkuu bila kuwa na huruma, watu hao wakiwa wanahitaji shilingi bilioni miambili za kitanzania mpaka raisi alishtuka sana.

“Heeey wanahitaji pesa zote hizo za nini?”

“Nadhani wanajua umuhimu wa mtu huyo kwenye nchi ndio maana wamefanya hivi kwa sababu wanajua kwa vyovyote vile nchi lazima imkomboe lasivyo wananchi watahitaji viongozi wa juu ikiwemo wewe wajiuzulu”

“Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani siwezi kuruhusu kirahisi namna hiyo itoke pesa kwa ajili ya mtu mmoja kama huyo ni bora afie huko huko bilioni miambili hivi wana akili kweli hawa kwanza nahitaji ripoti kamili huyu mtu ametekwa vipi wakati ana ulinzi wa kutosha. Una majasusi kibao kwenye taasisi yako watumie hao kuweza kumsaidia vinginevyo ni bora afe siwezi kusaini pesa yote hiyo itoke kwa ajili ya mtu mmoja” mheshimiwa raisi alikuwa anafoka kwa hasira pesa kwake kilikuwa ni kitu kikubwa mno hakuwa tayari kuipoteza pesa nyingi kiasi hicho eti kisa tu kusaidia maisha ya mtu mmoja kwake ilikuwa ni bora mtu huyo afe ila sio kupoteza pes azote hizo, mkurugenzi wa usalama wa taifa alimimina maji na kumpa kiongozi wake huyo kwa heshima ili atulize hasira kwanza wasije wakaharibu kila kitu.

What next? Mchezo bado unachezwa, niseme tu 63 natundika daruga sina la ziada

Bux the story teller
UNAWEZA KUZISOMA HADITHI ZANGU KWA WAKATI KUPITIA GROUP LANGU LA WHATSAP AMBALO KUJIUNGA NI SHILINGI 3000 TU KWA MWEZI. NAMBA ZA KUTUMA HIYO PESA

0621567672 (WhatsApp)
0745982347
zote jina FEBIANI BABUYA

Ungana na kalamu yangu kusupport kipaji na kazi lakini pia tuweze kuburudika pamoja.

Wasalaam,

Bux the storyteller
 

Attachments

  • 311593142_126840016830488_4281158983162031384_n.jpg
    311593142_126840016830488_4281158983162031384_n.jpg
    34 KB · Views: 38
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA SITINI NA NNE

TULIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA TATU..............


“Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani siwezi kuruhusu kirahisi namna hiyo itoke pesa kwa ajili ya mtu mmoja kama huyo ni bora afie huko huko bilioni miambili hivi wana akili kweli hawa kwanza nahitaji ripoti kamili huyu mtu ametekwa vipi wakati ana ulinzi wa kutosha. Una majasusi kibao kwenye taasisi yako watumie hao kuweza kumsaidia vinginevyo ni bora afe siwezi kusaini pesa yote hiyo itoke kwa ajili ya mtu mmoja” mheshimiwa raisi alikuwa anafoka kwa hasira pesa kwake kilikuwa ni kitu kikubwa mno hakuwa tayari kuipoteza pesa nyingi kiasi hicho eti kisa tu kusaidia maisha ya mtu mmoja kwake ilikuwa ni bora mtu huyo afe ila sio kupoteza pes azote hizo, mkurugenzi wa usalama wa taifa alimimina maji na kumpa kiongozi wake huyo kwa heshima ili atulize hasira kwanza wasije wakaharibu kila kitu.

ENDELEA................................



“Mheshimiwa wazo lako la kuwatumia majasusi ni zuri sana lakini litachukua muda mrefu kukamilika kama unavyo wajua huwa wanahitaji wawe na uhakika na jambo wanalolifanya kwa asilimia miamoja ndipo waweze kufanya maamuzi sasa hiyo inaweza kupelekea muda kwenda sana tukachelewa wananchi hawawezi kuelewa hilo itaonekana serikali hakuna kazi tunafanya ebu lifikirie hilo mheshimiwa” maneno ya mkurugenzi wa usalama yalionekana kumuingia kiasi chake mheshimiwa raisi kichwani alimgeukia na kumuuliza mtu wake huyo.

“Nini kinahitajika?”

“Nadhani hili jambo tumkabidhi mkononi mkuu wa majeshi”

“Kivipi?”

“Yule anamiliki makomando ambao wana uwezo mkubwa sana tunaweza tukawapata kama watano ambao wataenda kama kupeleka pesa kwenye hilo eneo kisha baada ya hapo watawaua hao watu wote hapo watakuwa wameua ndege wawili kwa jiwe moja pesa zitakuwa salama na mheshimiwa atakuwa salama na cha kuongezea tu begi halitawekwa pesa bali zitawekwa nguo kwahiyo haitoki hata mia mbovu” viongozi siku zote huwa wanapenda sana kufanya kazi na watu ambao wapo imara na uwezo mkubwa sana kichwani, wazo la mkurugenzi wa usalama wa taifa lilimfanya raisi atoe meno yake yote 32 nje alimpiga piga begani kuonyesha wazi anaunga hicho kitu.

“Hahaahahaah sikufanya makosa kabisa kukuweka kwenye hiyo nafasi ebu mpigie simu mkuu wa majeshi mwambie namhitaji ikulu kwa dakika thelathini awe hapa haraka sana” kauli ya raisi haijawahi kuwa ombi hata siku moja huwa ni amri ndicho kilicho fanyia mkurugenzi wa usalama wa taifa alinyanyua simu yake na kuipiga kwa kiongozi mwenzake wa usalama ambaye alishangaa mtu huyo kumpigia usiku wa saa nane huo, alimjibu kwamba alikuwa amechoka na kazi hivyo wangeonana siku ya kesho ila baada ya kusikia ni raisi anamuita alinyanyuka kama anakimbizwa akiahidi ndani ya dakika ishirini atakuwepo ikulu, raisi alikuwa anajimiminia wine na kufurahia ni wazi tumaini jipya lilichanua kwenye uso wake.


“Nadhani umesikia kile ambacho kimeweza kutokea?”

“Ndiyo mheshimiwa”

“Hao watu wanahitaji pesa nyingi sana zaidi ya bilioni miambili ambazo hatuwezi kuzitoa kwa namna yoyote ile hivyo nahitaji uwaagize vijana wako wakaifanye hiyo kazi mara moja huyo bwana mdogo arudishwe haraka sana nisije nikakikosa kiti changu kwa ishu za kijinga hizi, kumbuka tu nisije nikaletewa taarifa ya hovyo hapa”

“Mheshimiwa hiyo kazi itafanyika ila sio kwa hiyo namna ambayo wewe unaitaka”

“Unamaanisha nini kusema hivyo kwamba unapingana namimi?

“Sijamaanisha hivyo mheshimiwa, kumuandaa komando mmoja tu ni pesa nyingi sana zinatumika na muda mrefu mno na madhara yake ukimpoteza komando mmoja nadhani unajua vizuri hasara yake na nchi bado haina makomando wa kutosha wengine mpaka tunavyo ongea hivi wapo kwenye mafunzo hivyo ni ngumu sana kuwapeleka kirahisi kwenye nchi kama ile ambako biashara zake ni tishio kwa usalama wa watu. Kuna komando mmoja ambaye tayari ameweza kuiasi nchi yake nadhani itakuwa ni vyema zaidi kama tukiweza kumtumia huyo hata akifa nchi itakuwa haijaingia hasara kubwa kwa sababu mpaka sasa hana kazi yoyote ile japo hata zamani alifundishwa kinyume na malengo ilikuwa ni hila za yule jasusi hivyo huyu bwana mdogo atolewe jela akaweze kuifanya hiyo kazi” maelezo ya mkuu wa majeshi sio raisi wale mkurugenzi wa usalama wa taifa aliye muelewa walihisi kama mtu huyo labda alikuwa amechanganyikiwa ni kitu ambacho kilikuwa cha kufikirika sana mtu ambaye walitoka kumkamata juzi tu kwa kuweza kujihusisha na mauaji ya makamu wa raisi akahukumiwa kifungo cha maisha jela ikiwa na kunyongwa pale atakapofikisha miaka 30 jela eti leo tena aachiwe ilikuwa ni hadithi ambayo mtu mwenye akili zake timamu asingepanga kabisa kukuelewa hata kama ungechagua namna sahihi ya kuweza kumsimulia hadithi hiyo kiufasaha.

“Hivi upo kwenye akili zako au umekuja hapa ukiwa umelewa, yaani mtu ambaye juzi tu kaumiza makomando kumi na nchi imempa hukumu akiwa kama gaidi leo unaniambia atolewe jela kwa misingi ipi?” raisi alionekana kurudisha hasira zake kubwa alizokuwa amezipoteza alimkazia macho mkuu wa majeshi huku akiwa anamuuliza hilo swali.

“Yes, hilo nalitambua vizuri ndio maana nimetumia hii njia, tutamtoa kwa masharti ambayo tutakubaliana naye sisi nayeye”

“Masharti yapi hayo labda”

“Tutakubaliana naye kwamba kama akifanikiwa kumrudisha mtu huyo basi moja kwa moja kesi yake itafutwa na atarudi mtaani kuishi maisha ya kawaida na kama ataamua kuja jeshini ni yeye tu kuamua ila kwenye hayo makubaliano mimi ndiye nitakaye jua cha kukifanya endapo ataikamilisha kazi hii maisha ya kule anakoishi hawezi kukataa kama tukimpa hii ofa ya pekee kwa ajili ya maisha yake” sasa mheshimiwa ni kama alianza kumuelewa taratibu mkuu wa majeshi kile ambacho alikuwa anakimaanisha.

“Tutaamini vipi kama atarudi? Kumbuka yule ndiye aliyeleta ushahidi wa kumfunga yule vipi kama ataamua kumbadilikia huko huko na kumuua?” mheshimiwa alihitaji kupata uhakika wa mambo, habari za kubahatisha kwake hazikuwa na nafasi kabisa na ndiyo sababu kubwa alipenda sana kuzungukwa na watu wenye akili kubwa ili kuweza kuwatumia kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe.

“Hilo niachie mimi mheshimiwa yule hawezi kukimbia kwa gharama ya aina yoyote ile, ana udhaifu wake mkubwa sana ambao wanadamu wengi hawaujui hapa duniani isipokuwa mimi tu ndiyo sababu hata siku ile ulivyo nipa taarifa ya kumkamata moja kwa moja haikuchukua hata muda mrefu kwa sababu naujua udhaifu wake” ulikuwa ni muda wake wa kutamba mkuu wa majeshi alikuwa anajichukulia ujiko tu kujisifia mbele ya mheshimiwa ili ajue wazi hapo hakuliweka galasa bali alimteua mtu mhimu sana kwake pamoja na kwa taifa kiujumla.

“Ana udhaifu upi huo ambao imekuwa ni siri kubwa sana mpaka mimi mwenye nchi sielewi chochote”

“Mheshimiwa kama utaniruhusu nakuomba kwanza unipe amri yako tulikamilishe hili kwanza halafu haya maswali yatajibiwa baadaye nadhani itakuwa ni vyema sana”

“Fanya hivyo hakikisha hakuna kitu kinaenda tofauti kabisa”

“Sawa mheshimiwa”

“Ni mji gani huo ndani ya Colombia?”

“MEDELLIN”

“OK” mkubwa wa nchi alikuwa tayari ametoa ruhusa ya kuweza kulifanya hilo tukio kama ilivyokuwa inatakikana hapa sasa kilichokuwa kinasubiriwa ni kuweza kumrudisha mwanaume mjini akaifanye kazi, ni kitendo cha dakika chache tu mkuu wa majeshi alipiga simu yake moja kwenye gereza la DERISHRAWAR PRISON na kuwapa taarifa kwamba mtu huyo usiku wa kesho alikuwa anatakiwa awe Dar es salaam aletwe na helikopta, kauli ya mkubwa huwa haipingwi hizo ni sheria za jeshi. Muda huo ambao mkuu wa majeshi aliweza kupiga simu ndio muda ambao Jamal alikuwa mevamiwa na wanaume watatu kwenye chumba chake ambacho ndicho kilikuwa kama kitanda chake, taarifa ambayo ilitoka kwa mkuu wa majeshi iliwatisha sana makomando ambao walikuwa humo ndani kwani kama mtu huyo angepelekwa akiwa na matatizo hakuna kati yao ambaye angeweza kupona ndiyo sababu kubwa iliyowafanya wawashe umeme haraka sana na kuwahi kwenye chumba cha Jamal ambaye hata hivyo walimkuta akiwa wa afya kabisa ila watu waliokuwa wamemvamia humo ndani ni mtu mmoja tu pekee ambaye alifanikiwa kutoka akiwa bado anapumua, pia hiyo ilifanya Jamal aachwe akiwa huru kabisaa ni hali ambayo hata yeye ilimshtua sana ila hakuwa na taarifa kama keshokutwa yake alitakiwa kusafiri mpaka kwenye nchi aliyopata kuiishi lejendari wa madawa ya kulevya Pablo Escobar.


Jamal alishtuka sana baada ya kusikia kelele za vyuma vikiwa vinajifungua kwenye vyumba vyao, hakuwa anaelewa ni saa ngapi na hapo amekaa muda gani ila aligundua kwamba ilikuwa ni siku ya kutoka kwenda kwenye chumba ambacho kila siku walipaswa kwenda kupumzika siku ambazo wanapata nafasi ya kwenda nje, alifurahi sana alitoka nje kwa haraka kubwa akiwa na hamu ya kuweza kukutana na mzee huyo ambaye alitakiwa kummalizia hadithi ndefu ya maisha yake pamoja na maswali ambayo ni wazi yalikuwa yanamsumbua sana kwenye kichwa chake tangu muda wa kwanza ambao alibahatika kukutana na mzee huyo.

“Vipi unanitafuta mimi?” alishangaa sauti inaita nyuma yake ilikuwa ya kizee mno bila shaka alijua wazi ndiye mtu ambaye alikuwa anamtafuta humo ndani kwenye chumba kilichokuwa kinatumika kufugia samaki na ndicho walikuwa wakikitumia kupumzikia.

“shikamoo mzee” salamu yake haikuitikiwa kabisa ila mzee huyo alitabasamu tu aliijua vizuri sana dunia heshima huwa inakuja pale watu wanapokuwa wanahitaji vitu kutoka kwako, siku ya kwanza hakupata salamu yeyote kutoka kwa kijana huyo kwa vile hakuwa anajua kama mzee huyo anaweza akawa mtu wa mhimu sana kwenye maisha yake ila baada ya kugundua hilo ndipo akaanza kumheshimu, dunia ina watu wa hovyo sana na mzee huyu alikuwa amekutana nao wengi sana tangu akiwa kijana mdogo mpaka anakuja kufikia umri wake hilo jambo lisingeweza kumsumbua hata kidogo.

“Leo unatakiwa uwe na akili iliyo changamka kidogo na uulize maswali yako yote kwa uharaka na ufasaha mno sijioni nikiwa na siku nyingi kwenye hii jehanamu tuliyopo, kila inavyo itwa leo nuru inapotea kabisa kwenye macho yangu hiyo ni ishara ya wazi MUNGU ananihitaji nikapumzike na haya mambo ya kutisha hapa duniani nayaogopa mno ni bora niondoke mapema”

“Mzee unamaanisha nini kusema hivyo? unatakiwa umshukuru MUNGU kwa kila nafasi ambayo anakupatia kwa wakati huu kuna watu wapo hospitali na hawawezi hata kunyanyuka lakini wewe umepata bahati ya kutembea ni jambo la neema sana hilo”

“Ebu uliza maswali yako mimi nikalale unazidi kunipotezea muda nimechoka sana unaweza ukayakosa majibu ya maswali yako ambayo hautayapata sehemu yoyote ile hapa duniani zingatia hilo usije ukaishia kujutia kama baadhi ya watu wanavyofanya huko nje kwenye dunia yenu”

Unadhani ni maswali gani ambayo Jamal ni lazima ayapatie majibu siku ya leo?....
64 naachia kalamu nakuachia uwanja wewe uniambie ni siri zipi nzito ambayo Leonard Malachi alikuwa nayo kwenye kifua chake.

Bux the story teller
Ipo yote mpaka sehemu ya 100, unaipata yote mpaka mwisho kabisa kwa shilingi 2000 tu za kitanzania.

Unaweza ukalipia kupitia namba

0621567672 (WhatsApp)
0745982347
zote jina FEBIANI BABUYA. unaipata yote muda huo huo
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA SITINI NA TANO

TULIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA NNE..............


“Mzee unamaanisha nini kusema hivyo? unatakiwa umshukuru MUNGU kwa kila nafasi ambayo anakupatia kwa wakati huu kuna watu wapo hospitali na hawawezi hata kunyanyuka lakini wewe umepata bahati ya kutembea ni jambo la neema sana hilo”

“Ebu uliza maswali yako mimi nikalale unazidi kunipotezea muda nimechoka sana unaweza ukayakosa majibu ya maswali yako ambayo hautayapata sehemu yoyote ile hapa duniani zingatia hilo usije ukaishia kujutia kama baadhi ya watu wanavyofanya huko nje kwenye dunia yenu”

ENDELEA...................................


“Mzee wewe ni nani” swali la Jamal lilimfanya mzee huyo akohoe kwanza kisha mikono yake ilikuwa inafuatia kwenye macho yake haikuonekana kulingana na ndevu na nywele nyingi ambazo zilikuwa zikiufunika uso wake huo lakini ni wazi kwamba alikuwa analia mwanaume huyu, alitazama juu kidogo ili kuufungua ukurasa wa maisha yake na Jamal aweze kumjua huyu mtu ni nani hasa mpaka aliambiwa ni lazima aweze kukutana naye alikuwa ni mtu wa mhimu sana kwenye maisha yake, alihitaji kumjua huyu binadamu alitokea wapi, je ana familia labda na kitu ambacho Jamal kilikuwa kinamchanganya kwanini mtu ambaye alikuwa usalama wa taifa tena ikisemekana kuwa mgurugenzi kabisa kuja kufungwa kwenye gereza la kutisha kama hili ambalo walikuwa wanafungwa wahalifu wa kutisha kwa sababu kama ni kosa alilolifanya alitakiwa kufungwa ndiyo kama adhabu ya kushindwa kumlinda raisi ila sio kwenye gereza kama hili.


Majina yangu halisi naitwa Leonard Makachi ni mwanaume ambaye ninalijua kwa usahihi sana maana ya neno familia, familia sio tafsiri ya herufi ambazo vijana wengi wa mtaani na baadhi ya watu ambao wamekosa weledi namna wanavyo zitamka familia ni kitu kikubwa sana ndiyo sababu huwa inakuwa na muunganiko wa mwili au damu, leo hii hata ukigombana na ndugu yako mpaka mkafika hatua ye kuweza kutishiana kuuana hata ufanye nini hautaweza kuutoa ukweli kwamba nyie ni familia moja ndiyo sababu wahenga wakasema kitu cha kwanza cha mhimu kwako na kwa maisha yako ni familia yako wewe na sio marafiki kama watu wanavyo danganyana kwenye huu ulimwengu wa utandawazi siku hizi. Marafiki utawapata wengi sana ila hao ni wa kupita tu wasikufanye ukaisahau familia, watu wote watakukataa duniani pale unapofikia hatua huwezi kujitendea msaada kwenye maisha yako ila familia yako lazima watakupokea hata kama mna visasi na ugomvi mkubwa kwenye mioyo yenu, kuna maana kubwa sana ya wewe kuweza kuzikwa nyumbani ulikozaliwa pale inapofikia wakati ukifa, sio pambo wala fasheni za mjini huo ni uhalisia wa maisha ya mwanadamu hata maandiko ya vitabu vitakatifu yanasadiki hilo jambo.

Mimi ninaweza kuelezea kwa mapana maana ya neno familia kuliko kitu chochote kile duniani nikukumbushe kitu kidogo kwenye haya maisha wanaume huwa tunapenda sana kujipa ukubwa kwa sababu tu Adam alikuwa wakwanza kuumbwa na Eva alikuja kuwa kama msaidizi wake hicho kitu kimefanya watu wengi sana ndani ya familia kujipa umungu watu usio na mhimu wowote kwa kuwaona wanawake ni dhaifu sana hilo ni jambo ambalo unapaswa ulikwepe sana lisije likakupanda kwenye kichwa chako litakuletea madhara makubwa na utakuja kujutia kuzaliwa wanaume wengi huwa wanapoteza muda wao kuwafuatilia wanawake ili wawaelewe falsafa ya maisha inasema mwanamke aliumbwa ili apendwe na sio kueleweka hakuna binadamu mwenye uwezo wa kumuelewa mwanamke isipokuwa mwanamke mwenyewe ndiye anaweza kujielewa kwa asilimia zote hiyo inakukumbusha kwamba mwanaume ni kiumbe dhaifu kupita kiasi mbele ya mwanamke. Kwenye mpira kila mchezaji kati ya wale 11 ambao huwa wanaanza kucheza wote ni mhimu sana ila mhimili mkuu huwa ni sehemu ya katikati hilo eneo likiyumba basi timu nzima huwa inayumba.

Leo unakuta mwanaume mzima kabisa mwenye akili zake zote hajawahi hata kuugua ugonjwa wa ukichaa akiwatukana na kuwasema vibaya makahaba ambao wanauza miili yao ili kuweza kupata pesa sasa jiulize mtoaji wa hizo pesa ni nani unakuta ni mwanaume, anayewafanya hao makahaba wawepo ni nani unakuta ni mwanaume maana yake kama sio wanaume kuendekeza hayo mambo basi hata hao makahaba usingewasikia maana wanaishi vizuri na wanapendeza kila siku, wanalipa kodi kwa pesa za wanaume ambao ndo wanajisifia kuwa akina baba bora wa familia hapo ndo ujue mwanaume ni miongoni mwa viumbe vya hovyo kuwahi kuumbwa duniani japo huwa tunalindiwa sana heshima na wanawake na hatulioni hilo

Sasa kwenye familia tunavyomzungumzia mwanamke ndiye kiungo wa familia yule asipokuwa sawa hakuna kitu kitafanyika hapo nyumbani, mwanaume unaamka mapema sana kwenda kuhangaika kisa tu unatafuta pesa basi unajivika kila kitu usifiwe wewe unasahau furaha ya watoto unao jivunia kwamba inatengenezwa na mama yao, huyo anahakikisha unasifiwa wewe una nyumba bora, huyo ndiye anakufanya wewe uwe baba bora hapa duniani hawa viumbe wanahitaji sifa nyingi sana, mwanamke ndiye kiungo mshambuliaji wa familia, ukioa mwanamke wa hovyo hata uwe na akili kama ambazo walipata kuwa nazo akina Albert Einstein hufiki popote mtatengeneza kizazi cha hovyo sana ila kama ukipata mwanamke mwenye akili nyingi hata wewe ukiwa wa hovyo familia yako itakuwa bora sana hilo linakukumbusha kuwa makini sana pale unapochagua mke kwa ajili ya familia yako jamii na mitandao isikuchanganye ukakurupuka kuchagua rangi nzuri, umbo zuri na sura ambavyo utavichoka kwa mwezi mmoja tu pekee na kujuta maisha yako yote, kuna mzee mwenzangu wa zamani kidogo siku moja nilisikia akisema kuna mke mke: huyu huwa hajali chochote, hana muda nawewe yani yupo yupo tu, kuna mke mke wenu: huyu ni cha wote hajui kukataa ukioa ni sawa na kuolea mtaa mzima kila atakaye hitaji atampatia haki yake, pamoja na mke mkeo: huyu ndiye mwanamke ambaye unapaswa kuwa naye kwenye maisha yako, anayajua majukumu yake kwa asilimia zote hata pale ambapo wewe utaanguka huyu mwanamke atakustiri akiamini wewe ndiye baba ya familia yake, niliishia kucheka tu kwa sababu lilitolewa somo kubwa sana tena la bure kabisa ila kwa bahati mbaya hadhira hawakuwa tayari kumuelewa fanani kwahiyo alionekana kama mpiga kelele kitu ambacho ni nadra sana kukipata bure kwa ulimwengu wa sasa.


Mimi ni miongoni mwa binadamu ambao tulipendelewa sana kwa muda ambao tumeuishi tukiwa vijana, nilipata mwanamke mrembo sana ambaye kila nikilala ni lazima nimuone akinijia kwa tabasamu na namwambia still I LOVE YOU my wife, uzuri wake haikuwa sababu ya kumfanya kuwa mwanamke wa hovyo alinitengenezea familia bora ambayo hata mimi sikuwahi kuifikiria kabisa kwenye dunia hii, hiyo haikutosha alinipa zawadi kubwa sana ya kunifanya niitwe baba kwa mara ya kwanza kwenye huu ulimwengu, mtoto mzuri sana wa jinsia ya kike nilimpata( alitoa picha ndogo akiiangalia kwa uchungu sana huku machozi yakiwa yanamshuka kwenye mashavu yake) jina la Brenda likampamba cha kucheka wangu, hakuwa mtoto wa kununa hovyo alikuwa na tabasamu muda wote na kumfanya kuwa kama pacha wa mama yake mzazi walifanana sana ila mpaka sasa maisha yangu yamebaki kuwa hadithi ya hovyo ya kutisha sana.

Nilikuwa ni jasusi ndani ya idara ya usalama wa taifa kwa siri ambayo sikuweza kuruhusu hata mke wangu wa ndoa aweze kuijua ili kuweza kuulinda usalama wake pamoja na mtoto wangu kwa kuzuga kwamba mimi nilikuwa ninafanya biashara zangu mbali mbali ikiwemo kuuza spea za magari kitu ambacho hakikuwa kweli, nilifanya vile kwa sababu kama ningemwambia ukweli mke wangu basi angeishi kwa mashaka na wasiwasi mkubwa sana ila najutia mke wangu amekufa bila hata kujua mimi ni nani kwenye maisha ya kweli ila naweza kusema kwamba muda ambao niliishi nao wale wawili ndio muda bora zaidi kwa mimi kuwahi kuupitia kwenye ulimwengu huu. Nilikuwa na likizo ya muda mrefu kidogo ambayo niliitumia kukaa na familia yangu kwa muda mrefu hatimaye likizo yangu iliisha nilirudi Arusha ambako nilikuwa nafanyia kazi zangu hizo za siri za usalama wa taifa. Ndipo lilipotokea tatizo la watoto kuanza kupotea kwenye jiji la Dar es salaam nilipigiwa simu na kuambiwa nilihitajika kwenda kuifanya hiyo kazi haraka sana ikiwa ni pamoja na kudhibiti hicho kitu kabla madhara hayajawa makubwa kwa kiwango chake.

Ilikuwa ni amri ya mkubwa wangu kwahiyo nilirudi haraka sana Dar es salaam kwa siri bila hata mke wangu kujua, safari yangu ya kwanza ilikuwa ni kwa kijana aliye itwa Banjuni huyu ndiye nilipata fununu huwa anawakusanya watoto mtaani, kweli nilimbana akaja kuniambia kitu ambacho kilinishtua sana alinitajia jina la Shabani Nyatiki ambaye alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi kwamba ndiye yupo nyuma ya hilo jambo. Ni kweli mtu huyo alinipigia simu na kunitahadharisha kwamba nisifanye chochote baada ya kumuua yule kijana wake ila kwa bahati mbaya kauli yangu moja ya jeuri iliweza kunizalishia maumivu makali sana kwenye moyo wangu mpaka leo huwa nakizingatia sana kinywa changu kwenye kila neno ninalo litoa huwa naangalia kama linaendana na mazingira niliyopo ila kama halifai huwa namezea moyoni tui li kuepusha majuto ya baadaye.

Kwa kujibu jeuri kwani nilipania sana kumkamata mhusika basi aliniambia kwamba niweze kuwahi nyumbani kwangu moyo ulinienda mbio sana nilikuwa nakimbia kama nina kichaa, asikwambie mtu watu huwa wanadanganyana kwamba kuna viumbe wana roho mbaya na ngumu kama nyoka, simba, majini na vingine visivyo onekana hapana hakuna ukweli wowote juu ya hilo binadamu ndiye kiumbe wa kutisha, hatari na mwenye roho ngumu zaidi duniani, wanadamu ni zaidi ya wanyama kuna mambo wanayafanya mpaka nafsi yako unaanza kuiogopa kila kunapoitwa leo. Nilifika nyumbani ila nilicho kikuta ndiyo siku ya kwanza jasusi mkubwa tu nilitamani nijiue pale pale sikuwa na kitu kingine kwenye maisha yangu cha kukipoteza zaidi tu alikuwa amebaki kijana mdogo ambaye nilimuokota akiwa anaosha magari akijulikana kwa jina la Timotheo Jordan nilikuwa namlea kwa siri na kwa wakati ule alijua kwamba mimi nilikuwa mkurugenzi wa taifa ila ukurugenzi nilikuja kuupata baadaye kidogo.

Kitu cha kwanza kukiona ulikuwa ni mwili wa mwanangu ambaye alikuwa na robo tatu ya moyo wangu wote sikupata hata nafasi ya kuweza kulia au kutoa sauti mke wangu alikuwa amebakwa vibaya sehemu zake za siri ziliharibiwa mno hakuwa hai alikuwa ameshakufa tayari kichwa chake kilikatwa na kuwekwa kwenye sofa, kazi ya usalama ni ngumu sana ndiyo maana hawa watu huwa wanakuwa wa siri sana ili kuziweka salama familia zao ule unyama hata shetani asingeweza kuufanya nilizoea kuona hivyo vitu kwenye filamu za kutengeneza za Hollywood huko kwa siku ile kile kitu kilikuwa cha kweli tena ndani ya nyumba yangu na mtazamaji nilikuwa npo mwenyewe hapo ndipo mwanzo wa ubaya huwa unaanza kwa wanadamu mhusika muda huo yupo anasherehekea na wenzake wakinywa pombe na kubadilisha wanawake. “NILIKWAMBIA MAPEMA UKAWA JEURI MPUUZI WEWE SASA UTAKUWA UMEPATA SOMO NA KUWAJUA WANADAMU” wakati meseji hiyo inaingia kwenye simu yangu nilikuwa nimeipakata miili ya mwanangu na mke wangu, niliisoma vizuri kisha nikaenda kwenye chumba changu cha siri ambacho kilikuwa na kamera zangu nyingi sana za mitambo ya usalama pale nyumbani kwangu nilishuhudia kila kilicho fanyika, lilikuwa ni jambo gumu sana kulivumilia ila niliamua kuyakaza macho mpaka pale ilipo malizika macho yangu yalikuwa yanawaka moto sikuwa kama mwanadamu wa kawaida tena kwenye yale maisha mtu aliyefanya hilo jambo nilikuwa namjua kwa asilimia miamoja kilibakia tu kumfuata huko aliko.

Niliweza kufuatilia na kuwajua wale wote ambao walihusika na lile tukio la ubakaji na kuua familia yangu, bahati ilikuwa mbaya sana baada ya kufanya maziko ambayo niliyafanya pekayangu bila kumshirikisha mtu yeyote yule ndani kwangu nilikuja kugundua yule waziri wa mambo ya ndani ya nchi alikuwa ana familia kabisa mtoto wake wa kwanza wa kiume alikuwa ametoka nchini marekani kusoma alikuwa ameanza kumkabidhi biashara zake pamoja na wawili mapacha ambao walimfuata yule mkubwa hawa walikuwa wa kike na wa kiume, MUNGU anisamehe sana kwa nilicho kifanya kwa wale ambao nadhani hata hawakuhusika kabisa ila sikuwa na uwezo wa kujizuia kabisa kwa kile ambacho alikifanya, niliiteka familia yake nzima kwa wakati ule alikuwa ameoa mwanamke mmoja mrembo sana ambaye alitoka kuwa miss Tanzania mkewe aliyezaa naye watoto alikuwa amefariki.

Mtu aliye toneshwa kidonda leo alikuwa na familia ya mtonesha kidonda, kipi atakifanya ikiwa hiyo ni familia ya mtu ambaye amemfanyia ukatili usio tazamika wala kuvumilika kwenye familia yake?.........65 nasema bye bye mpaka wakati mwingine.

Bux the story teller
Leo tunakula burudani tu
 
Mnaenjoy boli?😁 Au boli litembee? Huko tunako elekea hakikisha hauikosi hata sehemu moja utanishukuru baadae kuna hatari kubwa sana. Mpaka sasa najua haujamjua kabisa huyo Catherine Yudel ni kiumbe gani na kwanini amejiamini kurudi kwenye nchi yetu pendwa kulipigania penzi lake. Twende sawa.
 
Shukrani [mention]FEBIANI BABUYA [/mention] kazi nzuri…Boli litembee maana umeachia sehemu Tamu sana
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA SABINI

TULIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA TISA.............

Nusu saaa iliwawezesha kusimama nje ya geti kubwa la mtu huyo leo waligonga kistaarabu tu alikuja kufungua mwanamke mmoja mrembo sana nyuma yake akifuatiwa kijana mdogo ambaye hayakuhitajika maelezo juu yake kujua kwamba ni mtoto wa Dickson Mapande kwa namna walivyokuwa wamefanana sana, ni ugeni ambao moja kwa moja ulimshangaza sana mke wa askari mkubwa wa polisi mwanamke huyo alikuwa ni ni tofauti kabisa kwani ilikuwa ni sura kama ya kilatini kwa muonekano ila mwnaume aliyekuwa nyuma yake alikuwa ni mtanzania.

ENDELEA................................

Aliweza kuwakaribisha ndani kuwa mke wa askari kulimfanya kwake hapo kuweza kupokea wageni wengi sana hivyo hakuwa na tatizo na hilo jambo, walimtoa wasiwasi kabisa baada ya Rashid kumueleza kwamba walikuwa wanamhitaji mumewe kwa ajili ya ishu za kikazi hivyo hakutakiwa kuwa na wasiwasi wowote ule lakini wakati wako hapo Catherine ni kama alishtuka hali haikuwa sawa alienda dirishani ni kama aliona kivuli cha mtu kikikatiza kwenye ukuta wa geti hilo kisha kikapotea, alikimbilia mlangoni na kutoka nje haraka Rashid alimfuata kwa nyuma alimzuia mke wa Dickson alisiweze kuwafuata bali afunge mlango kwanza. Catherine alifika chini na kutulia alijua wazi humo ndani kuna mtu alikuwa ameingia ni kweli koti kubwa na buti kivuli kilionekana mtu akiwa na kovu kubwa kwenye uso wake wake hakuwa mwingine huyu ni Alexander alikuwa ametia timu hiyo sehemu akiwa hana hata presha alikuwa akihitaji kukipata kile ambacho alikuwa amekifuata kwenye hilo eneo.

“Who is this (huyu ni nani?)” ni swali ambalo wazi Catherine alikuwa akimuuliza Rashid sura ambayo ilikuwa mbele yake ilikuwa ni ngeni kabisa kwenye uso wake na hakujua kwanini mtu huyo aje kwa kuvamia hapo.

“He is the one who murdered all Jamal’s family members (ndiye aliyeweza kuua familia yote ya Jamal)” maelezo yake yalijitosheleza Catherine kuweza kuelewa kwamba huyu ndiye ambaye amemfanya Jamal aishi maisha magumu sana

“Whaaaaaaaat?”

“Yes, he is the one, he goes by the name Alexander, he also assisinated the former predisent of the United Republic of Tanzania” mpaka hapo ilimaanisha kwamba hakuwa mtu wa kawaida huyu mtu ilikuwa ni hatari kucheza naye vibaya, wakati huo Alexander macho yake yote yalikuwa kwa Rashid ambaye ni wazi alionekana anamtamani sana kumpata na ni mojawapo ya sababu ya yeye kuwepo kwenye hilo eneo.

“Unataka nini hapa?” Rashid alimuuliza huyo mwanaume akiwa ana hasira naye ila alimjua vizuri sana hakuwa level yake kabisa ya kuweza kupigana naye na alielewa kama wakicheza vibaya wanaweza kupoteza maisha wote

“Ok mwenzako yuko wapi?”

“Mwenzangu yupi?”

“Lenovatus Jonson”

“Kwani hujui kama yupo gerezani acha kuniulizwa maswali ya kipumbavu mbwa wewe” kauli yake ilifuatia na kukoswa na kisu kikali ambacho kilienda kukita kwenye kioo kikubwa cha dirisha, kumtukana mtu huyo kulimfanya Alexander arushe kisu hicho kikali huenda alikuwa anahitaji ukweli wa Jamal pengine alikuwa na taarifa za mtu huyo kuweza kutolewa gerezani Rashid ndiye alionekana kuwa mtu wake wa karibu hivyo kwa namna yoyote ile asingeshindwa kujua kwamba huyo mtu alikuwa wapi. Alexander alipigwa na kitu kizito ambacho kilienda kuchana kwenye shavu lake sehemu ambayo ilikuwa na alama mbichi kabisa ya kidonda alichoweza kuzamishiwa siku aliyo bahatika kukutana na Jamal ikiwa ndiyo siku yao ya kwanza kabisa kuweza kukutana uso kwa uso, alipiga kelele alipata maumivu makali mno, hakupigwa na kitu kizito kama alivyodhania huo ulikuwa ni mguu wa Catherine ulipita hapo kwa namna mwanamke huyo alivyokuwa mrembo usingefikiria anaweza kuwa na mambo ya kutisha sana namna hiyo inahitaji moyo wa ziada sana kuweza kuuogopa huo urembo wake. Mapigo ambayo mwanamke huyo alikuwa anakuja nayo huenda kama sio uzoefu wa Alexander asingenyanyuka tena.

Alikichomoa kisu chake kimoja ambacho kilikuwa kimebaki ni muda ambao huwa anakuwa hatari kupita maelezo alikuwa anjirusha kuelekea pale alipokuwa amesimama Catherine teke zito la mbavu lilimnyanyua na kumrushia hatua kadhaa kutoka hapo hakuweza kujua ni nani ameweza kufanya hicho kitu mpaka pale alipo yainua macho yake, Rashid na Catherine walikuwa wamesimama mbele yake yeye akiwa chini amedondoka, alijirusha kwa juu akijifuta damu nyingi ambayo ilikuwa inatoka kwenye uso wake kwa mkono wake macho yake yalikuwa mekundu huenda kwa sababu alizoea sana kunywa vilevi vikali ila hata hasira zilichangia sana yeye kuweza kubadilika hiyo rangi ya macho na kuwa mekundu kama nyanya. Rashid alirusha ngumi zito ambayo ilimpata Alexander tumboni hata hivi na yeye alipewa ngumi ya kichwa alihisi nyota zinazunguka ilikuwa ni ngumi nzito mno, Alexander alijirusha mkono wake mmoja ukiwa chini alimpatia double kick Rashid ambayo ilimfanya akajibamiza vibaya kwenye ukuta kwenye maeneo ya kichwa, yalikuwa ni meteke mazito mno alikuwa akicheua damu hakuchukua hata dakika moja alikaa kimya pale pale chini kichwa kikiwa kinatoka damu kwa mpasuko ambao kiliupata. Catherine hakuamini ila ndio ulikuwa uhalisia mwanaume huyo alikuwa anakuja kwa kujiviringisha ndani ya koti lake kisu kikiwa kinazungushwa kwa ufundi mkubwa mno alifanikiwa kukikwepa lakini alikutana na kisigino cha uso ambacho kilimfanya mdomo wake kuwa mwekundu kabla hajatua chini alisindikizwa na teke lililokuwa na ujazo wa kilogramu kadhaa alidondoka chini akiwa anavuja damu mdomoni na puani, hakukoma hapo alinyanyuka kwa sarakasi hatari ambayo hata Alexander ilimfanya arudi nyuma kidogo aina ya hizo style alizijua vyema huwa wanazitumia wauaji wakutisha kama yeye alivyo kwahiyo alitakiwa kuwa makini sana hakutakiwa kabisa kumchukulia kawaida huyo mwanamke ambaye alikuwa mbele yake uzembe wa kudharau vitu ungemsababishia matatizo makubwa mno ambayo huenda angekuja kuyajutia akiwa amesha chelewa, Catherine baada ya kunyanyuka alitabasamu na kuchomoa visu viwili kwenye buti za miguu yake vilikuwa ni vidogo ila vilikuwa ni vikali na vya kung’aa mno, hakuna kitu hivyo visu vinaweza kukikata kisikatike labda kiwe ni chuma na alikuwa akilijua hilo, leo kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake Alexander alitakiwa kuwa makini mbele ya mwanamke hilo jambo hakuwahi kulidhania kabisa na hakujua huyo mwanamke alikuwa ni nani hasa mpaka amvamie kwa hasira kiasi hicho na kwa bahati mbaya sana walikuwa wakipishana kwenye suala la lugha Alexander akiwa anaongea Kiswahili na mrembo huyo kiingereza ndiyo lugha ambayo alikuwa na uwezo wa kuzungumza na watu wengi wakamuelewa kwahiyo hapo ni mikono ndiyo ilikuwa inaenda kuamua ni nani ambaye alistahili kuondoka na mwili wa mwenzake ili kama atamhoji baadaye angeenda kujua mwenyewe mbele ya safari.

Mikono ya huyu mwanamke ilikuwa imekomaa sana kwa namna ilivyokuwa ikirushwa ukijumlisha na visu alivyo vishika jinsi alivyokuwa anavizungusha Alexander alikuwa akimshangaa sana utu uzima ulikuwa unamuingia Alexander yale makeke yake ya zamani yalikuwa yakipungua taratibu, shukrani za dhati alizipekeka kwenye koti lake ambalo alikuwa amelivaa maana kama sio hilo koti lake mpaka muda huo mwili wake usingekuwa na uwezo wa kusimama tena koti lilichanwa vibaya na hivyo visu akalitupa pembeni halikuwa na kazi tena alijiangalia tumboni alikuwa na alama kubwa ya kisu, Catherine alikuwa pembeni akimtazama mtu huyo kwa hasira sana kiasi kwamba mpaka machozi yalikuwa yanamtoka utadhani yeye ndiye aliyekuwa ameuliwa wazazi wake lakini alikuwa ni mpenzi wake tu. Alexander alirusha mateke mawili na ngumi huku mkono mwingine akiwa amekishika kisu kwa ukakamavu alifanikiwa kulifikisha teke moja ambalo lilimpata Catherine kifuani ngumi na teke lingine aliyakwepa alirushwa mbali mpaka chini akiwa anacheua damu Alexander alitaka kusimama kwa miguu yake yote alishangaa sana mguu mmoja ulikuwa unauma mno aligeuza macho yake chini kuangalia mguu mmoja ulikuwa umekatwa vibaya sana hakuelewa umekatwa sangapi mpaka kutengeneza alama kubwa sana ya jeraha namna hiyo alikumbuka vizuri kwamba wakati teke lake linampata mwanamke huo mguu mmoja aliukwepa ndio huo ambao alikuwa ameupitishia kisu hicho.

Mwanaume leo aliingia cha kike alikuwa akichechemea wakati huo Catherine alikuwa amepiga goti moja chini mguu mwingine ameusimamisha akiwa anatoka damu mikono yake miwili ilikuwa na visu vyake vikiwa vina damu ya kutosha kimoja alikizamisha kwenye tumbo la Alexander lakini kingine kilizungushwa kwenye mguu wa kiumbe huyo, alexander alijikuta akikubali kila kitu alitishiwa kama anapigwa ngumi usoni alikwepa wakati huo aliuchelewesha mguu wake ambao ulikuwa una jeraha alipigwa mtama wa nguvu baada ya kutaka kudondoka chini hakuweza kupewa hiyo ruhusa mateke manne ya haraka yalipita kwenye kifua chake na kumfanya adondokeee mbali ambako hata hivi alijiviringisha na kutua kwa goti moja, cheche za moto zilionekana wakati Alexander anadondoka alikiachia kisu chake kuelekea kule alikokuwa Catherine ambacho kilionekana na mrembo huyo naye alikirusha kisu chake vikakutana katikati na kutengeneza hizo cheche za moto.

Kitu cha kushangaza kilitokea Alexander hakuamini mwanamke huyo baada ya kusimama tu alidondoka chini na kuachia kisu chake akawa ametulia kimyaa, alimshukuru MUNGU maana mwanamke huyo alionekana kabisa anahitaji kutoka na roho yake japo hilo jambo lilimpa sana maswali haiwezekani kirahisi tu namna hiyo mwanamke imara kama huyo adondoke kirahisi hivyo lakini kwake ilikuwa ni nafasi ya dhahabu huyo mrembo hakutakiwa kabisa kuendelea kuwepo hapa duniani alitakiwa kumuua haraka sana alikimbia kwa spidi kali mno na kisu chake mkononi lengo kuikata shingo ya huyo mwanamke ambaye kwa muda huo hakuwa akijiweza kwa jambo lolote lile kisu kilikuwa kinaiteketeza shingo ya miongoni mwa wanawake warembo sana kuwahi kuumbwa duniani hili ni kosa ambalo hata MUNGU asingeweza kumsamehe kuweza kumuua mwanamke mrembo sana namna hii.

Ni bora angekutana moja kwa moja na jiwe au nyundo akiwa anajielewa hakuelewa kilikuwa ni kitu gani ila ni wazi hakuwa binadamu bali ni roboti kuna teke lilitua kwenye mkono uliokuwa na kisu, kisu kilienda mbali lilifuatia buti lenye uzito ambao hakujua kama ni kiatu kinacho valiwa na mwanadamu lilitua kwenye shingo yake alianza kuona nyota nyota ni kama aliona kuna mtu amevaa kombati ya jeshi hakuelewa vizuri kwani uwezo wa kuona ulipotea kabisa, mwanaume huyo ambaye alikuwa na mwili wa wastani ulio jigawa vizuri aliinama sehemu ambayo alikuwepo Alexander alipitisha vidole vyake viwili kwenye shingo ya mwanaume kwa nguvu sana hapo hapo Alexander alitulia kimya bila hata kutikisika haikujulikana kama amekufa au MUNGU angempendelea nafasi nyingine ya kuwa hai.

“Ni nani huyu kijana” ni sauti yenye kukwaruza ya mwanaume huyo akiwa anaangalia nyuma yake, kitu cha kushangaza huyo mwanaume alikuwa anaangalia sehemu ambayo alisimama Antony mlipa huyu hakuwa mwingine bali mkuu wa majeshi wa nchi ya Tanzania, hakuwa pekeyake hapo kulikuwa na wanajeshi sita ambao ni wazi walikuwa ni watanzania lakini mwanaume huyo aliyekuwa anauliza alikuwa na kombati ambayo ilikuwa ipo tofauti kabisa na hao ambao waliongozwa na mkuu wa majeshi wa Tanzania, yeye kombati yake ilikuwa ipo sawa na mwanaume mmoja ambaye alionekana kumpima Catherine kama yupo salama akiwa amepoteza fahamu zake.

“Ni kijana ambaye amempoteza dada yake hivi karibuni kwahiyo nadhani anahangaika kumtafuta mtu ambaye amehusika na huo unyama kwa ndugu yake”

“Sasa imekuaje mpaka awe anataka kumuua madam hapa” ni lugha ya kiingereza walikuwa wanaitumia ila wote walikuwa wakielewana vizuri kwahiyo hawakuwa na shida yoyote kwenye upande wa lugha.

“Huenda labda kwa sababu wamekutana kwenye eneo la tukio watu kama hawa huwa hawaaminiani sana kwenye sehemu za kazi”

“Siku yoyote huyu mwanamke akionekana eneo lolote lile asije akaguswa tena mtailetea hii nchi matatizo makubwa sana, mnafanya mzaha huenda kwa sababu hamumjui ni nani, watu gani wako nyuma yake ila mngelijua hilo ilitakiwa muda huu mpige magoti kuomba msamaha na hili jambo kama likijulikana basi kuna tatizo kubwa sana linaweza kutokea, pia nataka nikutahadhalishe huyu mwanamke huwa hapigani na mwanadamu wa kawaida kama huyu akiwa kwenye hasira zake zote, daktari wake mmoja aliwahi kusema kama mwanamke huyu atakuja kupigana kwa ajili ya mapenzi basi atakuja kuwa binadamu wa hatari kwenye huu ulimwengu, anapo badilika huwa hawi hivi kama unavyo muona mpaka mnaweza kuongea naye kistaarabu, niliwahi kukutana naye mara moja akiwa kwenye hali yake ambayo huwa sio mwanadamu wa kawaida nilitamani bora ningekutana na shetani.

Shukuru MUNGU tumewahi kufika hapa kabla hajaamka hapo alipo lala na kuwa kwenye hiyo hali tumeweza kumrushia sindano ambazo zitamlaza kwa masaa kumi na saba ndipo ataamka vinginevyo kama angeamka hapa kati yetu hakuna mtu angeweza kutoka nje ya hili geti zingatia sana hilo” huyu mwanaume ambaye haikueleweka yeye alikuwa ni nani hasa alitoa maelekezo ambayo hata mimi nawewe yanatushangaza sana kuhusu hali ya mwanamke ambaye sisi tunamchukulia kawaida sana Catherine, walimbeba na kuondoka naye hawa wawili huku wakimuacha mkuu wa majeshi na vijana wake kwenye mshangao mkubwa hata hivyo hawakuweza kukaa hilo eneo sana waliangaza huku na huku hawakuona mtu yeyote yule wakambeba Rashid ambaye hakuwa kwenye fahamu pamoja na Alexander ambaye naye haikujulikana kama yupo hai au amekufa.

Huyu mwanamke ni nani? ana siri ipi nzito ndani yake mpaka waseme akibadilika anakuwa ni binadamu wa kutisha sana, je walio mfuata ni akina nani na wanamjuaje yaani wametoka wapi hawa watu”

Bado hatujui hali ya Alexander ipoje mpaka sasa je atapona?........... kichwa kinasisimka mambo yanatisha sana niseme tu 70 inafika tamati tukutane tena wakati ujao.

Bux the story teller
1500 tu unaipata mpaka sehemu ya 100
 
1500 yako tu nicheki umalizie mpaka mwisho ila kujiunga na group letu la WhatsApp ni 3000 tu Kwa mwezi.

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

FEBIANI BABUYA
 
1500 tu kuimaliza mpaka mwisho

0621567672
0745982347

FEBIANI BABUYA
 
Moderator naomba nibadilishie hiyo heading inatakiwa kusomeka "I want to die judge" sio i want to die a judge
 
Back
Top Bottom