FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #121
UNAWEZA KUZISOMA HADITHI ZANGU KWA WAKATI KUPITIA GROUP LANGU LA WHATSAP AMBALO KUJIUNGA NI SHILINGI 3000 TU KWA MWEZI. NAMBA ZA KUTUMA HIYO PESASTORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA SITINI NA TATU
TULIPO ISHIA SEHEMU YA SITINI NA MBILI.........
Alifumba macho yake na kutulia ili kuuweka mwili sawa kwa utulivu masikio yake akitulia yalikuwa yanaweza kusikia vitu vingi sana kuna sauti alianza kuzisikia hazikuwa za kawaida hata kidogo usalama wa hilo eneo ulionekana kuwa mdogo sana, aliyafumbua macho yake na kujaribu kuchungulia nje kulikuwa na kiza kikali ambacho kwa siku kadhaa tangu afike hapo hakuwahi kukishuhudia na aliambiwa hiyo sehemu taa huwa hazizimwi hata sekunde moja kwanini umeme uzime muda kama huu akili yake iligoma kabisa kuweza kukubaliana na jambo kama hilo alisimama taratibu hatua za ujio wa watu wakiwa wananyata aliweza kuzisikia vizuri sana japo alishindwa kutambua wapo wangapi. Mlango wa chumba alichokuwepo ulisikika kwa mbali ukionekana unajivuta kufunguka hakuelewa imewezekanaje kwa maana unatumia umeme na kwa muda huo umeme ulikuwa umekatika.
ENDELEA..............................
“Una machaguo mawili hapa utuelekeze hicho kitu umekiweka wapi au tukutie ukilema uweze kutueleza kwa lazima” ni wanaume watatu ambao walikuwa wameingia kwenye hicho chumba mmoja wao alisikika kwa usahihi akiwa anaongea hiyo kauli mikononi mwao wawili walikuwa na vishoka na mmoja alikuwa ameshika upanga mkali ambao hata kizani ulikuwa unang’aa sana, hakuna jibu walilo lipata humo ndani.
“Hayupo mbali naisikia harufu ya jasho lake lazima yupo karibu sana hapa hapa” mmoja wao aliongea huku akiwa yupo makini kuchungulia kwenye kila pembe ya hicho chumba ila alihisi kama kuna mtu nyuma yake aligeuka kwa nguvu akiwa anaulazimisha mkono wake ambao ulikuwa na uzito kazaa aliirusha shoka yale ulisikika mlio mkali ikonekana kuna chuma kinakatika wenye meno madhaifu lazima wangehisi meno yao yanauma kwa kelele ya kuburuza chuma ambayo ilisikika, shoka hilo lilimkosa Jamal kwenye paji lake la uso na tumboni lilienda kukata minyororo ambayo ilikuwa ipo kwenye miguu yake mpaka ikakatika inamaanisha kama hiyo shoka ingetua hata mguuni basi huo mguu ungeweza kuokotwa vipande vidogo vidogo. Kamali ambayo Jamal aliicheza ilihitaji binadamu wajasiri kupindukia alisikia minyato ya hao watu alijirusha akajiviringisha na kwenye kunasa kwenye ukuta wa juu ndani ya selo wakati wanafika aliamua kutua nyuma ya mtu wa mwisho kabisa ambaye bado alikuwa yupo karibu na mlango akijua wazi mtu huyo atageuka kwa nguvu na silaha yake mkononi kama akigeuka kwa nguvu atamsaidia kupunguza hizo nyororo na hesabu zake zilifanikiwa kwa asilimia kadhaa.
“Mbona na usiku ndugu zangu mnataka nini mpaka mnawinda roho ya kijana mdogo kama mimi kwa mambo ambayo yanaweza kuzungumzika?” Jamal alikuwa akiwaongelesha ili kujipanga na kuwasoma vizuri kwani hakuwa na uwezo wowote ule wa kuweza kuwajua kwenye hilo giza japo alihisi ni wale watatu ambao kuna muda waliingizwa kama wafungwa wapya gerezani hapo.
“Fuata kile ulicho elekezwa kwa mara ya kwanza unaweza ukaipata nafasi ya kuishi tena” sauti moja ambayo ilitoka kwenye mdomo ambao ilipita zaidi hata ya mwezi bila kuujua mswaki ilitamka na kuacha harufu mbaya humo ndani.
“Huo mdomo wako unanuka sana ni vyema ukatafuta mwanamke wa kukufanya ukumbuke namna mwanaume anavyotakiwa kujiweka, hicho mnacho kitafuta mpaka kukipata inabidi watolewe sadaka watu wengi sana ndipo kipatikane hata nyie najua mmetumwa na hamna uwezo wa kuniua kwani na nyie mtauawa hahahahhaahahah” Jamal alikuwa ananunua muda kwa hao wanaume ili awasome aligundua hakuna aliyekuwa na wasiwasi hata mmoja. Ngumi ilitoka gizani aliiona bila shaka kwa mwanaume ambaye yeye alimpa kauli mbaya sana kumwambia atafute mwanamke ikiwa inakaribia kwenye uso wake aliikwepa kwa kurukia pembeni ambayo ilienda kugonga kwenye nondo na hakuwa na imani kama mkono ndio umevunjika au nondo kwenye mkono wake alikuwa bado ana minyororo ni miguu pekee ndiyo ilikuwa imefunguliwa hakupewa nafasi pale aliporukia alipigwa na kisigino ambacho kilimzoa mpaka ukutani alidondoka chini akiwa anatoka damu mdomoni. Hakuelewa ngumi zinapigwa muda gani alikuwa amepokea ngumi zaidi ya sita kwenye hilo giza ambazo zilimfanya ahisi nafsi inamtoka matokeo yake hakufa ila maumivu ndiyo aliyapata vya kutosha mpaka alijuta kuongea jeuri mbele ya wanaume wa kazi. Mwanaume mmoja alimbeba kwa nguvu na kumrusha juu sarakasi za kuvutia kwenye giza zilichezwa na wanaume wawili ambao walimbamizia ukutani na wateke yao manne ya pamoja, kifua chake kilikuwa kinawaka moto watu ambao alikutana nao walikuwa wana roho mbaya unaweza ukadhani hawakuzaliwa na binadamu wenzao.
“This is my time (huu ni muda wangu)” ni sauti ambayo ilionyesha wazi mtu huyo alikuwa kwenye maumivu makali ilisikika wakati wanaume hao wakiwa wanapongezana kwa kupeana tano kazi yao ilikuwa nyepesi kupitiliza, wote walishangaa walihisi huenda wamesikiana vibaya wenyewe ila kwa mbele walihisi kabisa kuna mtu ambaye amesimama. Mwenye upanga ndiye aliyetangulia upanga ukiwa umetangulizwa mbele paja lake lilipokea maumivu ya kutisha ambayo hakuweza kuyakabili aliunguruma akigugumia kwa maumivu hilo lilienda sambamba na kuinama chini kidogo mguu ulikosa balansi hesabu yake ilimalizwa na mguu uliokuwa peku ulikomaa kama mawe ya mlimani hakuongea neno lolote tena aling’ata ulimi wake huyo hata kuongea tena kwenye maisha yake ilikuwa kama ndoto alibaki anajirusha rusha pale chini hatimaye alitulia. Shoka ilikuwa inakuja kwa spidi, ukali wake uliifanye itoe mwanga mweupe kiasi Jamal aliiweka mikono mbele ili kama inamkata uso wake uwe salama MUNGU alikuwa upande wake shoka iliishia kwenye minyororo ambayo ilikuwa mkononi ilikuwa ni bahati mbaya kwa hawa wanaume ambao walikuwa wamebaki wawili humo ndani sasa alikuwa yupo huru kabisaaa mikono na miguu yake alijinyoosha kidogo kisha akainama na kuishika hiyo shoka.
Mmoja wao alisikika akitoa kilio kikali sana ndani ya hicho chumba hali iliyopelekea wafungwa wote kuweza kushtuka humo ndani shoka ilikuwa imepasua mguu wake sehemu ya goti na kuwa vipande viwili, umeme ulirudi ghafla sana kutokana na hizo kelele mwanaume alisogea kwa yule aliyekuwa chini analia kwa maumivu ya kupasuliwa mguu wake kama kuni mwenzake alikuwa ameyatoa macho akiwa pembeni bila kuongea wala kusogea shoka ilichomolewa maamuzi ya haraka sana Jamal aliinyanyua juu na kuukata huo mguu maeneo ya juu ya goti ukilema wa maisha ulikuwa umemvaa huyo mwanaume nadhani alijutia sana kuwafahamu wanadamu halafu anacheza nao vibaya. Shoka ilirushwa kwa yule mmoja aliyekuwa amebaki ilimkosa shingo na kwenda kukita kwenye ukuta alitetemeka mpaka shoka ambayo yeye ndiyo aliyokuwa ameishika kwenye mkono wake ilimdondoka aliinama na kuokota upanga wa mwenzake wa kwanza ambaye alipigwa kikatili kwenye kiza na kujing’ata ulimi akafia hapo hapo, aliokota upanga huo na kujizamishia kwenye tumbo lake yeye mwenyewe mpaka makomando ambao walifika hapo baada ya kusikia zile kelele walibaki wanashangaa baada ya kufika ndani ya hiyo selo, haikuwa kawaida mwanaume imara kama huyo aweze kuchukua maamuzi ya kujiua kirahisi sana namna hiyo walijiuliza sana ila wakati wanageuza macho yao mmoja alikuwa yupo chini amekufa, mmoja mguu ulikuwa kando ya mwili wake na alionekana anahema kwa mbali huyu ambaye alijichoma na kisu tumboni alikufa baada ya dakika moja. Jamal alikuwa ameiweka mikono yake nyuma akiwa hana mnyororo hata mmoja.
“Huyu kilicho muua ni hofu, hofu ndio udhaifu mkubwa sana kwa mwanadamu ukiwa sehemu yoyote ile halafu hofu ikakuingia hauwezi kufanya kitu chochote kile kama upo ni kwenye uwanja wa vita basi tafuta nafasi ya kuweza kukimbia kwa sababu vinginevyo lazima utajikuta unakufa kizembe sana mpaka wewe mwenyewe baadaye unaweza ukaanza kujilaumu na kujiona kama vile umekuwa mjinga. Mtu hatari kama huyu mpaka kachukua haya maamuzi maana yake ameshuhudia mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyafikiria kwenye maisha yake kabisa Professor Daniel alitueleza kwa undani sana wa hili jambo nilipokuwa kwenye chuo kimoja cha siri cha kiintelijensia huko Florida Marekani wakati tunafundishwa kuhusu saikolojia ya mwanadamu” ni mmoja wa makomando aliyekuwepo alikuwa anawaambia wenzake wakati ametoka kumpima mwanaume huyo na kumkazia macho Calvin wote walibaki wanamshangaa yeye alikuwa amefumba macho yake, hakuna aliye muongelesha wala kufanya chochote walimuacha huru na mikono yake alikuja kushtuka na kufumbua macho baada ya kusikia sauti ya nondo zikijifunga watu watatu waliokuwa wamekuja humo ndani na akafanikiwa kutoka salama mmoja ambaye alikatwa mguu na shoka miili yao ilikuwa imetolewa, Jamal hakuweza kuamini aliachwa bila kufungwa alikaa chini na kuwaza sana mpaka pale alipokuja kupitiwa na usingizi kwa mara nyingine tena.
Ilikuwa imepita siku moja tangu mwili wa mheshimiwa makamu wa raisi uweze kupumzishwa, watu walikuwa bado hawajamaliza stori za taarifa hizo mitandaoni zilianza kuzagaa tena habari nyingine za kuweza kupotea kwa manasheria mkuu wa nchi, KIZINGITI CHA KUTISHA CHAITIKISA SHERIA TANZANIA hilo ni gazeti moja lilikuwa limeupamba ukurasa wake siku ya asubuhi kama kawaida ya magazeti yetu jinsi yanavyopenda kuzipamba habari ili kuweza kuwavutia wasomaji. Watu walikuwa wanashangaa imekuwa vipi mtu juzi tu hapo wamemuona kwenye kesi ambayo ndiyo ilikuwa inatikisa nchi nzima leo awe ametekwa, waunganisha nukta za mistari na kuweza kutunga hadithi zao walikuwa tayari wameshayaunganisha matukio moja kwa moja walihusisha kukamatwa kwa Jamal pamoja na tukio hilo wengi wakidai kwamba lazima ni kundi la Kigaidi ambalo linashirikiana na Jamal ndilo lililoweza kumteka mwanasheria wao, wengi walilaani sana wakidai ni vyema Jamal atolewe jela aje auawe hadharani mbele ya watu wote au vinginevyo aeleze mwanasheria wao yuko wapi.
Raisi alikuwa amewaka sana hilo jambo lilikuwa linaenda kumharibia sana jina lake mtu huyo alikuwa mkubwa sana ndani ya taifa hili ilikuwa ni lazima apatikane ili aendelee kujisafishia njia ni siku mbili tu nyuma watu wametoka kumsifia baada ya kuweza kumkamata gaidi mkubwa ambaye aliweza kuondoka na maisha ya makamu wa raisi leo alihitaji kuendelea kulipata jina zaidi kwa kuwapofua macho wananchi wake wasiweze kuujua uhalisia na Ngozi yake halisi yeye yupoje.
“Umesema Colombia?”
“Ndio mkuu”
“How?”
“Hata sisi tumeshangazwa sana na hilo jambo mpaka sasa hatujajua imekuaje”
“Hizo taarifa mmezipatia wapi?”
“Ndani ya usalama wa taifa vijana wangu wameweza kutumiwa hizo taarifa na picha ambazo zinaonekana namna alivyoweza kupigwa huko aliko” mheshimiwa raisi alikuwa kwenye chumba chake cha mkutano akiwa na mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa aliongea huku akiwa anamuonyesha mheshimiwa picha hizo pamoja na video ambazo zilirekodiwa kwa lugha ya kikolombia video ikionyesha namna upanga ulinyofoa vidole viwili vya mwanasheria mkuu bila kuwa na huruma, watu hao wakiwa wanahitaji shilingi bilioni miambili za kitanzania mpaka raisi alishtuka sana.
“Heeey wanahitaji pesa zote hizo za nini?”
“Nadhani wanajua umuhimu wa mtu huyo kwenye nchi ndio maana wamefanya hivi kwa sababu wanajua kwa vyovyote vile nchi lazima imkomboe lasivyo wananchi watahitaji viongozi wa juu ikiwemo wewe wajiuzulu”
“Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani siwezi kuruhusu kirahisi namna hiyo itoke pesa kwa ajili ya mtu mmoja kama huyo ni bora afie huko huko bilioni miambili hivi wana akili kweli hawa kwanza nahitaji ripoti kamili huyu mtu ametekwa vipi wakati ana ulinzi wa kutosha. Una majasusi kibao kwenye taasisi yako watumie hao kuweza kumsaidia vinginevyo ni bora afe siwezi kusaini pesa yote hiyo itoke kwa ajili ya mtu mmoja” mheshimiwa raisi alikuwa anafoka kwa hasira pesa kwake kilikuwa ni kitu kikubwa mno hakuwa tayari kuipoteza pesa nyingi kiasi hicho eti kisa tu kusaidia maisha ya mtu mmoja kwake ilikuwa ni bora mtu huyo afe ila sio kupoteza pes azote hizo, mkurugenzi wa usalama wa taifa alimimina maji na kumpa kiongozi wake huyo kwa heshima ili atulize hasira kwanza wasije wakaharibu kila kitu.
What next? Mchezo bado unachezwa, niseme tu 63 natundika daruga sina la ziada
Bux the story teller
0621567672 (WhatsApp)
0745982347
zote jina FEBIANI BABUYA
Ungana na kalamu yangu kusupport kipaji na kazi lakini pia tuweze kuburudika pamoja.
Wasalaam,
Bux the storyteller