camerlengo
JF-Expert Member
- Jun 28, 2025
- 1,034
- 1,002
Dunga1. Dini zetu mpaka sasa hatujui funga ni lazima au hiyari
2. Dini zetu mpaka sasa hatujui tunafungafunga vipi?
3. Dini zetu mpaka sasa hatujui hii ibada inaanza lini na inatamatika lini na kwa utaratibu gani
4. Dini zetu mpaka sasa hatujui hata ibada ya funga imelekezwa vipi katika vitabu vipi? Huwezi elekeza ibada kubwa kama hiyo kwa mistari miwili.
5. Dini yetu haijatoa hata mbadala kwa mtu ambae hawezi kufunga afanye nini na nini kufidia,,
Hizi ndio sababu tuko bize kuwapopoa kobazi humu na hoja mara ooh wanashindilia misosi usiku,, ohh mara wana kula sana kipindi cha Ramadhani.
Tuacheni chuki za kipuuzi huu mfungo wa wenzetu ni maarufu na wanauheshimu kuliko sisi.
Tazama kuna Ramadhani na Kwarezma lakini swali je Funga gani inasemwa sana na kutrend huko mtaani??
Mpendwa umenifurahisha sana ulipolinganisha Quaresma na Ramadhani na ukauliza katika funga hizi mbili ipi inatrend!1. Dini zetu mpaka sasa hatujui funga ni lazima au hiyari
2. Dini zetu mpaka sasa hatujui tunafungafunga vipi?
3. Dini zetu mpaka sasa hatujui hii ibada inaanza lini na inatamatika lini na kwa utaratibu gani
4. Dini zetu mpaka sasa hatujui hata ibada ya funga imelekezwa vipi katika vitabu vipi? Huwezi elekeza ibada kubwa kama hiyo kwa mistari miwili.
5. Dini yetu haijatoa hata mbadala kwa mtu ambae hawezi kufunga afanye nini na nini kufidia,,
Hizi ndio sababu tuko bize kuwapopoa kobazi humu na hoja mara ooh wanashindilia misosi usiku,, ohh mara wana kula sana kipindi cha Ramadhani.
Tuacheni chuki za kipuuzi huu mfungo wa wenzetu ni maarufu na wanauheshimu kuliko sisi.
Tazama kuna Ramadhani na Kwarezma lakini swali je Funga gani inasemwa sana na kutrend huko mtaani??
Definitely Ramadhan lazima i trend kwa sababu vitabu vya wakristu kupitia Isaya 58 na Mathayo 6 vinaelekeza namna Bora ya funga.
Mathayo 6:16-18
16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Soma pia Isaya 58
Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;