Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


WASIFU WA AKWILINA AKWILINI

Akwilina Akwilini alizaliwa tarehe 1 April, 1996 katika Kijiji cha Olele-Marangu, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, akiwa ni mtoto wa sita kati ya watoto nane wa familia ya mzee Akwilini Shirima.

Akwilina alipata sakramenti mbalimbali katika kanisa Katoliki la Kitongoria. Sakramenti hizo ni pamoja na Ubatizo, komnyo ya kwanza na sakramenti ya kipaimara.

Marehemu Akwilina alisoma darasa la kwanza mpaka la saba mwaka 2004 – 2010, katika shule ya msingi Kitongoria.

Alijiunga na kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2011 – 2014, katika Shule ya Sekondari ya Higland iliyopo mkoani Iringa.

Akwilina aliendelea na kidato cha tano na cha sita katika shule ya Embarai Arusha na baadae Lugalo High School iliyopo mkoani Iringa.

Umahiri na uadilifu katika elimu yake ulimfanya Akwilina kujiunga na Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji, Oktoba 30, 2017 akiisaka shahada ya Ugavi na Usafirishaji NIT.

-----
Zoezi la kuaga mwili lasitishwa kutokana na idadi kubwa ya watu.

Zoezi la kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline limesitishwa katika viwanja vya chuo hicho kutokana na watu kuwa wengi na kutishia kuangusha jeneza lenye mwili.

Ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wengine wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuuchukua mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini ambaye anaagwa leo katika viwanja vya chuo hicho.

-----------------------
Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema. => Maandamano ya CHADEMA: Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

Padri Raymond Mayanga ameitaka Serikali imtafute aliyepiga risasi iliyosababisha kifo cha Aquilina. Pia amemtaka aliyetekeleza mauaji ya mwanafunzi huyo iwe kwa bahati mbaya ama kwa makusudi aliombe msamaha Taifa

---------

Padri Mayanga - Aliyempiga risasi Akwilina awekwe wazi, awaombe radhi watanzania

Padri Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohane Mbatizaji Luhanga amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka mtu aliyempiga risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafishaji (NIT), Akwilina Akwilini, kumweka wazi ili awaombe radhi Watanzania.

Akizungumza katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo inayofanyika katika viwanja vya NIT, Mabibo, Padri Mayanga amesema mtu huyo hata akifungwa miaka 30 hadi 40, Akwilina hatarudi.

“Awe amefanya kwa nia nzuri au mbaya vyombo vinavyohusika vikimaliza taratibu zake kama ni kupitia televisheni ama nini huyu mtu aombe msamaha, vinginevyo hatutafika mbali. Leo kwa Akwilina huenda mwingine,”

----

Waombolezaji wabeba mabango yenye jumbe za kuwataka IGP Sirro, Kamanda Mambosasa na Waziri Dr. Nchemba kujiuzulu
Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwamo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.

Ibada hiyo inafanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.

Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliponyanyuka kutoa salamu kwa wafiwa kama walivyofanya viongozi wengine, akiwamo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Baadhi ya ujumbe katika mabango hayo ni; “muuaji hawezi kujichunguza na Mwigulu, Sirro kwa mauaji haya bado mko ofisini.”

Juhudi za kuwataka waombolezaji hao kushusha mabango ziligonga mwamba kutokana na baadhi ya watu waliokuwa karibu yao kuja juu, wakitaka waachwe kwa maelezo kuwa wana haki ya kufanya hivyo.

Katika salamu zake za rambirambi, Profesa Ndalichako alisema: “Rais Magufuli ameshaagiza uchunguzi ufanyike na mimi kama waziri nasisitiza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi haraka.

“Matukio ya aina hii hayapaswi kuendelea, nimehuzunika kwa msiba huu na naomba Watanzania waungane kuiombea familia.”

----

RC Makonda - Tusinyooshe vidole kifo cha Akwilina

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wananchi kuacha kunyooshea vidole na kurushia lawama juu ya kifo cha mwanafunzi Akwelina Akwilin kwani Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wake na watakapomaliza watatoa taarifa kamili.

Makonda ameeleza hayo wakati aliposhiriki katika ghafla ya kuaga mwili wa marehemu Akwelina katika chuo cha Taifa cha Usafrishaji (NIT) ili aende kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Mkoani Kilimanjaro.

"Jeshi hili la Polisi litatupatia majibu watakapomaliza kazi yake, ombi langu kwenu wananchi wa Dar es Salaam hasa wale ambao hatujawahi kusomea mambo ya uchunguzi na wala hatuyajui tusiwe wa kwanza kunyoosha vidole na kuhukumu kabla hatuja hukumiwa. Mimi najua mtoa hukumu wa kweli ni Mungu na anazo siri zote kwa nini Akwilina ameondoka tarehe 16",


Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "naendelea kuwasihi tuwape nafasi wenye majukumu yao watimize kazi yao na hatimae na sisi tuunganike mkoa kama taifa kuhakikisha amani inatawala katika mkoa wetu kwa kila mtu".

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameitaka familia ya marehemu Akwelina iwe yenye uvumilivu katika kipindi kigumu walichonacho kwa sasa.

-----
Waombelezaji waliobeba mabango kwenye msiba wa Akwilina wanyang'anywa

 
Kwani wewe uko salama?! Akwillina alijua kama yuko hatarini?! Kemea upumbavu huu!!!
Anayedhani yuko salama asikilize vizuri clip ya mama Aquilina akimwambia prof Ndalichako kwamba alikuwa akisikia kwenye vyombo vya habari watu wanauawa na polisi lakini hakutegemea hata siku moja kwamba hilo litatokea kwa mmoja Wa wanafamilia wake. AJIDHANIAYE AMESIMAMA AANGALIE ASIANGUKE.
 
Vipi tena wanaongoza maandamano wakati hayaruhusiwi kabisa!!!! wamepata kibari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…