Ibada ya Wakristo kuabudu Jumapili imeanza Karne ya nne. Ni kwanini Karne 3 za kwanza watu waliabudu Jumamosi?

Unaijuaje Jumamosi? KWA KUANGALIA KALENDA. hiyo kalenda imeundwa na nani? NA PAPA GREGORY WA KANISA KATOLIKI. mpaka hiyo kalenda inaanza kutumika kulikuwa na kalenda kabla yake? NDIYO ZILIKUWEPO NYINGI TU ILA ZILIKUWA NA MAPUNGUFU MENGI. marekebisho yaliyofanyika yalihusisha kubadili siku na tarehe? NDIYO. Kama ni hivyo kuna uwezekano jumamosi ya sasa ni jumatano ya enzi za Musa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Nasadiki kwa Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume", period

Na ndiyo dini ya ukweli ya Ukristu ambayo ilianzishwa na Mtume Petro alipokabidhiwa kondoo awachunge na Bwana Yesu Kristu (Mathayo 16:18). Wengine wote ni waprotestanti na wapinga kristo.

Wasabato siyo DHEHEBU LA KIKRISTU bali ni CULT (Itikadi) iliyoanza baada ya Nabii wa Uwongo kushindwa utabiri wake juu ya mwisho wa Dunia kuwa ni mwaka 1844
 
Tuache hayo majina ya sunday na saturday. . .

Nazungumzia ibada ya siku ya 7 na ibada ya siku ya kwanza
Kirabu mwanzo sura ya kwanza kinaongelea kuwa Mungu alipumzika siku ya Saba je wakati anapumzika kulikuwa na kalenda kama tulizonazo leo?

Toa uthibitisho kuwa Mungu siku aliyopumzika ndio hiyo mnayoita Jumamosi

Jumamosi iko.wapi.kwenye kitabu cha mwanzo?

Hata kwenye torati Musa alipewa aliambiwa tu fanyeni kazi siku sita ya saba pumzikeni

Hakutaja siku.kwa jina kuwa ni jumatatu, jumanne nk sababu kalenda hizo hazikuwepo

Toa uthibitisho kuwa Musa siku alipowr amri 10.hiyo sabato aliambiwa ni Jumamosi
 
Umemjibu vyema sana .
Mimi ni mlokole na siku si kipaumbele kwangu.
Lakini najiuliza kwanini sisi ambao siku si kipaumbele kwetu jumapili ndio siku kuu kwetu?
Makanisa karibu yote Jumapili ndio siku kuu. Kwanini Kila kanisa lisipange siku yake ya kufanya ibada kuu?
Hii nadhani ni impact ya Roman waasisi wa Jumapili kwakuwa makanisa mengi bado yana miiko ya Roman.
Hata Sheria za ndoa makanisa mengi yamekopi Sheria za Roman Catholic
 
ni desturi tu, wala haimaanishi kwamba Mungu anapatikana zaidi siku ya jumamosi au jumapili.,Mungu anapatikana na anatakiwa kuabudiwa kila siku kila saa kila dakika kila sekunde moyoni mwako. unatakiwa kuishi na uwepo wa Mungu muda wote na uongozwe na Roho Mtakatifu muda wote.ndio ibada hiyo.
 
Ulivyoandika kama vile dunia iliumbwa. 😂😂😂 Mambo umeletewa alafu unataka uyachimbe unauhakika gani huko karne ya kwanza na pili hawakusali jumapili. Yaliopita yaache maana hukuyaanzisha wala kwenye line ya kizazi chako hakuna alieanzisha wote mmepokea iwe kwa mzungu au muarabu
 
Hiyo dini inayosema ua kuitetea halafu utapewa mabikra 72 wanakusubiri peponi.

Yaani kwenye uislamu cha maana ni ngono peponi tu.?

Vipi naye mwanamke akiua atapewa wanaume wangapi wamshughulikie?
Wewe mbinguni unataka uwe unafanya nini? Uwe Unakesha unaimba milele na milele bila kupumzika? Si Bora ufe tu.
Huoni Raha kupatiwa mabikra watamu walionawiri kutoka kwa Allah?
Kuhusu wanawake Mimi sijui, Allah ndiye anajua

Deen ya haq Kwa bin Adam ni moja tu, Islam.
 
Nao wanawake watapewa marijali 72
 
Sikia sifa za mnyama wa kutisha (Daniel 7:25)
1: Ataazimu kubadili Nyakati na sheria
-shika kitakatifu Siku takatifu
-Kunywa kidogo usilewe
-Husijifanyie sanamu, yeye kaweka Salamu Maria na mnara
2: Atanena kinyume chake Aliye juu( MUNGU)
- Sabato ni Jumamosi/ Sabato ni ya wayahudu, kwa hiyo salini jumapilii
 
Hahaaaaa, una akili sana
 
Hayo ni maagano ya Mungu kwa wayahudi kwenye agano la kale ambapo walikuwa na siku iitwayo sabato na sina uhakika kama ni hiyo Jumamosi unayoongelea hapo.

Vipi kuhusu agano jipya? Binafsi naamini Ijumaa ndio siku ya mwisho ya wiki.

Jumamosi - moja
Jumapili - mbili
Jumatatu - tatu
.
.
Kwa mtiririko huo. Ijumaa ndio siku ya saba ya wiki.

Pia kama kweli wewe ni mfuasi wa hizi imani ambazo tumeletewa na wazungu (ukristo) na waarabu (uislamu) nadhani kuna mambo ya msingi na muhimu zaidi ya kuzingatia katika kuishi maisha yenye kufuata misingi ya hizo dini lakini suala la siku gani ya kuabudu sio la msingi.

Ukienda nchi zenye mlengo wa dini ya kiislamu hata makanisa huwa yanaabudu na kufanya misa Ijumaa. Mfano Algeria
 
Sio kweli, Ilianzia na mfalme Constatino baada ya kuokoka na kuwa mkristo
Alichokifanya constantino ni kuruhusu uhuru wa ki-dini, na sio kuanzisha jumapili. Unaanzishe kitu kilichokuwepo kabla yako ?. Wafalme wote kabla ya constantino walitesa na kudhulumu kanisa kitu ambacho kilifanya wanakanisa waabudu kwa maficho, wasali kisirisiri na mafichoni, baada ya kuruhusu uhuru wa kidini kila kitu sasa kikawa open kwa uhuru kwa kila mmoja kusali na kuabudu achojua na kwa siku na muda anaoujua yeye.
 
Nasubiri mrejesho wa hili. Kwa mwenye jibu asaidie hapa
 
Mie nikifika hapo tu kwenye mambo ya dini vile kila mtu alikaririshwa imani yake ndo sahihi halafu wanachokiamini wengine sio sahihi huwa nachoka!
Kila dhehebu wanaamini ya kwao ndo njia sahihi! Mie naona hata kwenye hizi dini huenda tulipigwa ili angalau dunia iwe rahisi kutawalika ila sasa hawa walioleta dini walikosea wangehakikisha dini inakuwa moja dunia nzima na vizazi vyote wangekaririshwa dini moja tu mpaka hapa ingekuwa poa sana
Ila wakaacha dini mbili ukristo na uislamu halafu imani zao na vitabu vyao vinapishana sana mbaya zaidi dini hizi kwa sasa zimezaa matawi ya madhehebu tofauti ambapo kila mmoja anaamini ya kwake.
Anyway acha nibaki na kile nnachokiamini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…