Ibara ya 100 ya Katiba ya JMT imewapa wabunge Uhuru wa kujadili Hoja na Mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na Mhimili wala Mtu yeyote. Tusiwaingilie

Ibara ya 100 ya Katiba ya JMT imewapa wabunge Uhuru wa kujadili Hoja na Mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na Mhimili wala Mtu yeyote. Tusiwaingilie

Imetamkwa wazi kabisa wabunge wapo huru kujadili hoja na mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na mtu au mhimili wa dola. Ipo wazi katika ibara ya 100(1) kwa hiyo sioni haja ya kuwapangia nini cha kujadili...
Ila sio kwa mijadala iliyoendeshwa na kusimamiwa miaka ya hivi karibuni,kama ni kazi wasimamizi wameshindwa.
 
Pia katiba imetamka kila mtu yupo huru kutoa mawazo/maoni yake, hivyo katiba inaruhusu watu kutoa maoni juu ya mwenendo wa bunge

Hivyo usitufunge midomo
Kutoa maoni sio kuwapangia wajadili kitu gani. Tumia ubongo kufikiri.
 
Imetamkwa wazi kabisa wabunge wapo huru kujadili hoja na mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na mtu au mhimili wa dola. Ipo wazi katika ibara ya 100(1) kwa hiyo sioni haja ya kuwapangia nini cha kujadili...
Wabunge wakileta fyofyoko kwa kauli ya Rais stalivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine...Hilo likitokea ni robo tu ya wabunge was Sasa watarudi bungeni
 
Well said my friend!

Lakini kumbuka kama alivyotuambia JPM muhimbili mmoja - Executive umejichimbia zaidi ardhini

Au nasema uongo jamani 😆😆😆
 
Wabunge wakileta fyofyoko kwa kauli ya Rais stalivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine...Hilo likitokea ni robo tu ya wabunge was Sasa watarudi bungeni
Hakihusiani na ibara ya 100. Hata kukiwa na bunge lingine ibara ya 100 itabaki hivyohivyo labda ibadilishwe.
 
Kutoa maoni sio kuwapangia wajadili kitu gani. Tumia ubongo kufikiri.
Yani kwa akili yako finyu mtu akikwambia "badala ya kufanya jambo hili ungefanya lile" hayo sio maoni? Au hata maana ya neno maoni huelewi?

Alichokiongea Samia kuhusu bunge hata wewe unaweza kukiongea. Au unahisi sio maoni kwa kuwa aliyeongea ni Samia?
 
Kuna tofauti kati ya kilichoandikwa na uhalisia.

Hakuna mbunge huru hapa Tanzania, wote wanadhaminiwa na vyama. Chama kinaweka nidhamu kwa misimamo ya chama, Madam Hassan anaenda kuwa mwenyekiti, sasa akiongea halafu mbunge mmoja kutoka CCM alete fyokofyoko ndio atajua kama hajui.
 
Kwa hiyo wakijadili upumbavu na kudemka tueasikilize tu kwa sababu Katiba imewapa uhuru? Mbona tunaambiwa kuwa Uhuru nao una mipaka?
 
Hayo unayasema wewe. Katiba ni sheria kuu ya nchi. Hakuna aliye juu ya katiba.
Je sheria zote zinafuatwa hapa Tanzania? Au wewe Ni mbunge umekuja kujibu Kiana, bila Rais hakuna Bunge so elewa Hilo .
Hao wabunge wote Ni vibogoyo mbele ya Rais maana wote ili wawe wabunge lazima wapite mikonon mwa Rais kupitia chama Chao ambapo Rais ndie mwenyekit. Ni mbunge gan kwa Tanzania anaweza tumishiana msuli na Raisi? Sasa Kama wanajiweza waendelee kupiga kelele zisizo na tija nadhan majibu watayapata hasa 2025 wengi wataliwa vichwa .
 
Imetamkwa wazi kabisa wabunge wapo huru kujadili hoja na mijadala mbalimbali bila kuingiliwa na mtu au mhimili wa dola. Ipo wazi katika ibara ya 100(1) kwa hiyo sioni haja ya kuwapangia nini cha kujadili.

Ibara ya 100(2) imepigia mstari kabisa kuwa wabunge hawatashitakiwa kwa chochote watakacho jadili wakiwa bungeni.

My take; tuwaache wajadili na kufunguka ili tujue nani ni mwema na nani ni mnafiki.
Hayo mbona hamkusema wakati mnapangiwa ya kuongea na jiwe? Yaani wasukuma magufuli kawaharibu sana
 
Back
Top Bottom