Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,384
- 3,926
Boxer ni mchezo ambao unahitaji umpelekee mashambulizi mwenzako ili wewe ushinde. Lakini pamoja na mashambulizi hayo, yupo refa na Masecond ambao wote kazi yao ni kuwalinda mabondia ndani ya uwanja.
Lakini ni kazi ya bondia pia yeye mwenyewe kujilinda. Lakini la ziada kabisa ambalo mabondia nadhani wengi hawalijui ni kumlinda pia mpinzani wako pale inapofikia hatua ya hatari kama hatua ya kumuona jamaa anaelekea kupoteza fahamu au kufa.
Tarehe 16 mwezi wa kwanza Mwaka 1999 Mike Tyson alipigana na Francois Botha na akampiga Botha akadondoka vibaya sana, lakini Tyson hakushangilia. Alichokifanya alishirikiana na refa kumnyanyua Botha ili asianguke tena.
Huo unaitwa ubinadamu ndani ya mchezo, ule ni mchezo na sio vita.
Alichokifanya Ibrahim Classic kwa mpinzani wake Allan Pinna sio kitendo cha kiungwana kabisa, na sijapenda maana Pinna alikuwa keshalewa anaenda chini mwenyewe Ibrahim Classic alikuwa na haja gani ya kutumia nguvu za ziada kumpeleka chini haraka?
Lakini leo hii watu wapo kimya kwa vile labda Ibrahim Classic ni bondia wetu kampiga bondia wa kigeni. Imagine kama pinna ndiyo angempiga jamaa hivyo.
Leo hii watu wengi wangemtukana sana Pinna, tungekilaani kile kitendo kwa nguvu zote.
Pinna jana katoka salama ndani ya uwanja hilo ni jambo la kushukuru, ila kama Pinna atakuja kufa kutokana na athari zilizotokana na lile pambano nadhani Ibrahim Classic hawezi kukaa kwa amani kamwe katika maisha yake.
Mabondia wanatakiwa wapewe elimu ya kujilinda, kuwalinda wapinzani wao na utu na ubinadamu ndani ya ulingo.