Ibrahim Traore anatoa wapi fedha za kufanya maendeleo makubwa hivi Burkina Fasso?

Huna akili
 
Kwa hapa bongo CCM ni tatizo na sasa hivi tunaongeza majimbo ya ulaji
 
Hili mimi ndio waga silikubali kabisa kwa sisi waafrika kutafuta mchawi kwa matatizo yetu tunayojiletea wenyewe. Yaani tujiibie wenyewe kisha tusingizie wazungu ni unafiki wa hali ya juu sana.
 
Hili mimi ndio waga silikubali kabisa kwa sisi waafrika kutafuta mchawi kwa matatizo yetu tunayojiletea wenyewe. Yaani tujiibie wenyewe kisha tusingizie wazungu ni unafiki wa hali ya juu sana.
Ambacho saa nyingine unajifanya hujui ni kwamba hawa viongozi wezi ndio wanaopendwa sana na mabeberu.
Viongozi wasiotaka wizi na ufisadi katika nchi zao kama hawa akina Traore na Magufuli hawapendwi na mabeberu.
 
Mkuu, waafrika tunaweza sana, ila kila leo tunaambiwa na watu wabaya kuwa deni linahimilika
Kama linahimilika hizo hela zinaenda wapi?
Tumekuwa watu wa hovyo sana
Na wazungu watakupa misaada ili uendelee kuwa tegemezi
 
Tafuta documentary ya aljazeera,africa; changing direction ya burkina faso,hayo matrekta hayatoshi,watu wanakodi matrekta binafsi ambayo ni bei juu,mbolea inapigwa zengwe
 
Yeye anabana matumizi mabaya ya serikali, wizi wa mali za umma, anazuia rushwa na matokeo yanaonekana. Hapa Tanzania Magufuli alifanya hivi CCM wakamuua kwani alikuwa anawaumbua kwa kubana interests za watu wachache wasiokuwa na thamani yeyote katika nchi yetu mfano Mze Makamba na wapuuzi wenzake. Kwa muda mchache sana, Magufuli aliweza faya maajabu ambayo hata wewe unayaona......hii kitu inawezekana hapa Afrika sema tu hatuna viongozi wa ukweli, si mnaona hata Mama anavyoboronga hapa kwetu hivi sasa? Kwa hivi sasa wizi upo nje nje, machawa ndiyo wanaheshimika kwenye utawala huu wa Mama. Imagine, mtu hana hili wala lile lakini ndani ya CCM kwa hivi sasa anaheshimika shinda mbunge au waziri wa wizara. Nilishangaa majuzi pale Mlimani, niliona mawaziri na wajumbe wanamsujudu mtu kama Steve Nyerere, are we serious kweli.....yaani ndiyo tumefikia hapa baada ya kifo cha shujaa wetu Magufuli? Eti kuwadi anayenadi kina Mama na madada wa mjini anakuwa zaidi ya waziri? Ndiyo maana Afrika tunadharauliwa sana in World Politics kwa ujinga kama huu, nobody will take us seriously kama sisi wenyewe hatujiheshimu na kuwa serious na maamuzi yetu.
 
Hata kama humpendi jiwe yule mzee huwezi kumbagadha!
 
Chai
 
Swali la mada ni fikirishi, hiyo imenipeleka kuleta kijipande kidogo na fikirishi cha spichi cha D.Trump akigusia changamoto na masuluhisho ya Immigration US.

Raisi wa Marekani D.Trump, alisema

"...we must have legislation to secure the border. But it turned out that all we really needed was a NEW PRESIDENT..."

Kwa msingi huo, sidhani kama Tanzania ama nchi nyingine za Afrika zinahitaji, sheria au fedha per se kupata maendeleo, labda ni New President? Na Maamuzi magumu?

kwa hayo, sidhani kama ni fedha ndiyo iliyowasumbua na upatakanaji wa maendeleo, naona ni maamuzi magumu ambayo ameyachukua Rais Traore ndio yanayo wapatia wananchi wake matamanio yao ya maendeleo, kama ilivyomchukua D.Trump na maamuzi magumu kufikia tatuzi ya immigration.
 
Ambacho saa nyingine unajifanya hujui ni kwamba hawa viongozi wezi ndio wanaopendwa sana na mabeberu.
Viongozi wasiotaka wizi na ufisadi katika nchi zao kama hawa akina Traore na Magufuli hawapendwi na mabeberu.
Huo ni uongo wa wazi kabisa, wakati wa Magufuli ni nani alikamatwa na kuhukumiwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa mali ya umma na kwa nini alimtimua CAG kufuatia CAG kugundua wizi wa shilingi trilioni 1.5 za umma..!!??😧😧😧
 
Fedha za misaada amezikataa anaseme ni Ukoloni Mamboleo.
 
Mwamba anasafiri kwa kutumia Pickup utadhani Afisa Ugani. Halafu hapo nyuma yake kuna Mwamba amebeba Briefcase amenikumbusha enzi za Utawala wa JPM hapa Tz.
 
Niambie ni mikakati gani iliyo wekwa na Magufuri kubana matumizi ya hovyo?

Alafu Magufuri si ndo muasisi wa kugawa vyeo kwa misingi ya uchawa
Huyu mama si anaiga tu?
 
Mwamba anasafiri kwa kutumia Pickup utadhani Afisa Ugani. Halafu hapo nyuma yake kuna Mwamba amebeba Briefcase amenikumbusha enzi za Utawala wa JPM hapa Tz.
Magufuli na yeye alikuwa anapanda pickup?
 
Propaganda hizo mkuu.

Hakuna rwliable sources ya hayo mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…