Ibrahim Traore anatoa wapi fedha za kufanya maendeleo makubwa hivi Burkina Fasso?

Magufuli na yeye alikuwa anapanda pickup?
Hujanielewa Ndugu yangu. Sijasema Magufuli alikuwa anatumia pickup kusafiri ila nimesema kuna Mlinzi Mmoja wa Traore amebeba Briefcase kama alivyokuwa anabeba Mpambe mmoja wa Magufuli enzi za Utawala wa JPM.
 
Hapa kwetu wakulima wa mpunga wanafukuzwa mbugani kupisha hifadhi na uwekezaji kwenye michikichi! Njaa ikiingia nchini mnasingizia Mungu. Uimara wa Taifa ni pamoja na kuwa na chakula cha kutosha kwa watu wake, nimependa sana Traore anavyohamasisha wananchi wake wazalishe chakula cha kutosha ili Taifa lisikumbwe na njaa
 
Afrika tunawalaumu wazungu bure tu ila ukidhibiti ufisadi tu wa viongozi wa umma na taasisi zake unaweza kufanya maajabu refer JPM.
 
Pesa za misaada kataa, simamia rasilimali zako vizuri na utapata pesa za kigeni. Swala ni uongozi tu!
 
Huku kazi ni kulindana na kuteyeana ili mfumo husitoke madarakani upuuzi mtupu watu wamaliza rasilimali za nchi na watu masikini wanabaki kushangaa tu na kuteseka hongera kwa Mwamba kaweza
 
Haibi wala kutumia vibaya kama mama yenu na chawa wake. Simpo
 
Daaah my country people
 
Nimesoma nikiwa na furaha iliyochangamana na huzuni.

Viongozi wazuri na wanaojielewa wapo tatizo wajinga wajinga waliojaa Africa ndiyo wanalazimisha watawala wabovu ili wanayoyafanya yaende huku wananchi tukivuja jasho la damu bila mtetezi.
 
Una uhakika mkuu wewe hutumii hisia unapomzungumzia Magufuli?
 
Huna unachokijua ni bora ukae kimya tu. Inaonesha wewe ni miongoni mwa wale waliojeruhiwa na utawala wa JPM kwa either kwenye vyeti feki, uzembe, ufisadi au ubadhirifu.
 
Kitakachoiokoa Africa ni uzalendo wa viongozi wake na wananchi wala sio vyama vya siasa maana humo kwenye vyama ndipo mafisadi hujifichia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…