Ibrahim Traore: Huu ndo ujinga na upumbavu wa Waafrika!

Nilikuwa nasubiri uzi huu
Yaani huwa nacheka sana kwa ujinga wa baadhi ya watu.
Wanaamini kila kitu, halafu AI ndio imewapumbaza kabisa hawajui ukweli ni upi na uongo ni upi.

Kuna clips mpaka eti kashuka kwenye msafara kufukuza ng'ombe aliekuwa barabarani πŸ˜„

Ila mipakani mwa BF kuna magaidi wanaopiga kila siku

Hili hawalioni kabisa
Kuna mtu aliandika humu eti atamlinda kwa kila hali Ibra, halafu naona anaandika akiwa bongo
Hata njiwa zake hawezi kulinda huyo
Habari kama hizi hawazijui kabisa
Kweli binadamu wana mahaba acha na mimi nishambuliwe
 
Unakumbuka kile kipindi cha marehemu rufufu lugha zote anajua kutafsiri.
Waafrika kwenye udadavu hawapo kabisa ndio maana akili zime lala
 
Kwa nini watu wanampamba kwa mambo ya uongo na uzushi?

Hakuna nyomi lililojitokeza Paris na kuandamana kumuunga mkono..

Ila watu wanatengeneza videos na watu wanatoa maoni utadhani ni kweli!

Why?
Nakubaliana na wewe kwamba "habari nyingi kumhusu yeye ni za uongo" ila hiyo documentary au habari niliyotuma hapo juu ni kutoka kwa moja wa "youtuber" anayeaminika barani Afrika.

Kama umeingalia utaona dogo Lè Capitain Ibra Traore anavyoibadilisha Burkina na jinsi waBurkinabe wengi wanavyomkubali na kukubali mrengo wa uongozi wake.

Hizi chuki nyingine ni vile viongozi wengi wa Afrika ni vibaraka wa mataifa ya ulaya, hawafurahishwi na popularity ya dogo kwa kuhofia yasije tokea mapinduzi kwenye nchi zao pia.

So far so good nakubaliana na dogo. Nchi zetu inapaswa tuwe na mfumo/ mifumo yetu ya uendeshaji wa nchi zetu na siyo hii demokrasia tuliyokaririshwa miaka nenda rudi. Ni ngumu kutoboa ila inawezekana.

May GOD of our Ancestors guide and protect huyu dogo.
 
Sasa kama anafanya vyema kwa nini mambo mengi kumhusu yeye ni ya uongo?

Tena uongo ambao ni rahisi sana kuufuatilia na kujua ukweli wake?
 
Hiki kijamaa chenye mashavu kama kinapuliza moto wa kuni ndio kinaongoza propoganda za uongo za Ibrah Traore mtandaoni
Kushambulia muonekano wa mtu 1. Unaonekana bado una fikra duni, huwezi jenga hoja mpaka ushambulie muonekano wa mtu. 2. Haiondoi ukweli kuwa dogo anafanya makubwa kwa kadri ya uwezo wake na nchi yake.
Kama unaona huyo "kijamaa" kama ulivyo muita anafanya propaganda, chukua hatua panda 'pipa' nenda kwa ground utuletee habari za uhakika.

Bila udikteka wenye manufaa kwa nchi, ni ngumu mno kutoboa sisi waAfrika.
 
Sasa kama anafanya vyema kwa nini mambo mengi kumhusu yeye ni ya uongo?

Tena uongo ambao ni rahisi sana kuufuatilia na kujua ukweli wake?
Kwa Dunia ya sasa ngumu kuzuia watu kupenyeza habari za uongo. Kuna mdau hapo juu amesema ni namna watu wanapita/kutembea na upepo wa Traore ili account zao zipate watizamaji (viewers) wengi
 
Hakualikwa kuhudhuria uapisho wa Trump hivyo hakukataa mwaliko.

Huwezi kukataa mwaliko wa hafla ambayo hujaalikwa.

Pia, hakuna nyomi la watu lililoandamana Paris kumuunga mkono.
Habari hio ya watu kuandamana Paris ni Traore ndiye alipost, au muandishi wa habari wa ikulu ya nchi yake?
Mitandao ya kijamii kuna watu wana post uongo mwingi, uzushi n.k...

Hivi kuna nchi zenye propaganda technique kama nchi za magharibi, jamaa ni waongo balaa... nachofahamu kila raisi wa USA alishazungumza uongo kuanzia kwenye masuala ya vita, kodi hadi masuala ya afya..
 
Halafu sijui kwaninj nyie madiaspora wa kiafrika unaoishi huko kwa mabeberu ndio huwa mnaumizwa na kumchukia sana Captain Traore.

Nyie manyani mliowea kwa wazungu wengi wenu ni wapumbavu sana
 
Tatizo la waafrika ni kupenda kusifiwa huyu rais wa Burkina Faso naye yuko kwenye jahazi hilo hilo na hata Tanzania tuna rais sampuli hiyohiyo.

Rais wa kwanza wa Marekani George Washington alikaa ikulu kwa miaka minane tu na akiwa bado anapendwa sana na wananchi aliamua kuachia ngazi wakati katiba yao bado haikuwa na ukomo wa mihula.

Kwa waafrika ni shida kubwa sana mtu kuachia ngazi kwa hiari na nina hakika hata huyo Traore ni walewale wa kung'ang'ania madaraka.

Time will tell.
 
Mkuu hiyo siyo story,mzigo umeshaanza kitambo hata ukitaka nikutumie ushahidi wavideoz usiwaze .

Jealous down,dogo anajitahidi wazee
 
So issue ni watu kuuwawa ama??,wafuatuliaji wote wa mambo wanajua kuna vita vinaendelea kaskazini mwa nchi hiyo na ni ugaidi uliosababisha na mataifa ya magharibi hasa Ufaransa hilo lipo wazi.
 
Kwani hizo habari kazipost Traore mwenyewe au content creators wanaotafuta ugali wao kupitia wimbi hili la Traore?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…