Idadi kubwa ya Waislam (99%) inaweza kuwa kikwazo cha Uturuki kutokuwa mwanachama rasmi wa EU?

Kwani turkey wameomba kuingia EU au EU wanawaomba wao?
TURKEY ndo anaomba, na uko nyuma aliwatishia kuwa :, endapo wakizingua kuhusu OMBI lake, basi ataawachilia wahamiaji haramu walio kwenye makambi hapo Turkey waingie Ulaya.

NOPE:, kuna fungu umoja wa Ulaya inailipa uturuki ili kuwazuia wahamiaji wasiingie Ulaya.
 
Dini yao ndio tatizo, Wazungu wanaubaguzi sana kwa Uislamu, Ila tabia yao ya kuendelea kujipendekeza ni kuendelea kujiaibisha tu
SIO KWELI..
WAZUNGU NI WATU WASIO JARI SANA IMANI YA MTU..
HATA UKIWA UNAABUDU MAVI, WATAKUHESHIMU NA IMANI YAKO PIA.

Nb: mi naona shida ni living standard yao inaweza kuwa ndo tatizo.. (nina guess tu).
 
SIO KWELI..
WAZUNGU NI WATU WASIO JARI SANA IMANI YA MTU..
HATA UKIWA UNAABUDU MAVI, WATAKUHESHIMU NA IMANI YAKO PIA.

Nb: mi naona shida ni living standard yao inaweza kuwa ndo tatizo.. (nina guess tu).
Umejitahidi sana kufafanua mzee wa Yanga
 
Dini yao ndio tatizo, Wazungu wanaubaguzi sana kwa Uislamu, Ila tabia yao ya kuendelea kujipendekeza ni kuendelea kujiaibisha tu
Mkuu, ninadhani wanaendelea kujipendekeza kwa maana wapo NATO ambayo mpaka sasa haijawapa manufaa yoyote ya moja kwa moja zaidi ya kuwaingiza katika mgogoro na U.S.S.R kipindi kile jupiter missiles za USA zilipokuwa pale Turkey pamoja na Italy.
 
Mkuu, ninadhani wanaendelea kujipendekeza kwa maana wapo NATO ambayo mpaka sasa haijawapa manufaa yoyote ya moja kwa moja zaidi ya kuwaingiza katika mgogoro na U.S.S.R kipindi kile jupiter missiles za USA zilipokuwa pale Turkey pamoja na Italy.
Mkuu usipotoshe kati ya nchi iliyo nufaika na Nato basi ni Turkey, kwa sababu baada ya kuanguka kwa Ottoman Uturuki ilikuwa dhaifu sana ,na Wakati huo huo ilikuwa na uadui na Usoviet kwa hiyo ilikuwa ni lazima tu ajiunge na nato apende asipende kwa ajili ya usalama wake.
 
Kama Uturuki ina umuhimu kwa NATO, kwanini bado wanagoma/wanasita kuwapa uanachama wa EU? Au uislam wao ndio kikwazo?
Mkuu kumbuka EU na NATO ni taasisi mbili tofauti kabisa na zina majukumu tofauti.
Na kila taasisi ina mashariti yake.
Mfano NATO ina wanachama nje ya bara la ulaya ,wakati EU hairuhusu nchi kutoka nje ya bara la Ulaya.
 
Ukiachana na Ubaguzi kuna ishu ya Democrasia pia, Uturuki Democrasia yao ni ya mashaka mashaka sana, na EU kama huna Democrasia ya kueleweka huwezi jiunga.

So Uturuki hata kwenye mambo ya haki za Binadamu bado hajafikia kiwango cha EU,
 
Ila naona kama Erdogan ........ameanza kushtuka flank hiv .......kuanza relation na Russia .........
(1) Kuna ndege vita moja ya Russia ilipigwa na kombora la Uturuki wakati wa kupambana na ISIS. Putin na Erdogan walivutana sana katika suala hili.

(2) Kama sijakosea pia, kuna balozi mmoja wa Russia nchini Turkey aliuwawa mbele ya wanahabari wakati anafanya press conference ila mpaka leo imebaki kuwa ni siri kati ya nchi hizo mbili.

Pia unachokisema ni sahihi sana mzee baba kwamba Putin na Erdogan kwa sasa wapo katika mahusiano yanayoridhisha...
 
Yaaah mkuu coz nilisikia Erdogan anataka kununua mifumo ya
Ulinz wa Anga kutoka RUSSIA ad

Trump alimind turkey
 
Ukweli ni kwamba kijiografia eneo la Uturuki lipo katika mabara mawili, kuna eneo lipo Ulaya na kuna eneo lipo Asia.

Tukija kwenye hoja ya kujiunga katika Umoja wa Ulaya, ni wazi kuwa umoja huu umejengwa chini ya mikataba ya haki za binadamu zinazotambua usawa kwa kila binadamu. Uturuki ina waislam wengi, ndani ya uislam hakuna usawa wa mwanamke na mwanaume.

Kwa muda mrefu Uturuki imekuwa ikitaka kujiunga na huu umoja ila sharti lilikuwa ni kurekebisha sheria zake ili ziendane na zile za umoja wa Ulaya.

Ila kuna hoja iko hapa, members wa EU wana uhuru wa free movement kwa wananchi wa nchi husika, ukimruhusu Turkey kuwa mwanachama, waarabu wanavyopenda Ulaya watakuwa wamepata daraja, hivyo lazima ipigwe spana kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…