Idadi kubwa ya Waislam (99%) inaweza kuwa kikwazo cha Uturuki kutokuwa mwanachama rasmi wa EU?

1.2% , sawa na watu zaidi ya 1.5m ni waarabu au wana asili ya kiarabu, ni kundi la tatu kwa ukubwa nchini Uturuki
Wana asili ya kiarabu,haiwezekani wawe waarab wa uturuki,wahamiaji kwa vizazi,Kama mnyamwezi wa igunga kutoka iran
 
Uturuki ni nchi hata wakurdi wapo wenye uraia wa Uturuki, hivyo basi hata waarabu wapo wenye uraia wa Uturuki, hakuna jamii inaitwa waturuki ni nchi ile
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa JamiiForums

Je, idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislam (99%) inaweza kuwa ndio kikwazo kikuu cha nchi ya Uturuki kutokuwa mwanachama kamili/rasmi wa E.U mpaka sasa?

Walikubaliwa haraka kujiunga NATO kwa maslahi ya kijeshi kama daraja la Wazungu kuingia Middle East? Uturuki kama mwanachama wa NATO aliruhusu jeshi la Marekani kutumia anga lake wakati wa vita vya kumpiga Saddam Hussein mwaka 2003.

View attachment 1889338

Waliruhusu anga lao kutumika kupitisha ndege vita za Marekani lakini wakakataa Marekani kuweka kambi katika ardhi yao kwa lengo la vita ile.

Muungano wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi yaaani NATO ulianzishwa baada ya Vita vya pili vya dunia. Kusudi lake lilikuwa kupata amani huko Ulaya, kukuza ushirikiano kati ya nchi wanachama wake na kulinda uhuru wao - yote haya ilikuwa katika hali ya kukabiliana na tishio lililokuwapo kwa wakati huo kutoka kwa Umoja za Kisovieti (USSR).

Mkataba wa uanzishaji wa Muungano huo ulisainiwa jijini Washington nchini Marekani mnamo mwaka wa 1949 na nchi kadhaa za Ulaya pamoja na Amerika Kaskazini. NATO inawapa Washirika wake uhakika wa kuwa na serikali za kidemokrasia, uhuru wa mtu binafsi na utawala wa sheria, na vile vile utatuzi wa mizozo kwa njia za amani. Muhimu zaidi ni kwamba, mkataba huo unaweka wazi wazo la ulinzi wa pamoja, ikimaanisha ya kwamba "kuwa shambulio dhidi ya mshirika mmoja linachukuliwa kama shambulio dhidi ya Washirika wote".

Kwa sasa, NATO ina wanachama wapatao 30. Mnamo mwaka 1949, kulikuwa na wanachama 12 waanzilishi wa umoja huu yaaani Ubelgiji, Canada, Denmark, Ufaransa, Iceland, Italia, Luxemburg, Uholanzi, Norway, Ureno, Uingereza pamoja na Marekani. Nchi nyingine wanachama ni Uturuki (1952), Ujerumani (1955), Uhispania (1982), Jamhuri ya Czech, Hungary na Poland (1999), Bulgaria, Estonia, Latvia, Lithuania, Romania, Slovakia na Slovenia (2004), Albania na Croatia (2009), Montenegro (2017) na Macedonia Kaskazini (2020).

Jamhuri ya Uturuki iko kwenye peninsula moja maarufu sana ya Anatolia magharibi mwa Asia na mkoa mdogo wa Kusini Mashariki mwa Ulaya. Jirani kabisa ya Uturuki kwa upande wa kaskazini magharibi ni nchi ya Bulgaria; Ugiriki ikiwa magharibi; Armenia, Azabajani na Iran upande wa mashariki; Georgia upande wa kaskazini mashariki; Syria upande wa kusini; na Iraq upande wa kusini mashariki.

Uislamu ndio dini kubwa zaidi nchini Uturuki kulingana na takwimu za serikali, na 99.8% ya watu hapo awali walitambuliwa na serikali kama Waislamu na asilimia iliyobaki ya 0.2 ni Wakristo au wafuasi wa dini zingine zilizotambuliwa rasmi kama Uyahudi.

Uturuki ni mmoja wa washirika wakuu wa EU (kumbuka kuwa mshirika sio mwanachama) na wote ni wanachama wa Umoja wa Forodha (European Union–Turkey Customs Union). Uturuki ilisaini makubaliano ya Jumuiya ya Forodha na EU mnamo mwaka 1995 na ilitambuliwa rasmi kama mgombea wa uanachama kamili mnamo tarehe 12 mwezi Desemba mwaka 1999, katika mkutano wa huko Helsinki wa Baraza kuu la Ulaya.

Mazungumzo ya uanachama kamili yalianza tarehe 3 mwezi Oktoba mwaka 2005. Nchi zingine zinazotafuta kuwa wanachama wa EU ni zile zilizo katika mchakato wa 'kubadilisha' (au kujumuisha) sheria za umoja huo wa Ulaya (EU) kuwa sheria ya kitaifa ndani ya nchi zao. Nchi hizi ni pamoja na:

(1) Turkey
(2) Albania
(3) Montenegro
(4) North Macedonia
(5) Serbia

Tangu mwaka 2016 hadi leo hii 2021, mazungumzo ya kutanganzwa kuwa mwanachama kamili/rasmi yamekwama. Kwanini Umoja wa Ulaya (EU) unasita kuipa uanachama kamili/rasmi nchi ya Uturuki? Je, sababu kuu inaweza kuwa ni idadi yake kubwa ya waumini wa dini ya kiislam?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau;
==========

==========

==========
Nchi zilizo mwanachama wa EU zinakatiba insyofanana kwa kiwango kikubwa na Sheria za nchi na nchi hazimzuii mwananchi wa nchi flani kukosa uhuru changamoto ipo hapo cos uturuki kunamambo anastaili ayarekebishe ambayo ni magumu kwa uturuki cos wao bado wanalinda dini zaidi
 
Mkuu usipotoshe kati ya nchi iliyo nufaika na Nato basi ni Turkey, kwa sababu baada ya kuanguka kwa Ottoman Uturuki ilikuwa dhaifu sana ,na Wakati huo huo ilikuwa na uadui na Usoviet kwa hiyo ilikuwa ni lazima tu ajiunge na nato apende asipende kwa ajili ya usalama wake.
Naikumbukwe USSR alitaka kuishambulia uk na ufarasa ndio wakaikoa kumbukumbu cremia war
 
Hujui lolote mkuu ,,kesi ni kwamba Kambi kubwa ya NATO ipo Turkey Sasa nazani jibu umelipata,,. Nato wana mng'ang'ania Turkey kwa sababu Upinzani wao mkubwa upo ASIA na turkey wapo katkt yao ,,.,......EMBU JIJIBU MI NAISHIA HAPAView attachment 1730056View attachment 1730057
Hii ni news ya kuonesha udhaifu wenu enh... Nguvu za Kumshinda Israel mwajisifia alafu mkichokoza mkapigwa kelele Dunia nzima... Muslim hamuwezi kaa mkatulia mnapenda fujo fujo tu mkipata pesa... even tokea enzi dini yenu ilipoaanza... Msemo wenu Convert or Die!
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa JamiiForums

Je, idadi kubwa ya waumini wa dini ya kiislam (99%) inaweza kuwa ndio kikwazo kikuu cha nchi ya Uturuki kutokuwa mwanachama kamili/rasmi wa E.U mpaka sasa?

Walikubaliwa haraka kujiunga NATO kwa maslahi ya kijeshi kama daraja la Wazungu kuingia Middle East? Uturuki kama mwanachama wa NATO aliruhusu jeshi la Marekani kutumia anga lake wakati wa vita vya kumpiga Saddam Hussein mwaka 2003.

View attachment 1889338

Waliruhusu anga lao kutumika kupitisha ndege vita za Marekani lakini wakakataa Marekani kuweka kambi katika ardhi yao kwa lengo la vita ile.

Muungano wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi yaaani NATO ulianzishwa baada ya Vita vya pili vya dunia. Kusudi lake lilikuwa kupata amani huko Ulaya, kukuza ushirikiano kati ya nchi wanachama wake na kulinda uhuru wao - yote haya ilikuwa katika hali ya kukabiliana na tishio lililokuwapo kwa wakati huo kutoka kwa Umoja za Kisovieti (USSR).

Mkataba wa uanzishaji wa Muungano huo ulisainiwa jijini Washington nchini Marekani mnamo mwaka wa 1949 na nchi kadhaa za Ulaya pamoja na Amerika Kaskazini. NATO inawapa Washirika wake uhakika wa kuwa na serikali za kidemokrasia, uhuru wa mtu binafsi na utawala wa sheria, na vile vile utatuzi wa mizozo kwa njia za amani. Muhimu zaidi ni kwamba, mkataba huo unaweka wazi wazo la ulinzi wa pamoja, ikimaanisha ya kwamba "kuwa shambulio dhidi ya mshirika mmoja linachukuliwa kama shambulio dhidi ya Washirika wote".

Kwa sasa, NATO ina wanachama wapatao 30. Mnamo mwaka 1949, kulikuwa na wanachama 12 waanzilishi wa umoja huu yaaani Ubelgiji, Canada, Denmark, Ufaransa, Iceland, Italia, Luxemburg, Uholanzi, Norway, Ureno, Uingereza pamoja na Marekani. Nchi nyingine wanachama ni Uturuki (1952), Ujerumani (1955), Uhispania (1982), Jamhuri ya Czech, Hungary na Poland (1999), Bulgaria, Estonia, Latvia, Lithuania, Romania, Slovakia na Slovenia (2004), Albania na Croatia (2009), Montenegro (2017) na Macedonia Kaskazini (2020).

Jamhuri ya Uturuki iko kwenye peninsula moja maarufu sana ya Anatolia magharibi mwa Asia na mkoa mdogo wa Kusini Mashariki mwa Ulaya. Jirani kabisa ya Uturuki kwa upande wa kaskazini magharibi ni nchi ya Bulgaria; Ugiriki ikiwa magharibi; Armenia, Azabajani na Iran upande wa mashariki; Georgia upande wa kaskazini mashariki; Syria upande wa kusini; na Iraq upande wa kusini mashariki.

Uislamu ndio dini kubwa zaidi nchini Uturuki kulingana na takwimu za serikali, na 99.8% ya watu hapo awali walitambuliwa na serikali kama Waislamu na asilimia iliyobaki ya 0.2 ni Wakristo au wafuasi wa dini zingine zilizotambuliwa rasmi kama Uyahudi.

Uturuki ni mmoja wa washirika wakuu wa EU (kumbuka kuwa mshirika sio mwanachama) na wote ni wanachama wa Umoja wa Forodha (European Union–Turkey Customs Union). Uturuki ilisaini makubaliano ya Jumuiya ya Forodha na EU mnamo mwaka 1995 na ilitambuliwa rasmi kama mgombea wa uanachama kamili mnamo tarehe 12 mwezi Desemba mwaka 1999, katika mkutano wa huko Helsinki wa Baraza kuu la Ulaya.

Mazungumzo ya uanachama kamili yalianza tarehe 3 mwezi Oktoba mwaka 2005. Nchi zingine zinazotafuta kuwa wanachama wa EU ni zile zilizo katika mchakato wa 'kubadilisha' (au kujumuisha) sheria za umoja huo wa Ulaya (EU) kuwa sheria ya kitaifa ndani ya nchi zao. Nchi hizi ni pamoja na:

(1) Turkey
(2) Albania
(3) Montenegro
(4) North Macedonia
(5) Serbia

Tangu mwaka 2016 hadi leo hii 2021, mazungumzo ya kutanganzwa kuwa mwanachama kamili/rasmi yamekwama. Kwanini Umoja wa Ulaya (EU) unasita kuipa uanachama kamili/rasmi nchi ya Uturuki? Je, sababu kuu inaweza kuwa ni idadi yake kubwa ya waumini wa dini ya kiislam?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau;
==========

==========

==========
Wazungu wanaamini Kobazi bado ustaarabu wao uko chini, na zaidi watatumia Uturuki kama lango la kukimbilia Ulaya kueneza ugaidi.
 
Uturuki yenyewe kuanzia raisi wao hawajakaa kama nchi ya Ulaya kabisa!
Walitakiwa wawe kule jirani na Iran
 
Jumuiya ya Ulaya (EU) una msingi fulani wa ukristo ndani yake kiasi kwamba nchi yoyote, kama Uturuki, ambayo haina huo msingi haiwezi kuruhusiwa kuwa mwanachama.

Ni hii ndiyo inayovuruga si ukristo maana ukristo unaelekea ukingoni huko Ulaya

The rights of lesbian, gay, bisexual, transgender, and queer (LGBTQ) people are protected under the European Union's (EU) treaties and law.

Same-sex sexual activity is legal in all EU member states and discrimination in employment has been banned since 2000.
 
Back
Top Bottom