Duniani kote hakuna kitu kinachoogopwa na serikali dhalimu kama idadi kubwa ya wapiga kura.
Baada ya Tume inayosimamia uchaguzi TAMISEMI kudanganya idadi halisi ya waliojiandikisha, kazi iliyo mbele yao kwa sasa ni namna gani watabadilisha hiyo idadi ziwe kura.
Kwa mfano; Mwanza, Sensa ya 2022 idadi ilikuwa 1.95M zaidi ya nusu wakiwa ni watoto chini ya miaka 14, leo wameandikisha 2,08M. Siku ya kupiga kura watawatoa wapi hao watoto waje kupanga foleni wapige kura, mashuleni au mitaani?
Kwa hali halisi ilivyo mitaani na vijijini, chuki ya wananchi kwa CCM na viongozi wake wa mitaa na vitongoji ni kubwa sana, hasira ya ugumu wa maisha kwa wananchi hasa vijana wataimalizia kwenye sanduku la kura.
Mbali na hiyo chuki ya wananchi, ndani ya CCM kwenyewe kuna makundi hasimu yanayotaka mgombea wao apite hivyo kugawa kura.
Kwenye chaguzi zilizopita CCM ilikuwa inasingizia wananchi hasa vijana hawajitokezi kujiandikisha, walitoa hicho kisingizio kwa vile ilionekana vijana wengi walikuwa wanaviunga mkono vyama vya upinzani, safari hii takwimu zinaonesha vijana wengi wamejiandikisha.
Ukichukulia hali hii na idadi kubwa ya waliojiandikisha iwapo wote wataamua kujitokeza kupiga kura, basi CCM watakuwa na kazi kubwa ya kuiba zaidi ya nusu ya kura kitu ambacho ni next to impossible.
Kati ya kura 1,000,000 unaweza kuiba kura laki moja (100,000) lakini siyo laki tano (500,000), hilo likitokea basi utakuwa ni wizi mkubwa kuwahi kutokea na utaweka historia Tanzania.
Kwa idadi hii nadiriki kusema CCM wamejichimbia kaburi lao wenyewe kinachotakiwa kwa vyama vya upinzani sasa ni kuhamasisha watu hasa vijana wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura.