Chulumeshy
Member
- Jul 27, 2022
- 17
- 11
''Penye miti mingi, hapana wanjenzi''
Kauli hii imekuwa dhahiri sana na yenye uhalisia ukizungumzia suala kuu la uchumi na maendeleo ya jamii hasa kuhusiana na idadi ya watoto na ustawi wa kila mtoto katika suala zima za elimu, afya na mahitaji mengine ya kimsingi.
Tukiongelea suala la miti mingi inavyokosa kuwa na wajenzi katika nchi nyingi za Kiafrika tunaongelea suala zima la uzazi wa watoto wengi kwenye familia zetu ambazo nyingi zinakuwa na mjumuiko au mkusanyiko wa watu wengi (extended family). Ni jambo lililo na ukweli kuona familia moja ya Kiafrika kuwa na watoto wengi ukilinganisha na ubora wa familia yao kwa madai ya kuwa watoto ni baraka au watoto ni mali.
Katika nchi nyingi za Kiafrika wanaamini kuwa ukizaa watoto wengi ndiyo chanzo cha mapato kwa mfano hao ndio watakaotumika katika masuala yote ya kilimo, masuala ya ndoa (mahari inapolipwa huwa inaongezea familia kipato) na kazi nyingine jambo ambalo linadumaza uchumi wa familia nyingi za Kiafrika kwa kutegemea zaidi watoto na kushindwa kuwawekea misingi au malezi bora kama vile elimu bora, afya, malazi na mahitaji yao muhimu.
Jambo hili linatiliwa sana msisitizo na wachumi wakubwa wakiwemo Gary Becker (aliwahi kutumikiwa tuzo ya Nobel kwa masuala ya Sayansi ya Uchumi 1992) pamoja na Lewis na wengine wengi kwa kuonesha ni kwa kiasi gani uzazi unavyoongeza gharama na kupelekea kukosekana kwa Rasilimali watu, anaongelea hayo katika model yake ya Trade-off Q-Q inayohusiana na uzazi na watoto kwa masuala ya kiuchumi.
Anasema kuwa, kuna uhusiano kati ya kipato na Rasilimali watu na ndiyo maana watu wenye watoto wachache wamekuwa na uwezo wa kutoa mahitaji ya muhimu kwa watoto wao na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi bila kuathiriwa na kitu chochote na hivyo inapelekea ushindani wa watu hasa katika suala la elimu kwani watu wakipata elimu bora basi inawasaidia kuwe na ushindani haswa katika soko la ajira.
Dai hili lina ukweli usiopingika kwa kuangalia nchi mbalimbali mfano China, kutokana na kuwepo kwa sera nzuri za uzazi inapelekea nchi hiyo kuweza kuwa''manage'' haswa watoto wa nchi yake na idadi au takwimu yao inapokuja kwenye suala la uchumi na hivyo imewekwa wazi kwamba idadi ya watoto inapaswa kuwa na kizuio fulani katika kuepusha ongezeko la watoto ambapo itapelekea kushindwa kuwahudumia katika mahitaji yao muhimu.
Mfano wa kuonekanana uliozoeleka kwa wengi,
Ukiangalia katika idadi ya watoto kwa matajiri wengi wa dunia wamekuwa na idadi ya watoto wachache ukilinganganisha na watu ambao hawajaendelea kiuchumi haswa katika nchi zetu za Kiafrika ambapo familia utakuta ina maisha duni lakini bado ina watoto wengi jambo linalopelekea uegemezi na utegemezi mkubwa na kuilaumu serikali kwa kushindwa kutoa mahitaji muhimu kwa wananchi wake kulingana na idadi kubwa ya watu na rasilimali mali zilizopo hivyo huduma muhimu au zenye ubora zinakuwa chache na zinaweza kupatikana kwa wale wanaoweza kuzimudu.
Hivyo ili kupunguza haya yote, elimu itolewe juu ya umuhimu wa kuwa na uzazi unaoweza kuleta rasilimali watu kwa taifa na pia kuwe na sheria madhubuti zitakazoweza kuleta uzazi uliobora na wa maendeleo kabisa, kuachana na imani ambazo zinapotosha kuhusiana na uzazi wa watoto wengi kuwa ni faida kwa familia, pia vyanzo vinavyoweza kupelekea suala hilo kuangaliwa kwa jicho la tatu mfano mitala n.k. Ili kuweza kuwa na maendeleo dhabiti ya nchi na familia kwa ujumla.
NB:
''Miti michache huwa na wajenzi watakaoweza kulifanya pori kuwa mji''.