Mamaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 5,298
- 4,861
Kuna shule mwaka jana pale rombo imesajili watoto 7 tuPale kwetu kijijin kuna hilo tatizo. Wachagga wote wamehamia mijin wamebaki wazee shule ni nyingi hazina wanafunz
Kuna shule mwaka jana pale rombo imesajili watoto 7 tuPale kwetu kijijin kuna hilo tatizo. Wachagga wote wamehamia mijin wamebaki wazee shule ni nyingi hazina wanafunz
Inategemeana na akili ulizonazo.Ila wanakuwa hawana furaha.
Hawawezi kukubali waafrika weusi kujazana katika nchi yao.Kwa sasa wazee wenye umri zaidi ya miaka 65 ni asilimia 20 ya watu wote nchini humo. Hali sio nzuri. Halafu kuhusu kuajiri raia wa mataifa mengine kwa location yao itakuwa rahisi kupata watu wengi ? Sidhani kama wanazungukwa na nchi zenye njaa au umaskini eti waende Korea Kusini kutafuta maisha. Lakini hata hivyo ndege zipo, hata wabongo wanaweza kwenda Korea
Wakenya wako wengi balaa Korea Kusini. Hata Wajerumani walikuwa hivyo hivyo, na sasa wahamiaji wapo kibao.Hawawezi kukubali waafrika weusi kujazana katika nchi yao.
Stress za maisha(kufeli malengo)Wakorea bwana, sababu mojawapo ya kujiua ni WIVU wa kipumbavu,
Si huwa tunaambiwa Korea Kusini wanaishi amisha ra raha mustarehe maana wanaishi kama Marekani na Ulaya. sasa hii ya watu kujitoa uhai kwa kiwango kikubwa inatoknana na nini tena wakati wanaishi kwa rahaTakribani shule 49 zinatarajiwa kufungwa mwaka huu nchini Korea Kusini kutokana na ukosefu wa wanafunzi. Asilimia kubwa ya shule hizo zilizokosa wanafunzi ni zile za awali na msingi.
Ukosefu wa wanafunzi wanaoandikishwa mashuleni unasababishwa na idadi ndogo ya watoto wanaozaliwa nchini humo.
Mnamo mwaka 2023 takribani shule 22 zilifungwa kwa sababu hiyohiyo huku mwaka 2024 shule 33 zikilazimika pia kufungwa. Vilevile mnamo mwaka 2024 takribani shule 112 nchini Korea Kusini hazikuandikisha mwanafunzi mpya hata mmoja.
Korea Kusini ni miongoni mwa nchi zenye idadi ndogo zaidi ya watoto wanaozaliwa . Kwa wastani mwanamke mmoja nchini humo anazaa watoto 0.75( chini ya mtoto mmoja) huku wastani unaotakiwa ikiwa watoto 2.1
Licha ya kuwa na idadi ndogo ya watoto wanaozaliwa, nchi ya Korea Kusini pia ni miongoni mwa nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaojitoa uhai duniani.
CHANZO: The Korea Times.
Upweke na msongo wa mawazo. Nchi "zilizoendelea" hayo ni masuala ya kawaida. Korea ni miongoni mwa nchi ambazo watu wanafanya kazi sana kwa masaa mengi, hii husababisha watu kuwa na muda mchache wa kukaa na familia. Wengine huweza kuamua kutokuwa na mwenzi au watoto. Kukosa muda wa kutosha kuwa na familia husababisha matatizo ya afya ya akili ambayo huweza kupelekea mtu kujitoa uhai.Si huwa tunaambiwa Korea Kusini wanaishi amisha ra raha mustarehe maana wanaishi kama Marekani na Ulaya. sasa hii ya watu kujitoa uhai kwa kiwango kikubwa inatoknana na nini tena wakati wanaishi kwa raha