Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Pia hata wale wabunge kupitia jimbo la ikulu pia wafutwe tu
In God we Trust
 
Tuligawa majimbo kutafutiana kazi, kweli chukulia Ukonga na Segerea, Kawe na Kinondoni, Ilemela na Nyamagana, Sengerema na Buchosa, Temeke na Mbagala etc etc,

Ni kutafutiana kazi kwa gharama ya taifa.

Asante

Hilo wazo zuri sana na mm ningeshauri tuwe na wabunge wawakilishi wa kanda na ikiwezekana iwe hivi wabunge 20 toka Kaskazini,20toka Kusini,20 Kanda ya ziwa,20 kanda ya kati na 20 kanda ya Pwani pamoja wawakilishi wa visiwa vyetu Jumla 100 na baraza la mawaziri liziwe zaidi ya mawaziri 20 na ikiwezekana wafute kabisa vyeo wa RC na DC

Tutaokoa hela nyingi sana na uwakilishi utakuwa na tija kwa taifa
 
Back rasimu ya Warioba
 
Yaani ccm kila idara imeharibu
Tuligawa majimbo kutafutiana kazi, kweli chukulia Ukonga na Segerea, Kawe na Kinondoni, Ilemela na Nyamagana, Sengerema na Buchosa, Temeke na Mbagala etc etc,

Ni kutafutiana kazi kwa gharama ya taifa.

Asante

In God we Trust
 
Naona hapo unamtafuta maneno jiwe

In God we Trust
 
Naona akili yako ndiyo imekaa kipashukuna pashukuna Zaidi

In God we Trust
Uzi wake ni mzuri, ila jambo la kushangaza ni pale alipoanza kuja na hoja za kusema kuwa ''Itatumika kama jaribio la kuzima wingu la wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu''., Huoni kuwa kaingiza ushabiki usio na tija katika uzi wake?

Unapozungumza mbele ya wanaume tafakari kwanza!!!
 
Mkuu nakukumbusha tu ya kuwa muosha huoshwa!
Nalog off
 
Naunga mkono

Hizi nafasi za mkuu wa mkoa na wilaya zingefutwa abakie mbunge...

Wabunge viti maalum hawana umuhimu...

Wabunge wapunguzwe kwa kuonganisha majimbo... Ili kuwepo na wabunge wasiozidi 150...

Viti maalumu vimejaa baba na binti, mume na mke, mtu na mchepuko n.k., waanze na hivyo kwanza

Hao viti maalum sijaona umuhim wAo wakiwepo bungeni....
 
Mawazo mazuri lkn Nani wa kufanya hayo mabadiliko!?

Wabunge hawawez kukubali au kupitisha sheria ili idadi ya wabunge ipungue...

Tuligawa majimbo kutafutiana kazi, kweli chukulia Ukonga na Segerea, Kawe na Kinondoni, Ilemela na Nyamagana, Sengerema na Buchosa, Temeke na Mbagala etc etc,

Ni kutafutiana kazi kwa gharama ya taifa.

Asante

Aisee... Kumbe Ni kutafutiana ulaji na kuongeza idadi ya wabunge ndiooo...!!?

Huku Ni kupoteza pesa za walipa Kodi..
 
Kwenye katiba ya Warioba wananchi tulipendekeza suala hilo na kutilia mkazo & msisitizo suala la wakuu wa mikoa & wilaya, ajabu ilipofika bungeni wazee wa bunge wakapiga chini.

Ukweli ni kwamba wabunge wa kuteuliwa, wakuu wa mikoa na wilaya wapo kulinda maslahi ya vyama vya siasa.
 
Kuna haja gani ya kuwa na wabunge wengi ambao wakati wote wanasusia na kuzomea vikao utadhani wabeba lumbesa wa shimoni Kariakoo,wacha wapunguzwe hakuna kazi yoyote wanayofanya
 
Mawaziri na washauri wa Rais ndio wangepunguzwa ...hawana lolote wanalofanya zaidi ya kutumbua hela za walipa kodi
Hii inaonyesha usivyo na imani na Rais wetu. Ikiwa umeshauri hivyo basi umeona mapungufu yake. Kwanini usingeshauri asigombee tena, kamti kuu ccm watafute mwingine.
 
Hii inaonyesha usivyo na imani na Rais wetu. Ikiwa umeshauri hivyo basi umeona mapungufu yake. Kwanini usingeshauri asigombee tena, kamti kuu ccm watafute mwingine.

Na wewe ni mmoja wa washauri wake kwani?πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…