Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Mimi naunga mkono idadi ipungue kila wilaya iwe na mbunge mmoja tu. Dar ina wilaya tano lakini ina wabunge 9 hao 4 waliozidi ni hasara tupu na hakuna tija yoyote tuliyo ipata kwa kuongeza wingi wa wabunge. Viti maalumu pia vufutwe watu wagombee majimboni. Huu ujinga wa kugawa wilaya eti mashariki na magharibi au kusini na kaskazini ni ujinga mtupu! Mbona mkuu wa wilaya anakuwa mmoja wilaya nzima na mambo yanakwenda? Hao waliozidi ni wa kuchota na kutupilia nje!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waanze kuwaondoa wanaoitwa "Wabunge wa viti maalum" inamaana wanawakilisha viti maalum au wananchi? Watolewe kwakuwa hakuna wanaowawakilisha.

Pili kusiwepo na wakuu wa wilaya as long as kuna Wabunge, Wakurugenzi watendaji na pia kuna makatibu tawala mkoa na wakuu wa mikoa pia.

Utumiaji mbaya wa pesa za walipa kodi kulipa mishahara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Heko
 
sheria inaweza kubadilishwa ili kuendana na mahitaji ya wakati huo
Well said mkuu. Inawezekana Waziri sio lazima awe mbunge tukaondoa utitiri wa wabunge maalumu
 
Sasa MTU anasema ni LA saba anatafuta nini kwenye mambo ya nchi yanayohitaji IQ kubwa wakat mwingine
 
Kupunguza idadi ya MPs ni Jambo jema na lenye tija Ila tunapunguzaje, dhamira ya kuanzisha special seat ilikua njema kwa wakati huo ingawa sasa hauna tija tena, ikiwa lengo ni kupata uwakilishi wa wanawake bungeni katika kufikia 50/50 kwanini tupuuze ushauri wa uwepo wabunge wenza kila Jimbo? Kwa jinsia mbili tofauti, viti maalumu sasa ni sehemu ya kupeana ulaji, hata utaratibu wa chama kuwapata hauwekwi sana wazi na wengi wanaopata nafasi hizo ni wale wenye mahusiano ya karibu na viongozi.
 
Au waongeze akishinda ccm mmoja aende na mwenza wake Tue nao 600+ ndio watafurahi
 
Inabidi kufahamu jimbo kama jimbo la uchaguzi linatakiwa kuwa na idadi ya juu ya watu wangapi badala ya katiba kusema tu inategemea na sensa ya watu wote ndani ya Jamhuri. Halafu katiba inasema hakuna mahakama yoyote kusikiliza shauri la Tume juu ya utendaji kazi wake.
 
Futa viti maalum tu, mambo yataenda sawa kabisa
 
Pamoja na kuwa wazo la kupunguza wabunge ni zuri na labda ndio litakalokuwa wazo langu la kwanza kuunga mkono toka kwa serikali hii, nashauri vile vile kupunguzwa kwa ukubwa wa serikali yote.

Mikoa ipunguzwe toka 26 hadi 18 na wilaya zipunguzwe toka 160+ hadi 80, kisha pesa zitakazookolewa zipelekwe kwenye elimu kujenga madarasa na nyumba za walimu pia kujenga mahospitali na zahanati na kununua vifaa/zana za kisasa za tiba.

Serikali hii ikae ikijua kuwa sasa kwa vile walivyo na mahusiano mabovu na wahisani, wasitegemee kupata tena hisani (Free Lunch Coupons) toka kwao. (It's the end of the honeymoon and that the government must learn to stand on its own feet).

Pia ofisi zile feki feki ambazo zipo kisiasa kama za ma-RC, ma-DC na za makatibu tarafa, zote zifutwe kwani sababu zilizofanya ziwepo kipindi hicho, hazipo tena na ni mizigo tu kwa wananchi.

Serikali lazima ibane matumizi kwa kupunguza unnecessary bureaucracy and red tape. Viti maalum kwa wabunge na madiwani pia vifutwe kwani havina tija na vinachangia tu kuvuruga ndoa za watu.

Marekani na utajiri woote huo na population ya watu 300+ million, wana majimbo (Mikoa) 50 tu na wilaya 435; Wabunge 435 wa baraza la wawakilishi na maseneta 100. Sasa sisi watu 50+ million na umasikini wa kutupwa eti tuna mikoa 26, wilaya 160+ na wabunge zaidi ya 370. Very hopeless.
 
Haishangazi. Kule Zanzibar mbinu hiyo imetumika sana ya kupunguza majimbo na kuunganisha.

Zanzibar ilikuwa na majimbo 50 ya uchaguzi Pemba 24 na Unguja 26.

Siasa zilipelekea Pemba kupunguzwa 3 hadi 21 na kuongezwa unguja kuwa 29. Hayo yote yalifanywa kwa hesabu za siasa.

Pemba yakapunguzwa tena nakubaki 18 na unguja 32.

Hio haikutosha kulifanywa mabadiliko ya mipaka ya majimbo mara kadhaa na hayakuwasaidia CCM.

Hitimisho ilikuwa ni 2015 pale mipaka ya majimbo yalipobadilishwa zaidi na kuleta sintofahamu na kuongezwa

Hata hivyo CUF wenyewe waliita MABAILIKO HAYO KUWA NI KASHATA popte utakapoikata ni tamu.

Na kweli kilichotokea kwenye uchaguzi wa 2015 CCM hawatakisahau.


CCM wakahamia kwenye JECHAISM hadi leo wanaishi kwa Principle hiyo kule Zanzibar.


Sasa hali hiyo ikija Tanzania Bara Haishangazi
 
Tao kabisa wabunge wa viti maalum hawana tija zaidi ya kugonga meza, vile vile waongeze kiwango cha elimu kwa mbunge angalau iwe kuanzia diploma la sivyo kuna siku tutajikuta wabunge wote wameishia la nne B.
 
Katika kile kinachosemekana kuwa ni mwendelezo wa kuwa na idadi ndogo ya wabunge ,itakayokuwa rahisi kuisimamia , inasemekana kuna jambo lipo jikoni kuja kama pendekeza laku merge majimbo ili idadi ya wabunge ipungue ikibidi bunge liwe na idadi isiyozid wabunge 200.
Kumbuka Kwa Sasa wabunge ni 300+.

Ikumbukwe kuwa Serikal ya awamu ya tano tayari kupitia kamati zake kuu na halimashauri kuu yaan NEC ,imekwisha punguza idadi ya wajumbe Kwa idadi kubwa.

Hii pia itatumika kama jaribio la kuzima wingu Wa wabunge Wa upinzan kwenye uchaguzi mkuu.

Mfano mnyika anaweza jimbo lake likaunganishwa na jimbo lenye ushwishi mkubwa Wa CCM,ili jumla ya Kura zimtoe.

Hapa kutakua na mtego mkubwa sana ,Na majimbo yatakayolengwa ni yaliyo na upinzan mkali

Exactly what I was thinking all along!

Na inakuja kweli!
 
Baba isijeikawa mnachukua dodoso ili muone watu watalipokeaje
 
Katika kile kinachosemekana kuwa ni mwendelezo wa kuwa na idadi ndogo ya wabunge ,itakayokuwa rahisi kuisimamia , inasemekana kuna jambo lipo jikoni kuja kama pendekeza laku merge majimbo ili idadi ya wabunge ipungue ikibidi bunge liwe na idadi isiyozid wabunge 200.
Kumbuka Kwa Sasa wabunge ni 300+.

Ikumbukwe kuwa Serikal ya awamu ya tano tayari kupitia kamati zake kuu na halimashauri kuu yaan NEC ,imekwisha punguza idadi ya wajumbe Kwa idadi kubwa.

Hii pia itatumika kama jaribio la kuzima wingu Wa wabunge Wa upinzan kwenye uchaguzi mkuu.

Mfano mnyika anaweza jimbo lake likaunganishwa na jimbo lenye ushwishi mkubwa Wa CCM,ili jumla ya Kura zimtoe.

Hapa kutakua na mtego mkubwa sana ,Na majimbo yatakayolengwa ni yaliyo na upinzan mkali
Haya ndo mawazo mfu! Majimbo mapya yalipokuwa yakiundwa, tuliambiwa inafanyika ili kuongeza wabunge wa CCM. Sasa unasema wakipunguza majimbo ni kuumaliza upinzani.

Hili lilishaletwa hapa JF kwa msimamo kwamba hatuhitaji bunge kubwa kiasi hiki. Kwa nini wilaya moja iwe na wabunge 2 au 3? wna nini? Wkati huo hakuna surgeon hata mmoja! Yaani unataka yawe mengi ili tu wapinzani wapate nafasi? Let's get the best! Kama Mnyika wako ni muhimu na mzuri atapita, kama ni kelel tu kama tunavyosikia, aanze shule sasa!
 
Naunga mkono wazo hilo. Mimi nililifikiria sana toka siku nyingi. Napendekeza kuwa kila wilaya iwe na mbunge mmoja tu kama alivyo mkuu wa wilaya. Mkuu wa wilaya ni mmoja tu kwa kila wilaya. Na yeye huwa anatakiwa asimamie taasisi zote za serikali zilizopo katika wilaya husika zikiwemo halmashauri za wilaya ambapo kuna wilaya huwa na halmashauri hadi mbili au tatu. Lakini ni ajibu kuwa kila halmashauri huwa na mbunge au wabunge. Kwa hiyo wilaya moja inaweza kuwa na wabunge wawili au watatu hadi sita. Nakumbuka kati ya kipindi cha mwaka 2005-2015 wilaya ya Masasi pekee ilikuwa na Mbunge wa Jimbo la Lulindi Kumchaya, Mbunge wa Banda Mrope, Mbunge wa Masasi Mariam Kasembe,Wabunge viti Maalum Anna Abdallah na Agnes,na Mbunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki Kate Kamba. Na sasa hivi wapo watano wilaya hiyo moja ya Masasi.
Mbunge ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya maoni ya wananchi na kuyapeleka bungeni hahitaji kuwa na eneo dogo hivyo. Jambo la mhimu ni kumuongezea vitendea kazi.Lakini aongezewe eneo kwa kufuta baadhi ya majimbo.
 
Back
Top Bottom