Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Wazo la kupunguza idadi ya wabunge si wazo baya; litaokoa fedha nyingi na labda linaweza kulazimisha mabadiliko ya utendaji wa Bunge hilo. Jambo la kwanza ni kuondoa wabunge wa viti maalum. Hawana wanayemwakilisha ambaye hawakilishwi na mbunge wa jimbo.
Ni kweli mkuu,Viti maalum vufutwe tu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Wafanye yoote wapendayo ila CCM itambue kuwa kuna MWISHO!!

Magufuli ajifurahishe apendavyo ila atambue kuwa “YANA MWISHO”

Hakuna aliyewahi waza Sumaye na Lowassa Leo watakua upinzani!! Hawa watu Magu hawezi zifikia kariba zao hata robo lakini Leo tunaongea lugha moja!!

Muda ndiye hakimu wa yote!!

Nakumbuka riwaya pendwa ya KULI “lakini yana mwisho”


Sent using Jamii Forums mobile app
Nani kakwambia wapo upinzani? Low thinking
 
Pia waondoe na wabunge wa kutoka jimbo la ikulu pia itapendeza

In God we Trust
Wabunge wa chato na kolomije watapewa wizara ya Ulinzi, Utawala bora, mambo ya ndani, fedha , madini na ujenzi wizara zingine watapewa kabla zingine
 
Katika kile kinachosemekana kuwa ni mwendelezo Wa Kua na idadi ndogo ya wabunge ,itakayokuwa rahisi kuisimamia , inasemekana kuna jambo lipo jikon kuja kama pendekeza laku merge majimbo ili idadi ya wabunge ipungue ikibidi bunge liwe na idadi isiyozid wabunge 200.
Kumbuka Kwa Sasa wabunge ni 300+.
Ikumbukwe kuwa serikal ya awamu ya tano tayar kupitia kamati zake kuu na halimashauri kuu yaan NEC ,imekwisha punguza idadi ya wajumbe Kwa idadi kubwa.
Hii pia itatumika kama jaribio la kuzima wingu Wa wabunge Wa upinzan kwenye uchaguzi mkuu.
Mfano mnyika anaweza jimbo lake likaunganishwa na jimbo lenye ushwishi mkubwa Wa CCM,ili jumla ya Kura zimtoe.
Hapa kutakua na mtego mkubwa sana ,Na majimbo yatakayolengwa ni yaliyo na upinzan mkali
Kumbe serikali ina kamati kuu na halmashauri kuu (NEC)?
 
Hapo watakaopungua wengi watatoka upande ule.....
 
Hili mimi naliunga mkono kabisa

1. Kwanza futa viti maalum havina msaada wowote zaidi ya kuwapa individuals ulaji

2. Unganisha hayo majimbo, tena inafaa Jimbo liwe na ukubwa wa Wilaya nzima

Nchi hii masikini sana, Ulaji katika siasa inabidi upunguzwe na badala yake pesa zipelekwe kwenye maendeleo

Katika mambo machache ya maana ambayo JPM atakuwa amefanya katika utawala wake ni hili.

Hii nchi siyo kubwa kivile kiasi cha kuhitaji wabunge wote 300+, wote wa nini hao, wameongeza tija gani zaidi ya kumbebesha zigo mlipa kodi?
 
Shida ya kumpa uongozi asiejua uongozi ni nini ,tutashuhudia vitimbi vya kila aina visivyokuwa na kichwa wala miguu hivi huyu mzee hana hata work plan ,vipaumbele kwenye uongozi wake au anajiendea tu .Leo hili kesho hili shaghala baghala ,wapongezaji juhudi wajiandae kuandamana .
 
kwanini jiwe anateseka hivyo? ana wabunge wengi hivyo apeleke mswada wa kufuta vyama vingi ili tupumue
 
Katika kile kinachosemekana kuwa ni mwendelezo wa kuwa na idadi ndogo ya wabunge ,itakayokuwa rahisi kuisimamia , inasemekana kuna jambo lipo jikoni kuja kama pendekeza laku merge majimbo ili idadi ya wabunge ipungue ikibidi bunge liwe na idadi isiyozid wabunge 200.
Kumbuka Kwa Sasa wabunge ni 300+.

Ikumbukwe kuwa Serikal ya awamu ya tano tayari kupitia kamati zake kuu na halimashauri kuu yaan NEC ,imekwisha punguza idadi ya wajumbe Kwa idadi kubwa.

Hii pia itatumika kama jaribio la kuzima wingu Wa wabunge Wa upinzan kwenye uchaguzi mkuu.

Mfano mnyika anaweza jimbo lake likaunganishwa na jimbo lenye ushwishi mkubwa Wa CCM,ili jumla ya Kura zimtoe.

Hapa kutakua na mtego mkubwa sana ,Na majimbo yatakayolengwa ni yaliyo na upinzan mkali
Jiwe akifanya hayo,hata akitawala milele poa tu,apunguze idadi ya mikoa,wilaya,wabunge ni wengi sana,hakuna uhusiano wa maendeleo na kuwa na mbunge,
Wabunge wawe 100 tu,wizara zipungue idadi,vyeo na idara zipungue katika utumishi wa umma,taasisi za umma zipungue,kuna haja gani kuwa na Tarura,wakati Tanroads ipo,?
Hayo mapesa,yapelekwe kukopesha vijana wasome elimu ya juu,wawezeshwe waende huko duniani wakatengeneze pesa,kama hakuna bidhaa za kuuza nje,basi tuuze wasomi wetu,wahandisi,madakitari,tuwe kama India,wamejaa kibao US,kwenye sekta za IT,na udakitali.
Wabunge 75 wanatosha,wilaya zipungue,Zamani dar ilikuwa,Kinondoni,Ilala,na Temeke,Leo tunaambiwa kuna Ubungo na Kibamba!!!kilichoongezeka hapa ni idadi ya watu,sio eneo LA kijiografia,sasa kwanini kuongeza gharama ya uendeshaji,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukubwa wa baraza la mawaziri ni eneo lingine muhimu sana kuliangalia. Inafaa kuwa na serikali ndogo yenye mawaziri wasiozidi 20 ili kubana matumizi na kuongeza tija
Usipende kuingilia mambo ya wakubwa, juzi tu imeanzishwa wizara mpyaaa kapewa yule mama wa mavito ya thamani. Hakuna kumuingilia alishasema.
 
Mimi naona ni bora hata tusipokuwa na Bunge kabisa, kusiwe na vyama vya siasa tuache iwe jeshi la mtu mmoja.
 
Nani alikuja na wazo la kujaza hao wabunge? je alikuwa ni sababu zipi? hizo kwa nini sababu hizo zikose tija kwa sasa?
 
Ukubwa wa baraza la mawaziri ni eneo lingine muhimu sana kuliangalia. Inafaa kuwa na serikali ndogo yenye mawaziri wasiozidi 20 ili kubana matumizi na kuongeza tija
Well,...eneo jingine ni kupunguza magari ya thamani kubwa kwa viongozi kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, hayo magari kuyamaintain ni gharama kubwa mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom