Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Wazo la kupunguza idadi ya wabunge si wazo baya; litaokoa fedha nyingi na labda linaweza kulazimisha mabadiliko ya utendaji wa Bunge hilo. Jambo la kwanza ni kuondoa wabunge wa viti maalum. Hawana wanayemwakilisha ambaye hawakilishwi na mbunge wa jimbo.
Wazo ni zuri vipi ma DC na ma RC hawa hawana faida yoyote kazi zao imepitwa na wakati, au niseme hazipo ni sawa sawa na kuajiri copy typist kwa wakati huu. Kwenye nch nyingi duniani kama siyo zote kazi zao zinafanya na wabunge. Kwa ufupi inaonekana hawana kazi kabisa wakammaliza kodi zetu bure ndiyo maana inawabidi waingilie kazi za watu hawana cha kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wakuu wa wilaya nadhani nafasi zao zinagaliwe upya mana kama hawana kazi yaidi kueneza sera za chama zinazoweza fanywa na makamu wa ccm wa tarafa
 
Kabla idadi ya wabunge haijapunguzwa, napendekeza rais apunguziwe madaraka. kama rais asingekuwa na madaraka aliyonayo sasa kwa nchi, basi bunge na mahakama zingekuwa ni taasisi imara sana.
 
Katika kile kinachosemekana kuwa ni mwendelezo Wa Kua na idadi ndogo ya wabunge ,itakayokuwa rahisi kuisimamia , inasemekana kuna jambo lipo jikon kuja kama pendekeza laku merge majimbo ili idadi ya wabunge ipungue ikibidi bunge liwe na idadi isiyozid wabunge 200.
Kumbuka Kwa Sasa wabunge ni 300+.
Ikumbukwe kuwa serikal ya awamu ya tano tayar kupitia kamati zake kuu na halimashauri kuu yaan NEC ,imekwisha punguza idadi ya wajumbe Kwa idadi kubwa.
Hii pia itatumika kama jaribio la kuzima wingu Wa wabunge Wa upinzan kwenye uchaguzi mkuu.
Mfano mnyika anaweza jimbo lake likaunganishwa na jimbo lenye ushwishi mkubwa Wa CCM,ili jumla ya Kura zimtoe.
Hapa kutakua na mtego mkubwa sana ,Na majimbo yatakayolengwa ni yaliyo na upinzan mkali
Pendekezo zuri kabisa maana hatuhitaji kuwa na bunge kubwa ambalo halifanyi chochote zaidi ya kuongeza gharama za kuendesha nchi
 
Wafanye yoote wapendayo ila CCM itambue kuwa kuna MWISHO!!

Magufuli ajifurahishe apendavyo ila atambue kuwa “YANA MWISHO”

Hakuna aliyewahi waza Sumaye na Lowassa Leo watakua upinzani!! Hawa watu Magu hawezi zifikia kariba zao hata robo lakini Leo tunaongea lugha moja!!

Muda ndiye hakimu wa yote!!

Nakumbuka riwaya pendwa ya KULI “lakini yana mwisho”


Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli! Muda huwa ni hakimu mzuri
 
Wazo la kupunguza idadi ya wabunge si wazo baya; litaokoa fedha nyingi na labda linaweza kulazimisha mabadiliko ya utendaji wa Bunge hilo. Jambo la kwanza ni kuondoa wabunge wa viti maalum. Hawana wanayemwakilisha ambaye hawakilishwi na mbunge wa jimbo.
Mzee hawa viti maalum wakiondoka watapunguza idadi ya wabunge wanawake na huenda wanaharakati (feminists) wasilipende hili pia hao ni mtaji mkubwa kwa Ccm kwa kuunga mkono kila kinacholetwa na Serikali humo pia Ccm huwenda wasilipende hili.
 
Wazo la kupunguza idadi ya wabunge si wazo baya; litaokoa fedha nyingi na labda linaweza kulazimisha mabadiliko ya utendaji wa Bunge hilo. Jambo la kwanza ni kuondoa wabunge wa viti maalum. Hawana wanayemwakilisha ambaye hawakilishwi na mbunge wa jimbo.
Ikiwa idadi ya wabunge wakuchaguliwa itakuwa sawa na idadi za wilaya,harafu wakaondolewa wabunge wote wenye viti maalum,lakini wabakie wabunge 10 wateule wa Raisi ni wazi wabunge wasiopungua 178 watapoteza ubunge ambayo inakaribia nusu ya idadi ya wabunge wote.

Faida zake ni kupunguza mzigo kwa mlipa kodi
Na vilevile muda wa kujadiri miswaada unaweza ukaongezeka.

Lakini sifa za mbunge zingeangaliwa upya kwa mfano mtunga sheria inambidi awe na uelewa wa sheria.Ifike mahala mtu anaetaka ubunge ajiandae kielimu kusoma na kufahuru sheria angalau ngazi ya cheti.
Mgombea ubunge ikiwezekana watokane na wajumbe wa halmashauri yaani madiwani.

Aweze kuzungumza,kusoma na kuandika lugha ya English na Kiswahili kwa ufasaha.
 
Ukubwa wa baraza la mawaziri ni eneo lingine muhimu sana kuliangalia. Inafaa kuwa na serikali ndogo yenye mawaziri wasiozidi 20 ili kubana matumizi na kuongeza tija
Ni kweli wangepunguza Naibu Waziri wote pia Naibu katibu mkuu wote na kuondoa vyeo vya wakuu wa Mikoa RC vyeo ambayo hivitumiki duniani sasa, Nchi nyingi wanatumia Mameya wa kuchaguliwa au Gavana huu mfumo ni nafuu hata kenya South Africa ulaya America Asia ndiyo unatumika.
 
Usishangae jimbo la Hai likaunganishwa na Chato!
Ku utawala huu hakuna lisilostaajibisha.
Mshauri mkuu wa mtukufu malaika toka chato ni Naibu Rais ndugu Daud Arbaty Bashite asiye na vyeti unategemea nini? Kama aliweza kumshauri wampige Risasi mh Tundu Lisu sembuse mengine?
 
Waafrika tunawekeza zaidi katika utawala siasa kuliko elimu ndo maana nchi za Afrika ni masikini

Wapungue tu.
Trilion 1.5 imepigwa badala ya Spika kusaidia ajulikane mwizi halisi sasa Spika anatumika kuwashambulia wabunge wanaoshupalia huo wizi ukomeshwe na watuhumiwa wakamatwe. Kwa Bunge la hivyo ni bora kuwe na bunge moja tu la wabunge wachache kuliko kuwa na utitiri wa wabunge wa CCM ambao wengi ni vilaza sana kutwa ni kugonga meza na kusema ndiyooo kwa kila jambo.
 
Zanzibar kwenyewe kuna utitiri wa wabunge kama nzige ka Nchi kadogo kama kiroboto na vijimbo vidogo kuliko hata vijiji vya Tanganyika na wote pesa zao zinatoka Hazina na BOT kwa kifupi utitiri wa wabunge wa CCM kwa Tanganyika na Zanzibar ni shiiida hasa ukizingatia kuwa idadi kubwa ya wabunge vi vilaza hawajielewi ni mbumbumbu kiasi cha kutisha mfano juzi simbachawene kafanya vioja kaongea maneno ambayo hata wale wabunge wajinga wajinga akina Musukuma na Livingston Lusinde kibajaji walimshangaa.
 
Back
Top Bottom