Idadi ya wanaofeli Law School of Tanzania yazua utata

Idadi ya wanaofeli Law School of Tanzania yazua utata

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Idadi iyo ni sawa na 4.1% pekee kati ya wote waliofanya mtihani, huku wengine 484 wakitakiwa kurudia mtihani na 265 wakiondolewa kabisa baada ya kufeli.

Hali hiyo imefanya Wanasheria na wadau wengine kutaka iundwe Tume ya kuchunguza sababu akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu Gabriel Malata aliyesema nguvukazi kubwa inapotea kwa wahitimu wengi kukwama shuleni hapo.

Takwimu zaidi zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 4,397 na waliofaulu ni 792, waliotakiwa kurudia mtihani ni 2095 wakati waliofeli ni 1,074.
 
Kupata Leseni ya kazi ni ngumu kuliko Degree nchi hii ngumu sana kukwamishana ndio sifa kuu ya mtu mweusi...kama mnaona hiyo ni muhimu na watu hawasomi mnachotaka ninyi iwekeni kwenye mitara ya vyuo huko sema mnafurahi kuona watu wengi mkiwaferisha kwa vitu wanavyovijua..
 
Kupata Leseni ya kazi ni ngumu kuliko Degree nchi hii ngumu sana kukwamishana ndio sifa kuu ya mtu mweusi...
Lakini inawezekana. Unajua vyuo vikuu vingi vya Bongo siku hizi ni bora liende. Kuna wahitimi wa degree ya sheria nawafahamu ni vilaza kweli kweli. Sijui kama madaktari wana mitihani kama hii lakini nadhani huko pia vilaza wengi. Ni kila sekta.
 
Believe me, hizi "excuse" mnazotoa ndio zinawapa sababu hao walimu wa Law School wazidi kufelisha wanafunzi wengi zaidi.

Ni kawaida, kila tasnia lazima iwe na competence ili kuiletea mafanikio, sasa kwa hao walimu wa Law School wanaoongoza kwa kufelisha, ubora wao utapimwa kwenye kitu gani? au ndio kwa kufelisha wanafunzi wengi?! Ajabu.

Au kwa hizi "excuse" zenu, mnakubali kuwageuza hao walimu wa Law School kuwa miungu watu wasiopimwa perfomance yao popote?!

No, this is unacceptable.
 
Najua unacholalamikia na mimi nakuunga mkono. Mtihani wowote wanapofeli watahiniwa wengi inaonyesha kuna kasoro mahali, na mara nyingi tatizo linakuwa siyo kwamba watahiniwa hawana elimu ya kutosha. Hili tatizo liko hata kwenye vyuo vikuu vyetu.

Unaweza kukuta wanaofeli na ku-sup ni wengi mpaka unashangaa. Hili linaonenyesha kuwa elimu yetu imejikita kwenye kuwakaririsha wanafunzi na upimaji ume-base zaidi kwenye mitihani na siyo uelewa.

Lakini pamoja na hayo, vile vile ma-graduate wengi wa siku hizi, kwenye sekta zote wengi ni vilaza. Si mainjinia, madaktari au wanasheria.
 
Wapeleke mtaala wao huko mkuu kama wanaona vyuo havitoi watu sahihi vichaguliwe vilivyo bora kuliko kuwapotezea muda wadogo mpaka muda wa kuishi na familia unaongezeka pamoja na kuwa na watoto watu wapo busy kusoma tuu wanakuja kuoa au kuolewa wazee unauliza eti wanarudia mitihani ya sheria...
 
Idadi iyo ni sawa na 4.1% pekee kati ya wote waliofanya mtihani, huku wengine 484 wakitakiwa kurudia mtihani na 265 wakiondolewa kabisa baada ya kufeli.

Hali hiyo imefanya Wanasheria na wadau wengine kutaka iundwe Tume ya kuchunguza sababu akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu Gabriel Malata aliyesema nguvukazi kubwa inapotea kwa wahitimu wengi kukwama shuleni hapo.

Takwimu zaidi zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 4,397 na waliofaulu ni 792, waliotakiwa kurudia mtihani ni 2095 wakati waliofeli ni 1,074.
Duh, inasikitisha!

Ingefaa kupata mchanganuo wa hizo data ili kujua background ya hao waliofeli, ili kuona kama kuna pattern fulani ya kushughulikia.
Hii ingewezesha kutambua kama tatizo ni la vyuo walivyosoma mwanzo au ni waalimu wa Law School.

Siku hizi kuna vyuo vya kawaida, ambavyo havina miundo mbinu ya vyuo vikuu (Universities), lakini vinatoa Bachelor degrees na Masters degrees !!!
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Idadi iyo ni sawa na 4.1% pekee kati ya wote waliofanya mtihani, huku wengine 484 wakitakiwa kurudia mtihani na 265 wakiondolewa kabisa baada ya kufeli.

Hali hiyo imefanya Wanasheria na wadau wengine kutaka iundwe Tume ya kuchunguza sababu akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu Gabriel Malata aliyesema nguvukazi kubwa inapotea kwa wahitimu wengi kukwama shuleni hapo.

Takwimu zaidi zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 4,397 na waliofaulu ni 792, waliotakiwa kurudia mtihani ni 2095 wakati waliofeli ni 1,074.
Waliofeli wengi ni waliotoka open university, Tumaini university, ect ila wanaotoka UDSM wamefaulu wote.
 
Dar es Salaam. Anguko kwenye mtihani wa uwakili katika Shule Kuu ya Sheria Tanzania (LST) limefikia hatua mbaya na kuwaibua wanasheria na wadau wengine wakitaka utafiti ufanyike kubaini chanzo cha tatizo hilo.
Pendekezo hilo na mengine yamekuja kufuatia matokeo mabaya kupindukia katika mtihani uliofanywa mwaka huu na wanafunzi 633.
Katika mtihani huo wanafunzi 26 (sawa na asilimia 4.1) pekee wamefaulu, 342 wametakiwa kurudia baadhi ya masomo (suplimentary) huku wengine 265 (asilimia 41.9) wakifeli na kukatishwa masomo (dicontinued).
Hali hiyo, ingawa si jambo jipya katika shule hiyo, mwaka huu imepindukia ukilinganaisha na miaka mingine ya karibuni.
Katika mwaka wa masomo 2018/2019 kati ya wanafunzi 1,735 waliofanya mtihani 347 (asilimia 20) walifaulu kuendelea, 484 walirudia mitihani na 468 (asilimia 26.9) walifeli.
Kadhalika, mwaka wa masomo 2016/17-2017/18 kati ya wanafunzi 2,662 waliofanya mtihani 445 (sawa na asilimia 16.72) walifaulu, 1,611 (sawa na asilimia 60.53) walirudia na 606 (sawa na asilimia 22.76) walifeli.
Uongozi wa shule hiyo umejibu malalamiko ya wadau ukifafanua changamoto zilizopo, ikiwemo ya maandalizi duni waliyoyapata wanafunzi hao katika vikuu vikuu mbalimbali walivyosomea shahada zao.
Utafiti ufanyike
Akizungumzia hali hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Gabriel Malata alisema jawabu la changamoto zote zinazoikabili hatua hiyo ya taaluma ya sheria litapatikana iwapo utafanyika utafiti.
“Kabla hatujaenda mbali lazima tujue tatizo na kuliwekea nguvu, bila shaka ufumbuzi utapatikana. Tujue kwanini hali hii inajitokeza? Mtalaa unaweza kuwa sehemu ya tatizo lakini tukifanya utafiti tutabaini na mengine mengi,” alisema.
Kwa kuwa jambo hilo linahusu maisha ya watu, Jaji Malata alisema si vema mwanafunzi anahitimu shahada kisha anakwama miaka kadhaa katika Shule Kuu ya Sheria, sababu anafeli.
“Watu wanakukuruka hawatoki, watu wamemaliza shahada zao, ni nguvu kazi hao, wakiachwa watachangia uchumi, lakini kwanini wanashindwa kutoka, haya yote yafanyiwe stadi kujua tatizo. Swali gumu lina majibu magumu pia,” alifafanua.
Mtazamo wa Jaji Malata unaungwa mkono na Wakili Fulgence Massawe aliyesema kuna haja ya kuundwa tume kuchunguza tatizo lililopo.
Kwa kuwa LST hukutanisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali waliofundishwa na mifumo tofauti, alisema tume ya uchunguzi ni muhimu kuundwa.
Mbali na tume, Massawe alitaja changamoto katika ufundishaji wa ngazi hiyo ya sheria kuwa ni mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi takriban 800 katika darasa moja.
“Kwa sababu hii, hakuna namna inayomwezesha mwalimu kujua kama ameeleweka au la, lakini hata wanafunzi kuuliza maswali wakati wanafundishwa inakuwa vigumu.
“Tuunde tume ichunguze, tutajua tatizo ni shule ya sheria au walikotoka wanafunzi, lakini tukisema walikotoka, kuna watu wanatoka kwenye vyuo vinavyoaminika lakini wanakwenda pake wanafeli, kuna haja ya kujua lilipo tatizo,” alisema.
Mtalaa watajwa
Mwanataaluma mwingine, Dk Neema Mwita, mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza, alitaja mtalaa wa t sheria kuwa sehemu ya sababu za changamoto ya ufaulu katika masomo hayo.
Katika Shule Kuu ya sheria, alisema mwanafunzi anajifunza kwa vitendo kile alichokisoma kwa nadharia alipokuwa chuo kikuu, hivyo huo unakuwa utaratibu mpya katika masomo yake.
Alishauri mtalaa wa sheria chuo kikuu uweke ulazima wa mafunzo kwa vitendo kwa kila mwanafunzi wa sheria, ili anapofika Shule Kuu ya Sheria asikutane na vitu vipya.
“Katika masomo ya shahada kuwe na fani ya kuandaa nyaraka za kisheria ili mwanafunzi akifika Shule Kuu ya Sheria angalau awe anajua, maana hivi ndivyo vitu anavyokwenda kujibia mtihani,” alisema.
Iwapo kila chuo kitakuwa na utaratibu huo, alisema idadi ya wanaofeli itapungua kwa kuwa tayari watakuwa na msingi mzuri.
Mfumo wa ufundishaji
Mmoja wa wanafunzi wa LST (jina limehifadhiwa), alitaja mfumo wa ufundishaji kuwa tatizo katika matokeo hayo.
Alisema mafunzo katika shule hiyo hutolewa kwa muda mfupi, ikiaminiwa kuwa tayari mwanafunzi alishasoma akiwa chuo kikuu, jambo ambao si kweli.
“Somo moja mnamaliza kwa wiki moja, somo hilo hilo mlipokuwa chuoni mlisoma kwa mwaka mmoja, vitu havifanani, wao wanaamini mlishajifunza lakini uhalisia ni kwamba mnakutana na mambo mapya,” alisema.
Alishauri shule hiyo ipunguze idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa na iongeze muda wa masomo ili kuongeza ufaulu.
“Bora LST ichukue wachache na wasome kwa muda mrefu ili ufaulu usibaki kuwa bahati ya wachache,” alisema.
Mwanafunzi mwingine alidai kinachowafelisha wengi ni utaratibu wa shule hiyo ambapo, unachofundishwa sicho utakachoulizwa kwenye mtihani.
Changamoto nyingine , alisema ufundishaji wa chuo kikuu hauhusishi zaidi uchambuzi wa sheria, jambo ambalo linafanyika katika shule ya sheria.
“Chuo Kikuu unaweza kufundishwa na mwalimu asiyepita hata katika Shule Kuu ya Sheria, hajui huku tunakuja kukutana na nini, hatujengewi msingi utakaotuwezesha kuyamudu ya huku,” alisema.
Walivyoandaliwa shida
Akijibu hoja hizo, Makamu Mkuu wa Chuo (Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo na Utafiti), Profesa Zakayo Lukumay alisema tatizo kubwa linatokana na namna wanafunzi hao walivyoandaliwa katika vyuo vikuu walivyotoka.
“Waliofundishwa na walimu wazuri wanafaulu, lakini waliofundishwa vibaya ndiyo hao wanaofeli kwa kuwa wanakuja na uelewa mdogo ilhali asili ya mafunzo yetu (shule ya sheria) ni kufanya kwa vitendo,” alisema.
Kinachotokea kwa wanaofeli, alisema maana yake mwanafunzi anashindwa kukitafsiri alichofundishwa kwa nadharia kwenda kwenye vitendo.
Alisema katika shule hiyo kinachofundishwa ni jinsi ya kuifanya kazi ya taaluma husika, mathalan namna ya kumuhoji shahidi na kuandaa nyaraka za kisheria, wakiamini kuwa tayari mwanafunzi huyo alishafundishwa maana ya shahidi.
“Kule chuoni alijifunza kitu kinachoitwa hukumu, kinatakiwa kuwaje, lakini huku shule ya sheria tunamtaka aandike hukumu,” alisema.
Alisema wanaofeli wengi wao, hawajui kufanya vile walivyoelekezwa kwa nadharia.
Kuhusu mitihani, Profesa Lukumay alisema inahusisha kueleza mlolongo wa tukio na mwanafunzi anatakiwa kujibu kwa kushauri kisheria na kuandaa nyaraka zinazohitajika.
Kwa bahati mbaya, alisema wanafunzi wengi wanajibu kwa kueleza utaratibu badala ya kuandaa nyaraka kama ambavyo swali linahitaji na hapo ndipo wanapokosea.

Chanzo: Mwananchi
 
Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

Credit: Malcom Lumumba
 
Sijui kwa nn akil yangu huniaminisha cjui wanasheria, mawakili naonaga hawanaga akili....yaan naonaga kama wamewehuka...cjui ni aina ya mavaz ya kaz zao...tena hii ya kujiita wakili msomi afu ukimtazama ndio mbufi kabisaa...na ukimdate mwanamke mwanasheria yaan utachanganyikiwa na hata barabara ya vumbi tuu unaweza vushwa na katoto ka chekechea....

NB : wamefeli kihaki kabisaa...ni akili hawana...mbona hao wengine wamefaulu..
 
Kupata Leseni ya kazi ni ngumu kuliko Degree nchi hii ngumu sana kukwamishana ndio sifa kuu ya mtu mweusi...kama mnaona hiyo ni muhimu na watu hawasomi mnachotaka ninyi iwekeni kwenye mitara ya vyuo huko sema mnafurahi kuona watu wengi mkiwaferisha kwa vitu wanavyovijua..
Angalia wewe mwenyewe hapa hata hujui Kiswahili fasaha, sasa niambie hao wa TLS ambapo kitu cha kwanza kwa wakili ni kujua kiingereza fasaha maana hukumu zote zinaandikwa kwa Kiingereza. Hivi ulisikiliza ile petition ya Kenya majuzi kati ya mawakili wa Odinga na Ruto? Ingia you tube usikilize mchuano wa mawakili. Vijana wengi wanamaliza chuo huko Kiingereza ni shidaaa sasa utafaulu vp huko law school? Wakiwa chuoni siku hizi wengine unakuta thesis wanaandikiwa, wengine tunasikia digrii za nguo za ndani na makando kando kibao, wakifika huku juu ambapo hakuna mambo ya michongo wanalia lia.
 
Lakini inawezekana. Unajua vyuo vikuu vingi vya Bongo siku hizi ni bora liende. Kuna wahitimi wa degree ya sheria nawafahamu ni vilaza kweli kweli. Sijui kama madaktari wana mitihani kama hii lakini nadhani huko pia vilaza wengi. Ni kila sekta.
Hata madaktari ni the same mkuu, na mimi ningeshauri madaktari nao wawe na taasisi mfano wa hii law school kwa sababu bila kuwachuja hawa huko ma hospitalini itakuwa balaaa kabisa.
 
Najua unacholalamikia na mimi nakuunga mkono. Mtihani wowote wanapofeli watahiniwa wengi inaonyesha kuna kasoro mahali, na mara nyingi tatizo linakuwa siyo kwamba watahiniwa hawana elimu ya kutosha. Hili tatizo liko hata kwenye vyuo vikuu vyetu.

Unaweza kukuta wanaofeli na ku-sup ni wengi mpaka unashangaa. Hili linaonenyesha kuwa elimu yetu imejikita kwenye kuwakaririsha wanafunzi na upimaji ume-base zaidi kwenye mitihani na siyo uelewa.

Lakini pamoja na hayo, vile vile ma-graduate wengi wa siku hizi, kwenye sekta zote wengi ni vilaza. Si mainjinia, madaktari au wanasheria.
Nakuunga mkono kabisa
 
Ni kweli, unapata degree baada ya kukidhi vigezo, ila unabaniwa usipate leseni, roho mbaya na ubinafsi tu.
Sasa kama umepata degree ya mchongo uachwe tuu uende mahakamani na serikalini kuingia mikataba ya ajabu ajabu kama ile ya makanikia?? [emoji12] [emoji12]
 
Believe me, hizi "excuse" mnazotoa ndio zinawapa sababu hao walimu wa Law School wazidi kufelisha wanafunzi wengi zaidi.

Ni kawaida, kila tasnia lazima iwe na competence ili kuiletea mafanikio, sasa kwa hao walimu wa Law School wanaoongoza kwa kufelisha, ubora wao utapimwa kwenye kitu gani? au ndio kwa kufelisha wanafunzi wengi?! Ajabu.

Au kwa hizi "excuse" zenu, mnakubali kuwageuza hao walimu wa Law School kuwa miungu watu wasiopimwa perfomance yao popote?!

No, this is unacceptable.
Vijana mkiwa Universities someni, achaneni na hulka za kufanya chuo kikuu ni sehemu ya kula bata, kufanya biashara, kuchukua mademu etc.. Vijana hamsomiii, na majority wanakariri, hamuendi library kukuelimisha zaidi, nyie mnakomaa na ma past papers kama vijana wa sekondari. Nina vijana wangu wawili wako Universities aisee yaani nikisikiliza mazungumzo yao kwa kweli hakuna kitu. Kazini kwangu kuna volunteers 3 wote graduates kiukweli uwezo wao ni mdogo sanaaa, mpaka najiuliza tatizo ni mfumo wetu wa elimu au ni nini hasa? Unawatuma kazi pamoja na kuwapa guidelines za hiyo kazi na format ya ripoti lakini kama hutawapa mtu wa kuwasimamia jua hiyo kazi utakuja kuirudia...
 
Back
Top Bottom