Idadi ya wanaofeli Law School of Tanzania yazua utata

Idadi ya wanaofeli Law School of Tanzania yazua utata

Najua unacholalamikia na mimi nakuunga mkono. Mtihani wowote wanapofeli watahiniwa wengi inaonyesha kuna kasoro mahali, na mara nyingi tatizo linakuwa siyo kwamba watahiniwa hawana elimu ya kutosha. Hili tatizo liko hata kwenye vyuo vikuu vyetu.

Unaweza kukuta wanaofeli na ku-sup ni wengi mpaka unashangaa. Hili linaonenyesha kuwa elimu yetu imejikita kwenye kuwakaririsha wanafunzi na upimaji ume-base zaidi kwenye mitihani na siyo uelewa.

Lakini pamoja na hayo, vile vile ma-graduate wengi wa siku hizi, kwenye sekta zote wengi ni vilaza. Si mainjinia, madaktari au wanasheria.
Hiyo paragraph ya mwisho umemaliza kila kitu, call spade a spade..
 
Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...



Credit: Malcom Lumumba
Well spoken...naomba uwekwe kwenye jopo la utafiti. Una hoja za msingi sana.
 
Angalia wewe mwenyewe hapa hata hujui Kiswahili fasaha, sasa niambie hao wa TLS ambapo kitu cha kwanza kwa wakili ni kujua kiingereza fasaha maana hukumu zote zinaandikwa kwa Kiingereza. Hivi ulisikiliza ile petition ya Kenya majuzi kati ya mawakili wa Odinga na Ruto? Ingia you tube usikilize mchuano wa mawakili. Vijana wengi wanamaliza chuo huko Kiingereza ni shidaaa sasa utafaulu vp huko law school? Wakiwa chuoni siku hizi wengine unakuta thesis wanaandikiwa, wengine tunasikia digrii za nguo za ndani na makando kando kibao, wakifika huku juu ambapo hakuna mambo ya michongo wanalia lia.
Mkuu unanikosoa kiswahili muda huu nipo kwenye ukaguzi wa Engine za Scania ni kunionea tuu...hiyo kesi nimeangalia kwenye ilikua ikionyeshwa kwenye Luninga wakati kesi zetu hapa haziruhusiwi hata kupiga picha ndani ya chumba cha mahakama nimeona kesi nyingi zikirushwa tunaangalia ipo ya Zuma au wale wauza unga walipohukumiwa kwenye mahakama za USA ila hapa kutokana na watu wengi kukariri vitu vingi mnaambiwa haviwezekani na mnaishi hivyo...
 
Prof Shivji kasema pana sehemu wameteleza watafanyia marekebisho humu mtu ana ka Elimu hako hako anakomaa kuona wapo sahihi hakuna makosa...mkisoma ni vizuri mkapata na Exposure pia ya Vyuo vikubwa Duniani wanafanya nini mbona hawana Ujinga kama wa kwetu..
 
Wanafunzi wengi vilaza waache wafeli. Law imekuwa jalala la vilaza siku hizi. Mwanafunzi anaunga unga toka certificate hadi degree mnataka achukue uwakili kizembe?

La hasha.
 
Idadi iyo ni sawa na 4.1% pekee kati ya wote waliofanya mtihani, huku wengine 484 wakitakiwa kurudia mtihani na 265 wakiondolewa kabisa baada ya kufeli.

Hali hiyo imefanya Wanasheria na wadau wengine kutaka iundwe Tume ya kuchunguza sababu akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu Gabriel Malata aliyesema nguvukazi kubwa inapotea kwa wahitimu wengi kukwama shuleni hapo.

Takwimu zaidi zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 4,397 na waliofaulu ni 792, waliotakiwa kurudia mtihani ni 2095 wakati waliofeli ni 1,074.
Ni suala la kufanya uchunguzi kujua tatizo ni nini. Tusilazimishe hoja za upande mmoja. Changamoto za elimu yetu ni mjumuiko wa mambo mengi.
 
Idadi iyo ni sawa na 4.1% pekee kati ya wote waliofanya mtihani, huku wengine 484 wakitakiwa kurudia mtihani na 265 wakiondolewa kabisa baada ya kufeli.

Hali hiyo imefanya Wanasheria na wadau wengine kutaka iundwe Tume ya kuchunguza sababu akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu Gabriel Malata aliyesema nguvukazi kubwa inapotea kwa wahitimu wengi kukwama shuleni hapo.

Takwimu zaidi zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 4,397 na waliofaulu ni 792, waliotakiwa kurudia mtihani ni 2095 wakati waliofeli ni 1,074.
Mwanafunzi ananyoa kiduku, anabeti, anaenda uwanja taifa kuangalia mpira eti sosho life, wacha waliwe vichwa.
 
Believe me, hizi "excuse" mnazotoa ndio zinawapa sababu hao walimu wa Law School wazidi kufelisha wanafunzi wengi zaidi.

Ni kawaida, kila tasnia lazima iwe na competence ili kuiletea mafanikio, sasa kwa hao walimu wa Law School wanaoongoza kwa kufelisha, ubora wao utapimwa kwenye kitu gani? au ndio kwa kufelisha wanafunzi wengi?! Ajabu.

Au kwa hizi "excuse" zenu, mnakubali kuwageuza hao walimu wa Law School kuwa miungu watu wasiopimwa perfomance yao popote?!

No, this is unacceptable.
Sasa kama wakili siku zote unanyoa kiduku, unavaa mlegezo, unaongea kama kibaka ww unafikiri watakuacha salama? taaluma ya uwakili ni kama ualimu, ukiachana na content unayosoma darasani unaangaliwa na mienendo Yako nje ya darasa Kwa sababu ni taaluma ambayo inafanya kazi na jamii Moja Kwa Moja, waasisi wa taaluma ya uwakili walishaweka vigezo vya muonekano wa wakili ila vijana wa Sasa wanaingia darasani wamevaa mlegezo, kiduku, uongeaji mbovu, watu wanawaangalia tu na ni vitu ambavyo hauambiwi kama vinachunguzwa, mwisho wa siku watu wanakula vichwa mnakuja kulalamika, ngoja wafundishwe ethics Kwa vitendo akili ikae vizuri
 
Back
Top Bottom