Idadi ya wanaofeli Law School of Tanzania yazua utata

Hiyo paragraph ya mwisho umemaliza kila kitu, call spade a spade..
 
Well spoken...naomba uwekwe kwenye jopo la utafiti. Una hoja za msingi sana.
 
Mkuu unanikosoa kiswahili muda huu nipo kwenye ukaguzi wa Engine za Scania ni kunionea tuu...hiyo kesi nimeangalia kwenye ilikua ikionyeshwa kwenye Luninga wakati kesi zetu hapa haziruhusiwi hata kupiga picha ndani ya chumba cha mahakama nimeona kesi nyingi zikirushwa tunaangalia ipo ya Zuma au wale wauza unga walipohukumiwa kwenye mahakama za USA ila hapa kutokana na watu wengi kukariri vitu vingi mnaambiwa haviwezekani na mnaishi hivyo...
 
Prof Shivji kasema pana sehemu wameteleza watafanyia marekebisho humu mtu ana ka Elimu hako hako anakomaa kuona wapo sahihi hakuna makosa...mkisoma ni vizuri mkapata na Exposure pia ya Vyuo vikubwa Duniani wanafanya nini mbona hawana Ujinga kama wa kwetu..
 
Wanafunzi wengi vilaza waache wafeli. Law imekuwa jalala la vilaza siku hizi. Mwanafunzi anaunga unga toka certificate hadi degree mnataka achukue uwakili kizembe?

La hasha.
 
Ni suala la kufanya uchunguzi kujua tatizo ni nini. Tusilazimishe hoja za upande mmoja. Changamoto za elimu yetu ni mjumuiko wa mambo mengi.
 
Mwanafunzi ananyoa kiduku, anabeti, anaenda uwanja taifa kuangalia mpira eti sosho life, wacha waliwe vichwa.
 
Sasa kama wakili siku zote unanyoa kiduku, unavaa mlegezo, unaongea kama kibaka ww unafikiri watakuacha salama? taaluma ya uwakili ni kama ualimu, ukiachana na content unayosoma darasani unaangaliwa na mienendo Yako nje ya darasa Kwa sababu ni taaluma ambayo inafanya kazi na jamii Moja Kwa Moja, waasisi wa taaluma ya uwakili walishaweka vigezo vya muonekano wa wakili ila vijana wa Sasa wanaingia darasani wamevaa mlegezo, kiduku, uongeaji mbovu, watu wanawaangalia tu na ni vitu ambavyo hauambiwi kama vinachunguzwa, mwisho wa siku watu wanakula vichwa mnakuja kulalamika, ngoja wafundishwe ethics Kwa vitendo akili ikae vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…