Idadi ya Wapiga Kura inavyoshuka licha ya kuongezeka kwa waliojiandikisha – Taifa lenye hofu, hasira na kukata tamaa

Idadi ya Wapiga Kura inavyoshuka licha ya kuongezeka kwa waliojiandikisha – Taifa lenye hofu, hasira na kukata tamaa

Mmh! Ngoja tuone bwana, ila natamani kuona mabadiliko makubwa kwenye nchi yetu. Mabadiliko ya nchi yatakayobadili na hali za wananchi kuwa nzuri zaidi bila kujali kupitia chama gani.
Sahihi
 
Mimi hata wasipate hizo 99, wapate hata 200% lkn siwezi poteza huo muda wa kwenda kupanga foleni ya eti kupiga kura kwa uchaguzi ambao matokeo yanajulikana
 
Mimi hata wasipate hizo 99, wapate hata 200% lkn siwezi poteza huo muda wa kwenda kupanga foleni ya eti kupiga kura kwa uchaguzi ambao matokeo yanajulikana
Facebook Ambako kuna vilaza Kila mtu anasema No reforms no election
 
Yeyote atakaye kwenda KUPIGA KURA rasmi NI adui WA mabadiliko na NI adui WA Nchi yetu tutamtenga.
No Reforms No Election
 
Sipangiwi cha kusoma wala cha kupost

Nimependekeza jukwaa la uzushi

Mods Wana admin can reject pia

ILA huu uzushi wa huyo mpuuzi hauwezi kuachwa tu as if watanzania ni mabwege fulani
Sio watanzania, sema wanaccm.
 
mbona hii haijapelekwa kwenye Fact Check?
 
Facebook Ambako kuna vilaza Kila mtu anasema No reforms no election


Lazima uwe mwendawazimu wa uzao wa shetani, kuweza kwenda kupoteza muda kwenye uchaguzi ambao unajua kabisa siyo uchaguzi bali ni tukjo lililojaa hadaa na hila za mashetani kutaka kuwaunganisha wananchi na ibilisi mdhulumu haki.
 
Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Wakati Tanzania ikiendelea kujigamba kuwa nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi, takwimu haziungi mkono propaganda hiyo. Hii hapa ni grafu inayoonesha wazi takwimu kutoka mwaka 1995 hadi 2020 kuhusu:

1.Idadi ya watu (population)
2.Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura
3.Idadi ya waliopiga kura halisi (voter turnout)

KILA MWAKA, watu wanazidi kujiandikisha lakini idadi ya wanaojitokeza kupiga kura inazidi kuporomoka. Kwanini? Hebu tuangalie.

🗓 1995 na 2000:
Ni miaka ya mwanzo wa mfumo wa vyama vingi. Ushiriki ulikuwa mdogo kwa sababu ya hali mpya ya kisiasa, udhaifu wa upinzani na mfumo wa kiutawala uliorithiwa kutoka enzi ya chama kimoja.

🗓 2005:
Serikali ya awamu ya nne ilianza kwa kishindo, lakini bado mazingira ya kisiasa yalikuwa magumu. Hata hivyo, kulikuwa na matumaini ya mabadiliko. Ushiriki ukapanda.

🗓 2010 – Watu walianza kukata tamaa:
Mwaka huu ulikuwa wa kashfa kubwa. Tulishuhudia:
1.EPA
2.Richmond
3.Escrow
Kuongezeka kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Matokeo? Idadi ya wapiga kura ilishuka licha ya watu wengi kujiandikisha. Wananchi walihisi sauti yao haijalishi.

🗓 2015 – Chama cha upinzani kilipopata nguvu ya kihistoria:
Umoja wa UKAWA na kuhamia kwa Edward Lowassa na wanasiasa wengine wa CCM upande wa upinzani kulileta ushindani wa kweli. Watu waliona kuna uwezekano wa mabadiliko.
Matokeo yake? Idadi ya wapiga kura ilipanda kwa kasi – wananchi waliamka.

🗓 2020 – Anguko kubwa la imani ya wananchi:
1.Vyama vya upinzani vilizuiwa kufanya mikutano.
2.Wabunge walivuliwa uanachama kwa matamko ya kisiasa.
3.Vyombo vya habari vilinyamazishwa.
4.Wapinzani walihama kwa hofu, vitisho, au vishawishi.
5.Tume ya Uchaguzi (sasa INEC) ilionekana kuwa mkono wa chama tawala, si chombo huru cha kusimamia demokrasia.

Matokeo? Watu wengi waliamua kukaa nyumbani – haikuwa uchaguzi tena, ilikuwa “tukio la kichama.”

🎯 HITIMISHO:
Tanzania inazalisha kizazi cha watu waliokata tamaa, waliojeruhiwa kisiasa, na wasioamini tena katika mfumo wa uchaguzi. Watu milioni kadhaa wanajiandikisha, lakini wanajua kura yao haina maana. Hii ni hatari kwa mustakabali wa taifa.

📌 TUJIULIZE:
1.Kwa nini kila uchaguzi ni wa amani kwa chama tawala tu?
2.Kwa nini watu wanapewa ahadi kila baada ya miaka mitano na kisha kusahaulika?
3.Kwa nini tume ya uchaguzi isifanywe kuwa huru kabisa?

Ukiangalia takwimu hizi na historia ya matukio ya kisiasa, utagundua: matatizo ya ushiriki mdogo si uzembe wa raia, ni uonevu wa mifumo.

#NoReformsNoElections
#TumeHuruSasa
#KurayanguInaThamani
View attachment 3393666
Hizo takwimu tume inadangabya azitoa wapi? wakati wao huwa wanachukua taarifa zilizo pikwa miaka yote? hivyo hawawezi kupata uhalisia wa wapiga kura, maana wao wanawategemea wasimamizi wa uchaguzi ambao wanatengeneza kura feki kwa ku tik kwa wagombea wa ccm kwa maelekezo kutoka juu, hivyo waweza kuta kura halali ni 20% tu ya kura zote sasa hizo takwimu wanazitoa wapi?
 
Back
Top Bottom