Basi utachukua kikombe chako, au utaelekea kwenye sink hapa tuelezane lazima uwe na maji mengi kwa uchache lita moja, basi utatia dawa yako katika mswaki kiwango cha kuridhisha utaanza kusafisha kinywa meno pande zote, ukuta wa juu na ukuta wa chini, fizi lakini pia toa ulimi kwa nje safisha ulimi hadi uwe msafi kabisa, unaweza kutema povu hilo, unaweza kuweka dawa kidogo tena katika mswaki na kuanza tena kusafisha kama mwanzo basi utatema povu lile, halafu utatakiwa kukosha mswaki wako, baadae weka maji mdomoni tema, weka tena maji mengine mdomoni anza kupitisha na mswaki bila dawa ili kuondoa shombo ya dawa, maana mwingine ataswaki lakini kinywa kinanuka dawa ya meno tu, hivo utamaliza kwa kuweka maji ya mwisho kusuuza kinywa chako vizuri, unaweza usafishe ulimi kwa mswaki lakini kama unayo tongue wash utatumia pia, lakini pia kati na jino na jino kuna uzi maalumu unapitisha kuondoa mabaki ya chakula maana kule mswaki haufiki kwani meno yamebanana sana. Hapo taratibu za usafi wa kinywa kwa ufupi unakua umemaliza