Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?
Halafu hatuoni hata Maisha Yakiwa Afadhali Hata Kidogo

Hadi Pipi Yenyewe haijashuka Bei hata Watoto wafaidi
 
Ndiyo maana promotions zimesimamishwa kwa muda ili haya yafanyike. Hao nyuki dar mnafugia wapi?

Wewe unawaza kufuga nyuki tuu? Kuna ukaguz mbalimbali wa mazao ya nyuki. Matatizo ya division five, you have narrow mind
 
.
Kama ni kweli, hilo ni wazo zuri. Nimekaa huko wilayani na kuona mengi yenye mapungufu. Hivyo, kwa ajili ya ufanisi na uharaka, kama ningeulizwa, ningependekeza idara TANO zifuatazo katika Halmashauri zetu:

1.Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
2.Idara ya Elimu, Utamaduni na Michezo.
3. Idara ya Itikadi, Utawala, Fedha na Mipango.
4. Idara ya Oikonomia (yaani Uchumi), ikijumuisha Maliasili, Mazingira, Kilimo, Mifugo, na Ushirika.
5. Idara ya Ujenzi wa Miundombinu ya barabara, maji na makazi.

Idara tano tu zinatosha, kila moja ikiwa na vitengo vyake. Tuzikumbuke kwa msaada wa vokali za A-E-I-O-U, yaani: Afya, Elimu, Itikadi, Oikonomia na Ujenzi.

Mchana mwema.
 
Hakuna mtu atapoteza ajira bali wata hamishiwa kwenye vitengo vingine? Hivi unajua sheria za utumishi wa Umma? Kama mgelikuwa mna msikiliza waziri wa tamisemi bungeni wala msingalisema haya hili jambo halikuanza kuongelewa leo!
bunge likibaki na wale wa ndioooo sio bunge tena c unaona ka 18% kanavyowatesa. Wangekuepo wajenga hoja tusingekua na huu mjadala
 
kwa kwa kwi kwi acha nicheke mwana wa watu jina langu makata
 
Procurement ni idara nyeti sana, ipo na ni kiungo cha idara ya sheria ili serikali kuweza kununua. Labda wanaiua na PPRA
Singida mnajulikana kwa unafiki, kila kitu ni kupongeza tu.
 
Procurement ni idara nyeti sana, ipo na ni kiungo cha idara ya sheria ili serikali kuweza kununua. Labda wanaiua na PPRA
Singida mnajulikana kwa unafiki, kila kitu ni kupongeza tu.
Mtake radhi Mh Tundu Antipas Lissu
 
UTENGENEZAJI wa ajiira hakuna tena.Maana itakuwa zimepunguzwa.Huku kwenye sekta binafsi nako itakuaje?
 
Watz mnataka nin kulikuwa na wizara na idara nying mkalalamika sasa hivi znapunguzwa bado ni shida matokeo_2020?
 
Nivema kupunguza mrundikano wa ajira zisizo na msingi,watu wanaenda kazini kupiga stori na kuoneshana mavazi na misuko!! Ajira zienee kwenye Elimu,afya,polisi,zimamoto,kilimo kwenye field sio ofisini alllla
HEKO MAGUFULI, hizi ndio big brains safisha vizuri vijana wapate kazi
 
HAO wafanyakazi wa hizo idara zitakazopunguzwa watahamishiwa kwingine,kurudi walipokuwa awali kabla ya uteuzi au watapewa chao na kwaheri?
 
mkuu umesema watabaki 8, kwani mwanzoni walikuwa wangapi?
 
Watakaopoteza ajira hapo wataajiriwa kwenye viwanda vinavyojengwa. Nisicho na uhakika nacho ni kama wakati wa redundancy viwanda vitakuwa tayari vina operate! cc:MO11
Kufikirika huwaga kunaweza kukageuka kuwa kusadikika
 
Hakuna atakayepoteza ajira hata mmoja vitengo vyote vitajumuisha watumishi wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…