Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

Watapoteza Ajira wapi? Nenda Jiji la Nyamagana Kitengo cha ugavi na maeneo mengine kwa ndani ujionee vidada vya 50-50 na V ijana wa mtepesho wanachati na hata ya Ilemera hivyo hivyo je Mkoa mzima? Magu komaa nao wapungue hakuna namna nchi iende
 
Kila siku unakata miti. Unatengeneza jangwa. Halafu bado unategemea mvua inyeshe kwa wingi. Hatari sana.

Hapo unapoteza P.A.Y.E., unapoteza "purchasing power" iliyokuwepo. Unaongeza idadi ya wasio na ajira. Utakusanya kodi kutoka wapi? Inashangaza sana.

Haya ni madhara ya mawazo ya mtu mmoja kuendesha watu zaidi ya milioni 50....

Mkuu, P.A.Y.E utapoteza lakini utaifidia kwa kuokoa fedha nyingi iliyokuwa inatumika kuwalipa hawa watumishi wa hizo idara nyingi zisizo na tija. Waliokuwa wakuu wa idara zitakazofutwa ni sawa kuwapangia kazi nyingine au hata kuwapunguza kazi. Kuwalipa kwa kazi isiyoonekana ni mbaya zaidi kiuchumi. Na ndiyo maana tuna deni la taifa kubwa. Serikali haiwezi kuwa mwajiri wa kilamtu. Changamoto kwa serikali ni kukuza private sector, itoe ajira. Kwa miaka mingi sana serikali yetu imekuwa inatumia fedha ambazo kimsingi haina. Na ndiyo maana tuna madeni na umaskini umeendelea kutamalaki. It is time to break the circle of poverty. Tumecheza sana mduara kwenye huu wimbo wa umaskini. Kwa hili nitaiunga mkono serikali. Seriously, kuna watumishi serikalini wamekuwa wanafika ofisini wanalipwa mishahara na posho kwa kazi zisizoonekana. This needs to stop.
 
Utaratibu mzuri sana huu!Viva JPM na washauri wako kuhusiana na hili kupunguza idara.
Unakuta Maafisa Elimu 10,wakiwa hawana hata kazi za kufanya ofisini,zaidi ya kupiga umbeya na kutafuta dili za rushwa,jambo linalopunguza ufanisi wa utoaji elimu.Hii hutokea hata kwa idara zingine.
Mfano,unakuta
Elimu msingi wilayani kuna
1.Afisa Elimu
2.Taalum No.1,No.2,No.3,
3.Vielelezo No.1,No2,No3. 4.Ufundi.
5.Sayansi kimu.
6.Mazingira
7.Elimu Maalum
8.Michezo
9.Watu wazima
10.Vifaa
Pia unakuta kuna Waratibu TRC na waratibu elimu kata wakutosha, ambao wanahesabika wapo kazini lakini hawana vipindi darasani.
Narudia kuunga mkono mpango huu wa kurejebisha idara wilayani kuongeza ufanisi
Kichefuchefu kiko idara ya ardhi mkuu, jamaa ofisi uzifanya kama vijiwe au kampuni binafsi, uliza utaratibu wa kupima ardhi yako kama watakupa wanaishia kusema ni gharama kubwa, document moja kuweka saini tu inachukua miez 6 hadi mwaka, kazi yao ni kuongozana kwenye supu na chai.Jamaa wanakera sana hawa sijui mshahara wanawalipa wa kazi gani, mtu haonekani kazini wiki nzima kwa kisingizio eti yuko site, kumbe yuko kwenye shughuli zake binafsi, hivi kweli unaweza kwenda site posipo kureport kwanza kazini asubuhi.
 
watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?

Hii ni speculation kwanza. Pili kama itakuwa hivyo kuna mahali pamesemwa watafutwa kazi?
 
Magu anajitahidi kupunguza administrative cost watu wanajazana maofisini hamna kinachofanyika

Hamna tija yoyote kwenye maendeleo zaidi ya kuongeza garama za uendeshaji.

Ondoa watu kwenye halmashauri wakafanye kazi zenye tija kwa taifa.
 
Mkuu, P.A.Y.E utapoteza lakini utaifidia kwa kuokoa fedha nyingi iliyokuwa inatumika kuwalipa hawa watumishi wa hizo idara nyingi zisizo na tija. Waliokuwa wakuu wa idara zitakazofutwa ni sawa kuwapangia kazi nyingine au hata kuwapunguza kazi. Kuwalipa kwa kazi isiyoonekana ni mbaya zaidi kiuchumi. Na ndiyo maana tuna deni la taifa kubwa. Serikali haiwezi kuwa mwajiri wa kilamtu. Changamoto kwa serikali ni kukuza private sector, itoe ajira. Kwa miaka mingi sana serikali yetu imekuwa inatumia fedha ambazo kimsingi haina. Na ndiyo maana tuna madeni na umaskini umeendelea kutamalaki. It is time to break the circle of poverty. Tumecheza sana mduara kwenye huu wimbo wa umaskini. Kwa hili nitaiunga mkono serikali. Seriously, kuna watumishi serikalini wamekuwa wanafika ofisini wanalipwa mishahara na posho kwa kazi zisizoonekana. This needs to stop.

Mkuu, umeliona hilo la P.A.Y.E ni dogo? Nashangaa.

Haya tuchambue kidogo, japo kwa ufupi tu lakini: Umewafukuza kazi hao maelfu. Unawalipa kiinua mgongo. Umekosa hiyo

P.A.YE. Wamekosa ajira. Hawana uwezo mkubwa tena wa kununua. Waliotegemea nguvu yao ya kununua hawana tena uwezo wa kuuza. Mnyororo unaendelea.

Mwisho kodi uliyotazamia kukusanya ulipe mishahara ya uliowabakisha nayo itayumba. Lazima.
 
Jpm anipe kitengo kimoja basi.Kufa kufaana.
 
Nivema kupunguza mrundikano wa ajira zisizo na msingi,watu wanaenda kazini kupiga stori na kuoneshana mavazi na misuko!! Ajira zienee kwenye Elimu,afya,polisi,zimamoto,kilimo kwenye field sio ofisini alllla
HEKO MAGUFULI, hizi ndio big brains safisha vizuri vijana wapate kazi
Kiuchumi maana yake Ajira hazitakuwepo Vitengo na Idara ziki ungana Kazi aliyokuwa anafanya A inawezwa kufanywa na B wa Idara fulani.mfano mzuri ni wizara zilizoungana Mpaka sasa watumishi wake hawajapata muafaka wataenda wapi
 
Hii mkuu wacha ije tu kwa kweli nilikuwa nakasirika sana unalikuta pumbavu likuu la idara eti linashabikia ujinga wa ccm! Sasa wacha yaisome namba, ila nashindwa kuelewa ufanisi utakuwaje maana mtu aliyesoma ushirika akawe mkuu wa idara ya kilimo, mifugo, uvivu, umwagiliaji na ushirika sijui itakuwaje aiseee!
Hata mimi hii nimeipenda kuna afsa manunuzi hapo manispaa ya bukoba bw.Lubuva, huyo jamaa ni balaa, aacha apigwe chini na hivo elimu yake ni ya hapa na pale ataisoma namba alikuwa anajiona mungu mtu, usipomkatia chake invoice yako haiendi uhasibu.
 
LGAs zote hazifanani katika umhimu wa sekta. Mafia kwa kilimo na mifugo ni tofauti na Geita.
LGAs zingependekeza idara wanazohitaji na kushauriana na PoRalg.
LGAs siyo idara za central government., wala siyo chombo chake.
ni kweli mfano Kitengo cha nyuki kilichoanzishwa na Mizengo Pinda ktk Mikoa mingine hawafugu nyuki lakini unakuta sehemu hizo kuna Ma afisa nyuki
inatakiwa Vitengo na Idara ziendane na shughuli za kiuchumi za Halmashauri
 
Hakuna mtu atapoteza ajira bali wata hamishiwa kwenye vitengo vingine? Hivi unajua sheria za utumishi wa Umma? Kama mgelikuwa mna msikiliza waziri wa tamisemi bungeni wala msingalisema haya hili jambo halikuanza kuongelewa leo!
Idara zikichanganywa vitengo vinapungua sasa unasema wataamishiwa kwenye vitengo vingine, vitengo hewa ama??
 
watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?
Ufanisi na tija unatuelekeza kuwa kazi ya mtu mmoja isifanywe na watu zaidi ya 1. Nchi hii ni ya Watanzania, nao wanastahili kuhudumiwa na watumishi wa umma wanaowajibika na kulipwa hali stahiki. Lakini kwa mawazo yako unataka Serikali ijaze watu 18; kila mmoja afanye theruthi moja ya kazi lakini alipwe tatu ya tatu ya mshahara! Kuweni wazalendo jamani. Looh
 
Kichefuchefu kiko idara ya ardhi mkuu, jamaa ofisi uzifanya kama vijiwe au kampuni binafsi, uliza utaratibu wa kupima ardhi yako kama watakupa wanaishia kusema ni gharama kubwa, document moja kuweka saini tu inachukua miez 6 hadi mwaka, kazi yao ni kuongozana kwenye supu na chai.Jamaa wanakera sana hawa sijui mshahara wanawalipa wa kazi gani, mtu haonekani kazini wiki nzima kwa kisingizio eti yuko site, kumbe yuko kwenye shughuli zake binafsi, hivi kweli unaweza kwenda site posipo kureport kwanza kazini asubuhi.
Ha
eti nyuki nacho ni Kitengo na Mkuu wake wa Idara analamba 3.4 M

Alafu utakuta hiyo wilaya haina hata msitu wenye mizinga 20
 
Kichefuchefu kiko idara ya ardhi mkuu, jamaa ofisi uzifanya kama vijiwe au kampuni binafsi, uliza utaratibu wa kupima ardhi yako kama watakupa wanaishia kusema ni gharama kubwa, document moja kuweka saini tu inachukua miez 6 hadi mwaka, kazi yao ni kuongozana kwenye supu na chai.Jamaa wanakera sana hawa sijui mshahara wanawalipa wa kazi gani, mtu haonekani kazini wiki nzima kwa kisingizio eti yuko site, kumbe yuko kwenye shughuli zake binafsi, hivi kweli unaweza kwenda site posipo kureport kwanza kazini asubuhi.

Umesema ukweli tupu!!
 
Wakuu wenye vitengo naona Serikali imeoverlook kuiuwa au kuiunganisha procurement. Sababu ni moja, hii inahitaji kuwa na kitu kinaitwa independency na pia accountability. Ikiwa hayo mawili hayatazingatiwa Serikali iandike maumivu.
 
Idara zikichanganywa vitengo vinapungua sasa unasema wataamishiwa kwenye vitengo vingine, vitengo hewa ama??
aulize watu walioko wizara zilizounganishwa kama Wizara ya Afrika Mashariki atapata Jibu watumishi hadi sasa hawajajua hatima yao ingawa wachache wanachomolewa kupelekwa wizara zingine
 
watarudi kwenye ajira zao za awali mfano kama afisa elimu atarudi shuleni aliko anzia kazi
 
Back
Top Bottom