Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

.
Kama ni kweli, hilo ni wazo zuri. Nimekaa huko wilayani na kuona mengi yenye mapungufu. Hivyo, kwa ajili ya ufanisi na uharaka, kama ningeulizwa, ningependekeza idara TANO zifuatazo katika Halmashauri zetu:

1.Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
2.Idara ya Elimu, Utamaduni na Michezo.
3. Idara ya Itikadi, Utawala, Fedha na Mipango.
4. Idara ya Oikonomia (yaani Uchumi), ikijumuisha Maliasili, Mazingira, Kilimo, Mifugo, na Ushirika.
5. Idara ya Ujenzi wa Miundombinu ya barabara, maji na makazi.

Idara tano tu zinatosha, kila moja ikiwa na vitengo vyake. Tuzikumbuke kwa msaada wa vokali za A-E-I-O-U, yaani: Afya, Elimu, Itikadi, Oikonomia na Ujenzi.

Mchana mwema.
nimeipenda approach yako ya kuunga mkono hoja na kutoa mapendekezo. Ila nahisi itakuwa na mchanganyiko mkubwa sana na kutishia upatikanaji wa tija, maana Ardhi, kilimo,mazingira,mifugoMaliasili na ushirika ni tofauti sana unless uwezeshaji uwe mkubwa wa kutosha vinginevyo mkuu wa Idara atakuwa msalabani
 
Sasa hivi kuna idara nyingi na bado Majukumu hayakamiliki ifisini jee kulingana na kero kuongezeka za wananchi kupunguza wakuu wa idara kutaendana vipi na ongezeko la changamoto za maisha ya sasa? Serekali kukua ni lazima vitengo na idara kuongezeka
 
Mkuu sifurahii ila ninaandika kutokana na uhalisia wa jambo maana lengo leo la serikali kufanya hvyo ni kupunguza matumizi

Wauze magari yote ya serikali, watapunguza gharama kwa asilimia kubwa sana.
Watumishi wanunue magari yao ila wapewe mafuta na service.
 
watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?
Ajira zisizo na tija au duplication of functions wapi na wapi?! Kama ni wewe ungekuwa mlipaji wa mishahara na marupurupu hayo ungekubali kulipa kisa watu wabakie kwenye ajira for the sake of it?! Tafakari.
 
Kuna tetesi kuwa kutakuwa na mabadiliko ya Idara na Vitengo katika Halmashauri za Wilaya,Miji na Manisipaa.
Idara zitakuwa ni
1.Utawala,Mipango na Fedha
2.Majengo,Mitambo,Miundombinu na Maji
3.Maliasili,Ardhi,Nyuki na Mazingira
4.Afya,Usafi na Ustawi wa Jamii
5.Elimu
6.Kilimo,Mifugo,Umwagiliaji na Ushirika

VITENGO NI
1.Sheria
2.Ukaguzi wa Ndani
Hili jambo ni jema kwa kiasi fulani maana hadi sasa Idara na Vitengo Ndani za Halmashauri za Wilaya na Miji zilikuwa zaidi ya 18
kwa sasa kutakuwa na Wakuu wa Idara 6 na Vitengo 2 Jumla 8.

Tukichukulia kwa Dhana ya Kupunguza Matumizi (Mishahara) ina maana Wakuu wa Idara na Vitengo 12 katika kila Halmashauri za Wilaya,Miji,Manisipaa lazima Wapigwe chini. Hii inamanisha ktk halmashauri 185@12=2,220x 3,400,000 tutaokoa Tshs 7,548,000,000 kwa mwezi
Swali la msingi ni kuwa MISHAHARA YA HAWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO ITASHUSHWA?? NA KUREJEA KWENYE MISHAHARA YA MUUNDO WA VYEO VYAO VYA AWALI KABLA YA UTEUZI WAO???
Na kama ikiwa Hivyo Itabidi kanuni na Taratibu zinazohusu mishashara ya Mfanyakazi inabidi zivunjwe!!
Na kama wataendelea kulipwa Mishahara yao ya Million 3.4 kutakuwa na maana gani ya kupunganisha hizi idara??
Serikali ilifanya maboresho ili kupata hizo Idara na vitengo, labda kama ilikosea itatueleza wakati ukifika. Lakini aliyeandika hii sidhani kama anataka kuisaidia serikali iboreshe shughuli zake. Kwani kuokoa Fedha tafsiri yake ni nini? Serikali kulipa mishahara mizuri wafanyakazi wake inakuwa inapoteza Fedha? Objectivity katika meseji zetu ni Muhimu sana. Watumishi hawa wengi wao ni Watanzania na wanachangamoto nyingi katika kutoa huduma kwa wananchi wetu. Tuisaidie serikali kutatua changamoto za watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wetu.
 
Naunga mkono maamuzi haya!
ila tatizo ni kujifungia na kuja na haya maamuzi badala ya kuyafanya kuw ashirikishi kila mtu achangie then muamue.
 
Back
Top Bottom