Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?
Halafu hatuoni hata Maisha Yakiwa Afadhali Hata Kidogo

Hadi Pipi Yenyewe haijashuka Bei hata Watoto wafaidi
 
Ndiyo maana promotions zimesimamishwa kwa muda ili haya yafanyike. Hao nyuki dar mnafugia wapi?

Wewe unawaza kufuga nyuki tuu? Kuna ukaguz mbalimbali wa mazao ya nyuki. Matatizo ya division five, you have narrow mind
 
.
Kuna tetesi kuwa kutakuwa na mabadiliko ya Idara na Vitengo katika Halmashauri za Wilaya,Miji na Manisipaa. Idara zitakuwa ni:
1.Utawala,Mipango na Fedha
2.Majengo,Mitambo,Miundombinu na Maji
3.Maliasili,Ardhi,Nyuki na Mazingira
4.Afya,Usafi na Ustawi wa Jamii
5.Elimu
6.Kilimo,Mifugo,Umwagiliaji na Ushirika
.
.
Kama ni kweli, hilo ni wazo zuri. Nimekaa huko wilayani na kuona mengi yenye mapungufu. Hivyo, kwa ajili ya ufanisi na uharaka, kama ningeulizwa, ningependekeza idara TANO zifuatazo katika Halmashauri zetu:

1.Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
2.Idara ya Elimu, Utamaduni na Michezo.
3. Idara ya Itikadi, Utawala, Fedha na Mipango.
4. Idara ya Oikonomia (yaani Uchumi), ikijumuisha Maliasili, Mazingira, Kilimo, Mifugo, na Ushirika.
5. Idara ya Ujenzi wa Miundombinu ya barabara, maji na makazi.

Idara tano tu zinatosha, kila moja ikiwa na vitengo vyake. Tuzikumbuke kwa msaada wa vokali za A-E-I-O-U, yaani: Afya, Elimu, Itikadi, Oikonomia na Ujenzi.

Mchana mwema.
 
Hakuna mtu atapoteza ajira bali wata hamishiwa kwenye vitengo vingine? Hivi unajua sheria za utumishi wa Umma? Kama mgelikuwa mna msikiliza waziri wa tamisemi bungeni wala msingalisema haya hili jambo halikuanza kuongelewa leo!
bunge likibaki na wale wa ndioooo sio bunge tena c unaona ka 18% kanavyowatesa. Wangekuepo wajenga hoja tusingekua na huu mjadala
 
Karibuni mashetani.....karibuni sana maana barabara ya kuja huku kuzimu ni pana sana hivyo hamtabanana.

Mlizani hapa kazi tu ni kuwahi kuingia ofisini na tai? Hata kugombea rimoti na mwanao nyumbani baada ya kufukuzwa kazi pia ni Kazi.

Chagua jina linalokufaa katika utawala wa kuzimu,Makata? Maimuna?Subiani?
kwa kwa kwi kwi acha nicheke mwana wa watu jina langu makata
 
Utaratibu mzuri sana huu!Viva JPM na washauri wako kuhusiana na hili kuounguza idara.
Unakuta Maafisa Elimu 10,wakiwa hawana hata kazi za kufanya ofisini zaidi ya kupiga umbeya na kutafuta dili za rushwa,jambo linalopunguza ufanisi wa utoaji elimu.Hii hutokea hata kwa idara zingine.
Mfano,unakuta Elimu msingi wilayani kuna 1.Afisa Elimu 2.Taalum No.1,No.2,No.3, 3.Vielelezo No.1,No2,No3. 4.Ufundi.5.Sayansi kimu.6.Mazingira 7.Elimu Maalum 8.Michezo 9.Watu wazima 10.Vifaa
Pia unakuta kuna Waratibu TRC na waratibu elimu kata wakutosha ambao wanahesabika wapo kazini lakini hawana vipindi darasani.
Narudia kuunga mkono mpango huu wa kurejebisha idara wilayani kuongeza ufanisi
Procurement ni idara nyeti sana, ipo na ni kiungo cha idara ya sheria ili serikali kuweza kununua. Labda wanaiua na PPRA
Singida mnajulikana kwa unafiki, kila kitu ni kupongeza tu.
 
Procurement ni idara nyeti sana, ipo na ni kiungo cha idara ya sheria ili serikali kuweza kununua. Labda wanaiua na PPRA
Singida mnajulikana kwa unafiki, kila kitu ni kupongeza tu.
Mtake radhi Mh Tundu Antipas Lissu
 
UTENGENEZAJI wa ajiira hakuna tena.Maana itakuwa zimepunguzwa.Huku kwenye sekta binafsi nako itakuaje?
 
Watz mnataka nin kulikuwa na wizara na idara nying mkalalamika sasa hivi znapunguzwa bado ni shida matokeo_2020?
 
Nivema kupunguza mrundikano wa ajira zisizo na msingi,watu wanaenda kazini kupiga stori na kuoneshana mavazi na misuko!! Ajira zienee kwenye Elimu,afya,polisi,zimamoto,kilimo kwenye field sio ofisini alllla
HEKO MAGUFULI, hizi ndio big brains safisha vizuri vijana wapate kazi
 
HAO wafanyakazi wa hizo idara zitakazopunguzwa watahamishiwa kwingine,kurudi walipokuwa awali kabla ya uteuzi au watapewa chao na kwaheri?
 
Kuna tetesi kuwa kutakuwa na mabadiliko ya Idara na Vitengo katika Halmashauri za Wilaya,Miji na Manisipaa.
Idara zitakuwa ni
1.Utawala,Mipango na Fedha
2.Majengo,Mitambo,Miundombinu na Maji
3.Maliasili,Ardhi,Nyuki na Mazingira
4.Afya,Usafi na Ustawi wa Jamii
5.Elimu
6.Kilimo,Mifugo,Umwagiliaji na Ushirika

VITENGO NI
1.Sheria
2.Ukaguzi wa Ndani
Hili jambo ni jema kwa kiasi fulani maana hadi sasa Idara na Vitengo Ndani za Halmashauri za Wilaya na Miji zilikuwa zaidi ya 18
kwa sasa kutakuwa na Wakuu wa Idara 6 na Vitengo 2 Jumla 8.

Tukichukulia kwa Dhana ya Kupunguza Matumizi (Mishahara) ina maana Wakuu wa Idara na Vitengo 12 katika kila Halmashauri za Wilaya,Miji,Manisipaa lazima Wapigwe chini. Hii inamanisha ktk halmashauri 185@12=2,220x 3,400,000 tutaokoa Tshs 7,548,000,000 kwa mwezi
Swali la msingi ni kuwa MISHAHARA YA HAWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO ITASHUSHWA?? NA KUREJEA KWENYE MISHAHARA YA MUUNDO WA VYEO VYAO VYA AWALI KABLA YA UTEUZI WAO???
Na kama ikiwa Hivyo Itabidi kanuni na Taratibu zinazohusu mishashara ya Mfanyakazi inabidi zivunjwe!!
Na kama wataendelea kulipwa Mishahara yao ya Million 3.4 kutakuwa na maana gani ya kupunganisha hizi idara??
mkuu umesema watabaki 8, kwani mwanzoni walikuwa wangapi?
 
Watakaopoteza ajira hapo wataajiriwa kwenye viwanda vinavyojengwa. Nisicho na uhakika nacho ni kama wakati wa redundancy viwanda vitakuwa tayari vina operate! cc:MO11
Kufikirika huwaga kunaweza kukageuka kuwa kusadikika
 
Hakuna atakayepoteza ajira hata mmoja vitengo vyote vitajumuisha watumishi wote.
 
Back
Top Bottom