Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?

Hawapotezi ajira bali watarudi kwenye kazi zao walizoajiriwa mwanzo. Hayo madaraka walipewa tu lkn wana kazi zao.
 
Endelea kukurupuka - mbona hapo sikioini kitengo cha ugavi, tehema, uchaguzi n.k
 
Mkuu sifurahii ila ninaandika kutokana na uhalisia wa jambo maana lengo leo la serikali kufanya hvyo ni kupunguza matumizi

Matumizi yanapunguzwa wapi wakati hivi juzi ameteua lundo la viongozi mbona tunadanganyana kwenye hili ????
 
Ambalo sielewi ni kama idara ziliziunganishwa ziko chini ya wizara moja. Naona inaweza kuwepo ugumu kiutendaji iwapo idara zilizounganishwa zinashughulika na masuala ambayo yako chini ya wizara tofauti.


Nikweli kunauwezekano huduma kwa waananchi zikawa mbovu bila kuwa na tathimini yakinifu wakafanya kwa kukurupuka kama kwenye sukari.
Kuna majanga mawili makubwa ambayo yanaweza kutokea ambayo ni kusababisha wimbi la jamii isiyo na ajira na huduma mbovu kwa jamii .
 

Rais si ana washauri wachumi,wamsaidie kumweleza hiki unachokisema ili tusonge mbele bila kuleta madhara kwenye mzunguko wa uchumi.Mungu ibariki Tanzania
 
eti nyuki nacho ni Kitengo na Mkuu wake wa Idara analamba 3.4 M

Tatizo sio afisa nyuki.Tatizo ni kutoboresha majukumu ya hawa watendaji wazalisha kwa malengo na wakapewa targets .

Kwamfano Hawa watendaji wangewekewa mzingira ya uzakishaji kwa kupewa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na mitambo ya kisasa ya uzakishaji wa asali.

Hivyo ikiwa zao la asali ni moja ya mazao muhimu yenye faida ingeweza kuleta pato moja kwa moja serikalini.

Tatizo serikali inakimbia majukumu ya viwanda na kuachia sekta wabinafsi hii yote inasababishwa na kutokuwa na sera mbadala ya viwanda hasa inayomwezesha mtanzania na mzawa kuwajibika kikamilifu kwa faida na tumekosa dira.

Hii inanyima fursa ya kujenga wataalamu mbalimbali wazawa hivyo tutabaki kuburutwa na mabadiliko ya uchumi wa dunia tukiambulia kazi zisizo rasmi kwa serikali hii kutaka mafaniko ya haraka kwa njia ya mkato bila kujenga uwezo wa ndani .

Na bado tutaisoma namba haya matatizo yote yamesababishwa na kuwa na Viongozi wasio na dira au kwa makusudi na tamaa ya wachache tumefikia hapa tulipo .
 

Khaa, yaani kitengo kinaitwa "Utawala, Mipango na Fedha"? Sitaki kujadili rumor, lakini kama ni kweli, this is wrong. Mambo yaliyorundikwa hapa ndiyo mihimili ya Halmashauri, na Utawala (nina hakika wana maana ya HR and Administration) hayaendani kabisa na Mipango na fedha. Simple minds wanafikiri masuala ya HR and Admin yanaweza kuongozwa na watu wenye fani za uhasibu (Eti wanafikiri administration ya finance ndiyo ile ile admin ya Assets and HR!). Tuwe makini, tusije kuruka mkojo na kukanyaga mavi. Nitarudi habari ikishathibitishwa.
 
Kazi IPO Mwaka huu tuombe mungu
 
Shetani kuishi kama Malaika, atapata shida mwanzoni lakini baadaye atazoea tu!. Hatari sana kwa wale waliozoea kufanya kazi serikalini maana wengi wao wakitoka huko wanakosa muelekeo. Akichungulia private jobs anakutana na "Meet Target" hapo sasa inakuwa shida maana hawakuzoea kabisa. Kazi wanayo kwa MSUKUMA Yule!, Kumfurahisha msukuma hadi afurahi toka moyoni kwake wala si kazi rahisi.............!!!!!!
 
Rais si ana washauri wachumi,wamsaidie kumweleza hiki unachokisema ili tusonge mbele bila kuleta madhara kwenye mzunguko wa uchumi.Mungu ibariki Tanzania

Tatizo, kwa sasa hashauriki. Anaona nchi kapewa aiongoze yeye peke yake...
 
Mali asili na nyuki hapo sijaelewa,
kwa sasa Nyuki ni kitengo kinachojitegemea kama kilivyo Ardhi ila vyote vipo chini ya Idara ya maliasili kwa muundo pendekezwa vyote hivi vitakuwa combined na kuwa idara pasipo vitengo ndani yake
 
Akiingia president mwingine naye atakuja na mambo yake tofauti kabisa. Anabadili yazamani wala sio kuendeleza. Serikali itapoteza muda isipokuwa makini maana inajulikana malipo duni ndio sababu wafanyakazi wa umma hawaperform vizuri sasa akitumia time kubwa kufumua taasisi/idara za umma huku kitaa mambo hayaendi ni bure tu. Tulijaribu kilimo kwanza tumeishia njiani, tunajaribu viwanda......I doubt if we can make it. Binafsi naona bado hatujapata visionary leader.
 
Hivi Kati ya idara na vitengo ipi ni kubwa zaidi ya mwenzie? Naomba ufafanuzi Kwa anaye jua
 
Hamna manunuzi? Maana ndo wapiga dili hawa.
 
Nani aliyekwambia hao wamefukuzwa kazi?
 
labda tujue kwa nini mwanzo ilikuwa hivyo...kabla ya kufanya hivi...isije kuwa tunatengeneza tatizo jingine au mlundikano wa kazi kwa mtu mmoja nakupunguza effeciency...ila kama ilikuwa nikupeana ajira,then let it crush them down.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…