Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

nimeipenda approach yako ya kuunga mkono hoja na kutoa mapendekezo. Ila nahisi itakuwa na mchanganyiko mkubwa sana na kutishia upatikanaji wa tija, maana Ardhi, kilimo,mazingira,mifugoMaliasili na ushirika ni tofauti sana unless uwezeshaji uwe mkubwa wa kutosha vinginevyo mkuu wa Idara atakuwa msalabani
 
Sasa hivi kuna idara nyingi na bado Majukumu hayakamiliki ifisini jee kulingana na kero kuongezeka za wananchi kupunguza wakuu wa idara kutaendana vipi na ongezeko la changamoto za maisha ya sasa? Serekali kukua ni lazima vitengo na idara kuongezeka
 
Mkuu sifurahii ila ninaandika kutokana na uhalisia wa jambo maana lengo leo la serikali kufanya hvyo ni kupunguza matumizi

Wauze magari yote ya serikali, watapunguza gharama kwa asilimia kubwa sana.
Watumishi wanunue magari yao ila wapewe mafuta na service.
 
watu wengi watapoteza ajira ila wewe unafurahi eti unabana matumizi

hii nchi tunakwenda wapi ?
Ajira zisizo na tija au duplication of functions wapi na wapi?! Kama ni wewe ungekuwa mlipaji wa mishahara na marupurupu hayo ungekubali kulipa kisa watu wabakie kwenye ajira for the sake of it?! Tafakari.
 
Serikali ilifanya maboresho ili kupata hizo Idara na vitengo, labda kama ilikosea itatueleza wakati ukifika. Lakini aliyeandika hii sidhani kama anataka kuisaidia serikali iboreshe shughuli zake. Kwani kuokoa Fedha tafsiri yake ni nini? Serikali kulipa mishahara mizuri wafanyakazi wake inakuwa inapoteza Fedha? Objectivity katika meseji zetu ni Muhimu sana. Watumishi hawa wengi wao ni Watanzania na wanachangamoto nyingi katika kutoa huduma kwa wananchi wetu. Tuisaidie serikali kutatua changamoto za watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wetu.
 
Naunga mkono maamuzi haya!
ila tatizo ni kujifungia na kuja na haya maamuzi badala ya kuyafanya kuw ashirikishi kila mtu achangie then muamue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…