Mie nadhani kuna haja ya wananchi wengi kuelimishwa juu ya hulka za wanasiasa na athari zinazowapata kwa kukiuka maagizo ya vyombo vya dola.
Ona kwa mfano, polisi wamesema kuwa maandamano hayana kibali cha polisi na kwa hali hiyo ni batili, mjinga mmoja anajitokeza na kuanza kuwashawishi wananchi waandamane. Polisi wakitumia nguvu kuwatawanya mtu huyo anaanza kutengeneza chuki eti polisi wametumia nguvu kupita kiasi. Au polisi wamezuia watu kukusanyika mahali fulani kwa sababu yoyote ile.
Pia polisi wameimarisha ulinzi katika eneo hilo na askari wapo hapo kwa zaidi ya masaa 6' hawali wala kunywa. Anajitokeza mjinga mmoja anaanza kuwahamasisha wananchi waingie kwa nguvu. Polisi wakitembeza mkong'otomtu huyo anaanza kulalamika matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi.
Mie nadhani polisi ifike hatua badala ya kuhangaika na wananchi, ishughulike na huyu mchochezi