Idara ya Usalama wa Taifa ipewe Mamlaka zaidi ili kuinusuru Nchi

Kwahiyo Mkuu kumbe hawa watakuwa ni ' Masimbilizi ' tu wanaojifanya kuwa ni wana TISS wakati kumbe siyo? Vipi Mkuu na Wewe hauko huko ' manake ' una vimelea na viashiria vyote vya kama vile upo huko kwa wenye ' nchi '. Kuna Mtu huko ana jina kama la ID yako hii sijui ndiyo Wewe au ni majina tu!
Mimi siko huko mkuu, ila nilichokiandika ndicho.
 
Hivi unaweza kuwajua Wachawi kama na siyo mmoja au miongoni mwao? Mkuu nimeshaanza kukuogopa sasa na utanifanya nikae mbali na Wewe humu JF kwani nasikia nyie ( wana TISS au Eaglewing House ) ndiyo wenye nchi halafu hamshindwi jambo kama mkikivalia ' njuga '. Hongera kwa kuwa huko na bila shaka huwa unaonana sana na hawa wenzako ' Kimajukumu ' akina Mussolin5 na Evelyn Salt. Nawatakieni tu majukumu mema katika kutusaidia kutulindia usalama wa ndani na wa nje ili nchi yetu ibaki kuwa salama.
 
Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ni miongoni mwa Taasisi nyeti kabisa nchini kutokana na umuhimu wa majukumu yake.

Umuhimu wake unakuja kutokana na sabababu kwamba; nchi yeyote ile ni lazma iwe na maadui wa ndani na nje na ili nchi hiyo ipate kustawi, basi ni lazma maadui hao wadhibitiwe.

Baadhi ya maadui wanao hujumu nchi (wawe wa ndani au nje) wanaweza kufanya shughuli zao kwa siri sana lakini kwa ufanisi mkubwa na mazingira na mitandao wanayotumia kufanya uhalifu inaweza kuwa yenye utata na usiri mkubwa kiasi kwamba Jeshi la polisi kulingana na muundo wake haliwezi kugundua njama hizo bila kupata msaada wa vyombo vingine.

Kadhalika viongozi wa nchi huhitajika kufanya maamuzi wakiwa na taarifa za kutosha hivyo ni lazma wawe na njia inayoweza kuwapa taarifa juu ya mambo kadhaa ili wafanye maamuzi "With informed mind".

Pamoja na kuwepo kwa Taasisi hii inayoogopwa na wengi, kumekuwa na matukio mengi ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi kama vile Ujangili wa Tembo, Usafirishaji wa wanyama Hai nje ya Nchi,Ulipuaji wa mabomu ya kuua, Kuongezeka kwa ufisadi,Ufichaji wa fedha nje ya nchi,Uingizaji wa fedha chafu kwenye mzunguko,Rushwa kwenye mambo nyeti ya kitaifa na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja yanahatarisha usalama wa nchi yetu.

Kwa mujibu wa sheria iliyounda taasisi hii (TISS) ,yaani ; "TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE ACT 1996", Unakuta taasisi hii haipaswi kulaumiwa kwa kile kinachotokea nchini. Hii ni kwa sababu; kwa mujibu wa sheria hii,Taasisi hii imepewa majukumu ya kukusanya taarifa, kuzichambua, na kisha kushauri.

Wanaoshauriwa wanakuwa ni viongozi wa siasa wanaotokana na vyama vya siasa (Rais na Mawaziri) ambao licha ya kuwa viongozi wa kitaifa ; pia wanakuwa wamebeba ajenda zao za kisiasa,ajenda za vyama vyao na dhamira zao binafsi (ambazo zaweza kuwa za afya kwa taifa au hatari kwa Taifa). Kwa hiyo basi; Chombo hiki kinapokuwa kimemaliza majukumu tajwa hapo juu kwa kuishia na "kushauri"Kinakuwa kimemaliza majukumu yake kisheria (Bila kujali kama ushauri wake utafuatwa au laa) na hakipaswi kulaumiwa kwa kuwa sheria hairuhusu kufanya zaidi ya hapo.

Katika mazingira kama haya (ya kuipa TISS) Mamlaka kidogo namna hii, kimsingi kuna mambo mengi yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na huku kukiwa hakuna maelekezo ya kutosha ya kisheria kwamba nani afanye nini.Kwa mfano; Milipuko ya mabomu kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha; Upo uwezekano kwamba TISS Walijua, pengine wakashauri, na ushauri wao ukapuuzwa.(kama ambavyo naamini walikuwa wanajua kuhusu suala la kusafirishwa kwa Twiga hai lakini bado Twiga walisafirishwa). Kimsingi kama suala la Arusha lilikuwa ni tukio la kisiasa kama baadhi ya watu wanavyo sema,na ikiwa watekelezaji ni CCM; TISS, Kushauri ingekuwa ni sawa na kumshawishi boss wao asitekeleze kile anachodhani anatakiwa kutekeleza. Kwa hakika katika mazingira haya, inawezekana kabisa kwamba chombo hiki kinatekeleza majukumu yake lakini pamoja na hivyo matukio ya kuhatarisha usalama yanatokea kutokana na udhaifu wa kisheria.

Kwa kuendelea na sheria hii (1996) bado vyama vya siasa,Viongozi wa kisiasa, na baadhi ya watu wanaweza kuwa na nguvu kuliko TISS; Yaani TISS, inaweza kukusanya taarifa,kuzichambua na kuwashauri ila wakakataa ushauri na kutenda kinyume na kuvuruga usalama wa nchi.Katika mazingira haya upo uwezekano siku moja nchi ikaelekea tusiko kutegemea kwa kuwa si lazma kila mwanasiasa awe na nia ya dhati ya kuipeleka nchi mbele kwa kuwa viongozi wa kisiasa hupatikana kwa bahati nasibu kutoka katika jamii (jamii yenye watu wema na wabaya).

Katika mazingira haya mfanyabiashara mmoja wa madawa ya kulevywa anaweza kugombea ubunge, baada ya kupata ubunge akapewa uwaziri mkuu (by chance), baada ya kupewa uwaziri mkuu akawa anatumia nafasi yake serikalini na kinga za kiungozi kufanya mambo yenye manufaa kwake lakini hatari kwa taifa,TISS wakamshauri lakini akakataa.

Kimsingi taasisi hii ya Usalama wa Taifa sasa inatakiwa kupewa mamlaka zaidi na kuruhusiwa kuzuia matukio yoyote yanayoonekana kuwa ni tishio kwa usalama wanchi bila kujali mfanyaji ni nani(Wawe na nguvu ya juu kabisa katika masuala yanayoweza kuhatarisha usalama).Inatakiwa tuwe na dira,misingi na maadili ya taifa ambayo ni lazma yafatwe na kila mtu (kuanzia Rais na wengine wote) na mamlaka ya kuhakikisha kwamba misingi hiyo inafuatwa wapewe TISS. Hii itawasaidia kuwa na mmlaka kamili ya kutekeleza majukumu yao kama lilivyo jina la Taasisi yenyewe. Baada ya kukipa mamlaka hayo chombo hiki, mambo kama vile kuficha fedha nje, umafia kwenye siasa na mambo mengine kama mitandao ya madawa ya kulevya yanaweza kudhoofishwa sana hata kama yanafanywa na vigogo wazito.

Swali la kizushi:
Kama msajili wa vyama vya siasa anasema ikibainika kuwa waliolipua bomu Arusha ni CHADEMA atakifuta CHAMA, Lakini kama ikibainika ni CCM; Kwa kuwa ni chama tawala atakishauri. Je! ushauri wa Tendwa unaweza kuwa na nguvu kuliko wa TISS, na hivyo kuwa ni lazma ukubalike? Ikiwa sio, Je ikibainika ni CCM, halafu akawa shauri na wakakataa, TISS wakawashauri wakakataa, ni nani wakuwadhibiti? Je! Hali itakayofuata baada ya hapo itakuwa ya afya kwa nchi yetu kweli?
Safi sana ni uchambuz makin na wenye kujitosheleza kabisa
 
Ipewe meno zaidi ya sasa?Mbona sikuelewi mkuu?Hao ndio wanakuamulia Leo uishi vipi,wewe unasema wapewe meno?
 
Ukisikia yallalah fahamu jiwe limemgusa mwenyewe.nafuatilia tu huu uzi kwa miaka 4 kuna mengi nayapata.
Endeleeni kutujuza mnaojua.

Tueleze Ofisa vip Mkuu naona umekuja kivingine, jambo
 
Watanzania tuna safari ndefu sana. Sasa tumetoka kwenye siasa tunavamia kuijadili taasisi ambayo sio ya kisiasa na inaendeshwa kwa usiri mkubwa. Kazi kweli kweli. Wewe una uhakika hao waliokamatwa kweli ni watu wa usalama wa taifa? Unajaribu kuwaingiza watu matatizoni kuanza kuijadili TISS. Unachokitaka hao unaowajadili watakupatia kama unadhani upo salama sana ktk hili jukwaa au huko mitandao mingine. Kama mtu sio daktari wa mambo ya neural unaanzaje kujadili na kukosoa namna ya kufanya operation inayohusu ubongo? Tuheshimu taaluma za watu. Tuwaache TISS wafanye kazi zao kadiri ya taaluma yao na mafunzo ya kazi yao. Haya mengine ni mambo ya propaganda za mitandaoni.
Acha kumtisha Jamaa yeye ni Mlipa Kodi Hao TISS wanalipwa Kupitia kodi zetu kwanini asihoji? Mpaka imetungiwa Act 1996 ina maana Ni Taasisi inayotambulika kisheria sasa kwanini mtu asihoji?
 
TISS ina uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika shughuli zake wewe kijana wa juzi umetoka kuangalia series za "kijasusi" unakuja hapa unatema pumba unazoita ushauri

Pathetic
Mkuu mbona una mshambulia Mleta mata hata kama TISS iwe na miaka 100 je Tangu inaanza mpaka leo DG ni yule Yule kwanini Hubadilishwa? Jamaa ameshauri poa Sana kwa Uzi kwa kwanza apo.
 
Hivi si tuliambiwa waliovamia clouds ni kikosi maalum toka tiss? Aliyemtolea Nape bastola so walisema sio police? Kama sio polisi ni nani basi maana angekua RAIA Wa kawaida police wangeondoka nae...
 
Jamani TISS bado inafanya kazi hata ambazo hukuzitarajia, serikali hii ni kubwa. TISS nawapongeza, sana ila wajipange vyema kuwakamata hao wa ESCROW NA ACACIA BULYANG'HULU NA BARRICK COOPORATION.

Otherwise nawapa a GO AHEAD makanda hawa watiifu wa idara hii kwa kuitetea nchi na serikali, jamani wanafanya kazi kwa kiapo kikali kuliko hata cha Rais mwenyewe. I salute.

TISS, ur hero kiintelijensia.
 
tiss ingependeza kuwa taasisi huru yenye mamlaka ya kuchunguza na kufikisha mahakamani bila kuingiliwa..
lakini suala la kuingiliwa kisisasa na kuundwa kwake...imeinyima uwanja mpana wa kudeal na matishio ya kiusalama ktk nyanja zote za kitaifa...
ndio maana unakuta makashfa ya upigaji deal kubwa kubwa zenye kuyumbisha uchumi wa kitaifa imekuwa kawaida tuu kutokea.... kiasi masuala hayo yanaibuliwa na wapinzani kisha serikali ndio inayabeba kitu ambacho ni fedhea kwa tiss...
ila sijajua wao tiss wanawajibika wapi na kwa nani wanapokosea ktk uwajibikaji wao dhidi ya masuala ya kitaifa...??...
 
tiss ingependeza kuwa taasisi huru yenye mamlaka ya kuchunguza na kufikisha mahakamani bila kuingiliwa..
lakini suala la kuingiliwa kisisasa na kuundwa kwake...imeinyima uwanja mpana wa kudeal na matishio ya kiusalama ktk nyanja zote za kitaifa...
ndio maana unakuta makashfa ya upigaji deal kubwa kubwa zenye kuyumbisha uchumi wa kitaifa imekuwa kawaida tuu kutokea.... kiasi masuala hayo yanaibuliwa na wapinzani kisha serikali ndio inayabeba kitu ambacho ni fedhea kwa tiss...
ila sijajua wao tiss wanawajibika wapi na kwa nani wanapokosea ktk uwajibikaji wao dhidi ya masuala ya kitaifa...??...
 
Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ni miongoni mwa Taasisi nyeti kabisa nchini kutokana na umuhimu wa majukumu yake.

Umuhimu wake unakuja kutokana na sabababu kwamba; nchi yeyote ile ni lazma iwe na maadui wa ndani na nje na ili nchi hiyo ipate kustawi, basi ni lazma maadui hao wadhibitiwe.

Baadhi ya maadui wanao hujumu nchi (wawe wa ndani au nje) wanaweza kufanya shughuli zao kwa siri sana lakini kwa ufanisi mkubwa na mazingira na mitandao wanayotumia kufanya uhalifu inaweza kuwa yenye utata na usiri mkubwa kiasi kwamba Jeshi la polisi kulingana na muundo wake haliwezi kugundua njama hizo bila kupata msaada wa vyombo vingine.

Kadhalika viongozi wa nchi huhitajika kufanya maamuzi wakiwa na taarifa za kutosha hivyo ni lazma wawe na njia inayoweza kuwapa taarifa juu ya mambo kadhaa ili wafanye maamuzi "With informed mind".

Pamoja na kuwepo kwa Taasisi hii inayoogopwa na wengi, kumekuwa na matukio mengi ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi kama vile Ujangili wa Tembo, Usafirishaji wa wanyama Hai nje ya Nchi,Ulipuaji wa mabomu ya kuua, Kuongezeka kwa ufisadi,Ufichaji wa fedha nje ya nchi,Uingizaji wa fedha chafu kwenye mzunguko,Rushwa kwenye mambo nyeti ya kitaifa na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja yanahatarisha usalama wa nchi yetu.

Kwa mujibu wa sheria iliyounda taasisi hii (TISS) ,yaani ; "TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE ACT 1996", Unakuta taasisi hii haipaswi kulaumiwa kwa kile kinachotokea nchini. Hii ni kwa sababu; kwa mujibu wa sheria hii,Taasisi hii imepewa majukumu ya kukusanya taarifa, kuzichambua, na kisha kushauri.

Wanaoshauriwa wanakuwa ni viongozi wa siasa wanaotokana na vyama vya siasa (Rais na Mawaziri) ambao licha ya kuwa viongozi wa kitaifa ; pia wanakuwa wamebeba ajenda zao za kisiasa,ajenda za vyama vyao na dhamira zao binafsi (ambazo zaweza kuwa za afya kwa taifa au hatari kwa Taifa). Kwa hiyo basi; Chombo hiki kinapokuwa kimemaliza majukumu tajwa hapo juu kwa kuishia na "kushauri"Kinakuwa kimemaliza majukumu yake kisheria (Bila kujali kama ushauri wake utafuatwa au laa) na hakipaswi kulaumiwa kwa kuwa sheria hairuhusu kufanya zaidi ya hapo.

Katika mazingira kama haya (ya kuipa TISS) Mamlaka kidogo namna hii, kimsingi kuna mambo mengi yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na huku kukiwa hakuna maelekezo ya kutosha ya kisheria kwamba nani afanye nini.Kwa mfano; Milipuko ya mabomu kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha; Upo uwezekano kwamba TISS Walijua, pengine wakashauri, na ushauri wao ukapuuzwa.(kama ambavyo naamini walikuwa wanajua kuhusu suala la kusafirishwa kwa Twiga hai lakini bado Twiga walisafirishwa). Kimsingi kama suala la Arusha lilikuwa ni tukio la kisiasa kama baadhi ya watu wanavyo sema,na ikiwa watekelezaji ni CCM; TISS, Kushauri ingekuwa ni sawa na kumshawishi boss wao asitekeleze kile anachodhani anatakiwa kutekeleza. Kwa hakika katika mazingira haya, inawezekana kabisa kwamba chombo hiki kinatekeleza majukumu yake lakini pamoja na hivyo matukio ya kuhatarisha usalama yanatokea kutokana na udhaifu wa kisheria.

Kwa kuendelea na sheria hii (1996) bado vyama vya siasa,Viongozi wa kisiasa, na baadhi ya watu wanaweza kuwa na nguvu kuliko TISS; Yaani TISS, inaweza kukusanya taarifa,kuzichambua na kuwashauri ila wakakataa ushauri na kutenda kinyume na kuvuruga usalama wa nchi.Katika mazingira haya upo uwezekano siku moja nchi ikaelekea tusiko kutegemea kwa kuwa si lazma kila mwanasiasa awe na nia ya dhati ya kuipeleka nchi mbele kwa kuwa viongozi wa kisiasa hupatikana kwa bahati nasibu kutoka katika jamii (jamii yenye watu wema na wabaya).

Katika mazingira haya mfanyabiashara mmoja wa madawa ya kulevywa anaweza kugombea ubunge, baada ya kupata ubunge akapewa uwaziri mkuu (by chance), baada ya kupewa uwaziri mkuu akawa anatumia nafasi yake serikalini na kinga za kiungozi kufanya mambo yenye manufaa kwake lakini hatari kwa taifa,TISS wakamshauri lakini akakataa.

Kimsingi taasisi hii ya Usalama wa Taifa sasa inatakiwa kupewa mamlaka zaidi na kuruhusiwa kuzuia matukio yoyote yanayoonekana kuwa ni tishio kwa usalama wanchi bila kujali mfanyaji ni nani(Wawe na nguvu ya juu kabisa katika masuala yanayoweza kuhatarisha usalama).Inatakiwa tuwe na dira,misingi na maadili ya taifa ambayo ni lazma yafatwe na kila mtu (kuanzia Rais na wengine wote) na mamlaka ya kuhakikisha kwamba misingi hiyo inafuatwa wapewe TISS. Hii itawasaidia kuwa na mmlaka kamili ya kutekeleza majukumu yao kama lilivyo jina la Taasisi yenyewe. Baada ya kukipa mamlaka hayo chombo hiki, mambo kama vile kuficha fedha nje, umafia kwenye siasa na mambo mengine kama mitandao ya madawa ya kulevya yanaweza kudhoofishwa sana hata kama yanafanywa na vigogo wazito.

Swali la kizushi:
Kama msajili wa vyama vya siasa anasema ikibainika kuwa waliolipua bomu Arusha ni CHADEMA atakifuta CHAMA, Lakini kama ikibainika ni CCM; Kwa kuwa ni chama tawala atakishauri. Je! ushauri wa Tendwa unaweza kuwa na nguvu kuliko wa TISS, na hivyo kuwa ni lazma ukubalike? Ikiwa sio, Je ikibainika ni CCM, halafu akawa shauri na wakakataa, TISS wakawashauri wakakataa, ni nani wakuwadhibiti? Je! Hali itakayofuata baada ya hapo itakuwa ya afya kwa nchi yetu kweli?
5be50ecb94fa2e418a650a41df6b54fd.jpg
.jpg[/IMG]

Back
Top Bottom