Nyabutoro
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 1,342
- 1,596
Najua hapa JF wapo, nashauri yafuatayo:Wakuu moja ya idara ambayo inajiendesha kizamani ni Usalama wa Taifa. Idara hii haitaki kubadilika enzi na enzi.
Suala la Kukamatwa kwa Spies karibu 8 kama siyo 19 ni moja kati ya Mambo yanayoibua sintofahamu huku wengine wakiwanyooshea Bastola watu halafu Polisi wanakana kuwa hakua Polisi lakini pia hawakumkata nina Uhakika Kama angekua raia wa kawaida na akaonesha Toy tuu angekua kashakamtwa kwa sababu Viongozi wa Polisi walikuepo pale.
Usushushu Tanzania imekua kazi ya Kishkaji na Kurithishana bila kuangalia vigezo kwa wahusika wamekua wanashindwa hata kujua ni Viongozi wepi wa kuwatii Usalama wa Taifa unakuta anatumika na Viongozi ambao hawana hata mamlaka ya Kuwatuma.
Mwisho Niombe tuu Mkurugenzi wa Taasisi hii nyeti tafadhari punguzeni Ushikaji wakati wa Recruitment wekeni watu wenye Uwezo na wenye Taaluma Mbalimbali.
Tuige mifano ya CIA, Mi6, jinsi wanavyo operate kwa Weledi wa Hali ya Juu CIA kule ni taasis ambayo inafanya kazi bila kupokea maagizo ya mtu yeyote ndani ya Marekani.
Vitendo vya TISS kujihusisha na Kuwaibia Kura Wabunge ni vitendo vinavyoishushia heshima idara ya Usalama.
1.Neno intelligence ni weredi, upatikanaji wa watumushi katika idara hii ufanyiwe mchujo kuanzia shule za msingi kwa kuwa na maajenti/informers watakaochagua wanafunzi waliofanya vizuri
2.Maadili ya familia wanazotoka - ni muhimu watu hawa nyeti wasitoke katika familia zenye mitafaruku mf familia ambazo wazazi wameachana
3.Uzalendo :Wafundishwe uzalendo uliotukuka ili watumike kwa busara
NI HAYO, WAWEZA ONGEZA MENGINE